SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,214
- 5,011
Binadamu tunajiona viumbe waliobarikiwa kwa akili na maarifa. Tumegundua teknolojia, tumeandika vitabu, tumejenga miji mikubwa, na tumeunda tamaduni nyingi. Lakini tukichunguza kwa undani, yote haya hayajabadilisha ukweli wa msingi,,,, binadamu hakuja duniani kufaidika kwa namna ya kudumu.
Kwa sababu matukio makuu ya binadamu ni mawili tu .... ni kuzaliwa na kufa. mwisho wa yote bado ni uleule. Hakuna ugunduzi wa kisayansi, hakuna teknolojia ya kisasa, wala falsafa ya kina inayoweza kubadilisha ukweli huu wa kimsingi.
Binadamu tunaishi kwa muda mfupi, tukijidanganya kuwa tuna faida kubwa, lakini dunia yenyewe haijabadilika kwa ajili yetu.
Miti bado inakua bila kujali nani yupo, bahari bado inacheza mawimbi yake bila kuuliza ruhusa, na jua bado linazunguka ratiba yake bila msaada wa binadamu.
Hata ugunduzi mkubwa kama ndege au smartphone za mkopo, havibadilishi ukweli kwamba wateja wa watu credit tutaondoka duniani bila kujua siri kamili ya maisha.
Sisi ni kama mgeni tuliovamia tamasha bila tiketi. Tunafurahia muziki, tunacheza kidogo, tunabishana na wenzetu, lakini mwisho wa siku tunatolewa nje kwa lazima.
Dunia haikuwahi kutuomba tuje, na haitulili tubaki.
Kiuhalisia, binadamu hakuja duniani kwa faida yake. Yote tunayofanya ni michezo ya muda mfupi, tamthilia ya kujipa matumaini.
Mwisho wake unabaki pale pale: kuzaliwa na kufa.
Dunia inaendelea bila sisi, na sisi tunaondoka bila kubadilisha chochote cha msingi kwa nafsi zetu.
Usijipe stress, kumbuka kuna maisha hata bila hela za kausha damu na simu za watu credit