Je, ni sahihi baadhi ya shule kulazimisha wanafunzi kusoma kipindi cha likizo kwa kulipia Tshs.3,000 kwa mwezi?

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Nov 30, 2022
607
553
Habarini,

Nimekutana na hali hii ambapo kuna baadhi ya shule za sekondari zimejiwekea utaratibu wa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kulazimisha wanafunzi kusoma kipindi cha likizo bila kupumzika kwa malipo ya 3,000/= kwa madai kuwa vikao vya wazazi ndiyo vimeruhusu.

Huu utaratibu naupinga kwani ni kuwachosha wanafinzi na pia walimu wanatakiwa kupumzika ili kujiandaa na muhula unaofuata kitu ambacho kinsababisha wanafunzi kukinaiwa na shule kwa kupoteza hamu.

Serikali iliwahi kupinga utaratibu huu wa masomo ya ziada kwa malipo ikiwa na maana yake lakini baadhi ya walimu wamebuni huu mradi kwa kuubadilisha na kudai ni "by laws " za shule kila mwanafunzi lazima asome kipindi cha likizo kwa vikao vya wazazi ndiyo vimeridhia,je sheria,ratiba na taratibu za uendeshawaji wa shule zinapangwa na wazazi?

Mzazi analipia ada ili mwanafunzi asome kwa utaratibu uliowekwa na wizara siyo shule na wanafunzi wote wanatakiwa kusoma kwa muda uliopangwa na kwa pamoja lakini walimu wanasema mwanafunzi ambaye atakuwa haudhurii kipindi cha likizo atakuwa na kukosa yaliyofundishwa kipindi cha likizo hatafundishwa na atakuwa amepitwa,je hii ni sawa?

Kipindi cha likizo kuna wanafunzi wanasafiri au wanatakiwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ili kujijenga na kupata uzoefu kwani maisha siyo shule tu lakini muda wote walimu wanataka wafundishe walipwe 3,000 kwa kichwa je hiyo siyo tuition?

Hiyo siyo elimu bora bali bora elimu na kama walimu wanafanya wema basi wafundishe bure kwani huko siyo kujitolea bali ujanjaujanja.

Naomba waziri wa elimu uzuie hii kitu inakera na inaleta ubaguzi kwani kuna wazazi wengine hawana pesa hiyo na pia wanafunzi wanatakiwa wapumuzike kulingana na ratiba.

Uelewa wa mwanafunzi kama ni 20%hata akisoma miaka mia moja hautaongezeka utabaki uleule.

Asante.
 
Kwanini kunakuwa na masomo ya ziada?
1.Mwalimu ni mzembe?
2.Walimu ni wachache hivyo mzigo mkubwa kwa mwalimu mmoja?
3.Syllabus imetungwa bila kuzingatia mda?
4.Walimu wanatamaa tu ya fedha?
Ungejiuliza maswali haya mkuu.
 
Mwanao akiacha kwenda wanamfanyake?

Sasa nijiulize maswali haya ya nini wakati wizara ina wataalam walioajirwa kwa kazi ya kujiuliza na kuyajibu na wakatuleta ratiba ya kila mwaka ikieleza lini wafungue na lini wafunge?
 
Mwanao akiacha kwenda wanamfanyake?
Mwanzo walikuwa wanamuadhibu baadae niliwauliza wanafanya hivyo kwanini mwalimu mmoja akasema ni sheria za shule tukarumbana sana wakaniambia hawata mrudia waliyofundisha kipindi cha likizo kwa hiyo atajijua mwenyewe nikawaambia mwanangu nilishamuandaa kuwa mfanyabiashara na shuleni nataka apate exposure tu siyo kitu kingine na pia niwajibu wao kumfundisha waliyofundisha kipindi cha likizo kwani nimelipa ada kwaajili yake afundishwe kufuatana na ratiba.
 
Back
Top Bottom