Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Tumeumbwa na Mungu, ila Mungu mwenyewe sio huyo tapeli mnayemsikia kanisani na msikitini
Mungu ni NATURE. Na nature always inajua namna ya kujibalance, so kufa ni njia nzuri ya kubalance mazingira. Ingawa sijui kama Nature ina akili au la ila sijui kwa nini haikuamua watu wachache tu waishi milee
Nature ni nini mkuu? Labda naweza kupata hoja mpya
 
Naona anayo mkuu, hata Mungu ametoa nafasi ya kuchagua,
Kama sio kwa free will basi angetuchagulia.
Ametuchagulia maana ili uende mbonguni ni lazima ufate vile anavyotaka yeye, na option nyingine ya shetani ni mateso. Inakuaje usema ni kwa free will.
Asingeweka adhabu akasema wanaoamua kunifata wanofate na ambao hawatataka kunifata haina shida maamuzi ni yao na hakuna baya lolote litakalowapata hiyo ndo ingekuwa free will.
 
Acha bana😀😀
Unajua bora ingekuwa kuuliwa lakini wanasema ule moto unaunguza milele na milele hauzimiki, yaani unaungua lakini kufa hufi. Ukatili wa aina gani huu
Ndo ule raha wakati unasubiria huo moto 😂😂😂.

Sasa duniani kwanini ujipe moto wakati moto utakua nao milele
 
Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...

Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)

Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?

Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?
Sababu za kuubwa ipo wazi kabisa
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Sababu ya mateso na kifo nayo ipo wazi
Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

Mwanzo 3:18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;

Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Hatupo hapa kwa kupita kama watu wasemavyo hapana tupo kwa majibu wa kanuni hizo hapo juu je nini kitafaya baada ya kufa ni somo la pana sana na limejaaa siri ngumu sana kulingana na maandiko baada kufa kuna naisha mengine

Ufunuo wa Yohana 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufunuo wa Yohana 21:2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Ufunuo wa Yohana 21:3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Pamoja na hayo aliweka sifa na hizi ni sifa za wasio weza kuigia

Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Kwa mujibu wa biblia
 
Nature ni nini mkuu? Labda naweza kupata hoja mpya
NATURE ni Asili
Ninavyosema naamini Mungu ni "Mother Nature," namaanisha kwamba ninaona nguvu ya kimungu au ya juu iko ndani ya asili yenyewe—miti, wanyama, maji, hewa, na kila kitu kinachohusiana na mazingira ya asili. Wazo hili linatokana na imani yangu kwamba asili ndiyo chanzo cha uhai, inayoleta maisha, kuyalinda, na kuwa na usawazo wa kila kitu duniani.

Kwa maneno rahisi, badala ya kuamini Mungu kama mtu, roho au nafsi ambayo inatufuatilia kila tunachofanya (umbea) kama katika dini nyingi, mimi naamini kwamba Nature yenyewe ina sifa za kimungu, kama vile uwezo wa kuumba, kuhifadhi, na hata kuharibu. Hii inaweza kuwa imani ya aina ya "pantheism," ambapo Mungu na asili ni kitu kimoja, na ni njia kuelezea heshima kubwa kwa Nature kama nguvu ya maisha.
 
Kwanini atupe nafasi ya kuwa na chuki kama alitaka tumpende?
Tunawezaje kumpenda tukiwa na chuki
Ninachoamini Mimi, binadamu akiamua kuwa na upendo, chuki haiwezi kuwa na nafasi kwake na chuki likewise. Chuki ni tabia ambayo hupandwa moyoni, Kama vile unavyoweza kumpenda mama yako,ndugu zako,rafiki yako ama mpenzi wako.

Vilevile unaweza kujifunza kumpenda MUNGU. Siyo rahisi kwasababu ukiwa Duniani, utapitia mapito,pamoja na tafakari, itafikia hatua utasema hakuna MUNGU. Lakini ukiwa na Imani utaendelea kumpenda na utaendelea kuvumilia mpaka mwisho.

Chuki hupandwa moyoni na upendo hupandwa moyoni, you have everything to choose.
 
Ndo ule raha wakati unasubiria huo moto 😂😂😂.

Sasa duniani kwanini ujipe moto wakati moto utakua nao milele
Hivi ni raha gani hizo ambazo mwanadamu anazikosa kama akiamua kuishi maisha ya utakatifu kiasi cha kuona maisha ni mabaya kama akizikosa?
Ni tamaa mbaya? ulevi? Uchawi? Uzinzi? Ufiraji? Wizi? Kutokuheshimu wazazi? Mbona ni ubatili tu huu.
Mtu yeyote aliyepevuka hata kama hamuamini Mungu anaelewa kabisa hapo ni kujilisha upepo tu wala hayana faida ila hasara.
 
Unaposema kumtumikia, unamaanisha kuna mambo fulani unamfanyia. Sasa sisi binadamu tunawezaje "kumtumikia" mungu? Unamtumikia kwa lipi hasa?
We believers, we live under his dominion, we follow his commandments,we repent to him and so we serve him.
 
Back
Top Bottom