Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 799
Hii ni spi-off thread toka kwenye ile ya ditto na naamini kuwa itakuwa ni changamoto ya kutazama jinsi LAW inavyokluwa practised pale Bongo na je katika mazingira haya kutakuwa na wanafunzi ambao wamemaliza shule lakini kila siku wao ni ma runner katika law firms
anyways back to MKONO kuna poster mmjona humu ndani kwa jina la DUA ameposti hii na nadhani it will get interesting as time goes
anyways back to MKONO kuna poster mmjona humu ndani kwa jina la DUA ameposti hii na nadhani it will get interesting as time goes
Mkono anastahili kuchunguzwa ili afukuzwe Bungeni
Sheria ambazo inawezekana amezivunja makusudi ni:
1. Watu wenye madaraka serikalini kukoma utumishi wanapochaguliwa. Sheria ya 1992 Na. 4 ib. 23 sheria ya 1995 Na. 12 ib. 14 (ambayo ni lazima iwahusu chief executives wa private firms).
2. Masharti ya sheria ya maadili ya uongozi wa umma
3. Masharti ya kazi ya wabunge sheria ya mwaka 1984 Na. 15 ib 13
Kamati ya uongozi & kamati ya katiba, sheria na utawala ndizo lazima zishughulikie suala hili kama ilivyoelezwa katika
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania as specified kipengele 4 majukumu ya msingi na ya jumla ya kamati.
Kifungu 4.1 Bunge na kamati zake ndiyo darubini (oversight or watch-dog organ) ya kuhakikisha kwamba mambo yote ya uendeshaji wa kazi za dola unafanywa kwa kuzingatia katiba, sheria na kanunu zilizowekwa.
Wajumbe wa kamati hii ni :
1. Mwenyekiti –Spika
2. Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni
3. Kiongozi wa upinzani bungeni
4. Wenyeviti wa kamati za kudumu
5. Mwanasheria mkuu wa serikali
Hata kama itabainika kwamba hajavunja sheria kamati ya kanuni za bunge inaweza kufikiria na kutoa mapendekezo juu ya kufanya mabadiliko katika kanuni za Bunge – uchunguzaji huu utatokea iwapo taarifa ya kutoa pendekezo lolote na hususan hili hasa kutoka kwa wabunge wa opposition. (Mkono anafanya tenda nyingi kutoka serikalini na wakati huohuo yeye ni Mbunge)
Haya sasa wabunge wa upinzani hii ni changamoto kwenu. Tusikubali Mbunge kumtetea criminal.