Ni aibu kwa taifa letu kumuona Prof Abdulrazak Gurnah kama shujaa wa taifa letu, wakati huko nyuma hajawahi kutambuliwa kwa kazi alizofanya

Ni kweli huyu Prof ni mtu mwenye asili ya Tanzania visiwani na amekuwa akifundisha University of Kent tangu mwaka 1982. Amendika vitabu vingi tu lakini sijawahi kusikia serikali yetu ya Tanzania ikijisifu kuwa kuna mtanzania anafanya kazi nzuri za fasihi huko Uingereza. Sijawahi kusikia hata hapa nyumbani jina lake likitajwa.

Leo hii baada ya kushinda tuzo ya Nobel upande wa fasihi naona kila kiongozi wa serikali anataka kutuaminisha kuwa Prof Gurnah ni shujaa wa Tanzania.

Kama ni shujaa wa taifa letu mbona huko nyuma hamkumtambua? Mbona hamjawahi kuthamini kazi zake?

Kila jambo na wakati wake
 
Akija Tanzania ataruhusiwa kumiliki ardhi, kupiga kura na kugombea ubunge?
Nashindwa kuwaelewa watanzania kwa sasa.Wengi hamueleweki kabisa mnachoongea .Sasa nashindwa kuelewa ,kuwa hizi Nazi ni siasa au nikuilamu tu serikali?Huyo jamaa ,kaandika particular s zake mwenyewe kuwa ni mtanzania.Kawapa hao jamaa wa NOBEL .Ameshinda tuzo.Jamaa hao wa NOBEL wamtangaza wao wenyewe kupitia BBC ,Aljazeera kuwa mtanzania kashinda NOBEL ya literature. Je, tatizo la serikali lipo wapi ?Kama MTU kajileta mwenyewe na kusema ni mtanzania ,serikali imkatae ?Nendeni mmulaumu huyo Prof ,kwann anawapa serikali ujiko ,kuwa ni mtanzania. Serikali haina kosa.
 
nasema hiv mahali ambapo kitovu chako kikizikwa ndio kwenu.period.
gulnah ni mtanzania
kazi indeleee.#safari YA UNGA imeanza kuleta matokeo chanya.
kazi iendelee.
 
Sio watu wote ni wachawi wanaozika vitovu
nasema hiv mahali ambapo kitovu chako kikizikwa ndio kwenu.period.
gulnah ni mtanzania
kazi indeleee.#safari YA UNGA imeanza kuleta matokeo chanya.
kazi iendelee.
 
Ndugu yangu sina lengo la kuingilia mjadala wako na huyu ndugu mwengine, ila tu nataka kukuhakikishia kuwa huyu prof pamoja na wazanzibari wote walioondoka na Jemshid au waliondoka baada ya mapinduzi na kukimbilia uingereza kwa hifadhi ya ukimbizi wote kwa wakati mmoja au mwengine walipatiwa uraia wa uingereza.

Siwezi kukupa ushahidi wa passport yake, ila nitakwambia ninachokijua. Huyu Prof simjui in person zaidi ya kumuona mara kama mbili tu katika ghafla za wazanzibari hapa UK, hata hivyo ninawajua wengi wa walioondoka zanzibar wakati kama wa prof na ambao hadi leo wapo hapa UK. Yaani hata mmoja alikuwa ndio mwenyeji wangu nilipofika UK late 1980s. Nilichokuja kugundua ni kuwa ubalozi wa tanzania uingereza kwa kufuata amri ya nyerere ulikuwa unakataa kabisa kuwapa au ku renew pasport za wale wote ambao walikuja huku kama wakimbizi wa kisiasa katika miaka sitini.

Kwa hivyo ili kuweza kusafiri nje ya UK hawa jamaa wengi hawakuwa na jengine ila kuchukua uraia wa uingereza. Sasa kama utasoma historia ya huyu Prof utaona kuwa amesafiri nchi mbali mbali na kufanya kazi katika nchi mbali mbali, kuweza kufanya hilo ni lazima atumie passport, sasa hapo ndipo ujiulize mwenyewe ni passport gani alotumia ilhali passport za Zanzibar zilikuwa hazitumiki tena baaya ya muungano na wakati huo huo nyerere akiwawekea ngumu kuwapa passport za Tanzania?
Ndugu nami sina lengo la kukupinga... ni bahati mbaya sana, kuna wengine wanapenda kuingiza siasa hata kwa mambo ya kijinga, matokeo yake wanashindwa kuwa objective na matokeo yake kutawaliwana jazba! Na kwavile wanaweka jazba mbele, au inawezekana ni kwa sababu tu ya kuwa na uelewa hafifu, wanashindwa kuelewa hoja yangu...

Binafsi, SIJAKUBALI wala KUKATAA kwa sababu wanaofanya lolote kati ya hayo, wanafanya kwa kusukumwa na hisia, na si vinginevyo!!

Nikirudi kwenye mchango wako, post yako ya juu, umesema unamjua in personal lakini hapa unasema...
Hukukamilisha maneno yako. alikwenda uingereza kama mkimbizi siyo mhamiaji au mzamiaji, pia alikwenda kama mkimbizi kutoka nchi ya zanzibar sio tanzania kwani kwa wakati huo tanzania haikuwepo kabisa!!!!!
Maelezo hayo hapo juu yanatia shaka kumfahamu kwako kwa sababu nimesoma sources nyingi sana za kuaminika. Ingawaje kuna inconsistency lakini ZOTE zinaonesha aliondoka ZNZ wakati mapinduzi yameshapita kitambo!!

Kwenye Biography yake iliyoandikwa Chuo Kikuu cha Kent alikofanyia kazi kwa miaka kadhaa, inaonesha amezaliwa 1948 na aliondoka ZNZ akiwa 18! Hapo utaona ni somewhere 1966... 2 years of revolution!!

Kwenye mahojiano yake na The Guardian UK back 2001 alisema:-
They didn't call it asylum then. The phrase was illegal immigrant. When I came to England in the late 60s, Sergeant Pepper was ruling the land, de Gaulle was the Great Satan and it was only months before Enoch Powell made his classical allusion to the Tiber.
Unaona hapo anakuambia aliingia UK in the late 1960's! Je, hadi late 1960's hapakuwa na nchi inayoitwa Tanzania?!

Na kwa kawaida mtu unaweza kusahau yote lakini sio ubaguzi, na ndo maana bado alikuwa anamkumbuka Enoch Powell who made "his classical allusion to the Tiber"

What can we learn from it?

Waingereza wenyewe, kupitia BBC wanasema:-
Delivered to local Conservative Party members in Birmingham, days before the second reading of the 1968 Race Relations Bill, then MP Powell referenced observations made by his Wolverhampton constituents including "in 15 or 20 years' time the black man will have the whip hand over the white man".
Mzee Razak anakumbuka hiyo speech ya Kaburu la Kiingereza ambayo aliitoa 1968, just months baada ya kuingia UK!!

Na hata waliomfanya hivi atambulike duniani kote, yaani watoaji wa Nobel Prize, nao wanaandika bio yake kwamba:-
Gurnah belonged to the victimised ethnic group and after finishing school was forced to leave his family and flee the country, by then the newly formed Republic of Tanzania. He was eighteen years old.
Sasa how come mnadai aliondoka kabla ya Muungano,?! Ina maana wote hao wamedanganya?! Hata waajiri wake wamedanganya?

Na kuweka kumbukumbu sawa, sijamtaka yeyote atoe passport kwa sababu siwezi kuleta ubishani wa kijinga namna hiyo... yaani ubishani wa mtu umeshindwa halafu unajificha katika kutaka ushahidi unaojua kabisa sio rahisi kupewa!

I'm not that person!!

Nilichosema mimi ni kwamba, INAWEZEKANA kabisa kwamba Mzee Abdul Razak akawa ni raia wa UK lakini SIJAONA source HATA MOJA inayosema kwamba ni raia wa UK! Ambacho niliwaomba watu ni realiable source, na kwa muktadha huu, media inayoheshimika!!

That's a simple evidence to ask but no one yet has provided any! Na kuonesha kwamba sio NAKOMALIA kwamba yeye ni Mtanzania jambo ambalo HALINA faida yoyote kwangu, whether he's Tanzanian or not, ndo maana post yangu ya kwanza kabisa juzi nilihitimisha kwa kusema:-
Sema kama Babu Dully kama anajitangaza mwenyewe na kujiona ni Mtanzania, akitaka kujua kama kweli yeye ni Mtanzania basi autangazie ulimwengu kwamba "...hatimae nimeamua kurudi nyumbani kugombea urais ama wa ZNZ au Tanzania" kisha baada ya hapo aanze kutembelea pages za Msigwa na za Uhamiaji

Nachoipendea nchi yangu, wale wanaokupigia matarumbeta hii leo ndio watakaotangaza wewe sio Mtanzania na wale ambao leo wanasema wewe sio Mtanzania, ndio hao hao watakaosema "wewe ni Mtanzania swafi..."
 
Back
Top Bottom