Nimetengeneza shule ya kwanza ya kidigitali ambayo wanafunzi watasoma na kufanya mitihani wakiwa nyumbani

Barackachess

Senior Member
Sep 1, 2018
156
121
SHULE YA KIDIGITALI, SOMA MTANDAONI UKIWA NYUMBANI HUITAJI KUFIKA SHULE TENA

Habari naileta kwako TAIFA ONLINE INTERNATIONAL SCHOOL Ni taasisi mpya nchini Tanzania inatoa elimu kwa njia mtandao pasipo kujali eneo ulilopo. Tutembelee www.taifaschool.net

NB: NAPOKEA USHAURI WA AINA YOYOTE, MSIACHE KUNISHAURI NA KUNISEMA KAMA KUNASEHEMU NAKOSEA, PIA TUNAWEZA ONANA MOJA KWA MOJA KAMA UTAHITAJI KUONA NA MIMI KWA UFAFANUZI WA KINA NA USHAURI LAKINI PIA KWA AJILI YA USHAURI

Taasisi hii inatoa elimu kwa rika zote, makundi yote, rangi zote na imani zote kwa mafunzo yao yanafuata mtaala wa elimu inayomamiwa na wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Kiufupi wanatoa huduma zifuatazo:
1: Distance learning( live classes). Hapa watu husoma moja kwa moja kwa kumuona mwalim yaani audiovisual kuanzia saa mbili Hadi saa nne usiku. Wanafunzi waliosajiliwa wataweza kuuliza maswali na kujibiwa muda wa kipindi.

Gharama Yake ni Tsh 50,000/= kwa Mwezi Kujisajili ingia Sec Registration


2: Taifa online exams. Hii ni mitihani inayotolewa kila mwezi yenye muongozo mzuri kuanzia DARASA LA 4 hadi kidato cha sita. Mwanafunzi anafanya mtihani akiwa nyumbani au popote alipo kwa kutumia simu au kompyuta kwa usimamizi wa mzazi pia usimamizi madhubuti wa kisasa wa taasisi kwa kutumia hiyo simu na kompyuta yake.

Gharama yake ni TSH 1,000/= kwa somo, Kujisajili ingia TAIFA EXAM


3: Taifa online school library. Hapa mwanafunzi aliyesajiliwa atapata nakala (NOTES) na machapisho mbalimbali yaani nukuu (NOTES) za masomo yote. Pia mwanafunzi aliyesajiliwa atapa video za masomo yote husika. Mwanafunzi aliyesajiliwa atachagua kusoma nukuu au kuangalia video rekodiwa za nukuu (NOTES) husika.
Gharama ni TSH 0 yani BURE tembelea Taifa Secondary Online Library

4: Taifa online school tuition hii ni kwa wanafunzi wanaotaka kusoma tuition muda wa ziada pindi watokapo shuleni na nyakati za weekend pekee, Kwa siku za wiki (Jumatatu -Ijumaa) mwalimu atakuwa na kipindi na mwanafunzi kwa dakika 40 tu ili kumzuia kumchosha zaidi, Kwa siku za weekend (IJUMAA , JUMAMOSI, JUMAPILI) mwalimu atakuwa na kipindi na mwanafunzi cha Dakika 60 *Gharama ni * Tsh 10,000/= kwa somo la sayansi na Tsh 5,000/= kwa somo la Arts kwa mwezi kujisajili binyeza link hii (Maandishj haya ya Blue Tuition Registration

5: Kujifunza kiswahili kwa wageni. Hapa wageni wanajifunza lugha ya kiswahili popote walipo duniani kwa Gharama ya Tsh 800,000/= kwa vipindi 100, Kujisajili ingia Student Registration

6: Book analysis. Hapa mwanafunzi aliyesajiliwa atapata chambuzi za vitabu kwa njia ya maandishi na sauti. Mwanafunzi atachagua kusoma chambuzi za vitabu vya fasihi au kusikiliza sauti nzuri. Hapa Ni vitabu vya fasihi ya kiswahili na kiingereza yaani literature BURE PASIPO GHARAMA YOYOTE ingia Books Analysis

7: Taifa online school question and answer. Hapa mwanafunzi aliyesajiliwa atauliza swali na kujibiwa papo. Taasisi itamfahamisha mwanafunzi aliyesajiliwa kuwa mwalimu yupo kazini yaani yupo online uliza swali. Mwanafunzi aliyesajiliwa atauliza swali kwa njia ya sauti au maandishi ama video na kujibiwa muda huo huo BURE PASIPO NA GHARAMA YOYOTE ingia www.taifaschool.net

Pia tunatoa huduma zingine nyingi Kama online automatic quiz (Chemsha Bongo Ya Maswali Online Bure), learn English na events nk.

ZINGATIA: taasisi inafuatilia maendeleo ya wanafunzi wake na kutoa matokeo kwa wakati pia tunawatafutia wanafunzi vituo vizuri vya kufanyia mitihani yao ya NECTA, Usilipie huduma yoyote kupitia namba ya MPESA AU TIGO PESA AU MTANDAO WOWOTE WA SIMU PASIPO JINA LA TAIFA SCHOOL KUONEKANA, PIA USILIPIE HUDUMA KABLA UJAJIRIDHISHA NA HUDUMA KWA KUIONA. KWA WATEJA WA DAR ES SALAAM TUNASHAURI WAFIKE OFISINI MOJA KWA MOJA.Ofisi Zetu Zinapatikana
Acacia Estates,
1st Floor (Ghorofa ya 1)
Plot no. 84, Kinondoni Road
P O Box 38568, Dar es Salaam

Tunapatikana kwa nambari ya ofisi +255 (0)22-219-8079 (LandLine) au Whatsapp Number +255(0)652 428 842

Tufuhatilie moja kwa moja kupitia ukurasa wa instagram: @taifaschool facebook Taifa Online International School
 
Vijana wengi graduate mnajitahidi kubuni mambo mapya ila in most cases you misallocte nguvu zenu na mnafanya vitu bila feasibility study, tafiti yoyote anakua na lengo la kutatua changamoto sugu na inatowa simple alternative, ila hiyo digital school sio ya Tanzania ya leo, au mwenzetu unaishi first world country sio hi bongo yetu?
 
wazo zuri, ila kwa nini usingefanya mtu anafanya reg moja then anapata access kwenye module alizolipia Mfano kuwe na Module ya Sec Registration, Taifa Exam, Taifa Secondary Online Library, Tuition Registration, Student, Registration, Books Analysis etc...
 
Good idea,tafuta usajili wa kueleweka utawapata tu wasopenda kwenda!
 
Huko ndiko tunako elekea, Lengo lilikuwa kusajili kwa ajili ya cambridge syllabus (TUTAANZA KUITOA MWEZI WA 9 MWAKA HUU) , Lakini tukaona sio mbaya tukaleta pia mtaala wa NECTA
 
wazo zuri, ila kwa nini usingefanya mtu anafanya reg moja then anapata access kwenye module alizolipia Mfano kuwe na Module ya Sec Registration, Taifa Exam, Taifa Secondary Online Library, Tuition Registration, Student, Registration, Books Analysis etc...
Nashukuru sana kwa ushahuri huu, Nakuhakikishia mpaka kufikia jumamosi tutakuwa tumekwisha fanya hivyo (Umenipa wazo zuri) na nitakuletea mrejesho hapa kwamba nimikwisha rekebisha. Ahsante kwa kuchangia uboreshaji
 
Jamaa unakatisha tamaa sana
Kwani huu Ni uwongo. Kubadilisha watu behavior Ni kazi Ila inawezekana mkuu. So nimemwambia ivyo ili atie more efforts to make people change na asitegemee mteremko kiivyo. Na faida anaweza Anza Iona even after 20-50yrs. Sie blacks hatuanzishi projects kwa kizazi chetu. Tunategemea instant gratification ndio inayotumaliza. Unadhani ataanza Leo Leo na kuanza kuona matunda. It takes time. Time is our allies in many of our endeavors accomplishment
 
Vijana wengi graduate mnajitahidi kubuni mambo mapya ila in most cases you misallocte nguvu zenu na mnafanya vitu bila feasibility study, tafiti yoyote anakua na lengo la kutatua changamoto sugu na inatowa simple alternative, ila hiyo digital school sio ya Tanzania ya leo, au mwenzetu unaishi first world country sio hi bongo yetu?........
Nadhani Ni mwanzo wa mabadiliko,,,hapo nyuma kidogo Tanzania hatukuwa hata na barua Pepe lakini baadae tunapata kila kitu kiganjani
 
Back
Top Bottom