Inatokea post namba 155.
Baada ya kuagana na Arsis nikaenda kwenye gari, nikaondoka bila kukuta na yeyote, nilipofika nyumbani, mlinzi akanifungulia geti bila kuita au kupiga honi, nikaaiweka gari, nikaingia chumbani kwangu kulala. Usingizi ukawa hauji haraka. Nikaanza kuitazama ile pete, nikachukua mkebe wake nikautazama vizuri. Ulikua ni mkebe wa kizamani sana, ulikua na maandishi maatatu kama michoro yale ya Kimisri ya zamani. Nikasema nikikutana na Arsis nitamuuliza kimeandikwa nini. Nikarudisha mkebe, nikaichukua bakora nikawa naichezea, nailaza chini inanyanyuka yenyewe, naiweka upande inajisimamisha yenyewe. Mpaka nikawa nacheka tu mimi mwenyewe, Bakora haikubali kulala chini kabisa. Nikaiweka pembeni ya kitanda changu. Nikalala.
Maisha yakaendelea kama vile kabla sijaenda Tanga, haikupita muda nrefu nikawa noimeshafu ga ndoa, ilikua ndoa ya surporise kubwa kwangu, lakini hapa sio pahala kwake kuielezea.
Kuna siku, baada ya kama miezi miwili mitatu ya kuoa, nikasema leo ngoja nikamtembelee "mama mkwe" wa kwenye vitumbua asubuhi subuhi, lakini toka siku niliyoyaona Chalinze na pale kwao nikawa naogopa kula kwa mama lishe. Nikajisemea wacha niende tu nikawagtembelee. Kufika, mama mkwe akawa na bashasha kweli, "Ah bwna harusi, leo umefunguliwa?" Nikamwambia "mboina jamani saba iliisha siku nyingi/". Aaah huonekani nikajua "honey moon zenu, mwezi umekwisha bwana harusi huonekani" Nikamwabia aah si unajua tena, maisha ya ndoa tofauti na ya zamani. Akanambia "tena yafurahie bado ungali una nguvu mwanangu, usicheze na furaha yako hata kidogo> Nikamwambia 'poa".
Akanambia haya nikjupe vingapoi leo? Nikamwambia nimekuja kulusalimia tu, nyumbani si wameshakuja kuchukua? Akanambia haya kula viwili, imi ingawa hukumngoja bintoi yangu lakini najua kuna siku uytamuoa tu, ukwe uko pale pale. Nikamwabi tulikua nae harusini, kumbe ni partner mkubwa wa mke wangu. Khaa, nyinyi mmetufanyia voituko vinaogelewa Ilala nzima hii, miaka yote sisi tunajua yule dadako kumbe mmelelewa pamoja tu. Nikamwabia hata mimi nilikua najua tumezaliwa pamoja. Kumbe ni watoto wa mjomba na shangazi.
Mama mkwe; Aaahmkeo na binti yangu umesahau toka wadogo wako pamoja? Mimi nimewaambia na huyo mume atawaoa wote mkae pamoja.
Mimi; Mimi poa tu, wakikubaliana wenyewe mimi nipo. Niakbadilisha topis, vipi mama wa mandazi, sijamuona toka siku ile ya pirika?
Mama Mkwe: Kwani yaliompta madogo mwanangu, si kashikwa anawanga huko buguruni. Kututukana na kutuita sisi wachawi, kumbe yeye ndio mchawi.
Mimi; hatari kubwa, sina habari.
Mama mkwe: Makubwa mwanangu hata hayasemeki. Alikua anaongea huku ananong'ona. Tena hapa mwezi ujao hatupo tena, hii nyumba imeshauzwa, tunatafuta kijiwe kingine hivi sasa. lakini mimmisina wasiwasi, nitakua nyumbani kwangu palepale, hakuna wa kunihamisha, pale kwangu mwenyewe. Nitapika pale nitakwenda kuuza vitumbua vyangu pale nje ya msikitini mpaka tupate kijiwe.
Mimi: Kumbe tuko wote, hakuna tabu. Usihame kijiwe kipya bila kunijiulisha.
Mama mkwe: Kumbe huna habari? Wenye nyumba hii washama wote, wameiuza nyumba haraka haraka kwa aibu, kumbe walikua chama kimoja nayule muuza mandazi. Wameaibishwa wote, kwa aibu na jiji wamelihama.
Mimi; Kasheshe.
Mama mkwe, lakini toka wameondoka, hata uzito na mazonge zonge yamepungua, kumbe tunaishi na wanga hapahapa, sasa hivi baba kijiwe kimesafoshwa hiki, mbao walikua hawaji sasa wanakuja.
Mimi; Kwani aliepanunua kawaambia muhame?
Mama mkwe; Wala hajatwambia tena mteja wetu mzuri, anakaa hapo mtaa wa nyuma, shogake mamako , yule mwanamke mpambe wa Kiarabu? Aaah, nimeshamjua, ndio nilisikia kanunua nyumba nyingine, kumbe ndio hii?
Mama mkwe; Pesa imetulia pale kachukua hii na ya nyuma yake, zote kwa pamoja, pesa cash nq sisi wotw hapa tukapata sadaka yetu nono, tenono kweli kweli. Hatuna manug'uniko wala masikitiko. Hatutaki tumewekee kiza akianza ujenzi, mwenyewe kasema hachelewi ataanza ujenzi. Sisi tumeona wala hana ya kutwambia tuhame, tumeishi nae kama ndugu miaka yote. tena mwenzetu sana yule Mwarabu, sisi tumefurahi kununua yeye hizi nyumba, maana yule na mamako ndio kimbilio letu tukiwa na shida zetu. mwenyezi Mungu awajaalie kila heri, akapiga dua ndegu hapo. Kabla hajamaliza, mama muuza uji akasema bwana harusi kombe lako hili la uji, usiseme umeshiba nimekuongezea pilipili manga njia za mkojo zifunguke vizuri.
Mama mkwe: Kwani alikwambia ana shida na njia yake?
Uji: Koma bibi wee, sisi tunajua kutunza mabwana harusi, Watanga mwenzangu huyi, ulikua hujui?
Mama mkwe: Nawaju, wote wadigoi nyinyi.
Uji: Kwa hio usituingilie kabisa, tuwachie wenyewe. Bwana harusi usimsikilize huyumzaramo, hana alijualo zaidi kutingisha makalio tu.
Mama mkwe; Mboina unamwaga razi kwa mkwe wangu?
Uji; Tupishe huko, tukaoe mzaramo sisi hatuna akili? Nyie ndio mje kuoa kwetu msiojua kupika nyinyi.
Mama mkwe: Mkwe wangu usimsikilize huyu bibi, hata huko kwao Tanga kapasahau, toka aolewe hajaenda hata kutemnbea kwao, mzaramo alivyo mdhibiti.
Mimi; Jamani nilikua nataka kuwauliza kitu.
Wakakaa kimya wote wananisukiliza.
Mimi; Hivi kwanini hamuweki kijiwe kwenu pale msikitini kwa pembeni pale, uwanja mkubwa tu, hata mkiwa ishirini mtaenea pale.
Uji: Hwa wazaramo hawataki msikitini, wanga wakubwa wanapaogopa, mimi uji wangu nauanza na watu wa msikitini alfajiri, wakitoka tu msikitini wapo hapa. Hawa wanakua bado wamulalia.
Mama mkwe: Wewe mboina una mdomoi mchafu mbele ya mkwe wangu?
Uji: Nisamehe baba, mimi uji niytauuzia pale pale msikitini nikiondoka hapa, nimeshaongea na imamu kasema mradi nisipike pale tu, msikiti unatakiwa uwe msfi njje na ndani. Kai kwa hawa wachoma vitumbua na wapika chapati, watapoikia wapi pale?
Mama mkwe; Tutaongea na msikiti nyum aple tutapajenga wenyewe.
Uji; Hilo wameshakataa kama ulikua hujui, wanasema muda si mrefu msikiti unaongezwa ule unakua mkubwa na tena wagorogfa.
Mama mkwe: Hili nimesikia hata kimi, lakini hawajui lini utaanza lini.
Uji; Umelala wewe, msikiti kabla nyinyi hamjaondoka hapa utakua umeshaanza kujengwa.
Mama mke: basi poa, tutawauzia hao hao wanaokuja kujenga, tutabanana nao hapo hapo, watakula wapi?
Uji; Tena pla cheyameni wa wauzaji chkula mimi, mtanilipa mimi kila siku, mkitaka biashara pale.
Mama mkwe: Mdigo wacha utapeli wa mali ya msikiti, huo u cheyameni akupe nani wewe mwenzangu na mimi, nipishe huko.
Nikaona niage. Nikaaga nikaondoka zangu, uji kweli ulikua na pilipili manga ya ziada.
Itaendelea.