Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...
Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)
Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?
Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?
Tumeletwa duniani ili tupitie mtihani wa imani utiifu na matendo mema na ni Uhuru kila mtu achague atamtii nani Mwenyezi Mungu au matamanio ya nafsi
Kama tungeliumbwa moja kwa moja kwa ajili ya Pepo bila uchaguzi, hilo lingekuwa sawa na malaika lakini wanadamu tumepewa hiari ya kuchagua ndiyo maana kuna ujira kwa wema na adhabu kwa uovu Allah anasema katika Qur'an 👇🏽
Surat Al-Mulk (67:2)
"Ambaye ameumba mauti na uhai ili akujaribuni, ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kughufuria".
Maisha haya si lengo lenyewe ni darajatu la kuelekea kwenye maisha ya milele.
Surat Al-Ankabut (29:64)
"Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na hakika makaazi ya mwisho ndiyo maisha hasa laiti wangekuwa wanajua."
Surat An-Nisa (4:40)
"Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata chembe ya udongo..."
Surat Taha (20:123-124)
"...Hapo utakapokujieni uwongofu kutoka Kwangu, basi atakayeufuata uwongofu Wangu hatapotea wala hatataabika. Na atakaye puuza maonyo Yangu, basi bila shaka atakuwa na maisha ya dhiki..."
Surat Al-Mu’minun (23:115)
"Je, mlidhani kwamba tumewaumba kwa bure tu, na ya kwamba hamtarudishwa kwetu?"
Mwenyezi Mungu alituumba kwa lengo gani
Surat Adh-Dhariyat (51:56)
"Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu."
Surat Al-Baqara (2:286)
"Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yeyote ila kwa kadiri ya uwezo wake..."