Live on TBC: Revo wa TIC Azungumzia Uzinduzi wa Kituo cha Pamoja, TeIW Utakaofanywa na Waziri Mkuu Majaliwa 25 Sept. Mlimani City

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Watch TBC live !

View: https://www.youtube.com/live/WG68iDTH28I?si=g2NmH5hKoui5ZSRX

Anayezungumza ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wawekezaji wa TIC, Bw. Revocatus Arbogast Rasheli.
Kwa vile sio wote wenye access na TBC saa hizi, nitawaletea kwa uchache yale ya muhimu aliyozungumza.

Mkurugenzi Revo ameanza kwa kueleza majukumu ya idara yake ya huduma kwa wawekezaji, ni kuwahudumia wawekezaji kwa kuwapatia huduma mbalimbali kuanzia usajili miradi ya uwekezaji, kupata vibali, leseni na ridhaa na usaji mbalimbali kutoka idara mbalimbali za serikali. Nimefurahi kuwa hapa kuzungumza na Watanzania.

Mtangazaji akauliza kwanza kuhusu hali ya uwekezaji Tanzania kwa sasa.

Mkurugenzi Revo amesema, ewekezaji ni ushindani kwanza nipongeze jinsi serikali zote na awamu zote zimefanya juhudi mbalimbali kuboresha mazingira ya biashara kuvutia uwekezaji. Mnamo mwaka 1990 serikali ilitunga sheria ya uwekezaji na kuunda National Investment Promotion, mwaka 1996 tukatunga sera ya uwekezaji, na mwaka 1997, tukatunga sheria ya uwekezaji iliyoanzisha kituo cha Uwekezaji, TIC

Revo ameishukuru TBCnamesema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye sheria nzuri sana ya uwekezaji, ambapo mwekezaji wa nje, anapaswa kuwa na mtaji wa Dola $ 500,000 lakini kwa Mtanzania, anatakiwa awe na uwekezaji wa dola $ 50,000 tuu!.

Watanzania wenzangu, tuchangamkie fursa za uwekezaji kupitia TIC.

Karibuni.

Paskali
 
Revo amesema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye sheria nzuri sana ya uwekezaji, ambapo mwekezaji wa nje, anapaswa kuwa na mtaji wa Dola $ 500,000 lakini kwa Mtanzania, anatakiwa awe na uwekezaji wa dola $ 50,000 tuu!.
P
 
Uwekezaji ni mgumu kwa sekta/idara/taasisi/nchi ambayo baadhi ya sheria zinabadilika badilika kila uchao...bado ustahimilivu wa kisiasa na miundo mbinu mfano umeme /maji/barabara nk
 
Revo amesema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye sheria nzuri sana ya uwekezaji, ambapo mwekezaji wa nje, anapaswa kuwa na mtaji wa Dola $ 500,000 lakini kwa Mtanzania, anatakiwa awe na uwekezaji wa dola $ 50,000 tuu!.
P
Kuwekeza kwenye nchi yenye upungufu wa umeme ni upungufu.... sijui nilitaks kusema nini
 
TeIW ni dirisha ambalo limeunganisha taasisi 7, ambapo mwekezaji akitaka kujisajili, anatumia dirisha moja tuu, ukiisha jisajili TIC taasisi nyingine zote zitakuwa zimekuona huna haja kweda Brella, TRA, Nida, etc.

P
 
Watanzania wapewa wito kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazotolewa kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania, TIC.
P
 
Revo amesema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye sheria nzuri sana ya uwekezaji, ambapo mwekezaji wa nje, anapaswa kuwa na mtaji wa Dola $ 500,000 lakini kwa Mtanzania, anatakiwa awe na uwekezaji wa dola $ 50,000 tuu!.
P
Starlink walishindwa kuwa na 500k USD kweli ?

Mbona hizo ni peanuts.

Come again brother Pascal.
 
Bila stable energy tunapotaka kwenda ni pagumu kweli.
Vitoto vinazaliwa huko Ulaya mpaka vinazeeka vinakuwa havijawahi kuona umeme umekatika ajabu ukikatika vinashangilia
It's true umeme ni changamoto ila sasa baada ya kukamilika kwa JNHPP, kukatika katika umeme itakuwa ni historia!.
P
 
Back
Top Bottom