Vionjo vya Arsis 5-9
nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.
Siku hio ikapita salama, nikawa nafanya fanya mambo yangu nyumbani na karibu ya nyumbani bila events zozote.
Siku ya pili asubuhi tu, saa moja natoka kwangu nakwenda uani kwa mzee kijiwe chetu cha kahawa cha nyumbani, nikakuta mzee tayari yupo na mshikaji wanapiga kahawa, leo mshikaji yupo fresha kabisa, hana zile hangover. Nikasalimiana nao pale.
Mzee; Bora umekuja, mgeni wako huyu, mimi naondoka/ mzee ndio kawaida yake, hua hapendi kutoka nyumbani baada ya saa moja, ukitaimu nyumbani asubuhi muwahi kabla ya saa moja. Akaondoka.
Mshikaji; Oyaa mwanangu eeh, mimi nimekufata niongee na wewe. lakini usinione fala.
Mimi; Leo unaongea serious.
Mshikaji; usianzishe mengine tena, sisi tushakua watu wazima tunaotegewa kila sehemu. SZikiliza mwanangu, leo sijakuona msikitini Alfajiri.
Mimi; Hujaala na leo?
Mshikaji; Mimi nakuuliza swali la maana, nimelala vizuri sana, jana ulipoondoka niliongea sana dingi. Tukakubaliana leo alfajiri nikiwahi kuamka mimi impigie nimwamshe na akiwahi kuamkaa yeye anipigie tukasali alfajiri msikitini.
Mimi; Ndio maana unameremeta, umetokea msikitini na Mzee? Nani kamuamsha mwenzake?
Mshikjai, huwezi kuamini, mimi ndio nimestua dingi, bila noma wala kisirani akanambia tukutane msikitini, tukakutana tukasali jamaa wote.
Mimi; Mashaallh, habari nzito hio.
Mshikaji; Wewe mbona hujaja msikitini?
Mimi; Hua nawasalisha Alfajiri watu wa hapa nyumbani, ndio imam wao hapa, kwa hio wameshazowea kuniamsha mapema, na mzee anajua hgilo ndio maanahanichomoi alfajiri. Hii yako lakini mpya hii.
Mshikaji; Mpta nini, wewe hukumbuki amani tulikua tunasali wote saa zote?
Mimi: nakumbuka.
Mshikaji; Sasa mimi nilikua nakungoja sio kwa jambo hilo, hili jambo sedriasi sana nalotaka kuongea na wewe. Unajua jana nimeongea sana na Dingi ofisini, akanambia nikitaka mambo yangu yanyooke nisiache sala. ndio nimeanza tena, sasa siachi, sitaki kabisa mambo ya kishetani, hayana faida.
Mimi; Safi sana.
Nikajua hayo kweli ndio maneno ya mzee kwa kila mtu, anahimiza sana vijana tusiache kusali, tabata wengiu wameanz kusali kwa ajili yake, mpaka wengine walikua hawajui kaweka maalim anawasomesha Qur'an anawafundisha kusali na mambo mengine ya Kiislam, sikushangaa mshikaji alipokua ananieleza.
Mshikaji; Sasa mwanangu, nikuambie kwanini jana nikaongea na dingi ulipoondoka, nilikua nashukuru kweli ulipoondoka mapema, nikajua dua yangu imekubaliwa, nilikua naombea uodoke niongee na dingi kiutu uzima, manake wewe ungeharibu mazungumzo ungeleta rshikaji.
Mimi; Kumbe wewe ndio ulinifukuz kazini kichawi?
Mshikaji; Nia tu, hakuna uchawi mwanangu, nia tu, mie mwenyewe nikashangaa unaaga mapema kabisa. Sasa mwanagu sikiliza, mimi nilimwambia Dingi sio utani yule mwanamke nimezimia kinoma mwanangu, ndio dingi akanambia anza kusali utafanikisha kila. Mie mshikaji ndio nimeanza kusali.
Mimi: Mshikaji mwnamke wa Kiunguja yule utamunueza?
Mshikaji; Kwani ana nini mbona jamaa kibao wameoa Unguja, tena naona wako oa kweli kuliko vinyampwito vyegtu vya ilala. Vinajifanya vi sista du, kazi kubenjua makalio tu. Yule mtoto kenda shule kinoma. Si unajua mwanagu yule Daktari?
Mimi nikawa naguna na namuitikia tu napiga kahawa, mara mama akaja, njooni mnywe chai mwende kazini'.
Tukaingia sehemu ya kula mama akasema subirini niwakaangie mayai, kuna maandazi nimepika makavu.
Mimi: Mama unajua mwanao anataka kuoa, huki)u namuonesha mshikaji.
Mama; Hio story ananipa kuanzia alipotoka msikitini alfajiri, tupo nae saa nyingi na mzee hapa wanakunywa kahwa anakukungoja wewe uje.
Mimi; Kumbe wenzangu mshapata mipchapo yote.
Mama; Nakwambia, mwanangu kapenda mwaka huu, sijui daktarigani hiuko, mimi nimewaacha hapa wanampigia simu babu yako kwa hilohilo.
Mimi; Mpaka babu kapigiwa?
Mama; Muulize mwenyewe akuhadithie, mimi niliwaacha tena, sijui mwngine.
Mimi; Nambie mwanangu.
Mshikjai; Nilikua naongea na dingi, anasema yeye hamjui sana yule Dokta lakini babu ndio anaweza kumjua akampigia tukaomgea nao. Si unajua babu yako hapoindishi? Akasema yule kajulishwa na rafiki yake wa Sheikh mmoja Unguja huko, kanambia nionge nawewe unamjua huyo Sheikh, sasa mwanangu niulizie kwao yule binti, kwanza niukizie ana mume au hana? mana Dokta kama lile halikosi mume.
Mimi; kama ana mume utafanya nini mwanangu?
Mshikaji; Mie namwambia ukweli tu, kama ana mume nwamwabia siku akichwa sitafute mume mwungine, mimi nipo. Halafy mwanangu, si nimeanza kusdli, nipiga madua tu kwa nia moja tu.
Mimi; Masheikh wanasema. wenyezi Mungu hapendi kabisa mambo yalaka. sasa wewe wvipi unamuombea talaka?
Mshikaji; Sio hivyo, mimi simuombei baya hata siku moja, mimi naomba kama ndoa yake ina matatizo aachgike nimuoe mimi.
Mimi; Kwanini humuombe kama ndoa ina matatizo itengemae?
Mshkaji; Mimi nilijua tu wewe sio wa kuongea na e mambo haya, ndio maana jana nikaongea na dingi, wewe unapinga pinga kila kitu. Yaishe bwana, mimi naongea na dingi na babu. Wewe niulizie kama ana mume au hana? Au hata hio ni shida kwako?
Mimi; basi, punguza jazaba, nitakuulizia.
Mshikjai; Sasa unangija nini si migie huyo Shehe wa Unguja, mbona dingi kumwambia kampigia babu yako, hakulaza damu.
Mimi; Nitamuuliza mwanagu lakini sio ghafla ghafla namna hii, nipe muda kidogo nijue namuanza vipi, kumuuliza. Unajua dingoi kampigia babake, yule ni mtu najuana nae, tena si kiundani hivyo, mie leo hii nitakuulizia, kula twende kazini.
Mshikaji; Mimi tayari, basi mwanagu mimi sikungoji, wacha niende, wewe najua mbaka mbili unusu hapa, mimi mufa huk9 sishafika kazini, tena dingi kanambia kuna gari zinakuja kuchukuliwa leo. Unona milango inafunguka faster? Usiniwekee kauzibe. Au umezimia wewe yule demu?
Mimi; Yupo bomba kinoma.
Mshikaji; Si unaona tamaa hizo, sasa wewe mkeo hakutoshi? tuwachie sisi. Wacha niende kazini, tajuana na dingi, wewe tutaongea baadae, hata usifatilie hilo jambo.
Akaondoka zake hata kwaheri hakuna.
3
Mie kufika kazini kweli sikumkuta alikua kapeleka gari la mteja, tena lori kubwa. Saa nane nane akarudi, kuniona kaanza kucheka toka mbali.
Mshikaji: Hoyaa mwanangu, si unaona bwana , ulikua unanizingua asubuhi asubuhi, kuja hapa kumweleza dingi anaiulize, kanambia si muulize mwenyewe nama ya simu unayo. Mshikaji si nimemuuliza nimepata jibu.
Mimi; Kweli umemkamia mwanangu. Umemuuliza saa hio hio.
Mashikaji: Hakuna, nilishikwa na mchetu mchetu nianze z-anze vipi, halafu si unajua nilikua njiani napeleka gari la watu, na dingi si unajua, hataki kabisa tuongee na simu huku tunaendesha gari? Nikaifikisha gari salama kabisa, wakanipa mwenye boda anirudishe, kunirudisha ndio nikaona kwanza nisali mchana kabisa. Baada ya kusali ile natoka msikitini tu nikampigia.
Mshikaji; Unajua mwanangu, kumpigia ulifikiri alikua anangoja nimpigie, kanichangamkiia kishenzi, nikaona hata noma nimuanze vipi? Akaniuliza unasemaje? Nikavunga, vipi gari haijakupoa shida misi? Akasema haijampa shida lakini anahisi kweli haipo sawa,kaogopa hata kujaza mafuta maana tumemwabia yatamwagwa yote, kwa hio katia mafuta kidogo tu, alipotia mafuta ile kustuka stuka imeacha. Si unaona mwanangu?
Mimi; Duh, wee noma.
Mshikaji; Nikajifanya mwehu nikamuuliza, Dokta nambie nani mwenye bahati?
Dokta: bahati ya nini?
Dokta" Si aliekuoa? huyo ana bahati ya mtende.
Dokta; kwanini?
Mshikaji; Mtu kua na mke Dokta si nyota ya jaa hio? Kweli dokta una mume?
Dokta: Ninae.
Mshikaji: Wazuri wote mshaolewa, sasa sisi tutamuoa nani, mikanyagio tu?
Dokta: Usiseme hivyo, vibaya. hakuna mtu mzuri wala mbaya, ni mtazamo wa mtu tu.
MNimi: lakini wewe Dokta, upo vbomba kinoma.
Dokta: ahsante, utakuja Ijumaa kunipeleka bandarini?> Tena, nikipata ruhusa kazini, naweza kuondka kesho, leo mpaka jioni nitajua, utapata mafasi kesho nikifanikiwa?
Mshikaji; Kwa wewe dokta hata nikiwa sina nafasi nitaitafuta mpaka ipatikane.
Dokta: haya ahsante bye.
Mshkaji, unaona mwanangu? Ushaagwa bye na dokta wewe? Yule Dokta kama alivyo moyoni mwangu na mimi nipo moyoni mwake. Kama nilijua atanambia bye. Si unaona anahirisha Ijumaa aondoke kesho ili anione tu?
Mimi; Mshikaji, leo cha wapi? Maana unaongea kama chiriku.
Mshikaji: kamuulize babako ndio kanipa, sijui mimi, kwaheri/ Huyo akaondoka kuelekea ofiusini kwa mzee.
Mimi bikakaa kazini muda wangu wa kuondoka kufika nikamuaga mzee nikaondoka.
Usiku kama saa tatu, nikaingoia ofisini kwangu, nikamuita Jini1. baada ya kusalimiana pale.
Mimi: hebu nipe habari za hawa vibuki maana kesho naenda Unguja, mimi siwajui wala sijawahi kuwasikia.
Jini 1; hawa wapo aina nyingi na majina mengi duniani lakinia comoro na wa Japan wanaitwa hivyo hivyo Kibuki, sijui kwanini na tabia zao zinafanana. Hawa wale amabao hawajaingia Uislam ni wlevi sana, tena hawataki pombe za bei rahisi. Wanataka mwa whisky na brandy na mawine ya, ma shampeni ya hali ya juu yale. Haya ni majini mabaya sana. ynamvaa mgtuu na kupanda yakiitwa, yanmuotesha, hayataki kuonekana kabisa.
Mimi; Kwanini?
Majini machafu mengi hayana uwezo wa kuonekana, yanatumia miili ya watu kuongea na kufikisha ujumbe wao, sana sana wanawe kumuotesha yule mtu. Wenye kuonekana ni wale majini wenye elimu hio, na huipati bila majaaliwa.
Mimi: inakuaje hio elimu?
Jini 1: Tunasoma, kama mwanafunzi yoyote yule, Arsis ni mwalimu mzuri sana wa hio, mimi zamani nilikua sijui, hata mama alikua hajui, aliekua anajua hii Bakora tu na yeye ahajui kuifundisha. Zipo aina tatu kuu za kuonekana.
Mimi; Enhee nielezee.
Jini1; Aina ya kwanza nakuja picha tu sio uhalisia, hata ukinishika utashika hewa tu. Aina ya pili nakuja kimwili unaweza kunishika kama mtu yoyote tu. Aina ya tatu nakuja kwa kujibadilisha umbo lolote lile, nayo hio huwa ni kioo tu.
Mimi: Kioo vipi?
Jini 1; Si kama unatazama kwenye kioo tu inakua sio yuhalisia, myua anaeijua hio anakuja kwa kubadika kila aina aitakayo, unasema unamuona jini kumbe unaona kioo tu hakua lolote, ni mazingaombwe tu. Hii elimu ukitaka kuzijua kwa kina ukipata nafasi muulize Arfsis.
Mimi; Poa, Tulioongea kuhusu jini mtu, ukanambie nimuulize Atsis, hajakupa jibu unijibu?
Jini1; Muda uli ule alijibu, nikaona ulikua umechaka. Arsis anasema hao mbona hata kwenye Qur'an na hadithi wametajwa, soma juhusj Qareen na soma kuhusu Hinn, alisema ukishasoma hao sasa muulize atakufafanulia zaidi. Pia kasema kuna aya inasema, mimi sijiu vizuri itafute mwenyewe, msidhani wamekupa hai na wanaruzukiwa. Arsis alisema isome hio, utajua kuhusu Qareen ni nani. Akanambia mimi kuhusu QAareen mwingine, hilo sikuambii, utamuuliza mwenyewe litaleta utata sana kwenye elimu. Hilo wewe mwambie tu nimekwambia mimi sikuambii. ingawa sijakatazwa kulisema lakini binagsi nimekataa kulisema, muulize yeye atakufahamisha, mimi silisemi kwa kua nitashindwa kukujibu maswali yeke, linazaa maswali mingi hilo.
Mimi; Kuhus Kibuki, nitegemee nini, wewe si unawajua?
Jini 1: mimi nawajua na sherehe zao nimeshahudhuria sana zamani wakgti bado mtundu mtundu.
Mimi; kwani sasa sio mtundu?
Jini 1; Nime)eacha utundu na mambo yote yasiofaa, mimi mcha Mungu, siwezi hata kupoanda kchwani kwa mtu, ingawa najua. Mimi nikija au nakuja hivi au sauti, lazima pazia iwepo, hahya ni mawasiliano yanaokubalika. Siendi kinyume na mafundisho. Mwenyezi Mungu aniepushe.
Jini 1: Huko tegemea, wanawake mabisi wenye mihelea yao, wanaopewa na waume zao ua wenye vyeo vikubwa vikubwa, wafanhya biashra, kwa ufupi si mchezo hao, kuliko nyinyi simba wanavtopenda starehe hao.
Mimi; Nikacheka. Unayajuaje ya simba wewe?
Jini 1; Sisi kwani yupo leo na babu yako? Wewe tu ulikua hutjui, sisi tupo na babu yako miaka kabla ya kujuana na Arsis.
Nikaagane nae, nikawa najisemea kimoyomoyo, hawa majini wanazingua saa zingine.
Simba.
...5.10
Vionjo vya Arsis 5-10 Majini ya Kibuki - Unguja.
nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.
Siku ya pili asubuhi tu wakati nataka kwenda kazini, nikapigiwa simu na Sheikh...wa Unguja. Baada ya kusalimiana.
Sheikh; Babu yako kanambia unakuja lakini utafikia kwa wanene huko, isipokua mimi ndio mwenyeji wako, sawa?
Mimi; Sawa kabisa, babu kanifanyia mpango wa hoteli kwa rafiki zake lakini kanambia wewe ndio utanijulisha sehemu za hao vibuki na mimi nijionee.
Sheikh; Wale kama hauna kibuki na sio mmoja wao hawataturuhusu tuhudhurie sherehe yao, mimi nimewasihi sana, wamenikatalia wamenambia aje muhusika tu, nyinyi wengine inawahusu nini? kwa hio Simba babu yako kasema nikipuleke japo ukaonane nao kabla ya sherehe.
Mimi; Sawa.
Sheikh; Kwa hio atakuja mwanangu bandarini, kijana mwenzio akuchukue ajue hoteli uliofikia halafu yeye ana gari lake atakupeleka kote unakotaka lakini kula yako nyumbani, usituangushe, wewe mgeni wetu.
Mimi; Sawa.
Sheikh; Njoo mapema sana, kwani utakua huna muda. wale shughuli yao Jumamosi kuamkia Jumapili na Ijumaa si unajua siku yetu ya ibada? Na wao watakua na shughuli kubwa ya kuandaa sherehe yao ya Jumamosi, Wangazija hawana dogo.
Mimi; Usijali, hata Ijumaa mimi naweza kwenda huko, kwani si nakwenda kupajua tu, sina shughuli nao, dakika tano tu zinatosha. Sherehe zao mimi za nini, watanihadithia wanaozijua.
Skeikh; Wana siri hao, haparuhusiwi simu wala kamera aina yoyote ile, tena hio ni kwa hao wahusika wenyewe na hawaruhisiwi, wanaacha mikoba kwenye chumba kimoja wanaingia bila mikoba.
Mimi; Hayo Shekh mimi hayanihusu kabisa, sina haja ya kwenda huko siku ya sherehe.
Sheikh, nilikua nasisitizia, nani atakae kuhadithia na mambo na shere zao wanafanya siri kubwa?
Mimi; Si huyo Dokta akimaliza sherehe yao?
Sheikh...akisema wanayoyafanya huko ninyoe ndevu zangu kwa kigae Simba, huyo ataapishwa viapo vyao kabla hajaingia ndani huko.
Mimi; Hakuna shida. Wakati anaondoka na boti nitawajulisha na pengine wala msipate shida, kuna gari ya hoteli itakuja kunichukua, yanini niwatese, mimi nikifika hoteli nitawajulisha nilipo.
Sheikh; kama hivyo mwanangu atakuja bandarini japo muonanane tu, kisha ukishafika hoteli tutawasiliana zaidi.
Mimi; Sawa.
Kabla sijatoka, kaingia Mshikaji wangu. Tukasalimiana pale.
Mshikaji; Si nilikwambia mwamba, Dokta kafa kwangu?
Mimi; Maziko lini?
Mshikaji: Wacha ujinga, unajua sana nakueleza nini. Dokta kanipigia saa moja asubuhi. sasa madogo hayo? Toto kama lile linaniamsha na sauti yake ya Kizanzibari? kama hajafa ni nini hicho?
Mimi; Hapo sasa naamini kweli kafa.
Mshikaji; Dokta kanambia ninende leo saa saba na nusu nimpeleke bandarini ataenda na boti ya saa nane, halafu nirudi na gari itengenezwe kila kitu, yeye atanipigia tena siku ya kurudi nikamchukue bandarini. Halafu mwanangu, nikwambie?
Mimi; Sema.
Mshikaji; Kanirushia nauli 20, kaka asubuhi mapema naamka na 20 kibindoni. Unajua dingi wako yule mzee ana makarama, alinambia mambo yatakunyookea ukianza kusali. Sasa mtu kama mimi natafutwa na Dokta kama yule, ananimiminia tu minoti, unafikiri mchezo?
Mimi' Una sali lakini au unazuga tu?
Mshikjaji: Wewe mimi najua Qur'an kuliko wewe, au umesahau mwnangu, tulikuacha mbali kweli, mimi nipo mshafu qwewe bado upo juzuu. Sio kusali tu, nimeanza tena kusoma Qur'an, kila siku nasoma, eeh bwana wee imebidi niende kwa ustaadh pale msikitini, nimesahau mengi kweli. kanambia niwe naenda ananisikiliza tu, kanambia wiki moja au mbili kila kitu kitarudi kwao kuliko zamani.
Mimi; kwa hio utaenda huko kwa Dokta?
Mshikaji; Si mdio manake, mwambie Dingi mie leo siji asubuhi, nikitoka huko nakuja na gari mchana moja kwa moja. gereji.
Mimi; Mpigie mwenyewe pengine na kazi anakusubiria, wewe asubuhi yote utakwenda na umeambiwa mpaka saa saba nanusu mchana?
Mshikaji' naona kama nikienda Tabata nitachelewa.
Mimi; Wacha ujinga, twenda tabata, ondoka mapema huko kama saa sita hivi, au hata mimi narudi mchana naweza kukupa lifti mpaka hapa.
Mshikaji; Kama hivo poa. twede basi mwanagu, nipe kama nusu saa.
Mshikaji: basi mie niko nje , nawahi kutoa kabisa hii pesa niwe nayo mfukoni, utanikuta nje hapo.
Akaondoka zake.
Mie ikawa kama kawaida, napiga kazi zangu. Nilipopata nafasi nikampigia meneja nikamwabia mimi nakwenda kesho boti ya asubuhi, akanambia poa, akanielkeza gari nitakayoikuta pale, ki hiace kama kuna wageni tutaingia wote, akanipa jina la hoteli.
Siku hapili asubuhi sana nikaondoka na Mshikaji akanipeleka, bandarini, analalamika njia nzima.
Mshikaji; sasa wewe nini kinalupeleka Unguja au kwa kua umesikia demu wangu kaenda huko?
Mimi; Kishakua demu wako tena?
Mshoikaji; Bado rasmi lakini ndio ilikua inaelekea huko unnitili kauzibe. Ssa unaenda kufanya nini huko?
Mimi; Usiwe na shaka, mimi nakwenda kuonana na mumewe. Swahib yangu.
Mshikaji; Mbona kaenda peke yake? Tena nikwambie mwanangu?
Mimi; nambie.
Mshikaji; Yule dokta noma, jana katika kumbebea mizigo yake kulikua kuna boksi hilo zito kama kilo kumi hivi, halafu limefungwa dindindi. Si nikamuuliza lina nini ndani? kwani kanificha, kanambia lina wiski ndani, kuna watu wamemuagiza. Halafu mwanangu, ile gari jana nakuapia alipokuja nayo mchana, ilikua inanuka ganja ndani, yule lazima anachoma.
Mimi; hayo maisha yake binafsi, mimi yananihusu nini?
Mshikaji; Nakwambia tu, sasa mimi nimekua Shehe, tutawezana kweli miwiski na maganja, si atanirudisha pabaya yule?
Mimi; Wacha ndoto, itakua Dokta kishakujua wewe mtu wa ndumu na mitungi, lakini si ana mumewe?
Mshikaji: Inawezekana kweli ndio alikua ananijulisha hakuna noma, lakini hajui mimi si9ku hizi nimeacha mambo hayo. Mwanangu, anajulikana yule bandari ya kwenda Unguja, leo kwa mara ya kwanza nimefunguliw geti, gari lake limepaki chini ya ngazi za meli, bonge la VIP yule, ikabidi waje wachukuzi. Wale mabosi wa pale wanamshobokea ile mbaya. Mie nikakatoka zangu, ile naondoka, Dokta ananambia, Bye tutaongea kwa simu. Mbele yao, yote yakaanza kunitazama nani huyu, mimi nikauchuna tu.
Tukafika bandarini mshikaji bado anaongea tu, tukaagana nikaondoka zangu, kufika ndani ya meli nikapiga simu kwa Sheikh na kwa meneja. kama tulivyoagana nikamkuta mwanae ananingoja akanijua na mimi nikamjua tulikua nae mazikoni, kile kisanga cha msukule. Baada ya kusalimiana pale nikapanda gari la hoteli ki hiace niko peke yangu.
Kufika nikashuka mapokezi, pale wakaniuliza, wewe ndio Mr. Simba? ndio, wakanambia twende chumbani kwako, kuna kijana mmoja akanipokea begi na binti mmoja anaonesha wa Kinairobi yule kwa Kiswahili chake, wakanipeleka. Yule binti akasema, meneja alisema ukishaweka mizigo ukipumzika uje pale resepsheni anataka muonane. Utapajua au tukufate baada ya nusu saa?
imi; Nitapajua, nitakuja tu usijali.
Baada ya nusu saa nikaenda resepsheni, nikamkuta yule binti alienipeka chumbani yupo kwa nje, akanichukua mpaka ofisini kwa Meneja, nikamkuta jamaa kijana tu lakini anaonesha kakaa sana je ya Tanzania, maana ananukia na anang'ara.
Tukasalimiana pale, akajitambulisha, akanambia Simba hatujawahi kuonana, kwa babu yako?
Mimi: Sikumbuki.
Maneja; babu yako tarafiki yangu sana, unajua Afrika tena, wachawi na wanga wengi, lakini babu yako kiboko kanifanyia dua pale, na kuna mzee mmoja rafiki yake akanipa majani majani fulani hivi niwe kabla ya kulala nayachoma chumbani, toka siku hio hakuna tena wachawi mpaka leo, hzi hoteli zina makafara mengi, zina maajab ajabu mengi, yule afiki yake babu yako akaja hapa akafanya fanya mambo yake kila chumba mpaka nyumba za staff huko, sasa hivi hakuna shetani wala jini, watu kuotaota hovyo hakuna tena. Ndio toka siku hizo babu yako kawa rafiki yangu sana. NBilikua siamini kama unachawi, lakini niliokutana nayo hapa, hoteli hii, sasa hunambii kitu. Uchawi upo tena live kabisa.
Mimi nimempenda sana babu yako, sio mganga wa kuchanja yule wala kukwambia leta mbuzi. Hapa wamekuja wanga kila namna, tumechinja mpaka ng'ombe lakini visa vilikua haviishi, tukawa tunaogopa wafanyakazi wakianza kuogopa na kuongea na wateja mambo yale, tutakosa kabisa wateja, wanaambizana huko. na sisis kazi zetu zinategemea wateja wapeleke sifa nzuri ndio hoteli inapata wateja wapya.
Tukaongea ongea meneja akanambia usijali, kila kitu humu ndani ni kwenye hesabu yake na staff wote wanajua, wewe wakikupata karatasi usaini tu, usijali, saini tu, sio deni lako au la babu yako. Pia kuna gym hapa, naona mwenzangu mtu wa mazoezi, una swimming pool, kuna sauna, massge, Huduma zote zipo kwenye kitabu chumbani kwako. Kwa hio kula vizuri, anya mazoezi ukipenda, tembea popote hakuna kizuizi. Ukihitaji gari kwenda safari zako waambie tu pale resepsheni, sawa Bwana Simba? Mimi nipo hapa saa 24, sikai mbali na hapa, kuna nyumba za staff hapo mbele kidogo tu ndio nipo huko.
Meneja; Ukijisikia boring njoo hapa ofisini anytime au waambie staff watanitafuta niko wapi, sichezi mbali.
Mimi; Poa, ahsante sana.
Meneja; Twende nikusindikize, mimi nipo busy naelekea hukohuko lakini nakwenda hapo mbele kidogo tunajenga kiwanja kipya cha tennis, kuna wateja mabingwa wa tennis duniani huko hua wanakuja sana kutembelea Zanibar hakuna hoteli yenye kiwanja cha tennis wapige pige mazoezi, ndio nakagua ujenzi unaendaje huko, kitakua kiwanja kizuri, kuna kampuni ya jnje ndio inakitengeneza, sio cha kimatafa lakini pale pakucheea (pitch) patakua na vipimo vya kimataifa.
Akaniwacha resepshen yeye akaendele, yule binti akanifata. Mr. Simba ukitaka kujua restaurant ipo huku, ukitokea kwako, inabidi uje mpaka hapa, kama unaona tabu kuja ukipiga simu ugtaletewa chakula chumbani kwako, menu ipo kwenye meza na au unaeaeza kupoiga simu ukapikiwa uanachopenda, sio lazima menu. Nikamwabia, ahsante, nikaelekea chumbani kwangu, nikaanza kumpigia simu Sheikh, akanambia kapata habari nimefika na kwa gari ilionichukua wamejua hoteli gani, lakini kwanini wamekutoa nje ya mji? Huko kunaitwa Kiwangwa. Nikamwambia sio mbali, nimeona karibu tu.
Sheikh; Kwenu nyie kila sehemu mbali kwa hio hapo umeona karibu, ukitaka akufate huyu mwenzako anakufata wakati wowote leo lazima uje kula na sisi hapa ili tuongee kidogo, nikamwambia poa, mpo sehemu gan vile? Kuna gari ya hoteli hapa, nisiwasumbue. Akanielekeza jina nikamwabia kama sikupajua nitampa simu dereva muongee nae umwelekeze. Aksem sawa.
Sikukaa sana, nikaondoka, dereva, kumwabia tu dereva hio sehemu na kuntajia jina la Sheikh, akasema umefika mpaka mlangoni kwake, Sheikh Maarufu huyo, watoto zake rafiki zangu.
Basi tukafika pale, ikawa kahawa na nmaongezi ya hapa na pale mpaka mida ya kusali tukaenda kusali, nilishamjulisha dereva nitachelewa aende tu nitampigia nikimuhitaji maana nitachelewa huku.
Bd y KUL SIKU, BINGE KA MSI=OSI LA MGENI adhimu, sio mchezo, na watoto na wajukuu wa sheikh nikjulisha julishwa baafda ya kula babau yao akaniita, tukakaa ukumbini pekeetu tukaongea kuhusu Dokta. Akasema kishafika yupo kwao, huko ndio wanamfanyia mambo yao ya kibuki, hapa alikuja kiunisalimia tukmfanyia na dua kidgo. mwenyei Mungu amsaidie, lakini hana raha kabisa, madude ya memzonga zonga.
Mimi ; kwanini Sheikh ynamzinga hivyo?
Sheikh; Hii kukaa sana ulaya na kusoma huko, inawaketea shida sana nyinyi vijana, kuna wanaojishau na ibada wanafata mambo ya wazungu inakua miili michafu. Saka inasafisha mwili na moyo wa kishtani unaondoka, hataa awe jini au shrtani aina gani hakai kwa mtu anaesaki bila mchezo, sio kusali kwa kujionesha. Vijana msiache sala, wewe Simba unajua, babu yako msomi sana yule. Dini imetulia pale. hana tena ule usimba wenu, maana ule na hawa kibuki sijui nani zaidi, ni namna moja mambo yao, yanafanana sana. nagtumai na wee Simba jina tu, hujachukua mila za mizimu ya kisimba.
Mimi: Zamani sana, babu ameniachsha mambo yale ya kijinga.
Sheikh; Hilo muhimu sana, hata hao simba ukishika sala anakuheshimu, hawakusogelei. Hata hao kibuki, ukiona wanamsumbua mtu ujue bado hajadsshika sala na wngine wnawapenda wnapatia kufanya mambo yaoya kilevi na kujipatia pesa.
Mimi; Pesa kivipi Sheikh?
Sheikh; Mkisikia pesa vijana wa siku hzi masikio yanafunguka, pesa zao wale zinatoka kwa wnaume, kibuki karobia wanawakumba wanawake na mashoga, na wanaume wale wenye pesa zao wasio na adabu wanapatia mahitaji yao kupitia hao wanawake wenye vibuki.
Mimi; Kivipi Sheikh?
Sheikh; Kila si kama chama tu, hawana tifauti ba freemason, akiwepo mwenye mwanamke w kibuki ofisini biashra tampampa mwenzake, ak majini wanswasiliana ndio ndio wakienda kwa wanawake zo, wanaambiwa kajan fukani ofisinimkwako hivi na vile, mpaka majina wanawatajia, basi mijidume isivyokua na akili inawaamni wale majini na kuwaogopa wake zao kama nini, pesa zikiingia lazima ashike mwanmake na matumizi apange yeye, wana mbiunu zao wanawatisha mwanamme anakua haoni asikii. Oia Simba, wanakua wqanajua siri zao nyingi, kama wizi makazini, kam wala rushwa kama biashra za hatranu, inakua mwanamme kishabanwa hana ujanja, tena hawa kibuki wnakuwachia mpakamuchukue wanawake wa nje. Wengine unawaoan wanaume kabisa mabiss wanaingiwa kwenye ushoga na hawa vibuki, ili wapate siri zao za aibu, wanshike mtu vizuri.
MimiL Dah hai vibuki basi hatari.
Sheikh sana; lakiniu wapo amabao sio mashetani, hawaashirikiani kabisa na hawa mashetani na hawapandi wla hawadsogelei kwenye ushetani, hawana toifauti na wewe au mimi, kama sio mtu wa kishtani utaenda bar kufanya nini?
Niakafahamishwa mengi sana kuhusu vibuki kama saa tani hivi usiku nikamwabia Sheikh wacha niute gari ya hitek)li inifate. Sheokha akasem haina haja wtakupeleka hawa, utawaambia kesho wakufate saa ngapi au mtaagana wenyewe wakuoneshe mji, unaweza kwenda na kwa Bi S ukamtembelee yupo fuoni yeye, Bi S ni huyoi mama anaewachezesha vibuki.
Nikaondoka na wanawe wawili tukaenda na gari yao, kwa usiku jdio ikawa karibu kabisa, nikawambia nikiwahitaji keshoi nitawapigia, nikachukua kasdi ya chumba resepshen nikaenda chumbani kwangu, ile nakoga namaliza nasikia mlango unagongwa, kuchungukia naoimuona Jini 1. Nikamfungulia. Tukasalimiana pale.
Jini 1 snahani, nilikua nasubiri umalizane na Sheikh... nije tuongee, sasa sikiliza kwa makini, chukua kikombe cha kahawa kwanza, maana wewe bila kahawa kichwa hakifunguki.
Nikatia kahawa nikaanz akunywa.
Mimi; haya nambie.
Jini 1: hakun mengi ila sikiliza kwa makini. Keshoi mapema tu nenda kwa guyo bibu Fuoni, usishangae akikujua. Mtu wa majini ya kibuki makubwa makubwa yule, lakini sisi hatuoni wala hajui kimekuleta nini, isipokua atajua wewe ni simba na simba nyinyi ni marafiki wakubwa wa kibuki, tena utapewa heshima zote, Ujilinede tu na maasi wasikurus)dishe ulipotoka.
Mimi: hawawezi.
Jini1; Nafahamu hilo lakini lazima nikupe tahadhari, mimi nimepita kote huko na wale nawajua miaka imngi sio leo sio jana. Sasa mama anataka kuongea na wewe, yeye ndio mtaalamu nao sana. Mwache aje akupe ,awili matatu, dunia mbaya hii Simba.+Mimi: Mwache aje, mlango ukagongwa nikamabia fungua tu, Jini 2 akaufungua akaingia mamake. Bada ya kusalimiana pale.
Jini 2; Wameoina mimi wanlete lada nikupe moja au mawili. Sikili kwa umakini, huyo bibi utaekwenda kwake, yeye sio mchawi lakini yeye ndio ana lile jini la kifalme la hawa vibuki wa ukoo huu wake. Kama vile babako na simba, sema simba wao hawana kupandisha wala ujinga ujinga, wao starehe yao unaijua, sina haja ya kukueleza. Hawa vibuki hawana mipoaka na starehe na wanahizaya hawa, wapo tayari kufanya lolote ili mwanamme awe chuma ulete wao, wana mali, wana vyeo wao wanaume zao lakini hawatosheki, kwa sababu ya starhe na kujionesha nani zaidi kwenyue masherehe, hukjo bangi na pombe za ghali, kila aina kama hawana akili vizuri, sasa hii sherehe ya dokta peke yake unajua imegharib)mu shillingi ngapi? Na hii ndio ndogo kwa watu wachache tu hawatazidi u(ishirini. Heasabu wewe, shetehe zake Bi S ni shillingi million moja kila mtummmoja, ataefudhuriam wanaohudhuria wanalipoa wenyewe sio Dokta, Dokta yeye analipa million tatu kwa kua ndio alieitisha hio sherehe, kila kitu kitakuepo na kila anaekuja ayakuja nastarehe zake na raha zake, wanawawake wasgaji watakuwepo mashjoga watakuwepo na mabwana zao watakuwa wanawangoja nje huko wanajua wenyewem kila mmoja kivyake, hzi millioni ,illinponi waloztoa wanahakiksa zinarudi na faida Jumamosi hiohio. Hawa na hasara.
Mimi hapo sijaelewa.
Jini 2; hapo wale washoga kazi yuao kubwa ni ukuwadi na bibuki vyao, wanaume wenye pesa zao siku ya sherehe za kibuki, kuna wanawake makuwadi, kwani haoa wanawake ni wa maana mitaani huko, hakuna asiekua na hamu nao. Mfano wewe uwe nawaziri una moipea s(ya wizi uambiwe ukimtake mke wa Mkubwa fulani, umle, utakataa na unamjua mwanamke bomba na tamaa inakushika ukiwa na uhusiano nae zitarudi kwa nia moja au nyingine? Wana mbinu nyingi lakini zote za kishetani, hakuna muujiza wala nini ni ushetani tu. ni mlolongo wa kishetani. Utawaona.
Mimi; Nytawaonaje na mimi nimeambiwa naSheikh sit(ruhusiwi kuingia kabisa?
Jini 2: Wewe nenda ukamuone Bi S, ), nimekwambia wewe simba mkubwa sana, utajionea mwenyewe sitaki kukwambia, pengine uyasiwe, mimi sio mtabiri, lakini naju kwa sababu nimeshayaona zamani.
Mimi: Wewe umeonaje, kwani wanakurugusu kuingia?
Jini 2; Mimi zamni si nilikua nashirikiana kuwaroga waume zao, wewe hujiui sisi ukko wetu ni marafiki wa simba toka enzi na enzi/
Mimi; Sijui, nitajuwaje?
Jini 2: Muulize huyo manaewasiliana kila siku, anavyokupenda huyo toka akujue, atakwambia kila kitu huyo. Mie yangu yalikua hayo tu, ukiwa na mengine utamwabia huyoi patmna wako, Mimi naondoka.
Mimi; Ngoja, lakini kwanini mnanishirijisha kwenyue mambi haya ya kiji nga?
Jini 2: baaabu yako anataka ujue dunia ilivyo sio unaoyaona tu, ndio kufungiliwa maho huko, ulifikiri kufunguliwa macho kuffnyiwa upasuaji wa macho? Yaone simba, babu yako anatak yasikupe tabu haya, na amekuchagu weee ndio mrithi wake. Ingawa simba walikua wanakutaka sana kuliko kitu choch9ote.
Mimi; kwanini mimi simba wanitake?
Jini 2; Unajuam simba wa marehemu babu yako, baba wa mamako walikuchanjia usimba kuanzia mchanga, wakurithisha na mizimu ya kisimba, na upande wa babako wakauwachia usimba wao wao wewe. Babu yako huyu hakuoendezewa yale, yeye mtu wa dini, wale simba hajui mipaka ya dini, wanasali halafu wanafanya uasheratim huyu hakubakiani na hayo kabisa, anafanya sana ibada ndio maana ana nguvu kubwa ya kauli zake na wote hao wanamuheshimu, mambo yake mengine muulize mwenyewe na Arsis, mi kazi yangu nikugfahamishe kuhsusu vibuki tu.
Mimi; Si hata ri hao jamani?
Jini 2; Hakuna kwako hatari yoyote, wakikuona wewe wayakua wanaogopa hatari kwao, ni marafiki wakubw asana wa simba wewe kuanzia ukimuona Bi S, utakua mfalme hapa Unguja, utaheshimika kila mahali unapokwenda, usicheze na vibuki, wataeneza habari, vibuki wote hata amabao wamejificha watataka wawe karibu yako. Kwaheru bwna.
Mimi ; haya kwaheti, kama unanihsakikishia hakuna hatari nilale kwa amani.
hakinijubu, akaanza Jini1.
Jini 21: Wewe Simba, huna hatari yoyoitem sasa sisi kue na hatari tukupeleke au ytukuache uende? Faida yetu nini sasa?
Mimi; Majini hamuaminiki.
JIni1: hayo majini ya kichawi, sio sisi, sisi hatuna ushenzi huo labda ungenikuta wakati ule sijafanya toba. Hapo hata mwenyewe sijiamini, unafikiri ningeweza kuja hivi?> Kwanza elimu hio angenipa nani? Ningekua napanda kichwani kwa mtu, nikija nabatua mambo naondoka zangu mbio mbio.
Mimi: kwanini mbio mbio?
Jini 1; Unafikiri majini ya kichawi yana raha? Yanaishi kama majambazi tu kwa kujifichaficha yanawindwa kila sehemu, unafikiri ningekua naweza kutenbea popote wakati wowote kama sasa? Sasa hivi majini ya kichawi yananiogopa, yakiniona yanapita mbali kabida huko. Utajua tu kwanini siku za usoni, usiniulize kwanini. Maana ndio swali lako kubwa hilo, unamwacha mtu au)funguke tu hata yasisemeka. Kwaheri, pumzika ukaione Ungi)uja keshoi huijui wewe. Hio uiopewa ni utangukizi tu, kajionee mwenyewe sinema kamili.
Akaondoka, mimi nikalala zangu usiku nikaamka, nikatawadha nikaslai sala uy usiku nikasali na rakaa mbili za kumuoba Mungu anilinde na haya mashetani.
Simba.
...5.11