Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Viumbe wengine wote watahukumiwa,kisha baada ya hukumu kupita na kila mmoja kupata haki yake,itahukumiwa wageuke kuwa mchanga period
hot-cuppa.gif
 
H
Jumapili njema.

Nauliza tena.
Katika Dini inayotumia kitabu cha Biblia ikiwemo Ukristo Kuna Amri zinazo ainisha kuwa, ili uhesabike haki ni lazima uzifuate hizo Amri zote.
Na Ubatizwe.

Katika Agano la kale kulikuwa na Amri Kumi alizopewa Musa.
Eg. Usiue, Usizini, Usiseme uwongo, nk.

Katika Agano Jipya Kuna Amri Mbili tu
1. Kumpenda Mungu kwa dhati
2. Kumpenda Jirani kwa dhati.
Ukimpenda Jirani huwezi, kumwibia, kumwua, kumsingizia nk.

Je katika Dini ya Kiislamu Amri zake.
1. Zinasemaje ?
2. Ziko ngapi ?
3. Zimeandikwa wapi ?
4. Kwanini hawabatizwi ?

Niulizeni kwa Arsis,
Hili la ubatizo ni maigizo we angalia umbaji wa Mungu Toka unaumbwa tumboni kwa mama yako mpaka unazaliwa hiyo yote ni mwema ya Mungu alishakuchagua na kukuleta duniani Zen badae mtu anakuja na maji kwenye jagi eti ndiyo anakubariki uwe wa Mungu usipobatizwa we washetani inakuingia akilini hiyo..?!
 
kwani mimi mtoto mdogo? Hii ni story nilivyo balehe, mimi sasa hivi nina wajukuu kijana.

Wewe kwenu Duga au ulitembelea tu? Au polisi wa Duga, maana siku hizi kumejaa mapolisi na wagtu wasiojulikana huko, mnapiga pesa tu. Nasikia kuhamishiwa Duga siku hizi dil
Hapana mimi si polisi, ila ni mzaliwa wa huko na kukulia maeneo karbu na hayo. Ndio maana nimekuwa interested kupata uhalisia wa maeneo yetu haya
 
Habari za saa hizi wana ukumbi wote.

naomba mfahamu hii ID ya Arsis ndio mwanzo ilikua corazon Espinado nimeomba moderators waibadili.

Kwa kuwa tumeingia kwenye" vionjo vya Arsis" nikaona niitumie ID yake. Mtanisamehe sana kama italeta mkanganyiko wa hapa na pale mnisamehe sana. Pia naomba mfahamu nina ruksa ya kutumia ID kutoka kwa Arsis mwenyewe.

Nipo msibani Bagamoyo, nategemea kuondoka kesho kurudi kwangu. Binafsi nimeamua nichukue room Hotel nipumzike, kwa hio nitapata muda wa kupitia posts na kuzitolea majibu au ufafanuzi wangu au wa Arsis mwenyewe.
Tuambie pyramids za Misri zimejengwa na nani?
 
Swali langu Arsis
Kwanini nashindwa kupata msaada kwa watu kwenye suala langu la jamaa kutumia vyeti vyangu na anapata mshahara mzuri,posho, na marupurupu mengine?
Nimejaribu kufuatilia mpaka baraza la mitihani (NECTA) Kujua jina langu au vyeti vyangu vinatumika ofisi gani au idara gani iii nipate kuchukua hatua za kisheria?
Ukiwa kama unayeona mpaka mambo yasiyoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu au kwa sisi watu ambao hatuna Mamlaka yoyote kwenye hii nchi. Kinachonisumbua ni kupata upinzani kila mahali, hata watu ambao wana nafasi za kunisaidia lakini bado sifanikishi? Nilienda mpaka NECTA kuhakiki lakini nilikuta upinzani na yule niliyemkuta sehemu ya ukaguzi wa vyeti ikaonesha alijua naenda kufanya nini pale na ananijua. Ninapambana kwa sababu ni haki yangu Chuo ada niliilipa kwa jasho langu mwenyewe hata kuijenga na kuitengeneza CV yangu ni jitihada zangu. Nimeomba msaada kwa ndugu zangu ambao wana nafasi ya kutoa amri mara moja tu lakini nao wanapuuzia. Halafu mtu ambaye hakusoma wala hakupata uzoefu wa kutengeneza wasifu anakula kupitia jina langu. Nikifanya interview kwenye ofisi zingine nafaulu vizuri usaili lakini kuitwa kuanza kazi hakuna. Mpaka nimeamua kufanya mambo yangu binafsi tu na Alhamdulillah nayamudu lakini kwanini nadhurumiwa haki yangu? Na kwanini sipati ushirikiano kutoka kwa Ndugu, marafiki au watu niliosoma nao ? NECTA ni pagumu na UTUMISHI nako ni vikwazo na nimejiapiza sikubali haki yangu ipotee hivi hivi. Ingawa kuna mazingira fulani ya kutishia usalama wangu nayaona au kuhisi hatari ya kufuatiliwa na watu wasiojulikana. Ushauri wako na mwongozo wako nauomba.
Hili Arsis alikua hataki kukujibu moja kwa moja. Alinambia mimi nikasema nitakujibu. Jibu lake sio zuri sana.

Arsis alisema, Unaijua sababu.
Simba.
 
Hizi mambo aisee...

Nina maswali kadhaa hapa kama kuna wajuzi wanijuze ama huyo Arsis kwa njia ya mleta uzi mwenyewe...

1. Inasemekana binadamu ni kiumbe special, kiumbe unique, kiumbe mwenye nguvu etc, inakuaje huyu kiumbe akaingiwa na jini, kiumbe ambae ni dhaifu kwake, kiumbe wa chini yake.??

2. Jini kiumbe alie chini ya binadamu inakuaje anafanya mambo ambayo binadamu anafight kuyafanya for almost the rest of his/her life mfano; inasemekana jini anauwezo wa kusafiri umbali mrefu kwa muda mfupi kitu ambacho binadamu hawezi mpaka awe na elimu fiche juu ya hayo mambo na si ajabu akawa wa ajabu kwa binadamu wenzake wakati kwa jini wala sio kitu cha ajabu, na anaweza kasafiri hata kwa chini ya dakika 3 kwa umbali wowote duniani(kwa mujibu wa mleta uzi).

3. Jini anaweza kutoa uhai au kumuumbua binadamu au jini mwenzie wa chini yake(kwa mujibu wa mleta uzi) lakini binadamu hawezi kutoa uhai/kumuumbua jini au binadamu bila kutumia matungili, na kufukiza makitu mengi sana mpaka kupasua nazi, kuchinja wanyama na kafara za namna hiyo.

4. Mwisho ningependa kumuuliza mleta uzi, yeye anaamini Arsisi ni nani?? Sio binadamu, sio jini , sio shetani, sio Mungu ni nani hasa??
Anamuamini? Kama ndio/sio kwanini??
Arsis ni Jaduuu

download (1).jpeg
 
Tuambie pyramids za Misri zimejengwa na nani?
Arsis alishajibu hili, sina uhakika kama nimelileta hapa.

Zimejengwa na binadam, zipo dunia nzima, lakini zinazoonekana ni zile za Misri na nyinginezo tu huko Amerika ya Kusini.

Zipo za maiaka mingi sana zinatofautiana ujuzi na ufundi, zipo mpaka za miaka millioni nyuma. Zingine anasema zipo baharini hata kwetu huku.
Simba.
 
Kuna mtu anajidai wa Duga eti hapajui kwa mzee Mabruki hapo Maforoni. Inawezekana hio kweli?

Unapajua pwani ya mahandakini?
Simba.
Kwa kweli huwezi kuwa mtu wa Duga eti usipajue kwa mzee mabruki hapo maforoni ...haiwezekani!
Pwani ya Mahandakini naifahamu nishapita sana ujanani mwangu kuna chobingo kule za kwendea kenya ule upande wa jasini
 
Naomba unieleze kuhusu jini maiti, nini kinatokea baada ya mtu kupandisha jini maiti.

Lengo la jini maiti ni lipi, taratibu ya kulitoa ni zipi?
Waganga waongo na wachawi wanaojidai waganga, wanaita tu hivyo kutisha watu wajippatie pesa. Huyo ni jini yu hai, anakua ni mtumwa wa kijini aliezeeka sana, anatumiwa kishirikina. Huyo kumtoa ni kama kusukuma mlevi kwa anaejua na mkweli.

Nikupe dawa ya kumkimbiza jini kwenye mwili wa yeyote yule na jini yoyote yule kwa muda?
Simba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom