Hoja ya kuficha idadi vifo tuzipuuze, tuiaminie Serikali yetu. Idadi ya 16 waliokufa kwa Corona ni idadi ya ukweli na halisi, ila...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Kila nipatapo nafasi, huja na hoja za " Kwa Maslahi ya Taifa" zenye lengo la kuhamasisha uzalendo kwa nchi yetu, Mada ya leo, naizungumzia idadi ya kweli ya waliokufa kwa Corona Tanzania mpaka hapa ninapo andika bandiko hili, Tanzania wamekufa watu 16 tuu kwa ugonjwa wa Corona!, Kubali, Kataa, lakini huo ndio ukweli mpaka pale itakapo tangazwa tena update nyingine ambayo itatolewa leo na hoja kuu ya bandiko la leo hizi hoja na tuhuma za kuwa serikali yetu inaficha idadi halisi ya vifo vya watu wanakufa kwa Corona, wanaokufa ni wengi, lakini idadi inayotangazwa na serikali ni idadi ndogo, hivyo taarifa ya serikali ni taarifa ya uongo, idadi inayotangazwa na serikali ni idadi ya uongo!, jee rais wa JMT ni muongo?!, jee Waziri Mkuu wa JMT ni muongo?!, Jee Waziri wa Afya ni muongo?, Jee wataalamu waliochunguza na kutoa taarifa hiyo ni waongo?. Jibu ni hapana, data za idadi ya vifo inayotokewa na serikali ni data za ukweli.

Natoa wito nawaomba Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo wa ukweli wa nchi yetu, tuiaminie taarifa ya serikali yetu, kuwa idadi vifo 16 iliyotolewa na serikali kuwa ndio pekee waliokufa kwa Corona mpaka sasa nchini Tanzania, ni idadi ya ukweli wenyewe kabisa na halisi, ambayo ndio ya watu waliopimwa na kuthibitishwa wamekufa kwa ugonjwa wa Corona, ila pia kuna watu wengine wengi tuu na wanakufa kwa magonjwa mengine, na inawezekana miongoni mwa hao wanaokufa kwa magonjwa mengine ikiwemo haya ya matatizo ya kupumua, pia Corona imechangia, ila hawaja pimwa na kutthibitishwa kuwa ni Corona, hivyo mpaka sasa ninapoandika bandiko hili asubuhi hii, idadi rasmi ya vifo vilivyotokana na Corona na kuthibitishwa na serikali yetu ni watu 16 tuu na huu ndio ukweli wenyewe halisi, kubali, kataa, ndio ukweli.
naomba uandamane nami.
Utambulisho
Leo naomba nianze na utambulisho wangu, mimi ni nani, na nina authority gani kuasema haya ninayo yaandika, japo wengi mnanitambua humu jf kuwa mimi Pasco Mayalla ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea, na huu ni mwaka wa 30 ndani ya tasnia, na sio wengi humu wanaojua kuwa kabla sijajiunga na tasnia ya habari na kuajiriwa na Radio Tanzania ya enzi zile, nilipomaliza kitato cha 6, nilipitia JKT kwa mujibu wa sheria, kisha from JKT, niliunganisha straight kujiunga na JWTZ, hivyo pia mimi ni mwanajeshi!, hivyo kufuatia kila siku jf wanajiunga wanachama wapya ambao hatufahamiani, wengine ni vitoto umri wa watoto wetu, mkitofautiana hoja, vinatukana, hivyo kujitambulisha hivi from time to time kunasaidia kujenga kidogo heshima, maana vitoto vingine vinatukana vikijua vinabishana na vitoto vyenzao!.

Nguzo Kuu ya Tasnia ya Habari ni Ukweli, Truth!, Kuandika Ukweli, Kutangaza Ukweli, Ni Ukweli Tuu Pekee!.
Kla fani ina nguzo. yake kuu, fani ya jeshi ni utii na nidhamu, fani ya udakitari, uuguzi ni kuoakoa maisha, save lives, fani ya sheria ni utoaji haki, justice, fani ya ualimu ni kuelimisha, biashara is making money, serikali ni kutawala, to rule, Bunge ni kutunga sheria, Mahakama ni kutoa haki, etc, kwenye fani yangu ya habari, nguzo yetu kuu ni ukweli, truth, sisi tulipojiunga na fani hii enzi hizo, inafundishwa kwa kizungu tuu, sijui siku hizi, na baadhi ya waalimu wetu walikuwa wazungu, (enzi hizo vyuo vya uandishi wa habari nchini Tanzania vilikuwa viwili tuu, TSJ na Nyagezi, darasa letu lilikuwa 25 tuu na chuo kizima tulikwa 50, na kati ya hao, 50% tuliishia kuoana baada ya masomo!), hivyo waalimu wetu wazungu walitufundisha "tell nothing but the truth", seek the truth and the truth will set you free, hivyo ni wajibu wa Media, kuutafuta ukweli, na kuusema ukweli, hivyo kwenye hili janga la Corona, maadam idadi ya vifo mpaka sasa iliyotangazwa na serikali ni vifo vya watu 16 tuu, sisi kama media, jee tunapaswa kuishia hapo kuipokea tuu taarifa ya serikali kuwa vifo ni 16 tuu, na kuitangaza tuu kama kasuku, au media tunatakiwa kwenda mbali zaidi na kujiridhisha kwa kuupata ukweli halisi ya waliokufa kwa Corona, na kuutangaza?. Hao 16 ni wa umri gani, jinsia gani, wamefia wapi na walikufa lini?. Mfano najua leo serikali itatoa tena update kwenye blanket statement, wameongezeka vifo kadhaa, bila kutoa details zozote, jee huu ndio ukweli halisi au idadi inayotangazwa na serikali ni idadi ya serikali lakini idadi vifo halisi ni nyingine?.

Jee Ukweli ni Lazima Uwe Ukweli Mmoja?. Aina Mbili za Ukweli, Kuna Ukweli Wako na Ukweli Halisi Ambao Ndio Ukweli Wenyewe!.
Japo ukweli wenyewe halisi huwa ni ukweli mmoja tuu, lakini pia tukubali tukatae, kuna aina mbili za ukweli, kuna ukweli kuna ukweli wako, na kuna ukweli halisi wenyewe!. Kwenye janga hili la Corona, Ukweli wako, yaani ukweli wa serikali ni ukweli wetu wa idadi inayotangazwa mfano hii idadi ya vifo 16 mpaka leo, ni idadi ya ukweli wa serikali, halafu ukweli halisi, ni idadi ya ukweli kabisa ya vifo vyote vilivyotokea kiukweli ukweli na kusababishwa na Corona!.
Swali libaki Jee kwenye janga hili la Corona, ukweli unaotangazwa na serikali ni ukweli upi, ni ukweli wa serikali au ukweli wenyewe halisi?, Jee sisi Vyombo vya habari, wakiwemo wana wanasiasa na watu wengine wote wenye access to information ya ukweli wenyewe halisi, tunao wajibu gani?, wa wautangaze ukweli upi?. Tutangaza ukweli wa serikali wa vifo 16 au tutangaze idadi ya ukweli halisi ya vifo vyote na kila anayekufa, tumtangaze conclusive kuwa ni Corona, hivyo serikali yetu ionekane imesema uongo?, rais wa JMT aonekane muongo!, Waziri Mkuu aonekane Muongo?, Waziri wa Afya aonekane Muongo!, Wataalamu wetu wa Afya wanaokesha usiku na mchana na ndioa wanaotoa data, waonekane wango!, wanapika data!, jee huu huu ni uzalendo?. Ukweli upi usemwe, Ukweli wa serikali wa vifo 16 tuu au ukweli halisi wa watu zaidi ya 16 waliokufa mpaka sasa?.

Ukweli wa Serikali Vs Ukweli Halisi!, Upi ni Ukweli wa Kutangazwa na Kuaminiwa?
Kabla ya ujio wa janga la Corona, watu walikuwa wanakufa kwa maradhi mbalimbali, wengine wakifia majumbani, wengine wakifia njiani kukimbizwa mahospitalini, na wengine wakifia mahospitalini kwa maradhi mbalimbali kila siku, lakini hatuna utaratibu wa kutangaza idadi ya watu wanaikufa kila siku kila mahali na sababu za vifo vyao, lakini kutokana na kuibuka kwa janga la Corona, ambalo nalo linaua, hivyo automatically idadi ya vifo itaongezeka, lakini kuongeze huku hakumaanishi sasa baada ya kuja kwa Corona, vile vifo vingine vyote vilivyokuwa vinatokea kila siku kabla ya Corona, sasa vimesimama, hivyo sasa kila anayekufa ni Corona tuu!. No, kweli Corona inaua, na idadi ya vifo inaongezeka, lakini sio kila anayekufa ni Corona!. Swali linakuja, kama Tangu kuibuka kwa janga la Corona, tumeshuhudia kupitia mitandao ya kijamii miili ya watu wengi wakizikwa na serikali, wengine wakizikwa usiku usiku, kwanini idadi rasmi ya kiserikali bado ni 16 tuu huku tukishuhudia idadi halisi ya miili ni mingi zaidi ya hiyo 16 ya serikali?. Jee serikali inasema kweli?, jee serikali inaficha kitu?, jee ukweli halisi ni vifo vingi zaidi ya hivyo 16 vinavyotangazwa na serikali?. Jee hii idadi ya vifo 16 vya serikali ni idadi ya ukweli halisi au ni ukweli tuu wa serikali, lakini idadi halisi ni kubwa zaidi?. Jee wananchi waiamini idadi ya serikali ya vifo 16, au idadi ya mitandaoni inayotolewa na wanasiasa?.

Watanzania Sio Watoto Wadogo, Serikali Iseme Ukweli Kwanini Idadi Yake ni Watu 16 Tuu, Wakati Wanaozikwa ni Wengi?.
Ngoma iko hapa!, Tangu kutokea janga la Corona, kuna tatizo katika utoaji habari, both serikali haitimizi wajibu wake wa utoaji habari sahihi na fasaha kwa wakati, na tasnia ya habari, na sisi hatujatimiza wajibu wetu ipasavyo kuihabarisha jamii na kuielimisha jamii ya Watanzania kuhusu Corona, serikali inatoa taarifa hafifu ya idadi ndogo, huku sasa tunaishi kwenye dunia ya utandawazi, kila wanaofiwa na kukatazwa kuwazika wapendwa wao kwa serikali kujitolea kuwazika, wanatangaza kwenye mitandao ya kijamii hadi kupiga picha za mazishi ya miili mingi usiku usiku!. Wanasiasa wanapokea taarifa za kwenye mitandao ya kijamii, kuona ni kuamini, hivyo wanatangaza kuwa serikali haisemi kweli, kama Waziri Mkuu ametangaza idadi ya vifo 16, bila ufafanuzi wowote wa hao 16 ni jinsia gani, umri gani, vifo vimetokea lini, na wapi, kisha Waziri Mkuu kivuli akaibuka na kusema serikali inasema uongo, inaficha taarifa, waliokufa ni wengi zaidi, na kwa vile wanamchi wengi pia wana access na mitandao ya kijamii, in such scenario, wananchi wamuamini nani?, Waziri Mkuu wa JMT aliyetoa idadi ya vifo 16 butu butu bila any details, au Waziri Mkuu Kivuli akisema kinachoonekana kwenye mitandao ya kijamii, na kwa vile kuona ni kuamini, automatically taarifa za kwenye mitandao ndizo zitaaminiwa zaidi kuliko taarifa za serikali hivyo wananchi kukosa imani na serikali yao!. Swali kwenye utoaji habari za Corona, serikali ifanye nini katika kutoa taarifa za kina, na media ifanye nini ili wananchi waelezwe ukweli na kuzidi kuiaminia serikali yao inasema ukweli?.

Serikali Itoe Taarifa za Ukweli Daily na Detailed, Media Itimize Wajibu Wake wa Kuelimisha Umma Huku Wananchi Wakiruhusiwa Kuwa Huru Kuwatangaza Wapendwa Wao Waozikwa na Serikali!.
Kama nilivyoeleza pale mwanzo, sema ukweli na ukweli utakuweka huru. Serikali iseme ukweli kabisa wa idadi ya vifo vya Corona, na ukweli huu utaiweka serikali yetu huru, na sisi media tuuripoti ukweli huo wa serikali, hivyo kuwazuia wananchi kuuamini upotoshaji wa mitandaoni. Ukweli wa serikali ni taarifa ya serikali iseme wazi kuwa hiyo idadi ya watu 16 ni idadi ya wale tuu waliothibitishwa na serikali kuwa wamefariki kwa Corona, kwenye hivi vifo 16 visemwe vimetokea lini na wapi, na pia serikali iseme wazi kuwa kuna vifo vingine vinavyotokana na marandhi mbalimbali vikiwemo matatizo ya kupumua vimeongezeka, kutokana na vifo hivi vingine vyote havijapimwa na kuthibitishwa ni Corona au la, serikali iseme imeamua kujitolea kuwazika wote, hao 16 waliothibitishwa ni vifo vya Corona, na kuwazika wagonjwa wengine wote waliokufa wakati wa janga hili la Corona, kwa kuzikwa na serikali, mazishi ya kicorona corona kwasababu hao wengine wote waliokufa kwa maradhi mengine na wa matatizo ya kupumua, inaweza ni kweli corona au ni ugonjwa mwingine wowote, hivyo waliothibitishwa rasmi kufa kwa Corona ndio hao 16 tuu, lakini miili inayozikwa na serikali ni wengine wote waliokufa wakati wa janga hili iwe ni kufa kwa Corona au la, watazikwa na serikali, hivyo sasa inakuwa hiyo idadi ya vifo 16, ni idadi rasmi ya ukweli ya waliothibitishwa na serikali kufa kwa Corona, lakini idadi ya wanaozikwa ni idadi kubwa zaidi ya hao 16, hivyo kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa sio kila anayekufa ni kifo cha Corona ila kila anayezikwa ni maziko ya kikoronakorona.
Ili kuondoa mikanganyiko, taarifa itolewe daily, mfano kabla ya update ya vifo 16, update ya mwisho ni vifo 10 ilitolewa Alhamisi ya wiki ile, zikapita siku 6 hadi Jumatano iliyopita ndio ikatolewa upadate ya kuongezeka vifo 6, kwa wastani wa ongezeko la kifo kimoja tuu kwa siku, huku kwenye mitandao ya kijamii wanaonekana watu wanazikwa na serikali daily tena miili zaidi ya mmoja na wanazikwa usiku usiku!, nani ataiamini serikali yetu kuwa inasema kweli?. Kumbe tatizo hapa ni serikali tuu kutoa taarifa hafifu hawa 6 walioongezeka, walikufa lini na wapi?. Swali linabaki, kama idadi ya waliokufa na Corona ni 16 tuu, kwanini serikali izike watu wengine wote na kwa nini izike usiku usiku?.

Kama Waliokufa ni 16 Tuu, Mbona Wanaozikwa ni Wengi Zaidi na Kwanini Wanazikwa Usiku Usiku, Wanaficha Nini?
Eneo hili pia lingemalizwa na kutolewa kwa taarifa za ukweli na serikali sababu za kuzika watu usiku, sio kwa ajili ya kuficha kitu bali ni miongoni mwa procedures za disaster preparedness na sisi media tupaswa kusaidia!. Kama toka mwanzo serikali ingesema wazi kuwa kufuatia janga la Corona, idadi ya vifo hata vya magonjwa mengine na huu ugonjwa mpya wa tatizo la kupumua vimeongezeka, na kwa vile serikali haiwezi kuwapima wote kuthibitisha wamekufa na nini, lakini serikali itawazika wote, na kwa vile ni janga, kila anayekufa anazikwa ASAP, kutokana na ubize wa kushughulikia wagonjwa, muda muafaka wa kuzika ndio huo wa usiku, hivyo serikali inazika usiku sio kwasababu ya kuficha kitu, na wala sio uchawi wa makaburini usiku, bali ni timing tuu, Watanzania wangeelewa, hivyo hao wanatumia picha za mazishi ya usiku, taarifa zao zingekuwa ni no news.

Pamoja na Media Kusema Ukweli, Jee ni Lazima Kuusema Kila Ukweli?, Kuna Kweli Nyingine Unaipima Kwa Objectivity na Sio Lazima Kusema Kila Ukweli, Bali Kutanguliza Mbele Maslahi ya Taifa!.
Japo sisi media tunatakiwa kusema ukweli mtupu wakati wote, lakini sio kila ukweli ni lazima usemwe au utangazwe, kuna ukweli ukiuzikia, unauchakata kwa kipimo cha objectivity kuwa jee ukweli huu ukijulikana utalisaidia taifa?. Unapima kama ukweli huo una madhara, hata ukitangazwa badala ya kulisaidia taifa ndio kwanza utalichanganya au kuliparaganyisha.
Kipimo cha Ukweli ni Hiki.
Jamii zote duniani, na dini zote, zinafundisha watu wasifanye tendo mpaka waoe au kuolewa. Dini zote, mila zote zinataka watu wanaooana wafanye lile tendo kwa mara ya kwanza baada ya ndoa. Kwa vile kwa upande wa mwanaume hakuna alama yoyote inayowekwa mtu akianza kabla, lakini kwa wanawake wakianza tuu kabla, ile seal inaondoka!. Japo kila mwanamke alipaswa kuolewa akiwa na seal yake ili mtu wa kwanza kuifungua hiyo seal awe ni mume wake wa ndoa, katika kitendo kinachoitwa deflaration, sasa siku hizi ndoa ngapi zinafungwa unajikuta wewe you are not the first, jee umewahi kumuuliza mwenzi wako aliyeitoa seal yake ni nani?, atakutajia? . Kisha ulizia baada ya kutolewa seal, watu wangapi walipita kabla yako?. Hataambiwa, sio hataambiwa kwasababu una danganywa, lakini hautaambiwa kwasababu ukweli huo hauna maslahi kwenye ndoa yenu. Hivyo ukitokea ukweli fulani ambao haina maslahi kwa taifa, hata kama ni kweli, sio lazima usemwe. Unaweza kutembelea uzi huu ukaangalia jinsi mimi nilivyo jidai mkweli sana, halafu huo ukweli ukaja kuni cost,
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa? - JamiiForums

Hivyo hata kwenye janga hili la Corona, mfano kutokuwepo kwa daily update, inawezekana ni kwa nia njema badala ya kufanyika daily update inafanyika weekly. Kati ya Jumatatu - Ijumaa ni siku 5, kila siku wanakufa wagonjwa 3, hivyo Jumatatu unatangaza wamekufa!, J. 4 wamekufa!, J.5, wamekufa!, Alhamisi wamekufa!, Ijumaa ukionekane tuu hata kabla hujasema watazamani wanasubiri kusikia wamekufa, hivyo inakuwa ni waekufa wamekufa, wamekufa wiki nzima, jumla ni watu 15!, Huku japo ni ukweli lakini kunakuwa ni kuwaogopesha watu na kujenga hofu!. Hivyo unaamua badala ya kutoa daily update, utatoa weekly update, na kati ya hao 15 waliokufa, japo wamekufa kwa matatizo ya kupumua kama Corona, maada wameisha kufa, unawapima wa nini ili iweje?, then unaamua kutoa idadi ya vifo 6 tuu vile viivyothibitishwa ni Corona, na hao 9 unaachwa wasemwe ni matatizo ya kupumua, hivyo ile update wa weekly, itaonyesha ongezeko la vifo 6 tuu kufanya jumla ya vifo vyote Tanzania ni 16, lakini maziko mtawaziko wote, hivyo taarifa hiyo, inakuwa ja less impact, watu waendelee kuchapa kazi!.

Media Kutumia Nidhamu ya Kijeshi Kutii Mamlaka Bila Kuhoji.
Baada ya Corona kutangazwa ni janga na ikatangazwa vita, ikatatolewa list ya wazungumzaji 5. Taarifa rasmi ya serikali ikiishasema waliokufa ni watu 16, then waliokufa ni 16 tuu, hakuna kuhoji chochote na kazi ya media kwenye kuripoti update ni kuripoti tuu kilichosemwa na serikali, sio kuhoji wala kufanya uchaguzi wa kutafuta ukweli wowote zaidi ya huo ukweli wa serikali.
A Way Forward ya Nini Kifanyike
  1. Korona ni Janga, Ni Vita, Vita Ikiisha Tangazwa, Amri ni Moja, Umoja, Mshikamano, Ushirikiano Ndio Siri ya Ushindi!-Korona ni janga, ni vita, vita ikiishatangazwa, ili tushinde vita hii ni lazima viongozi wetu wa serikali, wanasiasa, wapinzani, wataalamu, wote tuzungumze kwa kauli moja, Amiri Jeshi Mkuu akiishasema waliokufa ni 16, sheria ya kivita inatumika, walikufa ni 16!, hata kama umeona na kushuhudia miili 100 inazikwa!, bado utasema ni waliokufa ni 16 tuu!. Leo Waziri Mkuu wtu katangaza idadi ya 16, halafu kesho anaibuka mtu mwingine kuleta idadi ya vifo vya mitandaoni!, what does this mean?. Tutawachanganya Watanzania!, hizi idadi za kwenye mitandao, tuachieni sisi watu wa mitandaoni, kwenye hili lazima serikali, wapinzani mzungumze kwa kauli moja kwa maslahi ya taifa!​
  2. Serikali Isijimilkishe Vita Hii ya Corona Kuifanya ni Vita Yake!, Vita Hii ni ya Watanzania Wote- Serikali Ifanye Ushirikishwaji!- Tangu janga hili limeanza, serikali ndio imehodhi ukamanda na wapiganaji wa vita hii, kwa kuunda kamati 3 za kiserekali za kushughulikia, 1 Mawaziri, 2. Wakatibu Wakuu 3. Wataalamu. Mawaziri ni ya serikali, Makatibu Wakuu ni wa Serikali, hao wataalamu ni kina nani?, hakuna ushirikishwaji umma, hivyo sasa uindwe kamati ya kitaifa, kwa serikali kuomba ushirikishwa wa Watanzania wote wenye mawazo yoyote chanya ya kusaidia, wakiwemo wa Diaspora, wayalete on line, out of mawazo hayo, inaundwa kamati shirikishi ya kitaifa ambayo itajumuisha sekta zote, sio hali ilivyo sasa, vita hii inaweza kuwa inaongozwa na Goliati, kumbe kina Daudi wapo na wamejinyamazia kwa sababu hawajashirikishwa!. Haiwezekani Waziri Mkuu ataje idadi ya vifo 16, halafu kesho yake waziri mkuu kivuli kuibuka na kusema serikali inasema uongo. Ile kanuni ya a collective responsibility inakuwa applicable kwenye hili la Corona tuongee kwa sauti moja na kupigana kwa nguvu moja.​
  3. Uwezo wa Serikali yetu kutoa elimu kwa umma ni mdogo - kama zilivyo vita nyingine zote, ma verenani huitwa kwenye kupanga mikakati, sisi ma veterani kwenye sekta ya media tupo, tuitwe, tushirikishwe, miongoni mwetu kuna mabingwa wa utoaji elimu kwa umma, tuwe recalled turudi newsrooms tukawasaidie hawa vijana wa sasa suala zima la utoaji wa elimu ya umma, hili lingefanyika tangu mwanzo, tungewasaidia sana Watanzania, ila hadi hapa tulipo, hatujachelewa!. Media zetu hazina uwezo wa utoaji elimu, hivyo media ziwezeshwe, maveterani tuitwe turudi newsroom tusaidie.​
  4. Japo Serikali inafanya hatua mbalimbali za utekeleza kukabiliana janga hili, hazitoshi, more needs to be done, naiomba serikali yetu iwe sikivu, isishupaze shingo kwa kujifanya yenyewe ndio inajua kila kitu, usikilize maoni ya wadau, mfano hoja ya partial lockdown, kwenye mikusanyiko ya ibada, Mungu ni Omnipresent, hakaini kanisani kwenye nyumba za ibada tuu yupo popote na watu wanaweza kusalia popote, kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Rais wetu asiwabeze viongozi wa dini kwa kutumia maneno ya ushetani, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani.​
  5. Kwa vile mpaka sasa Corona haina kinga wala tiba, naunga mkono juhuzi zote zinazochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na janga hili, tuendelee kufuata ushauri wote wa kitaalamu unaotolewa katika kukabiliana na janga hili, na kwa vile Corona ni adui asiyejulikana, tutumie silaha zote za ki hospitali za kiimali. tiba asili, tiba mbadala, na hata akitokea mtu akaotoshwa chochote, tusidharau, na hata kama ni kweli uchawi upo, na wachawi wapo, waruhusiwe kuiloga Corona ife iishe tuendelee na maisha yetu.​
Hitimisho.
Watanzania Tuiaminie Serikali Yetu, Serikali ni Wakweli, Data za Serikali ni za Kweli.
Namalizia kwa ule wito wa mwanzo wa bandiko hili, nawaomba Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo wa ukweli wa nchi yetu, tuiaminie taarifa ya serikali yetu, kuwa idadi vifo 16 iliyotolewa na serikali kuwa ndio pekee waliokufa kwa Corona mpaka sasa nchini Tanzania, ni idadi ya ukweli wenyewe kabisa na halisi, ambayo ndio ya watu waliopimwa na kuthibitishwa wamekufa kwa ugonjwa wa Corona, ila pia kuna watu wengine wengi tuu na wanakufa kwa magonjwa mengine, na inawezekana miongoni mwa hao wanaokufa kwa magonjwa mengine ikiwemo haya ya matatizo ya kupumua, pia Corona imechangia, ila hawaja pimwa na kutthibitishwa kuwa ni Corona, hivyo mpaka sasa ninapoandika bandiko hili asubuhi hii, idadi rasmi ya vifo vilivyotokana na Corona na kuthibitishwa na serikali yetu ni watu 16 tuu na huu ndio ukweli wenyewe halisi, kubali, kataa, ndio ukweli.

Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali
 
Kwa hiyo kila MTU sasa hivi ana mortuary na ana vipimo vya kuangalia maiti kuwa kafa kwa corona kiasi kuwa tumuamini yeyote hata mwandishi Wa habari?

Kwa hiyo magonjwa mengine yote kwa sasa yako likizo watu hawafi kwa magonjwa mengine?

Vipimo vya mahospitali ndio huongea sio porojo za vijiwe vya waandishi Wa habari hata kama wana miaka 30 kwenye tasnia ya habari
 
SawaPasco mm nimekusikia ukitangaza kwa Mara ya kwanza ni mwaka 1994kama sijakosea ukikuwa unatangaza toka USA KWENYE SHREHE ZA KUTOA GRAMMY AWARD WENGI WALITEGEMEA DENZEL WASHINTON APATE AWARD ILA Hakupata moja ya mambo ukiyosema ni kubwa kukosa kwake award kuna Husishwa na mambo ya ubaguzi wa rangi...ilikuwa ni mida ya saa nne ya huku Kwetu na kama sijakosea ilikuwa jumapili.....kuhusu Idadi ya Vifo tutajadili siku ingine Wenye watu wao waliofariki kipindi cha corona watajitokeza wenyewe
 
a siku jf wanajiunga wanachama wapya ambao hatufahamiani, wengine ni vitoto umri wa watoto wetu, mkitofautiana hoja, vinatukana, hivyo kujitambulisha hivi from time to time kunasaidia kujenga kidogo heshima, maana vitoto vingine vinatukana vikijua vinabishana na vitoto vyenzao!.
Main challenge kwangu hapa JF ni hiyo! Najikuta nawiwa kutoa lugha isiyo stahili baada ya VITOTO kutukana! Sijui nilifanyeje hili! Umeto hoja ya msingi!
 
Kwa hiyo kila MTU sasa hivi ana mortuary na ana vipimo vya kuangalia maiti kuwa kafa kwa corona kiasi kuwa tumuamini yeyote hata mwandishi Wa habari?

Kwa hiyo magonjwa mengine yote kwa sasa yako likizo watu hawafi kwa magonjwa mengine?

Vipimo vya mahospitali ndio huongea sio porojo za vijiwe vya waandishi Wa habari hata kama wana miaka 30 kwenye tasnia ya habari
Umeambiwa usichangie kitu. Hivi huelewi? Au wewe ni miongoni mwa vile vitoto?
 
Update ya mwisho ilikuwa ni lini? Kuiamini Tanzania kwenye data za Covid 19 ni sawa na kuamini China eti ina vifo elfu nne tu vya Covid 19.

Hata Spanish Flu nchi nyingi zilificha data,eti aibu ya kuonekana ugonjwa umewaelelea.
Iliitwa Spanish flu kwa sababu tu Spain walikuwa wazi,media za Spain zilikuwa free kureport huo ugonjwa.
 
Pascal Mayalla,

Kuwa na miaka mingi kwenye tasnia yako siyo kuwa na akili na uwezo mkubwa wa kufikiri na kidadavua mambo kiweledi.

Na hivyo vitoto siyo kwamba havina akili kwakuwa vingine vimesoma kuliko wewe na vinaakili kuliko wewe. (Usiudharau utoto wao)

Ukijiheshimu nao watakuheshi, ukijivunjia heshima nao hawatasita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,

Mzee Pasco Tanzania hakuna alie kufa na corona mbona unajichanganya au umesahau kuwa vipimo vinasema uongo ooooh ni vipimo vya mabeberu so mpak saiz Tanzania hakuna mgonjwa wala kifo full stop
 
KWANINI SERIKALI INALAZIMISHA KUAMINIWA?

TUNAOKUFA TUNATOKANA JAMII, TUNAHUDHURIA MAZIKO YA WAPENDWA WETU NA KUSIKIZA WASIFU WA MAREHEMU (kama majumuisho ya kura) SERIKALI INAFUNDISHA WATU SOMO LA HESABU TOKA SHULE ZA AWALI, MNAWAZUIAJE WATU KUJUMLISHA IDADI YA NDUGU ZAO WAPENDWA WALIOKUFA KWA COVID-19 ??
 
Back
Top Bottom