Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Tumeletwa duniani ili tupitie mtihani wa imani utiifu na matendo mema na ni Uhuru kila mtu achague atamtii nani Mwenyezi Mungu au matamanio ya nafsi

Kama tungeliumbwa moja kwa moja kwa ajili ya Pepo bila uchaguzi, hilo lingekuwa sawa na malaika lakini wanadamu tumepewa hiari ya kuchagua ndiyo maana kuna ujira kwa wema na adhabu kwa uovu Allah anasema katika Qur'an 👇🏽

Surat Al-Mulk (67:2)
"Ambaye ameumba mauti na uhai ili akujaribuni, ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kughufuria".

Maisha haya si lengo lenyewe ni darajatu la kuelekea kwenye maisha ya milele.

Surat Al-Ankabut (29:64)
"Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na hakika makaazi ya mwisho ndiyo maisha hasa laiti wangekuwa wanajua."

Surat An-Nisa (4:40)
"Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata chembe ya udongo..."

Surat Taha (20:123-124)
"...Hapo utakapokujieni uwongofu kutoka Kwangu, basi atakayeufuata uwongofu Wangu hatapotea wala hatataabika. Na atakaye puuza maonyo Yangu, basi bila shaka atakuwa na maisha ya dhiki..."

Surat Al-Mu’minun (23:115)
"Je, mlidhani kwamba tumewaumba kwa bure tu, na ya kwamba hamtarudishwa kwetu?"

Mwenyezi Mungu alituumba kwa lengo gani

Surat Adh-Dhariyat (51:56)
"Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu."

Surat Al-Baqara (2:286)
"Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yeyote ila kwa kadiri ya uwezo wake..."
Mkakariri hadi na Kiarabu ili tu mpate nafasi ya kwenda kwa Mnyaazi Mungu. Kiarabu ni kitukufu kuliko Kimakonde au sio 😂😂😂
 
Dunia ni darasa, la kutuwezesha kuishi na Mungu milele.
Huyo Mungu alishindwaje kutuumba binadamu tuishi nae milele hukohuko mbinguni?

Kulikuwa na haja gani ya Dunia?

Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?
Kama tukiamua kumpa Yesu maisha yetu tutapokea wokovu.
Tukimpa huyo Yesu maisha yetu anafaidika nini?

Tusipompa huyo Yesu maisha yetu anapungukiwa nini?

Huyo Yesu yupo so insecure hadi ahitaji maisha yetu?
 
Natamani Ndugu Kiranga uje uelimishe Watanzania wenzako juu ya hili maana mada hizi huwa unazielezea vizuri sana, uko vyema kwenye Philosophy
 
Kutokana na Maandiko Matakatifu tunapata fununu kuhusu kwa nini binadamu aliumbwa na kuwekwa hapa duniani.

Kwanza tunapata kujua ya kwamba binadamu aliumbwa kwa nafsi hai yenye roho na mwili ulioumbwa kwa mavumbi. Wakati wajoli wao malaika waliumbwa kwa nafsi hai kupitia pepo na miali ya moto.

Asili ya maisha ya binadamu ni juu ya nchi, ambayo ni nchi kavu yenye kuzungukwa na sura za maji na kuweza kuonekana kwa macho ya kawaida ya kimwili.

Asili ya maisha ya malaika ni juu ya nchi, yaani mbinguni ambapo ni pepo zinazoonekana kwa macho ya kiroho tu.

Kwa picha hiyo, tunapata fununu kuhusu viumbe vya aina mbili ambavyo viliumbwa na Mungu ili viweze kumtumikia katika ufalme wake.

Viumbe vilivyoumbwa hapo awali kabla ya uasi wa Ibilisi na malaika wake walikuwa ni malaika. Hawa waliumbwa moja kwa moja na kuwa viumbe vyenye nafsi hai.

Tofauti na mwanadamu ambaye uzao wake ulipata kuwa nafsi hai baada ya kujaamiana kwa mtu mume na mtu mke, mimba kutungwa, na hatimaye nafsi hai mpya kuzaliwa.

Kwa nini mchakato huu mpya wa uumbaji wa nafsi kupitia binadamu uje badala ule wa awali wa kimalaika?

Sababu kubwa ilitokana na uasi wa kule mbinguni na hatua zilizochukuliwa baada ya uasi huo.

Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwafukuza malaika wote waasi, na mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

Pili, ilikuwa ni kutupwa duniani, na kuwekwa katika vifungo chini kuzimu, katika sura ya dunia ambayo ilikuwa imezungukwa na maji.

Hapa tunapata kuona sababu ya Mungu Muumba kutotaka kuviangamiza viumbe hivi viasi, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, angalienda kinyume na asili yake ya haki, ili kiumbe chake kimtii kwa hiari na wala siyo kwa hofu.

Ndipo Mungu akafanya shauri na wale malaika watiifu kupitia uumbaji wa mwanadamu, ili kupitia kiumbe hiyu mpya, hukumu ya haki kwa wale malaika waovu ipate kutimia.

Tunaona awali ya yote akifanya uumbaji kwa kutenganisha nchi na maji na kumweka Adamu na Eva juu yake, katika sehemu hii ambayo Ibilisi na malaika zake waliwekwa vifungoni.

Huu ulikuwa ni mradi mpya wa kimbingu ukiwa mahususi kama kipimo cha uharibifu wa dhambi na hatima ya kwendwa kuitokomeza kabisa. Ndiyo maana mwanadamu alipoumbwa, Mungu alisema na tumfanye kwa mfano wetu, ya utashi wa kuamua kutenda mema ama mabaya.

Hii ndiyo sababu ya uwepo wa miti miwili, yaani wa uzima, na mwingine wa kuweza kutambua mema na mabaya, katika bustani ya Edeni ambayo kiumbe hiki kipya kilipewa amri ya kutokula matunda yake wala kuisogelea.

Adam ambaye ndiye aliumbwa kwanza alipewa amri moja kwa moja na Muumbaji wake, aliishi kwa kuitii amri hii. Lakini ujio wa baadaye wa Eva ulitumika kama sababu ya uvunjaji wa amri hii, ambayo ndiyo ambayo ilifanya uzao wa wanadamu kuagukia katika adhabu ya kifo na kuzimu.

Ibilisi alipewa fursa ya kumjaribu mwanadamu katika dunia hii. Nao wakawa dhaifu na kujikuta wameanguka.

Kwa hiyo sababu kubwa ya mwanadamu kuumbwa na kuwekwa duniani, ilikuwa ni mradi wa kimbingu ili hukumu ya haki iweze kutendwa juu ya wale malaika waasi. Hii ni sababu kwa nini hawakuangamizwa mara baada ya kufanyi uasi ule, kwa kufanya vile malaika waliobakia wangalikuwa na hofu kubwa kwa Muumbaji wao. Na ingalikuwa ni kinyume cha asili ya Mungu ya kuvitaka viumbe alivyoviumba vimtii kwa hiari wala siyo kwa vitisho.
 
Kutokana na Maandiko Matakatifu tunapata fununu kuhusu kwa nini binadamu aliumbwa na kuwekwa hapa duniani.

Kwanza tunapata kujua ya kwamba binadamu aliumbwa kwa nafsi hai yenye roho na mwili ulioumbwa kwa mavumbi. Wakati wajoli wao malaika umbwa kwa nafsi za hai zilizoumbwa kwa pepo na miali ya moto.

Asili ya maisha ya binadamu ni juu ya nchi, ambayo ni nchi kavu yenye kuzungukwa na sura za maji na kuweza kuonekana kwa macho ya kawaida ya kimwili.

Asili ya maisha ya malaika ni juu ya nchi, yaani mbinguni ambapo ni pepo zinazoonekana kwa macho ya kiroho tu.

Kwa picha hiyo, tunapata fununu kuhusu viumbe vya aina mbili ambavyo viliumbwa na Mungu ili viweze kumtumikia katika ufalme wake.

Viumbe vilivyoumbwa hapo awali kabla ya uasi wa Ibilisi na malaika wake walikuwa ni malaika. Hawa waliumbwa moja kwa moja kwa moja na kuwa viumbe vyenye nafsi hai.

Tofauti na mwanadamu ambaye alipata kuwa nafsi hai baada ya kujaamiana kwa mtu mume na mtu mke, mimba kutungwa, na hatimaye nafsi hai kuzaliwa.

Kwa nini mchakato huu mpya wa uumbaji wa nafsi kupitia binadamu uje badala ule wa awali wa kimalaika?

Sababu kubwa ilitokana na uasi wa kule mbinguni na hatua zilizochukuliwa baada ya uasi huo.

Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwafukuza malaika wote waasi, na mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

Pili, ilikuwa ni kutupwa duniani, na kuwekwa katika vifungo chini kuzimu, katika sura ya dunia ambayo ilikuwa imezungukwa na maji.

Hapa tunapata kuona sababu ya Mungu Muumba kutotaka kuviangamiza viumbe hivi viasi, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, angalienda kinyume na asili yake ya haki, ili kiumbe chake kimtii kwa hiari na wala siyo kwa hofu.

Ndipo Mungu akafanya shauri na wale malaika watiifu kupitia uumbaji wa mwanadamu, ili kupitia kiumbe hiyu mpya, hukumu ya haki kwa wale malaika waovu ipate kutimia.

Tunaona awali ya ya yote akifanya uumbaji kwa kutenganisha nchi na maji na kumweka Adamu na Eva juu yake, katika sehemu hii ambayo Ibilisi na malaika zake waliwekwa vifungoni.

Huu ulikuwa ni mradi mpya wa kimbingu ukiwa mahususi kama kipimo cha uharibifu wa dhambi na hatima ya kwendwa kuitokomeza kabisa. Ndiyo maana mwanadamu alipoumbwa, Mungu alisema na tumfanye kwa mfano wetu, ya utashi wa kuamua kutenda mema ama mabaya.

Hii ndiyo sababu ya uwepo wa miti miwili, yaani wa uzima, na mwingine wa kuweza kutambua mema na mabaya, katika bustani ya Edeni ambayo kiumbe hiki kipya kilipewa amri ya kutokula matunda yake wala kuisogelea.

Adam ambaye ndiye aliumbwa kwanza alipewa amri moja kwa moja na Muumbaji wake, aliishi kwa kuitii amri hii. Lakini ujio wa baadaye wa Eva ulitumika kama sababu ya uvunjaji wa amri hii, ambayo ndiyo ambayo ilifanya uzao wa wanadamu kuagukia katika adhabu ya kifo na kuzimu.

Ibilisi alipewa fursa ya kumjaribu mwanadamu katika dunia hii. Nao wakawa dhaifu na kujikuta wameanguka.

Kwa hiyo sababu kubwa ya mwanadamu kuumbwa na kuwekwa duniani, ilikuwa ni mradi wa kimbingu ili hukumu ya haki iweze kutendwa juu ya wale malaika waasi. Hii ni sababu kwa nini hawakuangamizwa mara baada ya kufanyi uasi ule, kwa kufanya vile malaika waliobakia wangalikuwa na hofu kubwa kwa Muumbaji wao. Na ingalikuwa ni kinyume cha asili ya Mungu ya kuvitaka viumbe alivyoviumba vimtii kwa hiari wala siyo kwa vitisho.
Wewe uliumbwa au Mama yako alikuzaa?
 
Hakuna, ila bado najiuliza wanawake wanafaidi nini zaidi ya pombe huko peponi
Wanawake hawakusahalika watarejeshwa katika hali ya ujana uzuri furaha na neema zisizo na mfano duniani watapata Nguo nzuri, mapambo na furaha ya milele na Kuishi bila Uchungu, Hedhi, wivu au mateso yoyote na Allah anasema hivi katika Surat An-Nisa (4:124)

"Na anayefanya matendo mema, akiwa mwanaume au mwanamke, naye ni Muumini basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kidogo".

Surat Al-Ahzab (33:35)
"Hakika wanaume Waislamu na wanawake Waislamu na waumini wanaume na waumini wanawake... Allah amewaandalia hao wote msamaha na ujira mkubwa."

Mtume Muhammad (SAW) pia alisema:
"Wanawake wa duniani walioingia Peponi kwa matendo yao mema watakuwa bora zaidi kuliko Hur al-‘Ayn."

(Sahih – Tabrani, Al-Bayhaqi)
Sheikh Al-Albani aliithibitisha kuwa sahihi
 
Jamani hayo ma surat al nini sijui yanakera. Tueleweshe tu na maneno ya Kiswahili
 
Hili ni fumbo la aina gani mkuu?

Vitabu vya Mungu vinaeleza kwamba binadamu wapo duniani..je ni uongo?

Science nayo imethibitisha kwamba binadamu wako Duniani kupitia theories nyingi...je tusiamini hizi hoja?
Hakuna vitabu vya Mungu.

Hakuna Mungu aliyeandika kitabu chochote kile.

Kuna vitabu vya binadamu vinavyodaiwa na kuitwa vya Mungu.

Hakuna Mungu.
 
Wanawake hawakusahalika watarejeshwa katika hali ya ujana uzuri furaha na neema zisizo na mfano duniani watapata Nguo nzuri, mapambo na furaha ya milele na Kuishi bila Uchungu, Hedhi, wivu au mateso yoyote na Allah anasema hivi katika Surat An-Nisa (4:124)

"Na anayefanya matendo mema, akiwa mwanaume au mwanamke, naye ni Muumini basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kidogo".

Surat Al-Ahzab (33:35)
"Hakika wanaume Waislamu na wanawake Waislamu na waumini wanaume na waumini wanawake... Allah amewaandalia hao wote msamaha na ujira mkubwa."

Mtume Muhammad (SAW) pia alisema:
"Wanawake wa duniani walioingia Peponi kwa matendo yao mema watakuwa bora zaidi kuliko Hur al-‘Ayn."

(Sahih – Tabrani, Al-Bayhaqi)
Sheikh Al-Albani aliithibitisha kuwa sahihi
Amen.
 
Ikawaje mungu wao awe na ahadi tofauti na Mungu wako, huku hakuna kula wala kunywa ni harusi moja tu ya mwana kondoo , na kwenu ni bikra 72 na mito ya faru john?
Kwasababu walibadilisha maandiko hata Yesu alikemea kuhusu kalamu ✏️ za waandishi zimeifanya Taurati kuwa uwongo
Yeremia 8:8 - Neno: Bibilia Takatifu
“ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara kwa sababu tunayo Torati ya Mwenyezi Mungu,” wakati kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi imeandika kwa udanganyifu?
 
Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...

Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)

Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?

Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?

View: https://youtu.be/y0f56lgP-Tw?si=DzXtC83Yv5BkfmMQ
 
Kwasababu walibadilisha maandiko hata Yesu alikemea kuhusu kalamu ✏️ za waandishi zimeifanya Taurati kuwa uwongo
Yeremia 8:8 - Neno: Bibilia Takatifu
“ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara kwa sababu tunayo Torati ya Mwenyezi Mungu,” wakati kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi imeandika kwa udanganyifu?
🚮
 
Back
Top Bottom