Wakuu,
Mimi nikiwa kama Mtanzania mwenye akili timamu, nimechukizwa sana na jinsi watanzania mbalimbali walivyolishadadia na kuendelea kuchangia maoni yao kwa wanafunzi waliokuja kutoka Sudan kufanya mafunzo yao ya udaktari kwa vitendo katika chuo cha Afya Muhimbili.
Nasema nimegadhabishwa kwa sababu mtizamo wa watanzania wengi umejikita kwenye utani wa kuwadhalilisha wanawake na kutweza uanaume kwa malengo yasiyofahamika.
Wachangiaji wengi wameonyesha kuwa vijana wengi wa Kitanzania hawana maadili na mawazo yao yamejikita zaidi kwenye masuala ya kingono kwa wanafunzi hao wa Ssudan na wameendelea mbele zaidi kuonesha kuwa wanaume wengi wa Tanzania fikra zao ni ngono tu na hawana jambo lingine wanalofikiria.
Nimestushwa hasa nilipoona kwenye baadhi ya magroup ya WhatsApp, redio, magazeti niliyodhani wana weledi wa kutosha kuhusu masuala ya kijamii kuangukia kwenye hoja kama hii, tena wengine ni wasomi wanaojinasibu kuwa wameelimika.
Tabia hii ya hovyo iliyooneshwa na wanajamii wenzetu inatuzalilisha kwa kiasi kikubwa na kutweza utu wetu sisi kama Watanzania, hasa nikirejea sakata lililotokea mwaka baada ya Klabu ya Simba kumsajili Mchezaji mmoja kutoka barani Ulaya ambapo waandishi wetu walijikuta wakifanya masihara kwa kumuita mzungu yaliyopelekea kuleta hisia za kibaguzi kwa mwana soka yule nguli kiasi cha kuamua kukatisha mkataba wake na kuondoka.