Baba Oruch
Member
- Nov 4, 2023
- 51
- 92
Leo nilikuwa nafuatilia mahojiano katika channel ya Zamaradi TV kati ya mtangazaji na Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania ndg Gilead Teri. Katika mahojiano hayo, Mkurugenzi alijikita zaidi katika kuangazia mageuzi makubwa yanayofanywa na kituo hicho na zaidi namna wanavyotembea kwenye ndoto na maono ya Rais Samia katika kuona uwekezaji unakuwa nguzo kubwa ya kukuza uchumi wa nchi yetu. Mambo ambayo yamenifariji na naamini wale wenye ndoto ya kuwekeza watajifunza ni kama ifuatavyo;
1. Kuwawezesha wawekezaji kuanza kutumia mtaji wao wa uwekezaji bila kulipia Kodi ya VAT na badala yake mwekezaji anaweza kulipia ndani ya miezi 36. Ametolea mfano wa kichwa/vichwa vya roli kwamba mwekezaji anaweza akaanza shughuli za usafirishaji na akizalisha ndani ya muda uliopangwa atawasilisha/kulipia kodi ya VAT. Hii imeleta/italeta unafuu kwa wawekezaji na haya ndio mazingira wezeshi yanayopigiwa kelele kila siku na wadau na Kwa hatua hii, hakika uwekezaji utaongezeka sana ndani ya nchi yetu.
2. Kufanya vikao vya mara Kwa mara na wadau waliopo kwenye mnyororo wa uwekezaji kama vile TBS, TRA n.k. Lengo ni kuchochea ufanyikaji wa tathmini na kupunguza mlolongo wa vikwazo katika uwekezaji na hakika ni hatua nzuri katika kuchochea uwekezaji nchini.
3. Kuwatambua na kiwaunganisha wawekezaji wa ndani wenye nia ya kushirikiana na wawekezaji toka nje pindi wakijitokeza katika eneo la uwekezaji lonalofanana.
4. Katika kuyaongea haya alikuwa akiirejea Sheria ya uwekezaji Tanzania iliyotungwa na bunge ya mwaka 2022. Hii Sheria nitaiweka kama attachment ili kila anayetaka kuifahamu iwe rahisi kwake.
Yapo mengi sana mazuri yaliyoongelewa na kwa kifupi haya ni baadhi tu kwa leo. Asante sana Rais Samia na serikali kwa ujumla kwa jitihada za kuendeleza uwekezaji wenye tija Tanzania, asante TIC.