Hapa ndio vitimbi ambavyo na ujanja wangu wote wa Usimba sikuvitegemea. Yaani H1 akaanza...
H1; Bora Meneja alivyoondoka maana nilikua nahamu ya bangi, nyie Waunguja kama mnaogopana shauri lenu.
akatoa ganja kwenye handbag lake akawasha atakatoa zingine mbili akaweka juu ya mezo.
H1: Haya jiripueni wenyewe, mlikua mnamuogopa Meneja. Na wewe Simba hebu ongea na huyu nduguyo Meneja, saa zote yupo tense tu. Naona ukiwepo wewe ndio kidogo ana relax.
Mimi; Labda mumemtisha?
Sh; kwani vituko vidogo wamemfanyia, hii mijimama ya Dar haifai kabisa. Wanamtia ushawishi na T.
H 2: Atiwe ushawishi na nani huyu T? Huyu anayajua mambo kuliko sisi, huyu dijitali, sisi analogi, unaona vile hajaolewa tu ndio unamuona mtoto sana asieyajua mambo?
Sh; Mwacheni T wangu jamani, juzi mmemsukumia Meneja, si bahati ,mngemsukumia jitu la hovyo hovyo si angefanywa kachumbari huyu?
H1; Unajuaje walichofanyana?
T; jamani mimi nimelala sijijui, na kama amenifanya kitu si ningejua nilipoamka? Huyo gentleman. msimtie dosari mwana wa watu jamani. Yeye kazi tu, utafikiri wote sisi hatuna kazi, mpaka anakera.
H1; Angekupagaza nao usingeona anakera, shwaini. Lala na simba au mwamba hapa uone kama hujafanywa samaki.
Mimi: Mimi ndio hata kulala nae nymba moja nisingelala nae, wanasema baina ya mwanamke na mwanamme ni shetani. Nigelala hata beach.
H1; Mnhhh, huyu anaejidai sie kumbe ndie. Simba mwenda kimya huyu. Wachezeeni na hawa basi kama hawajawa firimba hapahapa.
H2; Alieanzisha kumchezea Meneja si wewe, sisi tumeunganisha tu.
Wakati tunaongea, tukasikia hodi hodi kwa mbaili, kutazama chini kidogo ni yule Dada wa Kikenya anaekaa kaa resepshen kwa nje.
Mimi; Karibu dada Martha.
H1: hata majina ushawajua halafu unajidai ungelala beach, mtazame macho yake. Kama wewe mwema sana kingekushinda nini kujizuia hata ulale beach?
Mimi:; Si majina yao yapo kifuani wote, wanabeji za kushona zina nembo ya hoteli na majina yao.
Martha;Mr. Simba, nimetumwa hii note na Meneja. Martha akanipa kikaratasi.
H1: Si unaoana wanaongea kwa vi note.
Nikampa ki note yeye H1, kisome hiki, meneja kafanya heshima sio kumtangazia kila mtu.
H1; Sh Kisome mwenyewe chako hiki akampa kile kinote bi Sh.
SH; Ningeshangaa.
T; Nini tena Sh?
Sh; Mume wangu kaja ndio nimeitwa niende.
H1; Haya katoe upwiru mwanetu, ukihitaji msaada tuko hapa.
Sh; msaada wa nini? Wewe nakuachia mwamba na simba hapo, ushindwe mwenyewe. We binti ningoje twende wote.
Sh akaingia ndani kuchukua handbag lake naona kaingia na msalani maana kachelewa kama dakika kumi au zaidi ndio katoka.
H1: Nyoo, umeenda kuiosha, unajua kaja na .... mkononi.
Sh; T Nipeleke basi.
T; Ngoja na mimi nniingie ndani kidogo.
T hajachelewa kama dakika tano katoka. Wakaondoka na Sh na Martha. Tukabaki mimi, Swahiba na mijimama ya Dar.
H1; sasa nyie jamaa zenu wa Kiunguja washaondoka, pigeni ganja, pigeni whiski tunyanduane. Tena mie wangu hyu Mwamba wa Kiunguja. Nimuwahi kabla hawajaoana na T.
Mimi: Duh na harusi tayari?
H1; Wewe ishara huzioni, humuoni T alivyotulizana, kuja mwamba hapa, hata glass ya wine hajainyanyua kupeleka mdomoni, amkose mtoto wa Sheikh? Swahiba ikamtoka...
Swahiba: T mzuri kweli, tena toka mdogo namwania kweli lakini...
H1; Lakini nini? Usimtie walakin mtoto wa watu.
Swahiba; Sio hivo, huyo ana mashetani ya kibuki, siyawezi mimi.
H1; Bora Sh alivokua hayupo, maana huyo yakitajwa tu yanapanda.
H2; Huyo sio yanapanda, tuko nayo hapa muda wote, saa zingine anaekunywa hapa wala sio yeye ni vibuki. Hamumuoni anakunywa kuliko sisi wote halafu halewi?
H1 kweli nilikua sijalitazama hilo.
Mimi; Kwani mashetani ya kibuki yanalewa?
H1: Muulize huyu swahiba yako alielianzisha.
Mimi;Swahiba lete habari zao.
Swahiba; Simba, mimi sina ujuzi nao zaidi ya kusikia tu. Tunasikia vibuki bila whisky hawapandi na ni watu wenye fedha ndio wanawaweza maana shughuli zao nasikia michango yake kwa mamilioni.
H1; Enhee, endelea na sisi tuyajue.
Swahiba; Msije mkapandisha vibuki hapa, si ndio nyinyi watu wa vibuki.
Mimi; Haya jamani, tuache hayo tuendelee mengine. Hakuna raha kama kuogelea baharini saa hizi, hakuna jua. Twendeni tukaogelee.
Swahiba: Simba, huku hapafai kabisa kuongelea si mchana si usiku.
Mimi; Kwanini?
Swahiba: Hii bahari ya huku sisi toka wadogo tunaambiwa tusije kuogelea wala picnic, kuna vibwengo kibao huku.
Mimi: Ndio ni hivo?
Swahiba: Simba wewe umesema tuyaache haya mambo, wewe unayajua zaidi yangu, mie na uhakika huo. Tuyaache tu.
Mimi; haya tuongee biashara sasa.
Swahiba; Unajua dunia ndogo sana, kweli milima haikutani binadam wanakutana. Hivi Bi H1, wewe ndio pale kwa Bin Sulum juu unaeuza laptops?
H1; Ndio mimi huamini?
Swahiba: Unajua mimi nishanunua sana laptop, tukikua hatukosi pesa za matumizi, tunanunua, yule dada dukani, antwambia chagueni hapo kwenye hilo boksi yupo snmart huyo hatoi boksi lingine mpaka lile liishe, mtachagua wee mwisho mtaria zilezile mlizoweka pembeni, lakini mali ya Ulaya ni ya Ulaya tu, zipo bomba sana zile. Tmeziuza sana baada ya kutoa software labda na mtu mwenyewe akitaka anaongeza memory kidogo au harddisk ndigo tunamwekea kubwa. dah Bi H; Uliyanya maisha yetu kua mepesi sana Dar. Nikupe siri?
H1; Mwaga tu siri leo tuzijue.
Swahiba: Unajua DIT nzima kila mwanafunziw akawa anatumia laptop zako, wanafunzi wengi, karibia wote wamekuja kusoma pale hawana laptop kabisa na masomo ya komputa utasomaje? Lab ya chuo ilikua na komputa desktop kumi sijui, hazitoshi kabisa, mpaka ilikua watu wanahonga kupata nafasi kwa msimamizi wa lab. Dah, wewe ukawa muokozi wetu.
Sema siku za mwanzo wale vijana walioanza kupajua kwako waliwagonga bei watu. Halafu kuna walimu wajinga wakataka kuzuia kila mwanafunzi kua na laptop yake, eti kwa kua wao hawana. Ujinga mtupu. Tukafanya mgomo baridi mpaka waziri mdogo wa elimu akaja pale, pale kuna watu wa usalama kibao, walipelka habari faster, alipokuja naibu waziri ndio ikawa ruksa mtu aje na laptop hata kumi, na walimu wote wakapewa laptops mpya mpya za kutoka maduka ya wahindi huko.
H2; Sasa wizarani kwani wajinga, si wameshaona wajipigie kamisheni zao.
Swahiba; Tena wameletewa mabomu afadhali ya zetu za used. Unajua komputa kila unavyoitumia ndio inakua bora zaidi.
Mimi; Hilo wife wangu kawahi kunambia, yeye alikua anakuja kufundisha part time mambo ya software pale DIT.
H1: Wewe isiwe mkeo ni Nisha?
Mimi; Ndio yeye huyo.
H1; Kumbe wewe ndio Risha?
Mimi; Ndio.
H1; kweli dunia ndogo, kile ndio kifaa kinachotegewa kwa software Tanzania nzima kama ulikua hujui. Mpaka kesho. Yule ikiwashinda wote hawa software au hawajui software gani kwa kazi ipi, pale ndipo mwisho wa matatizo. n-Namjua sana tena sana. Sasa kifaa cha Kitanga kile kwanini hukuja nacho huku?
Mimi: kakataa mwenyewe, ana kazi na kule sasa hivi ana hizo kazi za masoftware zimemshika shati.
H1; Mimi nawajua basi mpaka mamako na babako, kumbeeeee. halafu hautujui vibuki na mishetani yenu ya Kisimba ya kidigo huko? mamako mbona kila mtu anamjua, yule mwanamke wa shoka, si mchezo. Mlitufanyia vituko nyinyi harusi yenu, sijui mpoje wa Tanga, ukaenea uzushi Dar nzima.
Mimi; Upi tena huo?
H1; Si mlivumishwa mmeoana mtu na dadake.
H2; Kumbe ndio huyu? Eeeh ilikuaje.
H
1; Watanga hawa bwana, walilelewa pamoja tu kama ndugu lakini ni watoto wa mjomba na shangazi. Watu wazushi tu.
Mimi; Kweli lakini, sio watu tu, hata kwangu ilikua ngumu sana. Mimi miaka yote najua yule dadangu kabisa, nimeambiwa kabla ya harusi tu. Yule mke wangu ni mtoto wa Shangazi yangu.
H1: Unamjua mamake mzazi wewe H2.
H2; nani?
H1; Si yule Mwana... alikua katibu mkuu wizara ya ...
H2: ndio namjua sana, akiwepo Dar sherehe zetu hakosi, hata za kibuki anakuja lakini yeye hana kibuki yule.
H1: hawa si simba, wanajuana wenyewe mizimu yao na ya kibuki.
Sasa huyu ndio wa kumuoa T. T akiolewa na huyu kafika, hana ujanja kabisa hapa kwa Simba. Huyu mamake Simba, simba kweli sio mchezo. Tena Simba ukimwambia mamako umeonana na sisi atafurahi kweli, mpambe yule si mchezo. Mwana hayupo Tanzania ningempigia sasa hivi nimwabie tupo wote hapa.
Mimi; Huyu mwamba muozeni T halafu mumtulize T.
H1; Tumtulize kwani ana nini, wakisha oana mambo yao watajuana wenyewe. Mimi nakushauri we, Mwamba usimuache huyu mtoto, ni bahati imekudondokea, hii kunywa kwake vi waini sijui kuvuta kwake vibangi wala kusikusumbue, utavi kontroli tu.
H2; Au atavizoea.
Swahiba; sasa mimi mwenyewe situmii hivyo vitu, si noma hio?
Mara kidogo akaja tena Martha. Tukamkaribisha.
H1; haya tena nani anaitwa safari hii?
Martha: Meneja anasema Mume wake Sh amewaalika chakula cha usiku kule hoteli wote mjitayarishe, baada ya one hour muwe kule.
H1; hayo ndio mambo, waamie ahsante sana tunakuja on time.
...
Nikawaambia haya kina dada, nyie jitayarisheni na sisi tunakwenda kujitayarisha kwangu kule..
H1; Haondoki mtu hapa, hata sisi tuna chumba chetu, tunajitayarisha kuondoka hapa, tupeni dakika 10 tu. Tufatane.
Mimi; Poa, mkiingia ndani humo mwambieni mhudumu atuletee kahawa wakati tunawangoja.
Wakaingia ndani, wakati wanaingia...
H2; Twendeni basi mkatukogeshe.
Mimi; Si mmesema hapa tuwape dakika 10 tu?
H1; Wewe nae mpaka tukufungikie, anagekua babako haambiwi mara mbili. twendeni tukanyanduane.
Swahiba; Astaghafirullah.
Mimi; Msisahau kumwambia mhudumu atuletee ahawa mbili.
Wakaingia zao ndani.
Swahiba; Si tunaweza kushuka beach wakati tunawangoja?
mimi; Sasa hivi huogopi vibwengo?
Swahiba; Siogelei hata kwa pesa huku. Natembea tembea tu mchangani.
Mimi; Ngoja basi kahawa ije.
Swahiba; Siendi tena. Kuna kitu nilikua nataka nikuulize lakini sikutaka kukuuliza mbele ya watu.
Mimi; Uliza tu.
Swahiba; Unajua mara ya mwisho ulipokuja hapa Unguja, tulikua hatujuani, lakini lile tatizo la yule binti lilivyokwisha Sheikh alikuwepo kwenye kikao, katiika kutuhadithia jina lako lilitajwa sana. wewe na Sheikh mmoja kutoka Tanga, Hata sheikh hamjui jina mpaka leo na kijana wa Kiarabu katokea wapi sijui, ulikua nae sana wewe. Lakini anaongea Kiswahili vizuri tu, sema Sheikh anasema unajua kua hiki Kiswahili cha Kiarabu...
... Ndugu yangu kile kisa kilituacha mdomo wazi Unguja nzima, Sheikh anahisi wewe ndio ulikua Master wa ile game mpaka binti akapatikana.
Mimi; Si alikuepo Sheikh wa Tanga.
Swahiba; Hilo mzee kalisema, na yule Sheikh wafiwa wote hawamjui, sio ndugu, jamaa wala rafiki. Bora wewe mama'ko anajulikana ni mtu wa karibu na wafiwa. na mkeo alikuepo. Kasema Sheikh, ulikua nao sana wale watu wawili.
Mimi; Mwarabu mgeni wangu, umetokea Msiba tuko nae. na Mzee yule mimi namfahamu, tumekutana kwenye boti akasema na yeye atakuja msibani kwa kua tunajuana.
Swahiba; Nipe kisa ilikuaje, maana wewe ulikuepo mwanza mwisho, mimi nimeyasikia tu kwa Sheikh.
Unajua mumewe yule mama mwenye mtoto yupo jela mpaka leo, halafu kuna jamaa alikua boss serikalini, na yeye yupo ndani mpaka leo, na wengine kama wawili watatu hivi sina uhakika...
...Yule mtoto wa kike, tulisikia alitoroshwa kimya kimya, yupo huko bara na mamake mpaka leo. Halafu yule jamaa wa serikalini katemeshwa mali zote kapewa yule mama amlee mwanae, maana mume ndio yupo jela, hata kesi zao hakuna anaezifatilia. Wamesuswa na watu wote. Simba usinifiche, kuna vitu unavijua sisi hatuvijui, maana hata Babangu kasema...
Mimi; Kasema nini?
kasema ' Mtazame swahiba yako pete anayovaa, sio ya kitoto ile na huwezi kumuona mtu yoyote kaivaa. Ina mambo makubwa ile. Nambie ukweli Simba.
Mimi; Mwamba usijitie wasiwasi kabisa.
Swahiba; haladu unajua Simba, yule mama ulivotoka nae ndani siku ile, alikua kama mtu ambae anauoga fulani hivi. Akatunyenyekea sana mpaka katusindikiza, unajua kasema siku nyingine tukienda tusiweke gari nje? Sasa Simba najiuliza, hawa kinadada wa Dar wamemjua mamako wakaasema yule ni kiboko, anahudhuria mpaka shughuki za vibuki lakini yeye hana kibuki. Hapo kuna maswali mengi.
Mimi; usiwe na shaka Swahiba, hata yule mama tulipokua ndani nikamtajia mamangu anamjua ni partner wao miaka, sema yeye hana kibuki, anamjua, ndio maana akatuwekea heshima.
Swahiba; Mimi bado akili haijaridhika. twende tukajitayarishe ku[iga misosi ya Kitalii.
Mimi; Mbona unaharaka sana, si tunawangoja kina dada watoke?
Swahiba; Imenitoka, nataka kuwahi kuongea na Meneja dili alilonambia la kazi za hapa.
Mimi; Si kakwambia mwenyewe, yule mtu wa misimamo, hata ukisahau yeye hasahau.
Swahiba, Mimi hata leo naweza kumuonesha game akiwa tayari.
mimi; Yule mpaka kakwambia ujue ana kitu mawazoni. Msikilize, umkumbushe mara kwa mara. Maana mimi si unajua leo nimeongezea siku tu, In sha Allah kesho bomba.
Swahiba; Saa ngapi hujasema.
Mimi; Hata mimi sijajua, lakini tukienda chumbani kwangu labda itakua nishapata taarifa, niliwaambia hapa hoteli wanifanyie booking ya ndege, nikitoka airport mie nashukia kazini kwanza. Tutajua tukienda chumbani kwangu.
Mijimama ya dar ikatoka.
H1; haya twendeni, bado mpo?
Tukaondoka tukaachana tulipofika karibu ya vyumba, wao wakaenda kushoto, sisi tukaenda moja kwa moja.
Nikafungua mlango wa chumba changu, nikamwambia swahiba kama unajmwagia maji jimwagie, hpa sioni bahasha yoyote ya ujumbe wangu wa safari, ngoja niende resepshen, wewe koga jifarague usiwe na shaka, mimi nakupa dakaika 30 hazikutoshi Mwamba?
Swahiba; Nyingi sana hizo dakika 10 tu zinanitosha.
Mimi; Wewe ukimaliza njoo pale resepshen, kuna sehemu ya kunywa kahawa pale, nitakua nakungoja pale, Usijali kadi ya mlango ninayo, wewe ukitoka funga tu mlango.
Swahiba; Poa.
Nikaenda resepshen.
Mimi; Aah Martha, leo boiss peke yako kote hapa?
Martha: leo Sunday na hakuna wageni wengi wakuja au kuondoka, staff wengi wanapumzika. Nikuhudumie nini Mr. Simba?
Mimi; Niliwaambia resepshen wanifanyie booking ya ndege kesho, sijaikuta note yoyote chumbani.
martha; Umetazama messages za simu yako? Siku hizi hakuna maticket kama zamani, wanakupa ticket numbar, ukija nayo hapa wanakuprintia boarding Pass.
Mimi; Ooh, ngoja nicheki, jinayo simu yangu.
Nikakuta miss calls kama ishirini, nikaenda kwenye messages, ya kwanza hio ya hoteli notification ya kuchukua boarding pass reception. Ya pili ya shirika la ndege, wana cnfirm safari yangu na maelezo nifike airport mapema, boardin time ni saa tano kamili. departure saa tano na dakika 20. Nikajua boarding time ndio hio hio derture time maana vindege vya unguja vodogo tu, abiria 20 au 25 tu, kuboard ni faster tu.
mimi; Martha nimeiona notification ya boarding pass, nikupe uni printie biarding pass? Akaitazama meseji kwenye simu yangu huku anaandika numbers, akanambia 3 minutes utapata boarding Pass. Nikamwambia nipo pale coffe table. Akasema; Sawa Mr. Simba nakuletea.
Nikaenda coffee table ile nakaa tu kaja mhudumu nikamwabia niletee fresh orange juice na sparkling water moja. Na martha akawa kishaniletea boarding pass. Hijapita muda, hata simu sijapiga kurudisha miss calls, Mwamba kaingia, kakoga yupo fresh. Nikamwabia kaa wewe sasa nisubiri, agiza chochote mimi nitasaini usijali. Ooh mwamba natakiwa niwe airpost kabla ya saa nne asubuhi, boarding ni saa tano kamili. Akanambia huo muda mzuri.
Nikaenda chumbani nikakoga faster, nikatoka nikaanza kupiga simu, kwanza ya wife.
Wife; Vipi huko, hutaki kurudi mume wangu? Tumekumiss kweli nyumbani, wanao wananisumbua huku. Dad wapi, dad wapi?
Mimi; hata mimi nawa miss sana.
Wife na mama hapa utafikiri mtoto wadogo, kila saa huyu anarudi lini, anarudi lini> Namwambia mpigie mwenyewe mwanao, labda kaoa huko Unguja. Nikacheke tu. Waambie wote nitawapigia baadae kidopo kuna mtu ananisubiri. Wife akachomeea, njaa kali huku.
Nikampigia Mzee, tukaongea kidogo; lini uanrudi kazi zinakusubiri au ushaoa huko Unguja?
Mimi: Wewe si ndio utakua wa kwanza kujua, unafikiri posa atanipelekea nani?
Mzee: Aah, wewe na babu yako siku hizi mna siri zenu, mnaweza kuozeshana bila sisi kujua. Mamako huyu ongea nae. Nikasalimiana na mama pale. Nikamwambia nimekutana na shoga yako mmoja anaitwa H1;
Mama; Huuyo basi huko kuna kupandisha vibuki, maana haendi Unguja huyo mpaka kuwe na shughuli za vibuki.
Mimi; Tumekutana hoteli niliofikia.
Mama; basi mwanangu umefikia Hoteli ya maboss huko, huyo hakai hoteli ndogo ndogo, hio lazima ya kitalii, huyo ana pesa kama njugu. Umejuje kama rafiki yangu huyo muhuni?
Mimi; katika kujulishana tu.
Mama; Wewe mwanagu nae, huyo humjui, na unampeleka mkeo na kumrudisha kila siku akiwa na kazi zake pale kwa BIn Sulum Kariakoo?
MImi; Nilikua simjui, ndio kanambia.
Mama: Unarudi lini, wanao wanakumiss huku.
imi;
n shaa Allah kesho joni maana nakuja na ndege, nikifika kabla ya kuja nyumbani niutapita kazini, mzee akitoka narudi nae.
Mama; Okay. safari njema.
nikaona nyingine ilikua miss call ya hapahapa hoteli, nadhani walikua wananijulisha kuhusu booking ya ndege. Namba zingine sizijui, nikasema hizi baadae nitazipiga. Nikatoka nje.
Ile nafika coffe table Mwamba ananambia, twende hapo chini beach, Menejea ameleta maagizo twende pale, wote watakua pale.
...