Guselya Ngwandu
Member
- Sep 17, 2021
- 39
- 84
Sio aibu. Hii nchi ina watu wengi sana ndani na nje. Hatuwezi kuwatambua wote kwa pamoja. Linapotokea jambo la kufanya mtu ajulikane kiasi hicho ni vyema kumpongezaNi kweli huyu Prof ni mtu mwenye asili ya Tanzania visiwani na amekuwa akifundisha University of Kent tangu mwaka 1982. Amendika vitabu vingi tu lakini sijawahi kusikia serikali yetu ya Tanzania ikijisifu kuwa kuna mtanzania anafanya kazi nzuri za fasihi huko Uingereza. Sijawahi kusikia hata hapa nyumbani jina lake likitajwa.
Leo hii baada ya kushinda tuzo ya Nobel upande wa fasihi naona kila kiongozi wa serikali anataka kutuaminisha kuwa Prof Gurnah ni shujaa wa Tanzania.
Kama ni shujaa wa taifa letu mbona huko nyuma hamkumtambua? Mbona hamjawahi kuthamini kazi zake?