Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Yaani mungu mwenye uwezo wote anataka tumtumikie? Tumpende? Ili iweje?
Ninachoamini Mimi MUNGU ni superior one, ni zaidi ya Emperor, ni zaidi ya king, kwahyo ni lazima nimtumikie, ni lazima nimpende kwasababu he own everything precious like eternal life.
 
Maisha ni fumbo.
Maisha ya duniani yalikuwa ni zawadi na sio adhabu, changamoto ni binadamu kutaka kuishi against nature, hapo ndipo mateso yanapo anzia.

Swali: Unauhakika gani kwamba upo duniani?
Umeshawahi kuota ndoto na ukajiona upo huko ndotoni? What if na hapa upo ndotoni na pengine ukifa hapa ndo unaamka kutoka usingizi uliokuwapo?
Eti tupo ndotoni. Man, wariz dhis
 
Na huo udhaifu ndo dhambi yenyewe adhabu yake ni kuchomwa moto wa jehanam
Kulikuwa na haja gani tupewe udhaifu ni kwamba hakujua kama utatupelekea kwenye kutenda dhambi?
Au kutuleta duniani tukiwa dhaifu na kutenda dhambi ndiyo furaha yake?
 
Shida ipo kwa jinsi alivyoniumba yeye. Mimi najiona sawa lakini sasa amri ni nyingi usifanye hivi usifanye kile
Je unachokiona kiko sawa, umewahi kufikiri kinaweza kuwa na madhara kiasi gani kwa wengine?
Kwa mazingira je?

Hapo ndo amri zinaanza sasa, maana binadamu wakikosa mipaka ni disaster.
 
Mi sidhani kama tupo hapa labda eti kuna kitu inabidi tukitimize. Tupo hapa naturally tu kama ilivyo kwa mbuzi, ng'ombe, nzi nk
Kwa hiyo usijiulize sana, hamna sababu ya msingi sisi kuwepo hapa. We ishi, struggle, kufa uache nafasi waje wengine
 
MAISHA ni Nyumba Ila sisi binadamu ni mafundi wa aina mbalimbali.

Kwahiyo tupo hapa kujenga Nyumba Inayoitwa MAISHA.

Kwahiyo kila mmoja atachangia kwa nafasi yake mwingine atakuwa mbeba zege , mwingine mpiga plasta mwingine , atakuwa anaezeka na wengine watakuwa wanabeba matofali huku wengibe wakichanganya udongo na baadhi watakuwa wanaiba misumali na cement n.k na hao wezi ndo useless creatures .

Kwahiyo ukishajua maisha ni Nyumba inayojengwa jitahidi ujichagulie kitengo unachokipenda usipofanya hivyo wajanja watakuchagulia .

Na ukichagua kitengo chako na kukifanyia Kazi effectively ukifa watu watasema you were a good man na ukiwa unaiba materials katika ujenzi wa hiyo Nyumba ukifa watu watafanya Kama kule kongwa .


So hayo ndo maisha do something with none benefits but benefits of others.
 
Kama asingetuumba uwepo wake usingejulika mkuu.
Uwezo anao wa kutufanya vyovyote anavyotaka kwahyo hata kwa kumjua yeye angetumia uwezo wake kutupa uwezo wa kumjua...
Sasa kwanini alituleta duniani je kwa lengo hilo la kumjua tu?
 
Mungu ni mwema sana, Maisha ni baraka. Unaefikiri upo hapa duniani kuteseka ebu jaribu kufa uone. Maisha ni matamu na kifo hasa ndo adui mkubwa.
Biblia inasema "Adui wa mwisho atakae batilishwa ni mauti."
 
Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...

Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)

Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?

Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?
Kwa mujibu wa hekaya za kiyahudi kikristo na kiislam Mungu katuleta duniani ili tutekeleze maelekezo yake yasiotekelezeka kwa kutuletea shetani duniani ili ahakikishe tunamkosea Mungu ili apate sababu ya kutuchoma moto MILELE baada ya maisha haya mafupi na mateso matupu


…… But don’t worry huyu mungu wa mchongo hayupo, uamizi ni wako namna ya kuyapa sababu na maana maisha
 
Ninachoamini Mimi MUNGU ni superior one, ni zaidi ya Emperor, ni zaidi ya king, kwahyo ni lazima nimtumikie, ni lazima nimpende kwasababu he own everything precious like eternal life.
Unaposema kumtumikia, unamaanisha kuna mambo fulani unamfanyia. Sasa sisi binadamu tunawezaje "kumtumikia" mungu? Unamtumikia kwa lipi hasa?
 
Nadhani kifo kipo ili kupata nafasi ya binadamu wengine kuzaliwa. Imagine watu wangekuwa hawafi tungebanana sana
Ni kwamba Muumba hana uwezo wa kubalance namba ya watu na eneo aliloliumba?
Una watoto 10 na wewe na mumeo inamaana mko 12 inakuwaje uamue kujenga nyumba ya kuishi watu 5 halafu utegemee wengine uwaue ili mbaki idadi uliyokusudia?
 
Back
Top Bottom