Nimepigwa na butwaa

Nimepigwa na butwaa

Wasalam wakuu.

Katika hali ya kushtukiza na kuchanganya leo hii nimekuta application ya jf kwa simu ya mama..

I don't know ni nani kamwekea hii application au imekuaje kuaje.

Nimeshindwa hata kuifungua ila nime unstaill aiseee....

Yaani imekuaje kuaje wakuu..
Humu ndani humu umakini unatakiwa wa kutosha aiseee

Bado najiuliza kama anatumia jf au laah..
Nimepigwa na butwaa...

Wakuu mjiheshimu kuna watu mna assume ni mtu flani.. nimesema sijajua kama kajiunga au laa
Mama yako sindiyo huyu mshangazi hapa jf au ujui ...hua anasema analitoto zero brain linawaza mademu 24hours
 
Mama mzazi mkuu...
Leo nipo hapa namsindikiza akasema kuna movies flan hv anahitaji nimrushie ndo nipo natoa kwa hard disk nahamisha nikaona storage kama inazingua nikawa. Nachek app za kufuta ndo nakutana na mzigo wa jf umetulia front page aiseee
Amesoma hadi ile ya kula tunda kimasihara. Anakuzoom tu 😅😅😅
 
Ndiyo maana binafsi tangu nimeanza kuitumia JF tangu ikiitwa Jambo Forum, sijawahi kuifungua mbele za watu achilia mbali ku-download App yake

Kuna Siku nilikuwa nasafiri kwa basi kutoka Dodoma kuja DSM kabla ya SGR, kutokana na addiction ya kutumia JF nikajikuta nime-Login.

Nilikuwa nimekaa na binti fulani around 27-32 hivi, Baada ya kuona yupo busy kutaka kujua ID niliyokuwa naitumia ikabidi haraka ni-Logout

Hachelewi kuja kusema humu amekutana na Mzee Grahams bure, na hivi ninavyotumia mkongojo kutembea 😜
Mimi siamini kama wewe ni mzee kiasi hicho, najua unatupanga tu
 
we hufai unaludisha nyuma juhudi za kuipaisha jf kimataifa kwanini umeiunstall sasa ? taila kweli wewe.jamiiforums ni kwa kila mtu
 
Usikute ulikaa na Binti Sayunii ungekoma kwa nyuzi,
Hahaha...........Kwa kweli ningekoma iwapo angejua ID yangu😅

Nilishangaa kuona anauliza kama nimewahi kuingia na kusoma nyuzi za Chit chat

Nikamwambia Mimi na Uzee huu, utanikuta jukwa la Kilimo na biashara tu 🤗
 
ID mbili muhimu mkuu kuna muda inabidi tu iwe hivyo sio kwa nia mbaya.
Hahaha..............ila Kuna watu wanaweza kumiliki ID mbili, Mimi hii moja pekee huwa Kuna muda nasahau nywila (password) 🙌

Labda kutokana na zee nilionao 😜
 
Back
Top Bottom