Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Fuatilia Mjadala wa Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2023/24, leo Juni 15, 2023 itakayosomwa Bungeni na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba.



Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mwaka 2022, thamani halisi ya Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 lilifikia Tsh. Trilioni 141.9 ikilinganishwa na Tsh. Trilioni 135.5 mwaka 2021.

Amesema pia kiwango halisi cha ukuaji wa pato la Taifa kilifikia 4.7% Mwaka 2022 ikilinganishwa na 4.9% Mwaka 2021, wakati huohuo Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji kwa mwaka 2022 ni; sanaa na burudani (19.0%), madini (10.9%), fedha na bima (9.2%), malazi na huduma ya chakula (9%), na umeme (7.6%).

Aidha, thamani ya Pato ghafi la Taifa linatarajiwa kufikia dola za Marekani Bilioni 85.42 mwaka 2023/24.

===

UWASILISHWAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24


Bajeti hii inawasilishwa kwa mujibu wa Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na Kifungu cha 23(3) cha Sheria ya Bajeti, Sura 439 pamoja na Kifungu cha 124(4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari 2023.

Makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 yameandaliwa kwa kuzingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwemo: Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 - 2025/26) ambao umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020; Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki 2050; Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063; Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2022 - 2027; makubaliano mengine ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia; na hotuba mbalimbali za Mheshimiwa Rais.

Uchumi wa Tanzania unatarajwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.4 kwa Mwaka 2023 kutoka Dola Bilioni 69.9 kwa Mwaka 2021.

Tanzania imepanda hadi nafasi ya 6 kiuchumi kwa nchi zinazopatikana kusini mwa jangwa la Sahara. Nchi ambazo zipo chini ya Tanzania ni Ghana, Ivory Coast, DRC na uganda.

Kampuni ya Moody’s Investors Service imeipa Tanzania daraja la B2 POSITIVE na Kampuni ya Fitch Ratings daraja la B POSITIVE, ambayo yanaashiria taswira chanya kwa nchi kimataifa. Matokeo hayo ni bora kuliko nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Pamoja na mambo mengine, matokeo hayo yamechangiwa na mwenendo mzuri wa ukuaji wa uchumi, usimamizi makini wa deni la Taifa, kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa sekta binafsi, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa pamoja na kuleta maridhiano ya kisiasa ndani ya nchi.

Kukamilika kwa zoezi hilo, kutaiwezesha nchi kutambulika katika masoko ya fedha ya kimataifa na hivyo, kuongeza sifa za kuvutia uwekezaji na kupanua wigo wa upatikanaji wa fedha kwa miradi ya Serikali na sekta binafsi.

Sekta ya Kilimo
Serikali itaendelea kuongeza bajeti ili kuongeza tija kwenye sekta hii, kuongeza pato la taifa pamoja na kuinua uchumi wa wakulima.

Kwa mwaka wa fedha 2021/22 bajeti ilikuwa bilioni 294, mwaka 2022/23 ilikuwa bilioni 954 na sasa inaweza kufikia bilioni 970.

Katika kumarisha sekta ya kilimo, Serikali itaendelea kuongeza fedha kwenye sekta hiyo kadiri ufanisi utakavyoongezeka, hatua hi inaweza kuongeza fedha zaidi kwenye ya miradi ya Kilimo na kufika Tsh. Trilioni 1.27 katika Mwaka wa Fedha, tunataka kupiga vita kwa vitendo.

Sekta ya Elimu
Waziri wa fedha amependekeza kuondolewa kwa ada kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha 4 na kupangiwa na Serikali shule za ufundi za DIT, MUST na ATC ili kuongeza ujuzi na wataalam kwenye kipindi hili cha mpinduzi makubwa ya Teknolojia.




Aidha, Serikali imeendelea kutenga Fedha kwa ajili ya kugharamia Programu ya Elimu msingi na Sekondari Bila Ada ambapo hadi Aprili 2023 jumla ya Tsh. bilioni 661.9 zimetolewa.

Kuanzisha program ya kutoa mkopo kwa wanafunzi wa vyuo vya Kati kwenye kozi zenye uhitaji maalum hasa Sayansi, Afya, Ufundi na Ualimu ili kuanza na Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa masomo kwa mwaka 2023/24

Kufuatia mabadiliko ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014, toleo la Mwaka 2023 na mabadiliko ya mitaala yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sira chini ya uongozi shupavu wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Tanzania, ambapo Serikali inalenga kutoa elimu ya amali kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali, elimu ambayo itamuwezesha Kojana wa kitanzania kujiajiri au kuajiriwa na hivyo kutoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa

Hivyo, napendekeza kuanzisha programu ya mikopo kwa Wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye Vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu, hatua hii itaanza na Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2023/24, MAMA yuko Kazini.

Kwa upendo wa MAMA yetu hakuishia kwenye mikopo ya Wanafunzi tu, pia aliamua kuongeza kiwango cha posho ya kujikimu maarufu kama Boom kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka shilingi 8,500 hadi shilingi 10,000 kwa siku.

Mafanikio mengine ni pamoja na kujengwa kwa vyumba vipya 27,235 vya madarasa ya msingi na sekondari ikijumuisha madarasa 15,000 ya UVIKO-19, madarasa hayo pia yanajumuisha madarasa 8,000 ya Sekondari yaliyojengwa kwa shilingi bilioni 160 iliyotolewa kupitia Pochi la MAMA ili kukabiliana na ongezeko la Wanafunzi wa kidato cha kwanza

Sekta ya Afya, Utalii na Kero za Muungano
Serikali itaendelea kununua na Kusambaza Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi kwa vituo vyote vya Umma vya Huduma za Afya, ambapo jumla ya Tsh. Bilioni 544.2 pamoja na Tsh. Bilioni 487.5 zimetolewa kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ambapo nia ya Serikali ni kuona huduma za Afya zinaimarika.

Hivyo katika Mwaka wa fedha 2023/24 Serikali itaendelea kutenga Fedha kwa ajili ya kuboresha Huduma za Afya ikiwemo kuipatia mtaji MSD ili ifanye kazi kama Bohari ya Dawa na sio kitengo cha ununuzi wa Dawa Serikalini

Kupitia Royal Tour aliyofanya Rais Samia, idadi ya watalii wanaokuja nchini iliongezeka sana hadi kufikia 1,154,920 kwa mwaka 2022.

Hoja 4 zinazohusisha muungano zimepatiwa ufumbuzi kwenye mwaka wa fedha unaoisha.

Sekta ya Madini
Kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya kusafishia dhahabu, Serikali itaendelea kuweka vivutio kwa viwanda hivyo ili vipate malighafi ya kutosha na ili kukamilisha hilo Serikali imepunguza mrahaba wa madini yanayouzwa kwenye viwanda hivyo kutoka 6% hadi 4%”


Nafurahi kulijulisha Bunge kuwa Serikali Serikali imekamilisha taratibu za kununua Dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu hapa nchini (Gold Reserve)

Tunataka tunapotaja akiba ta fedha za kigeni tutaje na akiba ya dhahabu tuliyonayo, hatua hii itawapatia Wachimbaji bei nzuri na kuimarisha sarafu ya Nchi yetu, hii ni baada ya kupokea maelekezo ya Mh.Dkt. Samia na michango ya Waheshimiwa Wabunge.

BAJETI YA FEDHA KWA MWAKA 2023/24
Mikakati ya kuongeza mapato ni kuboresha ukusanyaji wa mapato, kusimamia matymizi sahihi ya EFD, kuangalia misamaha ya kodi isiyo na tija, kuendelea kutekeleza mikakati ya miradi ya maendeleo kwa fedha mbadala na mengine.

Walipa Kodi waliopo Nchini, 1,641,173 ni TIN za Biashara na katika kipindi hicho takriban Tsh. Trilioni 16.75 (80%) ya mapato ya TRA yalilipwa na idadi ndogo ya walipa kodi ambao ni takriban 20% tuu ya walipa kodi wote.

Zamani Bajeti yetu tulikuwa tunajitegemea kwa 40% tu, Fedha nyingine zote tulikuwa tunategemea Mataifa ya nje, sasa hivi tupo zaidi ya 70%. Tusirudi nyuma, kujitegemea kuna Heshima.

Aidha, ameagiza kila Mtanzania mwenye sifa za kulipa kodi, awajibike kwa kulipa kodi halali kwa mujibu wa Sheria na kuhakikisha Risiti za mashine za EFD zinatumika kwa yeyote anayeuza na kununua bidhaa

Pia, kuna mwamko mdogo wa watu kulipa kodi hivyo kufanya mzigo wa kodi kuwa mkubwa kwa walipakodi waliosajiliwa.

Aidha, changamoto za kutokudai risiti, kuzungusha watu wanaonunua au kutoa huduma bila kudai risiti rasmi zinazotambuliwa hupunguza mapato. Wanaouza watoe risiti na wanaonunua wadai risiti.

Kumezuka dhana ya kuona kuwa kodi zinazotozwa ni kubwa bila kujali mzigo mkubwa wa Serikali kwa nchi yetu katika kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za jamii, kuna baadhi ya Wanasiasa wanasema kodi hizi ni za Samia, kodi hizi za Mwigulu, kodi hizi za TRA.

Kodi zote zinazokusanywa huwekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali uliopo Benki kuu ya Tanzania, na baadae kupelekwa kwenye Wizara za Kisekta, fedha hizo ndizo zinazotumika kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo mijini na vijijini ikiwemo miradi ya umeme, maji, barabara, madaraja, vivuko, reli, usafiri wa anga, madarasa, zahanati, ununuzi na usambazaji wa dawa na malipo ya mishahara ya Watumishi kama Walimu, Wauguzi na Madaktari.

Kila mmoja wetu ajue kuwa, Kodi sio jambo la Rais, kodi sio jambo la Waziri wa Fedha, kodi sio jambo la TRA, kodi ni jambo la Nchi, kodi ndio maendeleo ya Nchi yetu, kila Mtanzania mwenye sifa za kulipa kodi ana wajibu wa kulipa kodi stahiki na halali kwa mujibu wa sheria, ni lazima kulipa kodi, ni lazima tutumie mashine za EFD bila udhuru wowote, ni lazima kila anayeuza atoe risiti na anayenunua adai risiti.

MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA, TOZO NA HATUA NYINGINE ZA MAPATO
Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura 148 kama ifuatavyo:
  1. Kuongeza kima cha usajili kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani kinachotakiwa kwa mfanyabiashara kusajiliwa kutoka shilingi milioni 100 hadi shilingi milioni 200. Serikali itaendelea kuongeza kima husika hadi kufikia shilingi milioni 500 ili kuepusha athari za kimapato zinazoweza kujitokeza.
  2. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye malighafi za kutengeneza viuatilifu vya mimea (insecticides) na vya mifugo (acaricides) zinazotambulika kwa HS Code 2916.32.00 (Benzalkonium Chloride) na HS Code 2916.32.00 (Glutaraldehyde).
  3. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye hema za chuma (prefabricated structures) zinazotambulika kwa HS Code 9406.20.90 zitakazoagizwa na kutumiwa na wafugaji wa kuku.
  4. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye uuzaji na ukodishaji wa ndege, injini za ndege na vifaa vyake vinavyouzwa nchini.
  5. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye madini ya thamani, madini ya vito na madini mengine ya thamani yanayouzwa katika masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini vilivyoanzishwa na Tume ya Madini au vituo vya kusafishia dhahabu (refineries) vilivyopo nchini.
  6. Kuruhusu ahirisho la kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT Deferment) kwa bidhaa za mtaji zinazozalishwa ndani ya nchi. Aidha, utaratibu wa ahirisho la ulipaji wa kodi husika kwa bidhaa za mtaji zinazotoka nje ya nchi utasitishwa baada ya miaka mitatu (3).
  7. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye malighafi za kutengeneza vifungashio vya madawa zinazotambulika kwa heading 3902 (Polypropylene USP - Medical Grade); na heading 3907 (Polyethylene Terephthalate USP).
  8. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye moulds zinazotumika kutengeneza madawa ya binadamu.
  9. Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia 0 kwenye bidhaa za nguo zinazotengenezwa kwa kutumia pamba inayolimwa nchini kwa kipindi cha mwaka 1.
  10. Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia 0 kwenye mbolea inayozalishwa ndani ya nchi kwa kipindi cha mwaka 1.
  11. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye nyumba zinazouzwa na wajenzi wa nyumba za kibiashara zenye gharama nafuu isiyozidi shilingi milioni 50.
  12. Kufanya marekebisho kwenye Kipengele cha 20 cha Sehemu ya Kwanza ya Jedwali la Msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kuhusisha gaming odds na gaming software kwenye wigo wa bidhaa zinazopata msamaha wa kodi.
  13. Kufanya marekebisho kwenye Jedwali la Misamaha la Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura 148 ili kuakisi mawanda ya bidhaa zilizosamehewa pamoja nakuoanisha H.S Codes zilizomo kwenye kitabu cha Viwango vya Pamoja vya Ushuru cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community Common External Tariff) cha mwaka 2017 na zile zilizomo kwenye kitabu cha mwaka 2022 kama ilivyoainishwa kwenye Kiambatisho Namba 8;
  14. Serikali itaendelea kutoa misamaha ya kodi inayotolewa sasa kwenye Sekta za uzalishaji kama vile kilimo, mifugo na uvuvi.
Hatua zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 71,262.4.

Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332

Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura 332 kama ifuatavyo:
  1. Kusamehe Kodi ya Mapato kwenye mapato yanayotokana na uwekezaji unaofanywa na Mfuko wa Kitaifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye amana (fixed deposit), hati fungani za muda mfupi (treasury bonds and treasury bills) pamoja na gawio linalotokana na hisa.
  2. Kurekebisha kifungu cha 56 cha Sheria ya Kodi ya Mapato SURA 332 ili miamala ya utoaji wa hisa mpya na uhamishaji wa miliki ya kampuni unaofanyika ndani ya nchi isitozwe Kodi ya Mapato.
  3. Kurekebisha kifungu cha 82 cha Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 ili kuondoa takwa la kutoza Kodi ya Zuio kwenye pango kwa wapangaji wa nyumba binafsi wasiofanya biashara.
  4. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwenye ubadilishaji wa muundo wa ndani wa Kampuni (internal restructuring) unaofanywa kwa kuzingatia matakwa ya Mikataba ya Msingi iliyosainiwa baina ya Serikali na wawekezaji kwa lengo la kutekeleza miradi ya ubia ya uchimbaji wa madini baina ya Serikali na wawekezaji.
  5. Kupunguza Kodi ya Ongezeko la Mtaji (Capital Gain Tax) kutoka asilimia 10 kwenye faida hadi Kodi ya Mapato ya asilimia 3 ya thamani ya mauzo au thamani ya ardhi iliyothaminishwa, (thamani yoyote kubwa kati ya hizo) bila kujali gharama zilizowekezwa katika maeneo husika (investment costs) kwa walipakodi wasiotunza kumbukumbu za manunuzi au uendelezaji wa mali husika.
  6. Kurekebisha Kifungu cha 65T cha Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332, kwa kuweka utaratibu wa kukadiria kodi ya mapato kwa
    wasafirishaji wa abiria na mizigo kwa kutumia viwango elekezi vya kodi kwa kila gari. Utaratibu huu utahusisha walipakodi binafsi (Individuals) pekee ambao hawana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha ritani za kodi.
  7. Kutoza Kodi ya Mapato kwa kiwango cha asilimia 2 kwenye malipo ya wachimbaji wadogo wa madini (Artisanal and Small- Scale Miners).
  8. Kutoza Kodi ya Mapato kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye malipo yatokanayo na uuzaji wa hewa ukaa (Verified Emmission Reduction).
  9. Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania itasimamia utolewaji wa vyeti vya msamaha wa kodi kwa taasisi za huduma ya jamii kama vile taasisi za dini na kupitia mifumo ya kielektoniki ambapo sasa ndani ya siku 14 vyeti hivyo vitakuwa vinapatikana.

Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 51,960.1

Ili kuiwezesha nchi kuwa na sera za kodi zinazotabirika na kuweka mazingira bora ya uwekezaji napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147, kwa kuanzisha utaratibu wa kurekebisha viwango vya Ushuru wa Bidhaa kila baada ya miaka mitatu (3) kuanzia mwaka wa fedha 2023/24.


Aidha, napendekeza pia kufanya marekebisho kwa bidhaa nyingine kama ifuatavyo:
  1. Kusamehe Ushuru wa Bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa injini (engine capacity) kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme pekee yanayotambulika kwa HS Code 8702.40.11; 8702.40.19;
    8703.80.10; na 8703.80.90 pamoja na magari yanayotumia Nishati ya Gesi Asilia (CNG) pekee.
  2. Kupunguza Ushuru wa Bidhaa kutoka shilingi 4,386 kwa lita hadi shilingi 2,466.45 kwa lita kwenye vinywaji vikali (Ready to Drink) vinavyozalishwa nchini.
  3. Kutoza Ushuru wa Bidhaa kwa kiwango cha Shilingi 20 kwa kila kilo moja ya Saruji inayotoka nje ya nchi na inayozalishwa ndani ya nchi.
  4. Kutoza Ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye magari yenye uwezo wa injini (Engine Capacity) wa kati ya 1000cc hadi 2000cc yaliyotokana na ukuaji wa teknolojia ili kuwianisha na magari mengine yenye ukubwa unaofanana yanayotozwa ushuru huo.
  5. Kutoza Ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye magari yenye uwezo wa injini (Engine Capacity) wa zaidi ya 2000cc yaliyotokana na ukuaji wa teknolojia ili kuwianisha na magari mengine yenye ukubwa unaofanana yanayotozwa ushuru huo.
  6. Kutoza Ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye magari ya abiria yanayoingizwa nchini yanayozidi umri wa miaka mitano (magari chakavu) yaliyotokana na ukuaji wa teknolojia ili kuwianisha na magari mengine yanayofanana yanayotozwa ushuru huo.
  7. Kutoza Ushuru wa Bidhaa kwa kiwango cha asilimia 30 kwenye sigara na bidhaa za aina hiyo zinazotumia mbadala wa tumbaku zinazotambulika kwa Hs code 2402.90.00; tumbaku inayovutwa kwa kutumia bomba la maji inayotambulika kwa Hs code 2403.11.00; na sigara za kielektroniki, shisha na bidhaa za aina hiyo zinazotambulika kwa Hs codes 8543.40.10, 8543.40.90 na 9614.00.00.
  8. Kutoza Ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 20 kwenye mashine za Kamari zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na zinazozalishwa nchini.
  9. Kuongeza Ushuru wa bidhaa kutoka shilingi 589.05 kwa lita hadi shilingi 600 kwa lita kwenye vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy Drink) zinazoingizwa kutoka nje ya nchi.
  10. Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147 ili kuoanisha H.S Codes zilizomo kwenye kitabu cha Viwango vya Pamoja vya Ushuru cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community Common External Tariff) cha mwaka 2017 na zile zilizomo kwenye kitabu cha mwaka 2022 kama ilivyobainishwa kwenye Kiambatisho Namba 9.

Hatua hizi za Ushuru wa Bidhaa kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 448,989.9

SURA YA BAJETI KWA MWAKA 2023/24
Sura ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24 inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni 44.39 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika. Jumla ya mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 31.38, sawa na asilimia 70.7 ya bajeti yote.

Kati ya mapato hayo, mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 26.73 na mapato yasiyo ya kodi (Wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa) yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 4.66.
Misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 5.47. Aidha, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 5.44 kutoka soko la ndani ambapo shilingi trilioni 3.54 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na kiasi cha shilingi trilioni 1.90 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Vilevile, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 2.10 kutoka soko la nje kwa masharti ya kibiashara kwa lengo la kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Katika mwaka wa fedha 2023/24, katika mwakawa fedha 2023/24, Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 44.39 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.

Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 30.31 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha: shilingi trilioni 12.77 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama nyingine za Mfuko Mkuu; shilingi trilioni 10.88 kwa ajili ya mishahara ikiwemo nyongeza ya mshahara, upandishaji wa madaraja na ajira mpya; na shilingi trilioni 1.14 ni ruzuku ya maendeleo kwa ajili ya kugharamia elimumsingi na sekondari bila ada pamoja na mikopo ya wanafunzi elimu ya juu; shilingi trilioni 5.52 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC).

Aidha, matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 14.08. Kiasi hicho kinajumuisha gharama za utekelezaji wa miradi mbalimbali katika ngazi ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 30.31 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha: shilingi trilioni 12.77 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama nyingine za Mfuko Mkuu; shilingi trilioni 10.88 kwa ajili ya mishahara ikiwemo nyongeza ya mshahara, upandishaji wa madaraja na ajira mpya; na shilingi trilioni 1.14 ni ruzuku ya maendeleo kwa ajili ya kugharamia elimu msingi na sekondari bila ada pamoja na mikopo ya wanafunzi elimu ya juu; shilingi trilioni 5.52 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC).

Aidha, matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 14.08. Kiasi hicho kinajumuisha gharama za utekelezaji wa miradi mbalimbali katika ngazi ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 

Attachments

  • HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKIWASILISHA TAARIFA YA HALI YA UCHUMI KATIKA MWAKA 2022 ...pdf
    2.5 MB · Views: 20
Tupeane hapa Updates zote kutoka kwenye Bajeti Kuu ya Serikali Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 inayosomwa leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma

Pia Soma

UPDATE:
TAARIFA YA HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2022




UPDATE :

MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2023/24









 

Attachments

  • HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2022.. (5) (1).pdf
    18 MB · Views: 2
  • HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKIWASILISHA TAARIFA YA HALI YA UCHUMI KATIKA MWAKA 2022 ...pdf
    2.5 MB · Views: 6
Bajeti kusomwa na waziri wa fedha kwa mara ya kwanza imegeuka kua kichekesho. Waziri kwa uchawa anamtaja na kumtukuza rais kila sentensi hadi inakera.
Huyu jamaa mwigulu nchemba hakika ni master wa unafiki kujikomba na kujipendekeza. Watu tunategemea bajeti imetayarishwa na wataatam sio kumshukuru mama kila kitu hadi kulisha familia zetu. Inatia kinyaa. Ndio maana pamoja na kua ni mzigo tu kama waziri wa fedha amefanikiwa kubakia. Kwa kweli ni hodari sana kwa uchawa. Nampongeza.👏
 
Bajeti kusomwa na waziri wa fedha kwa mara ya kwanza imegeuka kua kichekesho. Waziri kwa uchawa anamtaja na kumtukuza rais kila sentensi hadi inakera.
Huyu jamaa mwigulu nchemba hakika ni master wa unafiki kujikomba na kujipendekeza. Watu tunategemea bajeti imetayarishwa na wataatam sio kumshukuru mama kila kitu hadi kulisha familia zetu. Inatia kinyaa. Ndio maana pamoja na kua ni mzigo tu kama waxiri wa fedhaa amefanikiwa kubakia. Kwa kweli ni hodari sana kwa uchawa. Nampongeza.
Bajeti ingefaa sana Kama ingeondoa tozo za mwigulu. Vinginevyo hamna jipya
 
Bajeti kusomwa na waziri wa fedha kwa mara ya kwanza imegeuka kua kichekesho. Waziri kwa uchawa anamtaja na kumtukuza rais kila sentensi hadi inakera.
Huyu jamaa mwigulu nchemba hakika ni master wa unafiki kujikomba na kujipendekeza. Watu tunategemea bajeti imetayarishwa na wataatam sio kumshukuru mama kila kitu hadi kulisha familia zetu. Inatia kinyaa. Ndio maana pamoja na kua ni mzigo tu kama waxiri wa fedhaa amefanikiwa kubakia. Kwa kweli ni hodari sana kwa uchawa. Nampongeza.
yaan hadi inakeraaa kwa kweli.
 
Back
Top Bottom