Nimesikiliza hotuba za nyuma kuhusu akiba ya Serikali , zinasoma Bilioni siyo Milioni; Gavana wa BOT na watu wako mnasikilizaga hizi hotuba?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kosa la uandishi lililopelekea kosa la matamshi lililotokea kwenye hotuba za Mhe Rais kuhusu akiba ya Taifa limekuwa likifanyika Katika hotuba za nyuma. Hotuba yake ya Juni alisema Tena USD Bilioni 4000+ na siyo Usd Milion 4000+, Juzi Bilioni 6000+ na siyo Milioni. Ukisoma vyombo vya habari yakiwemo magazeti huko nyuma na hata hii ya Sasa wameripoti Bilioni siyo Milioni.

Hapa unabaini lipo tatizo la wasaidizi wake kufanya copy na paste na hakuna anayeumizwa kichwa kusoma na kuandika. Lakini kosa la pili ni BOT na Hazina kushindwa kujua makosa haya Katika data wanazotoa. Tatu ni ukimya wa Waziri wa fedha may be nayeye ajipi muda wakusoma au kuzidua hotuba za mkubwa wake.

Nadhani upo umuhimu wakuondoa ndugu na makada ofisini nakuweka watendaji ambao Wana Moyo wakumsaidia Mhe. Rais. Watumishi wa umma awasomi Wala kufanya proof reading . Haya makosa yamekuwa yakijirudia hata kwenye teuzi unaona anateuliwa mtu Hadi watu wa nje wapige kelele ndipo unagundua ipo shida mahali.

Tunatakiwa kusuka upya hizi ofisi nyeti
 
Data huwa haisemwi, data inaandikwa na kila mwenye kujua kusoma ataisema mwenyewe.

Rais anaweza kukosea kusema akiwa anahutubia, lakini hotuba yake ya maandishi (data) haipaswi kukosea. Kwa hili la mama Samia utasemaje kakosea wakati alichokisema na kilichoandikwa kinafanana?
 
Na kama amekosea hili jepesi kabisa, tutaaminije mengine makubwa na mzito zaidi hayajakosewa?
 
Data huwa haisemwi, data inaandikwa na kila mwenye kujua kusoma ataisema mwenyewe.

Rais anaweza kukosea kusema akiwa anahutubia, lakini hotuba yake ya maandishi (data) haipaswi kukosea. Kwa hili la mama Samia utasemaje kakosea wakati alichokisema na kilichoandikwa kinafanana?

..je, raisi hawajibiki kutambua makosa ktk hotuba zake?

..je, akiletewa hotuba, taarifa, au data, anazichukua kama zilivyo?

..unakumbuka tukio la uteuzi wa DG wa Tpdc? Nini kilitokea? Chanzo cha uteuzi ili kilikuwa ni nini?

Cc Erythrocyte, Tindo, Pascal Mayalla
 
Dada Beatrice, mimi nashangaa mnavyojaribu kumtoa Samia katika hili. Wewe ungekuwa ndiye Rais ungesoma kitu toka kwa msaidizi wako bila kuhariri? Kama anasoma bila kuhariri basi hastahili kabisa kuwa Rais. Usisingizie wasaidizi. Rais ambaye alikuwa Makamu kwa miaka 5 iliyopita anatakiwa ajue kabisa kuwa ni impossible kwa Tanzania kuwa na reserve ambayo ni maelfu ya mabilioni ya USD.

Hata sisi tuna masekretari ofisini. Secretari akichapa barua lazima niipitie na kufanya marekebisho. Nikishaiweka sahihi yangu na-own makosa yake yote. Siwezi kuwaambia huko barua inakokwenda eti ni makosa ya sekretari.
Hapa unabaini lipo tatizo la wasaidizi wake kufanya copy na paste na hakuna anayeumizwa kichwa kusoma na kuandika. Lakini kosa la pili ni BOT na Hazina kushindwa kujua makosa haya Katika data wanazotoa. Tatu ni ukimya wa Waziri wa fedha may be nayeye ajipi muda wakusoma au kuzidua hotuba za mkubwa wake.
 
Mbona unalialia kada?

Anaona aibu kwa haya yanayotokea. Ila kwakuwa ww unajivunia kundi kubwa la wajinga kwako unaona sawa tu. Lete ule utetezi wa Zito tena maana ndio dalali wenu.
 
Kosa la uandishi lililopelekea kosa la matamshi lililotokea kwenye hotuba za Mhe Rais kuhusu akiba ya Taifa limekuwa likifanyika Katika hotuba za nyuma. Hotuba yake ya Juni alisema Tena USD Bilioni 4000+ na siyo Usd Milion 4000+, Juzi Bilioni 6000+ na siyo Milioni. Ukisoma vyombo vya habari yakiwemo magazeti huko nyuma na hata hii ya Sasa wameripoti Bilioni siyo Milioni.

Hapa unabaini lipo tatizo la wasaidizi wake kufanya copy na paste na hakuna anayeumizwa kichwa kusoma na kuandika. Lakini kosa la pili ni BOT na Hazina kushindwa kujua makosa haya Katika data wanazotoa. Tatu ni ukimya wa Waziri wa fedha may be nayeye ajipi muda wakusoma au kuzidua hotuba za mkubwa wake.

Nadhani upo umuhimu wakuondoa ndugu na makada ofisini nakuweka watendaji ambao Wana Moyo wakumsaidia Mhe. Rais. Watumishi wa umma awasomi Wala kufanya proof reading . Haya makosa yamekuwa yakijirudia hata kwenye teuzi unaona anateuliwa mtu Hadi watu wa nje wapige kelele ndipo unagundua ipo shida mahali.

Tunatakiwa kusuka upya hizi ofisi nyeti

Wao akili yao iko kwenye kuiba kura tu, wakishaingia madarakani wanafanya watakavyo, na ukihoji unapewa kesi ya uhujumu uchumi. Huo udhaifu upo kote serekalini na sio ikulu tu.
 
Back
Top Bottom