Simuoni ndugu mshana akitia neno kwenye huu uzi ! aidha siwaoni wadau wake wakimualika kuja kuona kama ilivyo sunna yao, kwa maana tumezoea kuona nyuzi zenye asili ya nguvu za asili basi zina mchango wake katika aidha utoaji wa maoni au uongezaji wa nyama. sina maana kuwa ni lazima awepo kwa vile JF ni kubwa kuliko Mshana na kwa kusema hivyo sina maana ya kumdogosha Mshana.
hii thread ni miongoni mwa zile nazoweza kuziita ni multifunctioning kwa maana ya kwamba kwanza ni burudani kwa vile ni simulizi lakini pili, ni kile nachoweza kusema ni elimifu na inaibua hisia kwa vile tumeweza kufahamu au kusoma habari ambazo tusingetegemea kuzisikia mahala kwingine kama tusingezisoma hapa. binafsi siwezi kutoa credit kuwa ni kweli au ni kinywaji cha wazee lakini i am there watching.
My attention kwenye thread hii ni kuwa khaa kumbe even spirits ie Arsis are or may put in application matumizi ya vitu vya kibinadamu kama vile simu na namna members wanavyojibizana na msadikika Arsis kupitia jukwaa ! hii inafanya nijiulize ni kwa vipi Simba anampatia kifaa cha mawasiliano ya kibinadamu rafiki yake wakati hawaonani ?. but whatever it may be.
Kitu kinachofanya niamini walau kwa mbaaali sana kuwa may be jamaa ni spirit kweli na ako hapa tunazungumza ni pamoja na uvumilivu wa kimazungumzo aliokuwa nao. anaambiwa maneno ya karaha lakini yeye hajibu karaha, ame relax sana anakutizameni mnavyorukaruka kuvitetea vitabu vyetu vitukufu. kwa mfano mtu kaambiwa alete maandiko yanayosema kuwa Adam ndiye mtu wa kwanza ndani ya Qur an, badala ya kusema kwanza hakuna then ndo alete excuse ya alternative verses ! and infact haipunguzi chochote katika imani yako kwani waislamu tunaelekezwa kuacha ujuaji pale tusipolielewa jambo kwa undani wake, lakini mtu huyo ataanza kuleta aya ambazo hazitoshi kujibu explicit question on table. na hakubali kuwa hakuna, and by the way kama haipo haipo tu na wala haibatilishi uhalali wa qur an kwa mujibu wa qur an yenyewe ukisoma sura ya kwanza aya ya pili.
Lakini pia ishara ndogo nyingine ya kwamba labda ni kweli jamaa ni spirit ni ; tabia ya utoto anayoionesha katika majibizano yake. binafsi sina elimu ya majini na watu wasioonekana kwa vile amesema yeye ni mtu, lakini ufahamu wangu mdogo katika dini yetu ni kwamba spirits wana ile inferiority complex juu ya mwanadamu ! wako na wivu juu vile mwanadamu ndio kiongozi wa dunia na hawakupenda kwahio, wherever they are in contact with us they want to show us that they are better than us na hivyo anachokisema yeye hataki kibishiwe, you don't have to reason before his or her eyes ,just say "yes sir", ndio kusema; badala waendelee na mazungumzo ya kuwa watu wengine ni kina nani before Adam, yeye anang'ang'ania ni lazima mkiri kwanza qur an haijasema kuwa Adam ndiye mtu wa kwanza na Hawa hajawa adressed ndani ya kitabu hicho. na nimeona mahala mtu akimpledge Arsis basi jamaa hufurahi sana. hahahaha ndo jamaa walivyo najua nyie mnafahamu watoto waking'ang'ania kitu how it appears, hususan wanaogombania nani mkubwa kuliko nani jaribu kuconnect.
Kuhusu juju wa majuju nilifurahi niliposkia wana dunia yao ya kujitegemea kutoka kwa mwamba huyu Arsis, lakini kuna fikra iliyopita kama umeme kwenye kichwa changu kwa vile nakumbuka when i was in my O level studies nilikuwa nimekwisha wiva kiasi kuhusu dini ya kiislamu[ nimesoma seminary ya kiislamu ilemela mwanza], sasa kuna kitabu kimoja kilichokuwa katika lugha ya kiarabu kilikuwa kinazungumza kuhusu dalili za kiyama, dini yetu inaeleza kuwa hao raia[AKINA JUJU] watakuja nyakati za mwisho kuifisadi dunia sasa, ndani ya kile kitabu sehemu inayowaeleza hawa wadudu wenye uzito wake palichorwa ukuta fulani hivi kama ngome na kwamba watakapokuja duniani kufanya ufisadi watapitia maeneo hayo.
hiyo ngome tuliisema kwa mengi na kimsingi yalikuwa ni mawazo yetu kama growing elites kwamba inawezekana ndio ule ukuta tulioambiwa na vitabu kuwa jamaa wanaula kuanzia asubuhi hadi jioni, kisha kitapobaki kipande kidogo kutoboa duniani basi jioni ingefika na wangerudi kulala huku wakisema aaah hapa tutapamalizia kesho bila kusema Allah akipenda[INSHAA ALLAH]. basi kesho wangeukuta hivyo na ikawa zoezi la kila siku mpaka siku watakapompa credit muumba wao basi watakuta mambo kama walivyotarajia na hatimae kuingia duniani.
kwa wale wapenzi wa movie ukuta huo umeoneshwa kwenye movie moja siifahamu jina lake kwa vile siyo mambo yangu hayo, ni movie ya kichina sasa kuna wanyama hao walikuwa na kazi ya kuvamia ngome ile ni wakali balaa na ni wengi kuliko walivyo hata ! najua umenilewa, so wanashambulia mpk watapoweza lakin badae wataondoka.
Sasa fikra zangu zinaniambia kwamba hahahaha eti kwa vile Qur an imeeleza kuwa hawa wadudu wapo lakini haikusema wapo wapi, na kwa vile Arsis anatuambia wapo dunia yao huko hapaendeki, na kwa vile wapo wanaojitahidi kusema kuwa hilo eneo hapo china ndo kuna mlango wao, basi najaribu kufikiri kuwa hapo kwenye hiyo ngome kuna mlango wengine mnasema cjui portal, ambayo inaweza kumtoa kiumbe hapa duniani kwetu kwenda dunia zingine ikiwemo hiyo ya kina juju, haya ni mawazo tu baada ya kula ugali sihitaji ligi pia mwenye mawazo au ufahamu zaidi basi tutaendelea kusomana.The story is telling kwa kweli , kuanzia kule sokoni chalinze, shinyanga, tabora, tanga na hata unguja huko,
Ushauri wangu kwa wasomaji, put away hizo fanatic feelings zote pembeni[udini], then open to learn utajifunza habari nyingi sana kwa vile walioishi kabla yetu hawakuswali swala tano wala kushika misalaba.
Mwisho niwaombe radhi kwanza kwa maneno mengi ilihali uzi sio wa kwangu, pili kwa makosa ya kiuandishi yatakayoonekana kwa vile sinaga kawaida ya kupitia mara mbilimbili nilichoandika.