Uuzaji wa akaunti za mitandao ya kijamii: Je, zinakidhi malengo ya soko la mnunuaji?

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
Watu wengi, taasisi, na makampuni wanazidi kuhamishia shughuli zao kwenye mitandao ya kijamii kila siku. Lakini kujiunga na majukwaa hayo na kukuza akaunti kutoka wafuatiliaji 0 hadi, labda tuseme 10,000, inahitaji jitihada na muda mwingi, na hilo limeacha watu wengi wakijiuliza, "je, naweza kununua akaunti za mitandao ya kijamii?"

Kununua akaunti za mitandao ya kijamii zenye wafuatiliaji sasa ni jambo la kawaida, na karibu kila mtu inaonekana anafanya hivyo ili kuharakisha ukuaji wa brand au biashara zao. Na sasa watu wengi mtandaoni wanawavuta wanunuzi watarajiwa. Hii ni ushahidi tosha kuwa biashara hii inakua kwa kasi.

Ni kazi ngumu kukuza akaunti changa kwakuwa watumiaji wachache sana wako tayari kutumia muda wao kujifunza kile ambacho akaunti mpya inaposti. Ni ngumu lakini inaeleweka. Hali inakuwa mbaya zaidi kwani algorithym kwa kawaida inapendelea wale walio na wafuasi wengi na wanaovutia ushiriki mkubwa.

Hilo ndilo linalofanya wengi wanasukumwa kununua akaunti ambazo tayari zina wafuatiliaji wengi. Akaunti zenye wafuatiliaji wengi huvuta hadhira zaidi, na hilo linamaanisha biashara na umaarufu zaidi. Sote tutakubaliana kuwa jambo la kwanza unaloliona ukipitia kurasa za taasisi au watu binafsi kwenye mitandao ni hali ya akaunti, hasa idadi ya wafuasi.

Lakini je, hizi akaunti zinakidhi malengo ya soko la mnunuaji? Je, wafuasi wa akaunti husika wanaendana na kile unachotangaza? Hauhitaji akaunti iliyo na wafuatiliaji wa masuala ya mitindo wakati unashughulika na mambo ya kilimo. Baadhi ya watumiaji watakuwa tayari kutohusiana na akaunti yako na kuifuta.

Nakumbuka kuna jamaa yangu alinunua akaunti ya Instagram yenye wafuasi 18,000 kwa ajili ya NGO yake changa. Ndugu yangu yule alikuwa hapati engagement kwakuwa mwanzoni nadhani akaunti ile ilikuwa ni ya udaku, sasa yeye kaleta masuala ya kilimo. Alikuwa anaishia kupata comments za akina “Mwajuma Mtamu” na “Najma Kiuno Temeke”. Lakini pia naamini kuwa huenda kuna walionunua na wakafanikiwa.

Kama umeshawahi kukutana na akaunti ukajiuliza ilikuwaje ukai-follow, basi huenda akaunti hiyo nayo ilibadilishwa mmiliki, hivyo na maudhui nayo yakabadilika.

Za Insta.jpg
 
Back
Top Bottom