Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Mkakariri hadi na Kiarabu ili tu mpate nafasi ya kwenda kwa Mnyaazi Mungu. Kiarabu ni kitukufu kuliko Kimakonde au sio 😂😂😂
Mimi mwenzio sifungwi na mipaka nipo huru kujifunza lugha yeyote Embu tuanze na kichina kwanza "Nihao" jifunze kutafuta maarifa na wala usijifunge kwa chuki

Mungu mwenyewe katupa uhuru wa kuchagua siyo kama kuku 🐔 au 🐄 ukienda ulaya lugha yao ni hiyo hiyo.
 
Mimi mwenzio sifungwi na mipaka nipo huru kujifunza lugha yeyote Embu tuanze na kichina kwanza "Nihao" jifunze kutafuta maarifa na wala usijifunge kwa chuki

Mungu mwenyewe katupa uhuru wa kuchagua siyo kama kuku 🐔 au 🐄 ukienda ulaya lugha yao ni hiyo hiyo.
Pitia satanic bible mkuu! Kuna la kujifunza
 
Kwani huko peponi kutakuwaje?
Kwanini asingeumba pepo akatupeleka moja kwa moja maana huko ni hakuna dhambi watu wanakula bata mwanzo mwisho
Maisha ya kwanza yalikuwaje kwani kama unasoma maandiko? Na Maana ya Eden ni nin?
 
Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...

Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)

Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?

Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?
Mkuu,

Twende kwa Socratic Method.

Kwa nini usipitie dunia yenye tabu na mateso mengi?

Tabu na mateso ni nini? Tabu na mateso kwa nani?

Kwa nini wewe , kqma wewe au hata hao unaowaita binadamu kiujumla, kwa nini muwe special sana msipate tabu na mateso?

Reuben Challe
 
Maisha ya kwanza yalikuwaje kwani kama unasoma maandiko? Na Maana ya Eden ni nin?

Kwa mujibu wa The Satanic Bible (Anton LaVey):
  • Eden si mahali pa utakatifu au usafi wa kiroho.
  • Inaonwa kama mfano wa wakati ambapo binadamu aliishi kwa kufuata tamaa zake, bila hatia wala kanuni za kidini.
  • Anguko la Adamu na Hawa linafasiriwa kinyume: badala ya kuwa dhambi, kula tunda la ujuzi linaonekana kama kitendo cha ujasiri na kujitambua binafsi.

Maana ya Eden kwa mtazamo wa Kishetani (LaVeyan Satanism):
  • Ni hali ya asili ya binadamu kabla ya kufungwa na dini, aibu, na kujinyima.
  • Ni uhuru wa kiakili na kimwili, ambapo binadamu alijua tamaa zake na hakujinyima.
-Shetani anaonekana kama mtoa nuru (Lucifer) aliyeleta maarifa, badala ya kuwa adui wa mwanadamu.

Kwa kifupi, kwenye The Satanic Bible, Eden si bustani ya kupotezewa, bali ni mfano wa maisha ya kufuata tamaa za asili, furaha, na uamuzi binafsi — kinyume na utii wa kipofu kwa mamlaka ya kiroho.
 
Mimi mwenzio sifungwi na mipaka nipo huru kujifunza lugha yeyote Embu tuanze na kichina kwanza "Nihao" jifunze kutafuta maarifa na wala usijifunge kwa chuki

Mungu mwenyewe katupa uhuru wa kuchagua siyo kama kuku 🐔 au 🐄 ukienda ulaya lugha yao ni hiyo hiyo.
Tatizo unachanganya Kiarabu kwa waswahili. Na mimi nikianza kuleta Kijerumani humu itakuwaje
Najua sijakatazwa ila sio peke yako unayejua lugha mbali na Kiswahili na Kiingereza. Address wabongo na Kiswahili au English mbona iko clear kabisa
We unatuchanganyia ma surat al nini sijui. Duh
 
Kwa mujibu wa hekaya za kiyahudi kikristo na kiislam Mungu katuleta duniani ili tutekeleze maelekezo yake yasiotekelezeka kwa kutuletea shetani duniani ili ahakikishe tunamkosea Mungu ili apate sababu ya kutuchoma moto MILELE baada ya maisha haya mafupi na mateso matupu


…… But don’t worry huyu mungu wa mchongo hayupo, uamizi ni wako namna ya kuyapa sababu na maana maisha
Sawa tufanye huyo Mungu hayupo...hicho kilichotuleta kwenye hii Dunia ambayo furaha na huzuni vinaambatana kwanini tusingekuwepo kwingine?
 
Hawaamini, wengi wao wanasema hawajui chanzo cha binadamu, wengine wanasema binadamu hana chanzo, wengine wanasema chanzo ni nothing.
Kwahiyo binadamu alitokea ni kama bahati mbaya tu?
 
Sababu za kuubwa ipo wazi kabisa
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Sababu ya mateso na kifo nayo ipo wazi
Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

Mwanzo 3:18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;

Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Hatupo hapa kwa kupita kama watu wasemavyo hapana tupo kwa majibu wa kanuni hizo hapo juu je nini kitafaya baada ya kufa ni somo la pana sana na limejaaa siri ngumu sana kulingana na maandiko baada kufa kuna naisha mengine

Ufunuo wa Yohana 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufunuo wa Yohana 21:2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Ufunuo wa Yohana 21:3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Pamoja na hayo aliweka sifa na hizi ni sifa za wasio weza kuigia

Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Kwa mujibu wa biblia
Kama lengo ilikuwa tuletwe duniani kutawala hivyo vitu vyote ambavyo muumbaji wetu aliviweka tukaviongoze kwa ajili yake kwanini alishindwa kumuumba mwanadamu kwenye mithiri ya kutosikia la mtu mwingine zaidi yake? Huoni hapa hakukuwa na nia njema kwa kumbe chake?

Bado majibu ya biblia yana mapungufu makubwa sana kuliko uhalisia na sababu ya kutupitisha kwenye hii Dunia ambayo ina karaha nyingi kwasababu kwenye kuviongoza hivyo vitu tusingewekewa vifo na maradhi ambavyo vinapelekea kutotawala vizuri vitu vyake
 
Ninachoamini Mimi, binadamu akiamua kuwa na upendo, chuki haiwezi kuwa na nafasi kwake na chuki likewise. Chuki ni tabia ambayo hupandwa moyoni, Kama vile unavyoweza kumpenda mama yako,ndugu zako,rafiki yako ama mpenzi wako.

Vilevile unaweza kujifunza kumpenda MUNGU. Siyo rahisi kwasababu ukiwa Duniani, utapitia mapito,pamoja na tafakari, itafikia hatua utasema hakuna MUNGU. Lakini ukiwa na Imani utaendelea kumpenda na utaendelea kuvumilia mpaka mwisho.

Chuki hupandwa moyoni na upendo hupandwa moyoni, you have everything to choose.
Kwanini hatukuumbwa na upendo tu maana ndiyo unasisitizwa hata kwenye vitabu vyake...
Kulikuwa na haja gani tukawekewa nafasi ya kupokea chuki, hila na fitina wakati vitu vyote hivyo havimpendezi Mungu
 
Sababu kubwa ya kuumbwa sisi bin adam ni kumwabudu muumba wetu aliyetuumba
Sawa hiyo ni sababu ya kuumbwa na je ni ipi sababu ya kutuleta hapa duniani?
 
Everyone loves themselves no matter they know it or not.
Hata anayejiua anajiua kwasababu anadhani ni jambo la upendo anajifanyia kuwa ni Bora asiwepo kuliko kuendelea kuwepo.

Kila kiumbe ni selfish na Unselfish at the same time. How?
Kwasababu there is no self.
So selfishness is just a made up concept.

We all depend on each other. So huwezi kuwa selfish kwakuwa lazima Kuna vitu/watu unawategemea ili usavaivu hivyo lazima uwaombee mema hao watu ili wewe usavaivu.
Hao watu/vitu unaweza kuwajua au usiwajue ila unawategemea.

Leo unaombea wafanyakazi wa Apple usiowajua wapate akili nzuri ili watengeneze Version mpya utakayoipenda. Unawaombea Moderators na IT wa JF waimaintain iendelee kurun ili u enjoy kuperuzi, unawaombea wachina wanaokutengenezea nguo unazovaa wanendelee kuthrive ili usitirike.

Hivyo huwezi kuwa selfish. Kwakuwa Kila kitu ni part of the same ecosystem.
There is no self without the other. It is the same thing.

Labda useme the whole universe is selfish for its own thriving.

nA ulifika level hiyo concept ya selfishness haisimami kwasabu ili uwe selfish lazima kuwe na other, Sasa universe haiwezi kuwa selfish kama hakuna other universe inayocompete nayo resources.
Na hata kama itakuwepo basi universes zote zitakuwa Kwenye same ecosystem.

Meaning Everything is one thing.
There is no self.
Uko vizuri sana we're all connected.
 
Tumeletwa duniani ili tupitie mtihani wa imani utiifu na matendo mema na ni Uhuru kila mtu achague atamtii nani Mwenyezi Mungu au matamanio ya nafsi

Kama tungeliumbwa moja kwa moja kwa ajili ya Pepo bila uchaguzi, hilo lingekuwa sawa na malaika lakini wanadamu tumepewa hiari ya kuchagua ndiyo maana kuna ujira kwa wema na adhabu kwa uovu Allah anasema katika Qur'an 👇🏽


Surat Al-Mulk (67:2)
"Ambaye ameumba mauti na uhai ili akujaribuni, ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kughufuria".



Maisha haya si lengo lenyewe ni darajatu la kuelekea kwenye maisha ya milele.

Surat Al-Ankabut (29:64)
"Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na hakika makaazi ya mwisho ndiyo maisha hasa laiti wangekuwa wanajua."


Surat An-Nisa (4:40)
"Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata chembe ya udongo..."

Surat Taha (20:123-124)
"...Hapo utakapokujieni uwongofu kutoka Kwangu, basi atakayeufuata uwongofu Wangu hatapotea wala hatataabika. Na atakaye puuza maonyo Yangu, basi bila shaka atakuwa na maisha ya dhiki..."

Surat Al-Mu’minun (23:115)
"Je, mlidhani kwamba tumewaumba kwa bure tu, na ya kwamba hamtarudishwa kwetu?"


Mwenyezi Mungu alituumba kwa lengo gani

Surat Adh-Dhariyat (51:56)
"Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu."

Surat Al-Baqara (2:286)
"Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yeyote ila kwa kadiri ya uwezo wake..."
Katika kumuabudu kwanini ametuwekea shida, mateso, karaha na dhiki vitu ambavyo vinamnyima binadamu wakati mwingine kufikia hilo lengo la kuabudu
 
Back
Top Bottom