Battor
JF-Expert Member
- Mar 21, 2019
- 2,111
- 3,728
Mkuu kila jambo lina chanzo chake na ukijua chanzo cha kitu ndio uhalisia wake, mfano mimi mtu niliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu hivyo chanzo changu ni Mungu na uhalisi wangu unatokana na yeye, ili niweze kuishi na kutimiza kusudi lake katika dunia hii ili nipasa niwe na mwili wenye kuendana na nature ya ulimwengu huu, hivyo nikafanyika mwili kisha akanipa nafsi ya uhai( pumzi), ambapo ikawa kiunganishi kati yangu mtu(halisi yangu) na mwili(asili yangu). Hakuna kitu kinachoweza kuwa chochote, halisi ya kitu haibadiliki kamwe.Hajasema anawezza kuwa kitu, amesema anaweza kuwa chochote. Labda mimi ndio sijaeleza vizuri. Yaani yeye anasema anaweza kuwa chochote ukitakacho wewe, sababu kuu, haonekani, mimi sijamuona mpaka leo. Kwa hio hapo ni fikra zako tu, ukifikiria mti unaongea na wewe, kwake sawa, ukifikiria jini anaonea na wewe kwake sawa, ukifikiria mtu anaongea na wewe kwake sawa.
Lakini mbona niliandika mwenyewe anasema yeye ni mtu. Au nimbishie hilo?
Hilo la kila kitu "lina uhalisi": wake sijakuelewa. Huo uhalisi unaupata kwa kuuona, kuusikia, kuusoma au vipi? Uhalisi wako wewe ni upi> Mimi siujui.
Simba.
Hapo kwenye kuwa chochote umenielewesha vyema kwamba mimi ndo naweza kumtafsiri vyovyote hiyo ni sawa kabisa.
Ni vyema ameweka wazi kuwa yeye ni mtu, swali langu je yupo katika dimension ipi, je bado ana nafsi hai? Kama sio, anawezaje kuwasiliana na kiumbe chenye mwili kwa kutumia milango ya fahamu( umesema huwa unaisikia sauti yake na una record), kwa nijuavyo mimi kiumbe kisicho na nafsi hai hutumia either ndoto ama kumtumia mtu mwenye nafsi hai kufikisha ujumbe wake, sasa inawezekanaje kwa Arsis kutumia sauti kukufikishia ujumbe bila kutumia medium yeyote.