Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Kwanini hatukuumbwa na upendo tu maana ndiyo unasisitizwa hata kwenye vitabu vyake...
Kulikuwa na haja gani tukawekewa nafasi ya kupokea chuki, hila na fitina wakati vitu vyote hivyo havimpendezi Mungu
Hatujawekewa nafasi ya kupokea chuki, tumepewa nafasi ya kuchagua kati ya upendo na chuki. Ninaamini katika kitabu cha mwanzo, MUNGU alipomuumba mwanadamu na kumuweka katika bustani ya amani.

Ni baada ya binadamu kujua kwamba Kuna mabaya na mema tayari alikuwa uchi, mema na mabaya yalipokuwa mbele zake, alifanya yale yaliyompendeza. Baya hupandwa moyoni kwasababu ya madhaifu na kwasababu ya asili zetu.
Wapo ambao walizaliwa Ili waende motoni. Utajiuliza kwanini MUNGU aliruhusu zipotee, Ni kwasababu hizo Roho MUNGU alijua haziwezi kubadilika kwasababu ya asili zao usaliti. Mfano mzuri ni shetani, ni kiumbe aliyeumbwa katika Hali ya kipekee lakini mwishowe alikuwa msaliti.

Unaweza kujiuliza MUNGU hakujuwa kwamba shetani atakuja kuwa msaliti? Na Kama alijua kwanini alimuumba? Kwanini MUNGU alifanya hayo yote? MUNGU pekee ndiye anayejua.

Binadamu alichagua kuishi Kwa uhuru, Binadamu aliamua kubadilika kwasababu ya tamaa zake. MUNGU habadiliki na Wala Sheria yake habadiliki.

Umepewa uhuru utachagua uutumieje!
 
Hukutengenezewa kama upungufu, ni zawadi, kwamba uwe na free will. changamoto tu ni kuwa will power haina mipaka, na unaweza ukafanya jambo hata kinyume na aliyekupa huo uwezo wa kuchagua. Hasa ndo kinachokutesa.

Hasira ya Mungu ipo kwasababu uliumbwa ukiwa mkamilifu. Kwa hiyo mapungufu uliyonayo ni ya kujitakia tu, ni kama unavyolea mtoto wako alaf afanye kitu tofauti na unavyo mwelekeza utakasirika
Kwanini atuumbe na mapungufu ya kujitakia makusudi ili baadae aje kutuchoma moto.
 
Wewe uliumbwa au Mama yako alikuzaa?
Mkuu, mimi nilizaliwa kimwili na mama yangu, lakini roho yangu ilitoka kwa Mungu wako. Huu ndivyo ilivyo mchakato wa asili wa uumbaji wa mwanadamu, ukiondoa uumbaji wa mwanzo wa Adamu na Eva.
 
Mkuu, mimi nilizaliwa kimwili na mama yangu, lakini roho yangu ilitoka kwa Mungu wako. Huu ndivyo ilivyo mchakato wa asili wa uumbaji wa mwanadamu, ukiondoa uumbaji wa mwanzo wa Adamu na Eva.
Unathibitishaje una roho?

Thibitisha roho ipo?
 
Mungu mawazo yake yapo juu sana kuliko sisi kuna wakati tunajitqhidi kuelewa lakini ni ngumu sana
Nilipoanza kuchunguza mambo sana kwa akili hizi za kibinadamu nilipata ufahama kwamba ili ujue uzuri lazima na ubaya uwepo hakuna namna yoyote ya kujua uzuri ila ubaya kuwepo hapo ndipo tunajua jua au nuru ni njema kwa sababu giza lipo,
Hata Mungu vilevile uwezi kujua yupo kama upande wa pili haupo so itoshe kusema Mungu alipenda tuwe na chaguo la kufata
Mungu hawezi kumbuumba binadamu anayeweza kujua uzuri bila ubaya kuwepo??
 
Hoja nyeti sana lakini mmoja amejibu kwa uelewa wake.Lakini je wale wanaosema hakuna Mungu,wewe wao wenyewe haitoshi kuwa ni alama ya uwepo wake?
 
Hatujawekewa nafasi ya kupokea chuki, tumepewa nafasi ya kuchagua kati ya upendo na chuki. Ninaamini katika kitabu cha mwanzo, MUNGU alipomuumba mwanadamu na kumuweka katika bustani ya amani.

Ni baada ya binadamu kujua kwamba Kuna mabaya na mema tayari alikuwa uchi, mema na mabaya yalipokuwa mbele zake, alifanya yale yaliyompendeza. Baya hupandwa moyoni kwasababu ya madhaifu na kwasababu ya asili zetu.
Wapo ambao walizaliwa Ili waende motoni. Utajiuliza kwanini MUNGU aliruhusu zipotee, Ni kwasababu hizo Roho MUNGU alijua haziwezi kubadilika kwasababu ya asili zao usaliti. Mfano mzuri ni shetani, ni kiumbe aliyeumbwa katika Hali ya kipekee lakini mwishowe alikuwa msaliti.

Unaweza kujiuliza MUNGU hakujuwa kwamba shetani atakuja kuwa msaliti? Na Kama alijua kwanini alimuumba? Kwanini MUNGU alifanya hayo yote? MUNGU pekee ndiye anayejua.

Binadamu alichagua kuishi Kwa uhuru, Binadamu aliamua kubadilika kwasababu ya tamaa zake. MUNGU habadiliki na Wala Sheria yake habadiliki.

Umepewa uhuru utachagua uutumieje!
Mkuu hivi huko PEPONI watakao ingia huko watakua na UHURU wa kufanya DHAMBI kama ilivyokua hapa Duniani?
 
Hoja nyeti sana lakini mmoja amejibu kwa uelewa wake.Lakini je wale wanaosema hakuna Mungu,wewe wao wenyewe haitoshi kuwa ni alama ya uwepo wake?
HAITOSHI kabisaa
Mungu muweza wa yote anatengenezaje dunia lenye mabalaa yote haya na binadamu wa mfano wake wenye UKATILI usio elezeka?

Kili mshinda nini kuumba dunia yenye AMANI tu?
 
Watu wengi “wanaamini” Mungu kwasababu ya VITISHO eti wanaogopa watachomwa moto wa milele Jehanamu 😂

Mind you kuna Miungu zaidi ya 1000 na kila mmoja ana lwake

Mimi sitaki kuamini nataka KUMJUA kama yupo na ni WAJIBU wake kuhakikisha watu wote tunamjua
Ndiyo kazi tuliyo nayo ya kusoma na kwa upande Mungu ameshatekeleza kwa kuweka ishara na kuleta Manabii

Na ukiangalia Dunia kwa kina si sehemu ya kujimwaga kustarehe unaitafuta pesa kwa njia za halali na haramu alafu unakufa kuna mengi ya kutafakarisha Mungu anasema katika Qur'an 29:64
"Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na hakika makaazi ya mwisho ndiyo maisha hasa laiti wangekuwa wanajua."
 
Malengo makuu ni 2
1. Kuwa ambassador wa Mungu duniani. That's why Mungu akamuumba mwanadamu kwa mfano wake.
2. Kutawala na kumiliki dunia yote.
Kitabu cha Mwanzo 1:27-28
Screenshot_20250820-085823.jpg
 
evolution.................................... hakuna cha Mungu hapa it is purely science..................
Kitu kina evolve vipi kutoka non life to life? Principle of biogenesis inasema life arises from pre-existing life.
 
Sawa hiyo ni sababu ya kuumbwa na je ni ipi sababu ya kutuleta hapa duniani?
Sasa wewe kwa akili yako unafikiri baada ya kuumbwa tulistahili kuwa wapi?
 
Back
Top Bottom