Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Simba,

Hapo kwenye dawa zako nina swali au maswali. Nimekusoma kuhusu diesel, kwangu siyo mara ya kwanza kusikiya hilo la diesel kukimbiza najinni kutokea kwako, nimewahinkudhuhudia kwa macho yangu mtu aliepandisha akapakwa diesel, akawa anapiga kelele kabisa. jini likamwachia huyo mtu likatoka nduki.

Nauliza, kwanini hao majinni wanaiogopa na kuikimbia diesel?

Huku kwetu tunafukuza nyoka kwa kumwaga diesel au mafuta ya taa au oil chafu sehemu ambazo hatutaki nyoka wafike.

Pia akionekana nyoka kaingia mahali basi itamwagiwa diesel au mafuta ya taa, lazima atatoka alipojificha na ukimwagia nayo yakimpata vizuri wanasema hana maisha huyo, lazima atakufa.

Kwanini nyoka na majinni wana ila hiyo ya diesel? Mafuta ya taa nayo kwa majinni ni hivyo hivyo? Petroli nayo vipi?
Nyoka ni jamii ya majini, huoni wanavojificha ficha? Jini ni neno linalotokana katika neno kutokuoneka kwa Kiarabu.

Kuhusu Diesel, ni kwa kua Diesel ikipakwa sehemu haipotei kwa muda mrefu mpaka ipanguswe au ifutwe (masaha) hai evaporate kwa haraka. Sio kama mafuta ya taa na petroli.

Hio "masaha" ndipo pia tunapolipata jina Masih kwenye Qur'an.
Simba.
 
So race ilikua ni black??
Hilo lilishajibiwa nyuma nyuma huko, kwa kua hujaliona, nakushauri pitia picha za mafarao kwenye mtandao, au tafuta picha ya Anwar Sadat aliewahi kua Rais wa Misri na picha za watu wa Sudan, utapata picha ya watu aina gani waliokuwepo.

Utawala wa Misri wa zamani ulikua kuanzia inapoanzia Nile mpaka inapoishia Nile.
Simba.
 
Hao wazungu mbona wapo wa dini zote ba wengine wao hawana dini kabisa, tena sasa makundi kwa makundi wsnsrudi kwenye Uislam.

Waarabu wapo wa dini zote, kuna dini zingine zipo kwao tu, hazijafika kwetu wala Ulaya. Sema wengi wao wameiyona nuru ya Uislam kama sasa inavyotapakaa dunia nzima.

Uislam haumlazimishi kipofu kutazama, humsafisha moyo wake uione nuru kabla ya macho yake.
Kama huioni nuru ya Uislam elewa kuwa upo kizani.
Mwaga elimu, tupe mfano wa dini ambazo zipo kwa Waarabu hazijafika kwetu wala Ulaya.

Mbona umekatiza?
Simba.
 
Sijafahamu hapo, malizia kuandika kipande hiko.
Simba.
Nilimaanisha ukiona watu wanakuomba uwape connection ya matibabu ujuwe wapo desperate na tiba,pia ni wewe ambaye umesema mahusiano yako na hao viumbe sio ya Kishirikina sasa unasita nini kutoa connection watu tustafidi kupitia wewe??
Pia baadhi ya maswali haujibu kwa mfano nilikuuliza kuna mahusiano(mechanisms gani kwa watu wenye majini mahaba kuwa na upungufu wa nguvu za kiume!??
 
Simba,

Hapo kwenye dawa zako nina swali au maswali. Nimekusoma kuhusu diesel, kwangu siyo mara ya kwanza kusikiya hilo la diesel kukimbiza najinni kutokea kwako, nimewahinkudhuhudia kwa macho yangu mtu aliepandisha akapakwa diesel, akawa anapiga kelele kabisa. jini likamwachia huyo mtu likatoka nduki.

Nauliza, kwanini hao majinni wanaiogopa na kuikimbia diesel?

Huku kwetu tunafukuza nyoka kwa kumwaga diesel au mafuta ya taa au oil chafu sehemu ambazo hatutaki nyoka wafike.

Pia akionekana nyoka kaingia mahali basi itamwagiwa diesel au mafuta ya taa, lazima atatoka alipojificha na ukimwagia nayo yakimpata vizuri wanasema hana maisha huyo, lazima atakufa.

Kwanini nyoka na majinni wana ila hiyo ya diesel? Mafuta ya taa nayo kwa majinni ni hivyo hivyo? Petroli nayo vipi?
Umenikumbusha kitu hapa ,ukiacha hiyo kuna ustaadh mmoja alisema kuna mafuta ambayo ukipaka mkononi na kuwanyooshea watu mkono mapepo yana panda na kukimbia,akasema kuna wajanja wa town hapo wanaongezea na jina la Yesu basi mnaamini Yesu ametenda

Watu hawakuamini akawaambia siku fulani mje na mjionee wenyewe,kweli bwana na akarekodi kabisa clip,alituonyesha hiyo clip siku ya ijumaa watu wanaanguka na kupiga makelele

Kwahiyo ni kweli kuna mafuta ambayo ni mtihani kwa majini
 
haya Lidafo, Etugrul Bey na waislam wengine tupeni msimamo wenu kuhusu malaika kwa ushahahidi wa Qur'an kama alivyotupa mambio kwa ushahidi wake wa Biblia.

Hizi elimu ndio kufunguana macho huku.
Simba.
Kwa mujibu wa quran malaika hawaaswi wao wanafuata wanayo amrishwa tu na Allah aya ifuuatayo inathibitisha hilo
QURAN 66:6
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوْا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا قُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ
"Enyi wale walioamini, lindeni nafsi zenu na familia zenu kutokana na Moto wa Jahannam, ambao mafuta yake ni watu na mawe. Juu yake wako malaika wa kali, wenye nguvu; hawaasi amri wanayopewa na wanatekeleza wanayoamrishwa."

Malaika wao wanatekeleza amri ya mola wao tu hawaaswi kamwe
 
Na yale majina ya Barhatiyah yamo humo ndani ya majina hayo 99
Majina hayo siyajui ingawa arsis alisemq hapa kuwa hayo majina ni shirki,so kama ndio hivyo basi si miongoni mwa majina hayo

Majina ya Allah ni sifa miongoni mwa sifa zake,mfano ya rahman (mwenye kurehemu) kwahiyo unapoomba rehma kwa Allah kisha unatàja na jina hilo,ya razaq (mwenye kuruzuku au mtoaji wa riziki) kwahiyo unapoomba riziki toka kwa Allah kisha unasindikiza na kutaja jina hilo,ya ghafur (mwenye kusamehe waja wake) unapoomba msamaha/maghfira unataja na jina hilo mara kadhaa

Kwahiyo majina ya Allah yanataja sifa zake,mengine unataja kwa idadi maalumu kama unashida ya watoto,au hali ya riziki kama ni mtihani na mambo kama hayo
 
...

Nilipoamka Alfajiri, nikaona nimeamka on time dakika 15 kabla ya muda wa Sala, nikaingia bafu nikakoga, nikatoka nikasali na dua zangu ndogo na nyiradi ndogo ndogo.

Nikachukua simu, nikakuta miss calls tatu za Swahiba na moja ya Sheikh. Nikapiga ya Sheikh kwanza. Baada ya kusalimiana.

Sheikh; Swahiba yako kanambia unaondoka leo, nimempa zawadi akupelekee bandarini, usiwe na shaka kanambia unaenda na ndege, sasa wewe pale Dar mpigie huyu kijana simu, mfahamishe mzigo ufikishwe wapi akiupokea. Nimeona nisikubebeshe mzigo na wewe unaenda kwa ndege.

Mimi; Ndio Sheikh.
Sheikh; Safari njema bwana Simba, In shaa Allah tutaongea zaidi ukifika. Mpigie swahiba yako alikua anakupigia hakupati.
Mimi; Sawa Sheikh, ahsante sana kwa ukarimu wako nikifika salama nitakujulisha.
Sheikh; In Shaa Allah utafika salama, mpigie Swahiba yako kabla hujatoka.

Tukaagana pale, kumaliza nikampigia swahiba. Hakuchelewa kapokea. Baada ya kusalimiana.

Swahiba; Simba, mijimama ya Dar ilikuteka nini nimekupigia sana hupatikani.

Mimi; Ulipoondoka tu, mimi nimeingia ndani,simu nimeiweka silence, mpaka alfajiri, ndio kwanza nimemaliza kusali nikampigia Sheikh, nilikua naongea nae.

Swahiba; Kitahanani cha kukupigia ni Sheikh, kumbe alikua kakutayarishia zawadi zako, matunda matunda ya Unguja ndio nayapakia sasa hivi bandarini, nitakutumia namba ya kijana umwelekeze avipeleke wapi vinaondoka na boti ya 12 kamili.

Alikua anataka nikuwahi usinunue halwa, sasa hizi ndio zina maelekezo, kuna za babu yako,, zote zimeandikwa babu. Kuna za H1 na H2, hizo zimetoka kwangu, najua Dar mtawasiliana watazipata. Na wao nawapigia sasa hivi wasihangaike kwenda kununua Halwa.
Mimi; mmejisumbua mwamba, ahsanteni sana Mwenyezi Mungu awajaalie heri zaidi na zaidi.

Swahiba; Tupo wote, mimi nakuja Airport kuna kimzigo chako kidogo hicho cha mkononi, hakina uzito kabisa.
Mimi; Sawa, si unajua Saa nne nitakua pale?
Swahiba: Usijali, mitaa yangu ile. Tutakutana huko, huingii ndani bila mimi kutokea. Nishaweka swahiba zangu nikichelewa wakwambie.
Mimi; Poa Swahiba.

Nikakata simu nikaona nikapige kahawa za hoteli za mwisho mwisho huku natazama bahari, sina haraka tena ya kwenda mjini. Vitu vyangu nikaweka sawa kwenye kibegi changu ili nikivichukua hakuna kupack tena, nisha pack tayari, nikibeba kibegi na kuondoka. Nikahakikisha sijasahau kitu. Nikaenda nje kwenye kahawa.

Nikaagiza orange juice na kahawa. mhudumu alieniletea akanambia Breakfast ipo tayari, ukitaka tukuletee au pale breakfast room yote sawa tu. Nikacheki muda, nikamwambia bado mapema sana kwa breakfast. Ahsante.


mara ikaingia simu ya babu tukaongea nae.
Babu; Sitaki mchezo na halwa yangu, ukifika tu mpe babako anajua nani wa kumpa aniletee ifike haraka.
Mimi: babu; Halwa yote hio Tanga unapiga alfajiri yote kwa ajili ya halwa tu?
Babu: Ha;wa ileile lakini mapishi tofauti hata ladha toifauti, halwa ya Unguja nzuri sana, ina ladha ya kipekee.
Mimi; Usijali babu In shaa SAllah nikifika tu nampa mwanao.
Babu: Vipi hali yako, hujaoa huko?
Mimi: Kwani ujlikua unashikilia nije ili unioze huku?
Babu; Si nilitaka kujua tu, kama umeoa kuna dadake unioze ma mimi.
Mimi; haya, ninaopota kuoa nitauliza kama wapo wawili.
Babu; Kwaheri bwana, nilikua nahakikisha halwa yngu hamuigfanyi yenu kwenu huko, Kwaheri.

Nikakaa kaa pale sa moja kamili niasema wacha nikapige breakfast, nikaenda breakfast room.

Uzuri wa breakfast room pake kila kitu kipo tayari na vile vya kupikwa pikwa kama pancakes namayai mayai unafanyiwa live hapo hapo.

Nikapiga breakfast yengu ile natoka tuj nikakuta na Meneja na mabibie wa Dar wanaingia, tukasalimiana pale.
H1; Imekua vizuri nimekuona, una halawa zangu na za huyu bibi kutoka kwa handasome la Kiunguja, amasema utagtupa Dar, zuilete kwangu.

Mimi: Poa Bi H; kwako sizileti naogopa mumeo asinikabe. Totozuri namna hii si kutafuta ugomvi na mtu.
H1; utazileta sana, kama huzi;leti wewe atazileta mamako au mkeo, au yule malata mkubwa babako. Tana umenikumbusha, mpoe babako aniletee. Kifaa cha uhakika kile.
Meneja; Basi mkimaliza breakfast tutaonana niwaambie gari saa ngapi mtakua tayari?
H1; Si wewe ndio unajua saa ngapi, mimi najuaje barabara za kwenu huku, sema unatutoa tu kwenye maongezi ya kunyanduana, unajidai tu. Na namngoja huyo mzungu wako, akija na fanay ushoga nae . Nimfundishe mambo ya Kibongo.
Mimi: jamani, tugtakutana au kwenye basi au airport.
H1; Nendeni hukoi, mimi halwa zangu tu.

Tukatoka mimi na Meneja wao wakaingia kula breakfast. Nikamwelezea Manager kua sina haja ya kwenda kununua halawa mjnini mapema, sas nangoja time ya kuondoka tu.

Meneja; Tatu kamili kuna gari igtawangoja, wote mnaondoka ndege moja. Na mimi nigtakuwepo, wacha nipige raundi za kazi tutaona saa tatu kamili.

Huyo akapotea na mizunguko yake ya kazi.

Mimi nikarudi chumbani kwangu, nikampigia Mzee, akanambia nipo kwenye garinitakupigia nikifika pfisini.

Nikasema nimpigie Mshikaji wangu anifate airport nikaona haina haja, ngoja niongee na Mzee.

Baada ya muda simu ikaita, kupokea Mzee, ytukasalimiana pale.
Mzee; Unasemaje Simba?

Mimi; Nkuja huko naingia saa tano na nusu, maana nenge yatu inandoka hapa saa tano, nataka nije moja kwa moja ofisini.
Mzee; Simba haina haja ya kufanya hivyi, hapa usijali tupo sisi, kila kitu kipo OK, wewe nenda moja kwa moja Nyumbani, sawa ngoja nimwambiae Mshikaji anifate Airport.

Mzee; na mimi akija hapa tamsisitiza, elo haja asubuhi nyumbani, si unajua mabo yake yule, siku hizi kawa Sheikh Mshikaji wako.
Mimi; Ma Shaa Allah. Ndoja nimpigie.

Nikampigia mshikaji. kabala hata ya kusalimia...

Mshoikaji; Wewe mwanga. Laim unitilie kauzibem japo kwa simu.
Mimi; Kwanino gtena?
Mshikaji; Hivi ndio nilikua nainia kwa Dokta kataka nimepeleke kazini nikamwache huko nikamchukulie mzigi wake kwenye boti hya Unguja aliusahau Unguja umetumwa leo.
Mimi; Kweli mahaba yamenoga, kwani siku zote alikua anachukuliwa na nani?
Mshikaji; Mavi ya kale hayanuki, sas hivi mambo yake yote yanapitia kwangu.
Mimi; Ndio maana nimempoigia mzee anasema leo hujaenda hata kuchukua lifti ya kazini.
Mshikaji; Tena ailikua nimpoigoie dingi sasa hivi nimweleze, wewe ndio umepiga, unasemaje mwanagu?
Mimi: nataka uchukue gari yangu hapo unifate airport saa tano kamili, usichelewe.
Mshikaji; Umeenda na boti unarudi na mwewe?
Mimi; Ndiyo.
Mshiikaji: Poa basi, usijali, mimi nawahi,

Mimi; Oyaa, kuna mzigo wangu na mimi ujmekuja huko bandarini na boti ya subuhi hii, lakini kuna mtu anao, ngoja nimuwahi nimpe namba zako tusimwangaishe kuupeleka mpaka Ilala, mwambie dokta kua kabla ya kumpelekea gari utanishushia mzigi wangu.
Mshikaji: Usijalki mwanangu, ukiongea na mimi ndio ushaongea na Dokta, yeye simfati mpaka saa tisa., kwa hio nakuletea mzigo home au sio? Halafu mimi nawacha hii pale, nachukua ndinga yako nakufta kiwanjani, nikikufikisha hapa, naondoka na ndika ya Dokta wangu.

Mshikaji: mziki wangu vipi?
Mimi; Nikija tutaongea, sijaenda kabisa madukani nilikua nakaa nje ya mji huko.
Mshikaji; Najua wewe huwezi kuniangusha, tutaonana kiwanjani, mwambie huyoi Muunguja anipigie tu, asiwe na wasiwasi.

Nikampigia jamaa niletumiwa namba zake, akasema mzigo umefika na ninao kuna boksi mbili ndogo ndogo, nizilete wapi?

MImi; Wewe upo bandarini au ushaoondoka?
Jmaa; Nipo hapahapa ndio nilikua nangija tuwasiliane nitoke.
Mimi; Basi usihangaike, kuna mtu anakuja hapo sasa hivi, nakurushia namba yuake anaitwa mshikaji, utampa yeye huo mzigigo.

Jamaa; Sawa itakua voizuri kweli maana mimi nafanya kazi kwenye boti, akiwahi naondoka na boti hii hii.

Mimi; Atawahi na mimi namsisitiza kwa simu, mpigie.

Niakrusha namba.

Baada kama ya nusu 1 hoir hivi mshikaji kanipoigia.
Mshikaji: Mwangu, yule dokta anajulikana huku kuliko Mkapa, hivi tayari jamaa kuiona gari yake mpaka ndani nikafiungulkiwa, kishawapa habari wameniltea mzigo wake faster, na viboksi vyako viwili mimi ndio naondoka hivi una maagizo mengine?
Mimi: ahsante sina, usinigandishe tu airport.
Mshikaji; Sikugandishi mwanangu, mie nikija huko ndio mnazidi kunitia uchungu na mimi nilikwee pipa nende maulaya huko, nikirudi huku uzeeni nishastaafu huko.


Nikasubiri kidogom tatu kamili nikawa resepshen na kibegi changu, nikaona na kina Bi H washafika, na Meneja yuko pale.
Meneja akatupaza wadi wote watatu, akasema hii ya hoiteli kwa kua wateja wema. Ndnai ya voboksi hivi, nikaitia kwenye bag langu, Tukatoka, tukaingia kwenye gari.

Meneja: nakuja Dar huko, tutawasiliana lakini.

Mimi; Anytrime bro.

Tukaondoka, ile tunafika airport kama nne kasorobo namuona Swahiba yuko na kimfuko kidogo hivi. Kinamama walikiua na mabegi makubwa kama walihamia Zanzibar, wakamsalimi Swahiba kujuujuu wakaongozana na wabebaji mizigi, naona wale wametayarishwa na hoteli,

Swahiba; Simbamimi nimekuwahi na hii, bwana, hizi Barghashia za Kiunguja, moja hii kaitoam, inatoka kwangu, moja hii ya Sheikh, moja ilikua weite hivi moja ilikua broen nyuzi zake. Niachukua ya shwahiba kuijaribu imekaa swaswa, nikwambia hii siivui, hio ya Dheikh lete niiweke. nikaitia kwenye bag.

Tujaagana pale nikaingia ndani, nikaona nikangoje saa tano ya boiarding hukohuko ndani.

Nikaingia nikaenda moja kwa moja na boarding pass yangu mpaka chumba cha kupandia ndege, kuna mjahawa pale nikaenda nikaagiza kahawa, mara kidogo mijimama ikanipita pele, ikanambia tutaona andani ya ndege. Kumbee wenzangu wameenda VIP, wana connection hawa kina mama kiupita kiasi

Muda ulivifika tukaoingoizw andani ya ndege on time, nadani ya ndage hatukuchelewa kama dakaiika kumi au kumi na tano tukaruka, kina BH walikua wamekaa viti vingine, mabli kidogo namimi, VIP wao naona wanaingizwa mwanzo kuliko sisi.

Tukatua Dar tano na kama 3 hivi, yaani kama dakika 20 tu tupo airprt tunateremka, kutoka kina mama wakasema sisi tumefatwa na mafgatri, tukupe lift? Na mimi nikawaambia nimefatwa ahasanteni sana>

H1: halwa zetu vipi?

Mimi; Si tmeshamalizana uklisema zile nizitoe dsadaka msikitini?
H1; Kuna sadaka ikatolewa sadaka, wacha ujuba wako huko, nataka nizipate kama zilivyo, nazijui mpaka harufu yake, usinibadilishie.
Mimi: Poa msijali, leo hiui mgtazipata.

Mshikaji: Mwanangu hio miji anti nilifikiri inakuja na sisis vipi sasa imeondoka?
Mimi; Wana gari zao hao.
Mshkaji; Kumbe lile anti ndio limekupeleka Unguja, sasa hivi nippo kwenye amani.
Mimi: Anti gani hilo?

Mshokaji; Si yule wa Kariakoo, wifee wako anaenda kumyengezea komputa zake. Mama lina mkwanja hiloi, sasa hio ndio mimama yakujuana nayo Kariakoo, nijulishe nayo, mara tu kinanitunukua nahamia Kariakoo.
Mim: Tunaenda nyumbani moja kwa moja.
Mshikaji: Dingi kishanambia, yule dingi anajua movement zetu zote.
Mimi; Unataka kulijua lile mama?
Mshikaji si ndo manake mwanangu.
Mimi ; Ukija kuchukua gari ya Dokta nakupa mzigi wake umpelekee upo kwenye vile voiboksi, sasa ushindwe mwenyewe.
Mshikji: Hayo ndio mambo, mwanangu, huku Dokta, huku jimama la kunipelekea Dubai, wewe nijulishe nayo hii mijimama mwanagu kismati kinaweza kunodondokea.

Mimi: Sasa Mwanagu Mzee ansema umekua Sheikh siku hizi? Sasa mijimama ya nini?
Mshikaji: Wale nawataka kwa ajili ya koneksheni tu, lile mama kunituma Dybai nikamlete mababoibui sijui nini kama mchezo tu. Si mamaetu nyumbani sana sana kwa mtu alenituma kwa Shangazi yako, na lile linamkanda kazini kwao, sema yule mumewe hata kutabasamu hatabasamu, anatisha huyo.

Tukafika nyumbani tukashusha viboksi, nikawa watoto kila mmoja ananikimbilia, yule mdogo ananililia kabebwa na bibi yake, Mama yao nae kapoke kibegi changu kakipeleka ndani.

Mshikaji. Maza eeh, leo mie nakuja kupiga msosi hapa gari yangu hio ndogo naiacha hapa, yule mtu wenu wa usafi aipitishe pitishe kitambaa.

Mama: mwanangu umenunua gari hata hujanambia?

Mshikaji: maza hio ya wofe tobe, si ndio kama yangu tu?Kwabi huyu si gari ya mkewe hio anatutambia nayo>
Mama: haswaa mwanangu,, huyo woife to be wako muoanae baso sio mnamfanya machafu wewe umeshakiua Sheikh siku hizi.
Mshikaji: Unafikiri kanipendea nini> Kanipendea anajua mimi mtu wa mkeka, sio mchezo, lakini huyu mwnao anaiytilia kauzibe, akaitaka yeye nimuoe yule, kesho tu gtunaoaana.
Mimi: Sasa pira limenidondokea mimi, na mimi ndio nilikujulisha nae?
Mshikaji; Kunijulisha tu haitoshi, nipelekee na [posa kabisa.
Mama: Ssa umeshaongea nae mambo ya posa?
Mahikaji: bado maza, si huyu Simba ndio mshenga wangu aongee nae yeye, ndio nishampoa kazi hivyo, ananizingua.
Mma: Wewe mambi ya pisa huyu ayajue wapi? Kishapeleka posa ya nani, mambo hayo mwambie mzee.
Mshikaji; Hayo ndio maneno, umenipa bonge la wazo, halafu si unajua dingi, hana unaa kabisa na mimi?
Mimi: AlhamduliLlah, nakama imeniondokea.
Mshikaji; Niniii? Mimi dingi namwambia na wewe nakwambia. Usinizingue. Mza eeh, wacha mimi nika[umzike, nakuja baada ya kusali tu, najua timing zako za misosi.

Akaondoka na mimi nikaingia ndani, watoto hawataki kuniacha.

Mimi: Wewe hujaensda shuke leo?
No 1: dad mama hajanipelekea, kasema weee unakuja.
Mimi: Oooh, mdio ulikua unaningoja mama?
Wife: Shule basi kwenda kujipaka marangi na kuchafua nguo tu huko.
Dogo: art mama.
Wife: okay darling najua art, naiona art yako kwenye nguo. Zinapendeza.
Dpogo 1: Dad, red and white.
Mimi; Oooh Okay ndio color hizo? Na mimi unifundishe.
Dogo 1' Okay dad.

Huyu yupo pre KG, ile day care lakini mwanamke wa kigoa wa Tanga, hodari sana, kutwa uatawakuta wanacheza na rangi tu huko. Mwenyewe anasema hizi za watoto spesho ni edible, yaa hata wakizila hazina tatizo , kama pipi tu, nilishangaa wife alivyonambia mpaka madafatri yao edible. hawajui tu. wangeyamaiza yote.
Mimi; Ndio maana ana gharama dada yule kuliko chuo kikuu.
Wife; Aaaha jamani chuo kiukuu gani laki kwa mwezi wanakukla na kunhya hukohuko mpaka time yoyote ninayo kwenda kuwachukua.
Mimi' na hizo gharama za rangi na madaftari kila siku, mchezo?
Wife si wanatumia jamania jamani. Hya darling nenda kwa bibi dad anataka kupumzika kachoka safari, huku ananitazama, darling njaa inanoiuma.
Dogo 1; Maa namwambia mama akufanyie chakula, njaa inakuuma?
Wife: Mtumeeee, haoana mama usimwambie mwache ana kazi nyingi, mimi mwenyewe nitakuja wewe nenda, dada apumzike.

basi mambo yakawa hivyo mpka time ya kusali ikafika nikaenda kukoga nikaenda msikitini, nikamkuta mshikaji tayari zamani yupo masjid, tulivomaliza kusali tukaja kula.

Mama: hapa kuna viboksi viboksi ndani ya hili boksi moja, njoo u sort kabisa, na hili lingine lina embe ng'onggo zinanukia hizpo kubwa kubwa za kiungukaj mashi)okishoki.
Hilo lote letu, hivo vingine vyote vimeandikwa ku a vobosi nda vimeandikwa babu. kuna vinne vineandikwa H2 na H2 na ka vonginehivi Vimensikwa simba.

Nikamwambia hivyo vya simba vyote vya hapa kwetu, hivyo vya H1 na H2 tunampa Mshikaji akishak kula anawapelekea wenyewe wapo kariakoo, hivyo vilivyoandikwa babu vya babake mumeo. Atajua mwenyewe namna ya kuvisafirisha.

Ikawa tumemaliza mambo hya mizigo tukala pale na mshikaji nikampa vile viboksi.

Mshikaji; Maza hivyo vilivyobaki kuna vyangu hapo, usinishau.
Mama: Vipo baba wala sikushahau usitaharuki, wewe tena?
Mshikaji: hapo ndio tunapowiva chungu kimoja maza. Nipe hizo za babu pia dingi atanambia nizidondoshe wapi, nampigia. Akapewa na halwa za babu.


Simba.
...

Siku ikaenda mbio sana, usiku nikakutana na Simba na mzee Masjid, tukarudi wote nyumbani.

Mshikaj: Kazi zako zote nimekufanyia mwanangu nangoja posho tu ya leo nataka kuking'oa kwa Barafaa.

Mama; Khaa, hapa leo kuna kuku kuliko wa Barafaa.
Mshikaji; Maza hao niwekee tu, wife to be ana hamu ya kuku chipsi na juisi ya Barafaa.
Mama; mwenzetu hatusemi neno siku hizi, kwa hio unaenda nae kula kwa Barafaa?
Mshikaji; Katamani kuku wa Barafaa, mimi napiga kuku wangu kwa Barafaa, yeye namrushia wake kwa boda faster tu.
Mama; Sasa hujamuoa unamzoesha kumtumia kuku wa Barafaa, huyo atapika kweli mkisha oana?

Mzee; Hii habari mbona mimi sina jamani, kuna nini nafichwa hapa?
Wife; hata mimi nasikia kijujuu tu, ngoja niwawekee chakula, leo mama hapa kaja mwanae hatusemi, hao kuku sijui wamepikwaje, maana mimi jikoni nimeona mifupa tu.
Mshikaji; Maza eeh, niwekee wangu, mimi nachelewa, wacha niwahi si unajua saa hizi kwa Barafaa kunaweza kua na bonge la foleni.
Mama; Wala usiwe na shaka, utakuja leo au nikuwekee kesho?
Mshikaji; Maza eeh, nipe maarifa, mimi wife to be nilipopeleka gari lake kaniachia 50 akanambia nimnunulie kuku chipsi na Juisi za Barafaa na mimi nile wangu na zinazobaki zangu.

Mimi; Sasa si ungesema umeagizwa, unajidai kutamba tukafikiri mnakwenda kula kwa Barafaa.
Mshikaji; Oyaa, sikiliza mwanangu, eti Shem huyu wewe humuagizi kwa Barafaa misosi ukampa pesa zako?
Wife; Mara nyingi tu, tena sana.
Mshikaji; Sasa unaona mambo hayo, hawa wanawake wanaojijua hawategemei pesa zetu, wao wakikuagiza wanakupa feza yao wanakwambia keep change.

Mama; Basi mwanangu, wewe pesa zako usinunue kuku wa Barafaa, njoo ule hapa.
Mshikaji; Haiendi hivo Maza, nishamwambia poa mimi nitavunjika nusu kuku mayai mawili macho ya ng'ombe na juisi kama lita moja, wewe maza changu niwekee asubuhi mimi namuwai Dingi hapa hapa kesho tunatinga wote ofisini. Tena dingi eeh, ngoja niwai kwa Barafaa nikiwakuta hapa mtaniona tena, kama mmeshaingia ndani kupumzika In shaa Allah tutaonana asubuhi. Dingi kuna bonge aa kazi la gereji nimekupatia.
Mzee; kama hivo siingii ndani mpaka urudi.
Mshikaji; Poa faza, wacha niwahi narudi faster.

Akaondoka zake.

Kweli bi mkubwa leo kafanya uku sio wa kawaida, mama mtaalamu sana wa kupika, kuku bila mfupa lakini ukimuona utafikiri ana mifupa yake, kumbe yote kaitoa, ndani kajaza wali na nini sijui, mtamu ile mbaya, unakula tu.

Tukajipiga vizuri pale.

Wife; Mama hii ndio mimi hujanionesha, unafanyaje?

Mama; Mbona rahisi tu, si nawashona tu na utumbo wao wenyewe.
Wife; Mbona hauonekani?
Mama; Upo mwembamba umeshikana na nyama ukiutazama vizuri utajua.
Wife: Utanionesha, kesho.
Mama: Aaah, kesho sifanyi tena, siku nikifanya takujulisha mapema, wana kazi ile kuwatia mifupa yote.
Wife; Hio nitafanya mimi, wewe uje kunionesha kuwashona tu, halafu mengine yote niwachie mimi.
Mama; Sawa, basi wewe kesho tayarisha kila kitu mie takuonesha namna ya kushona nakuwachia jiko mwenyewe.
Wife; Hivo sawa. No problem manake mzee anawapenda kweli namna hii. Mimi napenda kuku awe na mifupa yake.

Ikawa story ndio hizo, mie na mzee tulipomaliza kula tukaenda kwenye kahawa uani, tukaanza kupiga kahawa yetu, kulikua na kashata za karanga.


Mzee; Simba nipe habari ya safari yako ya Unguja, ilipoanzia tulikua wote.

Nikaanza kumueleza mzee yote niliokumbana nayo Unguja, yeye haniingilii anachomekea neno moja moja tu.

Mzee; Mie hua namwambia mamako asiende kwenye hao vibuki, huko ni noti tu zinatembea hanisikii, watamuingiza tu.
Mimi: Hawawezi kabisa, wanawaogopa sana Simba, huyo si simba, wnamuheshimu, huyo hata mchango wake wakimualika wanamlipia wao, kama unabisha muulize.
Mzee; Hilo najua, halipi kitu.

Ile tunaongea ongea kidogo akaingia mshikaji.
Fazaa eeh; leo bwana manao wa kwanza hapa alinipa mzigo nimpelekee maza fulani huko kariakoo, nikampelekea, kufika huko si ndio akaniuliza kama mimi dereva na yeye anatafuta dereva ampe kazi pale kwake. Nikamwambia mimi naendesha lakini mimi ni dereva wa kutesti magari gereji, kuwatajia, anakujua wewe anamjua maza anamjua na mkewe bro hapa. Akakakumbuka, akasema jamani njooni mchukue na gari zangu mzi test huko kama kila kitu kiko sawa, maana anajua madereva wanaendesha tu, wanakustukizia kimekufa hiki kimekufa kile.
Mzee; Ana gari ngapi?
Mhikaji: Ana gari mbili zake za nyumbani, sijui gari gani, ana ki town ace kimoja cha mizigo na ana pickup moja double cabin, anasema hio ndio inatumika sana, ana shamba lake sijui wapi huko ndio anakwenda sana huko.

Mzee; sawa, akiwa tayari uwe unaleta moja moja tunalitest.
Mshikaji; Unajua Faza, mimi nishaanza kukurisi, nimwemwambia hivo hivo, akaniuliza bei ya kuja kutesti. Nikamwambia mimi hio hainihusu atakwambia mzeew mwenyewe, akanambia nikuulize, ndio nikasema kitu cha kwanza kesho nikuulize hicho.
Mzee; Simba tunafanyake sasa, mfahamishe Mshikaji wako.
Mimi: Elfu hamsini kama wengine, hakuna toifauti, hizo zinakua kuchukua kurudisha na kuiosha gari, kuifanyia test zote, za mechanical na electrical.
Mshikaji: Mbna kidogo sana, jimama lina hela kishenzi.

Mimi; Hatutoi bei kwa kumtazama ana nini au hana nini. Nyingi sana hizo.
Mshikaji; Dingi unasemaje, nimwambie hivyo asubuhi mie niamkie kule?
Mzee; Mwambie kesho, usiwe na haraka sana, kesho kuna gari ya wale wahindi, unaikumbuka ile ruiser?
Mshikaji; naikumbuka sana ile, ina nini?
Mzee; Haina lolote, tutajua kesho, imefika muda wake wa kufanyiwa service.
Mshikaji: Wale ndio hukuti hata siku moja gari imewazimikia njiani, inabidi mzee unifundishe hizi siku za kufanya service za wateja na mimi nizijue.

Mzee; Utamwambia Simba atakufahamisha. haya jamani, mimi nakwenda kupumzika, nilikua nangoja habari njema za Mshikaji tu.
Mshikaji; kwa hio dingi mimi niwahi mapema kule kwao?
Mzee; Usiende kabla ya saa mbili, hata ukiwahi wewe subiri mpaka ifike saa mbili, lakini usichelewe.
mshikaji; Poa faza, hakuna neno, mimi kesho baada ya kahawa tu hapa, naanzia kule kwao. Kwaherini.

Akaondoka na sisi tukaingia wote kupumika.

Siku a pili ikapita salama mambo ya kazi ya hapa na pale. siku ya tatu kimbembe kikaanza.

Kama saa tano asubuhi hivi Dokta kanipigia. Baada ya kusalimiana.

Dokta: Simba nilikua kuna vitu nataka kukuuliza lakini nikavipuuza, sema jana Mzee Ali yule wa Buguruni kanipigia simu anataka niende Pemba wakashughulikie vijini vya Kipemba, anasema ni muhimu sana tena sana, ili kuondoa kabisa tatizo langu. Mimi nikampigia Sheikh... Unguja, akasema nisiende bila wewe na yeye atakupigia, umeshaongea nae?
Mimi; Hajanipigia. Sasa mimi wa nini tena?
Dokta; Mimi naomba nije tuonane, maana sio hii safari gtu, mimi nilikua nataka kukuona kuna kitu kimenikaa moyoni, najua bila kukuuliza wewe mwenyewe uso kwa uso, hakiondoki.
Mimi; Mimi kuniona anytime baada ya kusali Isha, nipo free kabisa.
Dokta; leo basi nakuja, maana mzee Ali kanishikilia nende anasema siku hio moja tukiikosa itakua mpaka mwakani na siku yenyewe wiki ijayo.
Mimi; Unapajua hapa kwangu?
Dokta; Si ntakuja mpaka kwa Barafaa napajua halafu dereva wenu si anaweza kunifata pale?
Mimi: Tena faster na anavo kukubali, anaweza kukungoja kuanzia saa 12 jioni.
Dokta; Kanambia ananikubali sana, aache kusema tena, kwani domo zege yule?
Nikacheka sana. Nikamwambia poa basi, leo usiku atakuleta nyumbani, usiwe na shaka.

Saa hiohio nilipomaliza simu nikamwambia mzee kule kule kazini, mzee akanambia ongea na babu yako.

Mimi nikamfata Mshikaji, nikamwambia kabisa kuhusu usiku, asije akapanga mambo yake mengine, maana anakua complicated kweli saa zingine.

Mimi: mshikaji; Dokta kapiga simu anataka kuja nyumbani kumuona maza na wife wangu, kasema yeye anaweza kuja mpaka kwa Barafaa, utaweza kwenda kumchukua pale umlete nyumbani?
Mshikaji; Saa ngapi mwanangu?
Mimi; Atakua pale tukimaliza Isha tu.
Mshikaji; Basi poa mwanangu, mimi tasalia kule kule Isha leo, nikitoka tu buu baa.

Mimi; Poa Mwanangu.

Naona leo hakua na maneno mengi nikajua huyu ana kazi za Mzee, maana akiwa na kazi ya mzee na mama hata uwe na kazi ya pesa anakutolea nje.

Mkasa wa Unguja umeishia hapo, tukirudi tunarudi na kisa cha Kojani, Pemba na vijini vyao.
Simba.
 
Mkuu ukisema shirki unamaanisha nini?
Katika Uislamu, shirki inamaanisha kuhusisha kitu chochote au mtu mwingine pamoja na Mungu katika ibada au sifa za Mungu, au kuamini kwamba kuna mungu mwingine anayeweza kushirikishwa na Mungu katika mamlaka Yake.
Shirki inajumuisha mambo kama kuabudu sanamu, Mizimu ,Majini ama viumbe vingine au vitu vingine au kuamini kuwa kitu au mtu mwingine ana uwezo sawa na Mungu
 
Dawa gani ya kawaida kung'arisha nyota na kuondoa husda za binadamu....kuondoa chuma ulete?
Elimu ya kiza ina wajanja wamebuni mambo ya nyote kujipigia pesa kwa kua watu wameshayazowea mambo hya mijjiza miujiza na yaliojificha ficha.

Ingawa kuna elimu inayoitwa ya nyota lakini ukitaka kiundani elimu hio kisayansi ina aina mbili, moja ni astronomy na astrophysics na inayohusishwa na elimu ya utabiri inaitwa astrology.

Zote hizo elimu tatu watu wamejitahidi na kubobea sana lakini wote wanasema yasio na ukweli ni dhana tu(conjecture) tu.

Ukija hio ya ya kiroho, ya ramli za nyota vijini kishetani na watu wa kishetani vimetambua hilo na vinacheza na akili za binadamu kuendelea kuwapotosha kua ni elimu ya kweli.

Hasad ipo na ni mbaya kuliko uchawi, inabidi tujilinde sana na Hasad au kuhusidiwa sisi au sisi kuhusudu wengine.

Ndio maana katika Uislam tumefundshwa kusema Ma Shaa Allah, Tabaraka Allah na mengineyo tunapokisifu kitu. Ili isiwe kusifu kwetu ni husda. Husda ni kijicho au "ain" kwa Kiarabu au Kingereza wanasema "evil eye".

Kutibu husda ikikupata kupo aina nyingi na zote zinafanya kazi lakini kuu sala na kusoma aya mbili za mwisho za Qur'an. Pia bakora aliwahi kunambia majani ya mkomamanga unajifukisa nayo kwa kuyachoma. Mara moja tu.

Kuna njia nyingi sana za toka mababu na mababu nazo zinasaidia mradi tusiingize shirki tu.

Kijicho au zongo zote zinadondokea kwenye hasad.
Simba.
 
Wala halina idadi maalum,ni wewe tu na juhudi zako,kikubwa udumu kulitaja,unajua Allah anapenda ibada za kudumu hata kama unafanya kwa uchache,mfano hata kama kwa siku unamtukuza mara tano tu kwa kusema Subhanallah [umetakasika Allah] basi hakika anapenda sana

Hilo ni miongoni mwa majina 99 ya Allah,na Allah anasema hakika yeye ana.majina mazuri mazuri basi niombeni kwa kupitia majina hayo
Kweli
Wala halina idadi maalum,ni wewe tu na juhudi zako,kikubwa udumu kulitaja,unajua Allah anapenda ibada za kudumu hata kama unafanya kwa uchache,mfano hata kama kwa siku unamtukuza mara tano tu kwa kusema Subhanallah [umetakasika Allah] basi hakika anapenda sana

Hilo ni miongoni mwa majina 99 ya Allah,na Allah anasema hakika yeye ana.majina mazuri mazuri basi niombeni kwa kupitia majina hayo
Ni kweli... Lakini njia hyo ni ndefu Sana japo ikileta matokeo huwa ni ya hakika🤝
Wengi huishia njian!!
Mm nilipewa uradi kama unaosema hapo.... Kumtaja Mungu mara 22000 kwa siku, mwaka mzima🤝🤝🤝

Kivumbi chake nilikiona japo ukitia nia na jitihada utafunguliwa Siri ambazo wengine hawana, utapewa uwezo wa ajabu pia utakuwa karibu na Mungu pamoja na mitume wake direct


Lkn nahakika vitakushinda maana kwenye watu 1000 hapo anayetoboa n mmoja tu🚶🚶
Tena unatakiwa usiwe na kazi, ukae sehem moja usiwe mtu wa kutembea ovyo (unavuta urad mpk mikono inatoa sugu😶😶

Masufi achana nao wewe!!!!

Sikatishi tamaa ila naongea ukweli wa mambo kwa uelewa wangu
 
Kweli

Ni kweli... Lakini njia hyo ni ndefu Sana japo ikileta matokeo huwa ni ya hakika🤝
Wengi huishia njian!!
Mm nilipewa uradi kama unaosema hapo.... Kumtaja Mungu mara 22000 kwa siku, mwaka mzima🤝🤝🤝

Kivumbi chake nilikiona japo ukitia nia na jitihada utafunguliwa Siri ambazo wengine hawana, utapewa uwezo wa ajabu pia utakuwa karibu na Mungu pamoja na mitume wake direct


Lkn nahakika vitakushinda maana kwenye watu 1000 hapo anayetoboa n mmoja tu🚶🚶
Tena unatakiwa usiwe na kazi, ukae sehem moja usiwe mtu wa kutembea ovyo (unavuta urad mpk mikono inatoa sugu😶😶

Masufi achana nao wewe!!!!

Sikatishi tamaa ila naongea ukweli wa mambo kwa uelewa wangu
Allah mwenyewe anasema katika quran tumtaje sana inaonekana kuna siri katika kumtaja Allah, Masiala ya nyiradi yana siri sana ila kikubwa mtu unapokuwa unafanya hizi nyiradi jitahidi usiache uwe ni utaratubu wako wa kila siku ukifanya hivyo utaona matokeo ata ndani ya mwezi ila kikubwa zaidi ni kujiepusha na madhambi kwani uchamungu hauji kwa kufanya mema tu bali kwa kufanya mema na kuacha madhambi.
 
Majina hayo siyajui ingawa arsis alisemq hapa kuwa hayo majina ni shirki,so kama ndio hivyo basi si miongoni mwa majina hayo

Majina ya Allah ni sifa miongoni mwa sifa zake,mfano ya rahman (mwenye kurehemu) kwahiyo unapoomba rehma kwa Allah kisha unatàja na jina hilo,ya razaq (mwenye kuruzuku au mtoaji wa riziki) kwahiyo unapoomba riziki toka kwa Allah kisha unasindikiza na kutaja jina hilo,ya ghafur (mwenye kusamehe waja wake) unapoomba msamaha/maghfira unataja na jina hilo mara kadhaa

Kwahiyo majina ya Allah yanataja sifa zake,mengine unataja kwa idadi maalumu kama unashida ya watoto,au hali ya riziki kama ni mtihani na mambo kama hayo
Nawaombeni na nawasisitiza ndugu zangu, msifanye maamuzi kwa kua mimi au Arsis kasema, fanyeni tafiti zenu. Na inawezekana hata kunitaka ushahidi kwa ninayoyasema, msikubali kijuujuu tu.

Leo nimechungulia uzi mmoja huko kwengine nikaona neno ninalolisema hapa limeletwa kwa Kingereza chake "Education is evidence based knowledge", mambo ya FaizaFoxy hayo, nakubaliana nae mia kwa mia.
Simba.
 
Allah mwenyewe anasema katika quran tumtaje sana inaonekana kuna siri katika kumtaja Allah, Masiala ya nyiradi yana siri sana ila kikubwa mtu unapokuwa unafanya hizi nyiradi jitahidi usiache uwe ni utaratubu wako wa kila siku ukifanya hivyo utaona matokeo ata ndani ya mwezi ila kikubwa zaidi ni kujiepusha na madhambi kwani uchamungu hauji kwa kufanya mema tu bali kwa kufanya mema na kuacha madhambi.
Katizame video ya SHEKH YUSUPH KIDAGO..... Andika hivi 👉Watu wa dhikr / daruwesh ni mtu wa aina gani

Utajifunza mengi kuhusu daraja na athari za kumtaja Mungu🤝

Note: Shekh huyo ni Murshid wangu (kwahyo ukisikia nataja taja mwalim kasema mwalimu kasema, mengi yametoka kwenye bloodline ya elim yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom