Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Ingia tu YouTube kaka.... Mimi nimejifunzia mtandaoni (nilianza na yoga then meditation then lucid dreaming mwisho nikajikuta nimedondokea kwenye astro projection 🤝
Kasome huko Kuna waalim wazuri Sana (utapata faida zake na hasara pia kabla hujaanza practical
Aisee mna hatari, ndo hiyo unatoka nje ya mwili??
Ulipata faida gani?
 
Itakua ulitumia mbinu za watu wanaodhani tu ipo hivi. Sijui ulifundishwa na nani au ulipitia stages zipi?
Simba.
Hii nilisoma mwenyew mtandaoni... Nikafanya Kama kujaribu tu🤝
Nikipata moyo baada ya training za Lucid dreaming kuwa really nikaona sio mbaya kutest na Astro projection maana waliisifia sana
 
Mimi sikufanikiwa, ila kila mtu huwa na sababu zake kutaka kufanya hvyo...... Kwa kipindi hicho mimi nilikuwa Natamani Sana kujua Siri za ulimwengu wa kiroho🤝

Nilitaka niwaone guardian angel, 😃😃n.k,,,,
Ohoo jamaa zangu huwa wanajaribu na kurudi na shuhuda kama zako za kushindwa ..

Ati ukifanikiwa kuna probability ya kutorudi ukikosea vijikanuni?
 
Yap inasemekana hvyo..... Kuna link baina ya nafsi na mwili wako ambayo Kuna mazingira yakitokea ikawa disconnected basi ile nafsi ilotoka inakosa namna ya kurudi kwenye mwili hvyo ndo huku Duniani unakuwa umekufa🤝🤝
(Wanadai hvyo wenye elim zao... Wengine maamuma tu
Hayo mambo ya kutest kifo sio kabisa
 
Hii ndo elim gani madam.... Nipe mwanga kidogo nikaifanyie kazi, ntaleta mrejesho hapa
Sufi
Na mimi ni simba vilevile.... Utani ndugu yangu nimeku tag wewe

Tuendeleee na mjadala tuliokuwa tunaendelea nao.

Asante
Simba wapo wengi duniani. Kawaida sana.

Binafsi nimeachana na mila na tamaduni za Kisimba lakini siwezi wala sitajaribu kuukimbia ukoo wa Kisimba.
Uzuri wa Simba wanaheshimu sana uhuru wa mtu, hawakuingilii kama huwaingilii mambo yao. Simba wanaamini Mungu.
Simba.
 
Sijawahi,mwaga elimu tujifunze
Tena ni wepesi sana, kwa watu wa Tariqa za Qadiriya, nafahamu Tanzania wapo wengi. Qadiriya hilo ni tawi mojawapo la Masufi, wengi wanaamini daraja ya kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida inafikiwa na Masheikh wao tu.

Binafsi Waislam wote kwangu ni Waislam sina Tariqa wala dhehebu bali dhehebu langu ni Uislam tu. naheshimu madhehebu na Tariqa zote. Nikiingia msikiti wa Ibadhi, Imamu hafungi mikononi akisalisha na mimi sifungi mkono, nikiingia msikiti Imam anayesalisha anafunga mikono na mimi nafunga.

Ili kuupata usufi kamili wanaamini kuna siri zake, mimi naamini siri ni Tahajudi, Nyiradi na kua na uvumilivu na ustahamilivu wa mazoezi ya kimwili na kiroho.

Kuufikia usufi, ni lazima usali sala tano zisikupite, halafu Aanza kwa sala za usiku, mpaka zikuzowee (uvumilivu na ustahamilivu).
Simba.
 
Ya nini yote hii?
Swali zuri sana hili.

Babu yangu alikua anasisitiza sana hili, kila kitu lazima kiwe na lengo na matukio tarajiwa, ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Tusifanye kitu kwa kua fulani anafanya tu, bila kujua malengo na matarajio yako binafsi kwa kukifanya.

Nasubiri majibu ya alieulizwa.
Simba.
 
Sheikh Mittoga una haraka sana, mambo yanaendelea.
Simba.
Ninachokusifu Arsis, umetulia sana.
Una busara na maarifa fulani ya hao viumbe wasio onekana.

Ila inaonesha una uwezo wa kupiga ramli na kuagua kupitia msaada wa hao viumbe wengine.
Je huoni kuwa una Fanya vitendo vya shirki ?
Yaani unategemea msaada wa hao viumbe eg. Majini katika kutatua shida za watu.
Hili limekaaje Simba.
 
Tena ni wepesi sana, kwa watu wa Tariqa za Qadiriya, nafahamu Tanzania wapo wengi. Qadiriya hilo ni tawi mojawapo la Masufi, wengi wanaamini daraja ya kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida inafikiwa na Masheikh wao tu.

Binafsi Waislam wote kwangu ni Waislam sina Tariqa wala dhehebu bali dhehebu langu ni Uislam tu. naheshimu madhehebu na Tariqa zote. Nikiingia msikiti wa Ibadhi, Imamu hafungi mikononi akisalisha na mimi sifungi mkono, nikiingia msikiti Imam anayesalisha anafunga mikono na mimi nafunga.

Ili kuupata usufi kamili wanaamini kuna siri zake, mimi naamini siri ni Tahajudi, Nyiradi na kua na uvumilivu na ustahamilivu wa mazoezi ya kimwili na kiroho.

Kuufikia usufi, ni lazima usali sala tano zisikupite, halafu Aanza kwa sala za usiku, mpaka zikuzowee (uvumilivu na ustahamilivu).
Simba.
Hapa ndo natambua vyema.... Kumbe mimi pia nimelelewa kiroho na hao watu, (masufi)

Balaa lao sio la kawaida, watu wa zuhud hao.... Japo niliwakimbia!!!

Mambo ya kupewa nyirad asubuh mpk saa 6 usiku ndo umalize nikashindwa🤐

Kuna huyo mwalim wangu kadum na uradi flan kwanzia 1985 mpk leo
 
Hapa ndo natambua vyema.... Kumbe mimi pia nimelelewa kiroho na hao watu, (masufi)

Balaa lao sio la kawaida, watu wa zuhud hao.... Japo niliwakimbia!!!

Mambo ya kupewa nyirad asubuh mpk saa 6 usiku ndo umalize nikashindwa🤐

Kuna huyo mwalim wangu kadum na uradi flan kwanzia 1985 mpk leo
Masufi mapaka ukiwaona utawaona kama wehu fulani kwa kushika kwao uradi.

Mimi nahisi wengi wao wanachukulia sivyo hayo mafundisho ya Kisusufi. Kina chotakiwa ni kua na yakini na kuuzowesha mwili na roho kwa jambo fulani. Mfano unafanya uradi kila siku saa 10 mpaka 11 alfajiri. Basi iwe ndio zoezi lako mpaka ufikie lengo lako, sio kua na uradi mchana kutwa usiku kucha, Utawehuka.

Huo ndio msingi wa kwanza, sala tano zisikupite na yanayofatia hapo ni hayo mazoezi mengine.
Simba.
 
Ninachokusifu Arsis, umetulia sana.
Una busara na maarifa fulani ya hao viumbe wasio onekana.

Ila inaonesha una uwezo wa kupiga ramli na kuagua kupitia msaada wa hao viumbe wengine.
Je huoni kuwa una Fanya vitendo vya shirki ?
Yaani unategemea msaada wa hao viumbe eg. Majini katika kutatua shida za watu.
Hili limekaaje Simba.
Uzuri ni kua sifanyi ramli na hata hawa viumbe hawafanyi ramli.

Arsis anasema anayajua yaliopita hayajui yajayo kasoro yale ualiopo kwenye vitabu vyake.

Arsis anasema vitabu vya Mwenyezi Mungu ni viwili tu, Tawrat ambayo sasa haipo, imefichwa na Qur'an. Basi.

Kujuana na na viumbe hawa na kushirikiana nao sio Shirk. Shirk ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

Si ushawai kusikia watu wanaitwa ma "genius"? Hio genius maana yake nini? Kwa ufupi ni msaada kutoka kwa wasioonekana.
Simba.
 
Na waarabu na wazungu walikatiana waumini kama siagi sio?
Hao wazungu mbona wapo wa dini zote na wengine wao hawana dini kabisa, tena sasa makundi kwa makundi wanarudi kwenye Uislam.

Waarabu wapo wa dini zote, kuna dini zingine zipo kwao tu, hazijafika kwetu wala Ulaya. Sema wengi wao wameiyona nuru ya Uislam kama sasa inavyotapakaa dunia nzima.

Uislam haumlazimishi kipofu kutazama, humsafisha moyo wake uione nuru kabla ya macho yake.
Kama huioni nuru ya Uislam elewa kuwa upo kizani.
 
Inatokea post namba 299.


Baada ya kihadithiwa hayo na Arsis nikawa na hamu kubwa sana ya kumsikia babu yangu tanieleza nini kuhusu tukio hilo lililowakutanisha na Arsis. Nikaweka nia ya kufunga safari kwenda Duga kwa babu.

Ikapita muda, ikawa kuna msimu mdogo wa Kamba, nikamwambia wife kuhusu kwenda kwa babu, akanambia kule neda tu mume wangu, mzee si anakwenda fatana nae. Nikamwabia ndio nilikua namtaimu niende nae. Mke wangu akaniuliza umeshambia, si unajua mzee? Anawez kuondoka akapiga simu yuko Tanga. Nikaona ni kweli, nikampigia simu mzee muda huo huo.

Mzee akanambia msimu haukai,nilikua nafikiria leo niende. Nikamwabia mzee muda sassa hivi umekwenda, na mimi nataka kwenda twende wote Alfajiri, akanambia itakua vizuri nimepata kampani. Mke wangu akanambia si umeona usingemwabia asubuhi unemsikia kwenye bomba tu, msimu akae hapa, kwani ana wazimu?

Nikamuuliza mke wangu, kwanini wewe na mama hampendi kwenda msimu wa kamaba na kuna pesa za nje nje? Mke wangu akanambia tatizo, kutwa nyie mnavuna kamba, watu wote wanavuna kamba, tunalua pekeetu nyumbani, mpaka jioni aa zingne mpaka usiku. Nikamwabia twende tutakua tunakwennda kuvuna woite kamba. Akagoima kabisa, akasema wewe kawele tu mimi nitakupikia, kwenda kuchomwa chomwa na ile miba yao, sikuwezi kabisa.

Tukaondoka na mzee, kama kawaoida kituo chake cha kwanza Chalinze, tukamkuta Halima, na mimi kishanizowea sana lakini hajawahi kuniona na mzee pamoja. Alivyoniona nae siku hio, akaanza.

Halima; Nilijua tu utakuja nae, ingawa jana hukunambia kwenye simu, ulijifanya kama unapita peke yako. kahawa nishakuwekea kwenye chupa, hii kunyweni hapa. Handsome na wewe kopo lako la visheti lipo tayari;
Mzee; na mimi visheti vyangu vipo tayri, unakumbuka nilikuagiza jana?
Halima; Vipo, nikusahau wewe tena?
Mzee tuna haraka leo, toa tuondoke.
Halima; handsome usinisahau kamba, wale sijui bibi yako anawakausha vipi, si ulinambia unakaushiwa na bibi yako? maana mimi nilikua najua uduvi tu wa kukausha kumbe hata wale wakubwa bibi yako anawakausha. baba yako kupita kote hapa huwa ananipa kamba wabichi tu.
Mimi: Wale huwa sio mzigo wake ule, wale bibi anawapack anpelekewa mama nyumbani. Mimi nilimwabia aniwekee pembeni wangu, tofauti na wa nyumbani, ndio maana safari iliopita ukawapata.
Halima akatoa visheti vyetu akatupa, tukaondoka zetu.

Tanga hatukukaa, mzee akapita kwa bibi yangu mzaa mama, tukawasalimia alikua na mizogo yao, mimi nikampa noti mbili tatu, akafurahi, dua nyingi, tukaondoka zetu.


Tukafika Duga mapema tu. Tukamkuta babu yupo bize na wateja wake, anawauzia kamba kwa mizani, walikua wanapima kamba kwake. Wengi wengi tu. baada ya kusalimiana, mzee akasema mimi nashuka nakwenda kuvuna huko, akachukua vina pale, anakingia stoo akachukua nyavu zake za mkono, akashuka chini huko. Mimisafari yangu ilikua kwa babu na bibi tu, sikua kabisa kwenye mpango wa kuuza kamba.

Mimi; Babu huu, mguu wako huu, sio wa kamba.
Babu; Sema bwana mkubwa.
Mimi; Sio saa hizi tukisha sali usiku, nataka kuongea na wewe peke yako.
Babu; aknambia sawa bwna mkuba, tutaongea usiwe na shaka.
a
Nikamtafuta bibi nikampata yupo bize kweli kweli na kamba, Baada ya kusalimiana akanambia...
Bibi; Mie toka asubuhi nipo mavunoni huko, tunahofia bamvua, likija linaondoka nao wote.
Mimi; mnalitegemea mapema safari hii?
Bibi; ndio wakati wake huu, maji yashaanza kupanda b, , aharini, lakini tumewahi kuvuna wengi tu, si unajua huu msimu mdogo.

Bibi huyo akachomoka huku ananambia, chakula chenu kipo nenda ukale, babu yako kishakula, babako yuko chini huko, usimngoje kula, anavuna.

Basi ikawa mambo ndio hayo ya shamba. Nikaingia kula mimi, kama kawaida, bibi chakula chake kitamu, anajua kupika.


Usiku baada ya kusali, babu akanitazama akanambi twebda hapo nje babu, kahawa tutainywea nje. Tukatoka, akanambia babu maongezi maerefu au mafupi? maana kama maregfu kidogo twende pale kilingeni, haji mtu, hapa sasa hivi watajazana. Nikamwabia tushule pale babu. Tukashuka kilingeni kwake.

Babu; kwanza nipe habari za mjini.
Mimi; Kwema babu, mjini wewe unayajua mambo yake kuliko mimi, labda unipe wewe mambo ya mjini.

Babu akacheka, unaendeleaje na kazi zako?
Mimi: Babu siku hizi nazimudu sana, hata mzee akiondoka sina wasi wasi kazini, nafanya mwenyewe kazi zote.
Babu: Vizuri sana, haya nambie babu.
Mimi: babu mimi sina mengi sana, mimi nina maswali mawili matatu, kuhusu wewe na rafiki yako Arsis.
babu akacheka sana.
Babu; Kakwambia uniulize mimi? Yule kuna swali linamshinda kujibu?
Mimi: Sio hivyo babu, mimi nilimuuliza mlivyofahamiana, akanielezea kwa upande wake, sasa nataka kujua kwa upoande wako.
Babu: Sawa bwana mkibwa ulia unachotaka kujua maana kisa ni kirefu sana.
Mimi: babu, nataka unieleze ulipoivunja chupa pngoni uliona nini?


Babu: mambo makubwa sana bwana mkubwa, kwani Ramsis hajakwambia?
Mimi; Kanambia yake mimi nataka kusikia yako.


Uzuri wa babu alikua ana namna fulani ya kuongea amabyo hutaki awache kuongea, hajui kukasirishwa na swali.

Babu; Siku ile Bwana mkubwa, niliona mabo ambayo nao,mba nisiyaone tena na namshukuru Menyezi Mungu kunitoa uoga, maana nikiyakumbuka huwa naogopa mpaka leo. Babu nilipewwa kisu kikali halafu kigumu hicho, niliambiwa hicho hara chuma naweza kukatia kwa kukigonga na hakiweki meno. Kipo hicho kisu mpaka leo, sina pa kukitumia, kili[potea siku ile lakini huyu Ramsis kupitia Jini Bakra wakajulisha kiko wapi, Jini Bakora akaniletea.

Babu; Hicho kisu nilipewa kazi yake ilikua moja tu, kukata seal ya chupa, ilikua inaonesha ni ngumu kweli lakini kile kisu kiliikata mpaka mimi nikawa naona raha. babu mambo yalilkua kabla sijaikata hio lakiri, babu kma umewahi kuwaona ma dragon wale wanatoa moto kinywani, basi walikua watatu mmoja wa kijani kulia ya chupa mkubwa ajabu, kafungua mdomo unatia moto, moto sauiti yake inatisha unafika mpaka karibu ya chupa, kulia ya chupa kuna mnyama mbwa si mbwa mkubwa kuliko simba, ana miguu sita na yeye anatoa moto mdomoni. Juu ya chupaa kuna joka lina vichwa vitatu, joka kubwa kweli linaning'ginia saw nachupa, kidogo nikimbie, ikanijia sauti huku nasoma Qur'an inanambia wahi fanya kilichokuleta hawana ujanja mbele ya Qur'an, basi babu nikaibeba, nikafanya kama naichinja ile chupa, ikakatika lakini na mfuniko wake, sikuona kilixhotaka, wale wanyama sasa wananikaribia mimi kila upande, kuna mawe nilipewa ndio ya kuivunjia ile chupa, nikaivunja nikaitupia kwenye moto, babu kulikua na moto mpaka mimi ulikuwa unaniwivisha naona ule moto ndio salama yangu pia ile midudu ilikua hainifikii, maana kila ikinisogelea ule moto kama unapanda kuwachoma, moto wao hakufua dafu, walikua wakubwa sana babu. Baada kuitupa ile chupa na kisu kikawa kimeniponyoka na chenyewe kikaingia kwenye moto. Nikarushwa huko babu sijui na nini, bahati sijapigizwa kwenye pango, nimeangukia chini kama futi kumi kutoka ule moto, kuna kichanga pale, si unalijua lile pango kichanga chake, nikafikia hapo.

Muda wote huo sikuacha kusoma Qur'an. Kuna Jini moja tulikua nalo pale, limejigeuza kama Mzee mmoja alikua Sheikh Wakigunya, alikuwa maarufu sana huyo mzee kwa elimu, Mwenyemungu amrehemu, hajakaa sana baada ya ile kazi, akatangulia mbele ya haki, wanawe wapo Tanga, wengine wametawanyika. Tunajuana sana, lakini hicho kisa sidhani kama wanakijua maana babu hii ilikua siri kubwa, wewe ingekua Ranses hajakuhadithia mimi nisingekuelezea, ulivyonambia, kakuhadithia nikapata na meseji, ndio nafunguka babu. Hakuna ajuae hicho kisa mpaka leo hii, ni mimi, wewe sasa Bwana mkubwa, jini bakora na Ramses. kama wengine wanajua anajua Mwenyezi Mungu babu.


Babu yangu alikua anamwita Ramses, kuna siku nilimuuliza, mbona mimi najua anaitwa Arsis, kwanini Babu unamwita Ramses? Babu akanambia, ndio hao hao babu. Haina shida.

Mimi; babu ikawaje baada ya hapo?
Babu; twende tukale kwanza babu, tutaongea tukisha kula, babako na watu pengine wanatungoja sisi kula.


Itaendelea.
Aisee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom