Paul Makonda awekewe ulinzi mkali sana kumzunguka kwa sababu ni hazina kwa Taifa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
17,745
11,987
Ndugu zangu Watanzania,

Kupata viongozi aina ya Mheshimiwa Paul Makonda Wenye ujasiri wa kiwango cha juu kama alicho nacho katika kuwatetea, kuwapigania, kuwasemea, kuwakingia kifua wanyonge ni ngumu sana. Ni kazi inayohitaji kujitoa na kujitolea, ni kazi ambayo haihitaji kumuangalia mtu usoni katika kufanya uamuzi, ni kazi inayohitaji moyo wa chuma, moyo wa ujasiri, moyo wa kujitoa ,moyo wakusema acha nikosane na mapapa lakini niwaokoe na kuwafuta machozi wanyonge.

Paul Makonda ni aina ya kiongozi kijana ambaye Taifa letu linapaswa kumlinda kwa wivu mkubwa sana kama mboni ya jicho. Kwa kuwa ujasiri alio nao ndani ya moyo na kifua chake anatufaa sana huko mbele ya safari . Ni mwanadamu wa kipekee sana aliye zaliwa katika ardhi ya Tanzania. Ndio maana unaona kwa sasa namna watu na wananchi wanyonge wanavyo miminika na kufurika kwa wingi katika mikutano yake ili kufikisha kero zao.ndio maana wananchi wanapigana vikumbo huku wakibubujikwa machozi ili wasaidiwe na kuponywa majeraha ya mioyo yao.

Paul Makonda alindwe kwa nguvu zote na kwa gharama za aina yoyote ile,kwa sababu wenye kuguswa maslahi yao hawawezi kufurahi wanapoona akiendelea kuwapambania wananchi. hivyo watampiga mishale ya Majungu,fitina,uzushi,uongo na kila aina ya mishale ya maneno ili kutaka kumdhoofisha na kumrudisha nyuma katika juhudi zake za kuwatetea wanyonge. Watataka wafanye kila liwezekanalo ili kumchongea uongo kwa Mheshimiwa Mwenyekiti wetu.

Taifa letu na katika nchi za kiafrika ni muhimu sana na kwa gharama zozote zile kuwalinda kwa nguvu zote viongozi aina ya Mwamba Paul Makonda.hasa ikizingatiwa ukweli kuwa wengi wetu wa Afrika tukiwa mezani tunakula hatusemi mpaka tumalize chakula.ndio maana leo unaweza kuta mtu alikuwa ni kiongozi mkubwa kama waziri au mkuu wa wilaya au mkoa au mkurugenzi au katibu ndani ya chama au serikali ,alikuwa kimya muda wote lakini anapotolewa katika uongozi anaanza kutoa maneno ya chuki na uzushi kwa serikali na chama na kwa baaadhi ya watu walio uongozini kwa sababu tu hayupo uongozini Au madarakani.

Lakini ukimuangalia na kumfuatilia Mwamba na komandoo Paul Makonda unaona Namna yeye alivyo mtu wa tofauti sana.yeye ni mtu ambaye muda wote na wakati wote anajikita kutatua kero na kuwasikiliza wanyonge. Makonda hata leo hii ukimpa uenyekiti wa kitongoji basi ni lazima kitongoji hicho kitafahamika Tanzania nzima na hata nje ya nchi.kwa sababu Makonda ni mtu mbunifu sana na kiongozi mchapa kazi sana.

Jiulize kabla ya Paul Makonda hajawa DC kila mtu aliona kama nafasi ya kawaida lakini alipoingia na kupewa Ukuu wa wilaya kila mmoja akajuwa kumbe mkuu wa wilaya anaweza fanya mambo makubwa katika wilaya kusaidia wananchi? Hata alipokuja kupewa ukuu wa mkoa napo watu ndipo wakaja kutambua nguvu ya mkuu wa mkoa na mamlaka makubwa aliyo nayo mkuu wa mkoa.mpaka kuamsha wengine kutoka usingizini. Haya yote ni kutokana na ubunifu, uchapakazi,ujasiri,uzalendo na moyo wa kujitoa alio nao Paul Makonda.

Leo amepewa ukatibu wa itikadi, uenezi na mafunzo ya chama cha Mapinduzi Taifa kila mtu anaona namna mchaka mchaka unavyopigwa mitaani.namna moto unavyowaka na kuwashwa ,namna watu walivyoamka na kutambua nguvu ya chama katika kuisimamia serikali iliyotokana na CCM.kila mtu anaona namna mikutano yake ilivyogeuka kuwa kimbilio la wanyonge .jiulize ni kwanini? Jiulize je hakuna viongozi katika maeneo hayo anayopitia?

Jiulize kwanini wananchi hawapeleki kero huko na badala yake wanaona Makonda kama tumaini jipya katikati ya giza na kukata Tamaa? Wapi tumekwama? Viongozi ngazi za mikoa na wilaya wanajisikiaje wanapoona hali hiyo? Hawaoni kuna mahali wameshindwa kutimiza majukumu yao? Hawaoni wananchi wamekosa msaada kutoka kwao? Hawaoni wanapaswa kuwa wanyenyekevu na wasikivu kwa wananchi na kujenga mazingira ya kufikika na kuaminika na watu?

Makonda ni kama kiraka tu ambaye popote utakapo mpeleka na kumpachika lazima akupatie matokeo makubwa na Chanya. Shida yetu wa Afrika unakuta mwingeni badala ya kumsaidia na kumuunga mkono anaanza kuona wivu ,chuki na kuwa na kinyongo kuona Makonda anasifiwa na kukimbiliwa na watu wenye shida.swali ni kuwa wewe unayeona wivu ni nani anayekuzuia kuzuia kufanya kama Makonda kuwasikiliza watu? Nani amekuzuia wewe kuchapa kazi kama Makonda?

Mliopewa uongozi sehemu yoyote ile acheni kufanya kazi kwa mazoea, acheni Umungu mtu,acheni Majungu, uzushi, fitina, uchawi na uzembe.kuweni wanyenyekevu, waungwana, wapole, wasikivu, wenye utu,wacha Mungu, watenda haki na wazalendo wa kweli.jueni uongozi ni dhamana tu. Acheni viburi na roho mbaya. Mtu unafanya ofisi ya umma kama mali yako? Unamzungusha mtu anayetaka msaada ofisi ya ofisi ya umma mpaka mtu anatokwa machozi halafu wewe huna habari.

Hongera sana sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Dr Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kutuletea Paul Makonda. Nafikiri unaona na unafuatilia kila kinachojili katika ziara zake. Unaona malalamiko ya wananchi, unaona na kusikia kero za wananchi. Unapata taswira nzuri ya kazi ya watendaji na viongozi mbalimbali uliowateua huko ngazi za mikoa mpaka chini huko.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Tunasonga mbele
IMG-20240120-WA0007.jpg
IMG-20240114-WA0016.jpg
IMG-20240118-WA0000.jpg
IMG-20240114-WA0037.jpg
IMG-20240115-WA0007.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kupata viongozi aina ya Mheshimiwa Paul Makonda Wenye ujasiri wa kiwango cha juu kama alicho nacho Mheshimiwa Makonda katika kuwatetea ,kuwapigania ,kuwasemea, kuwakingia kifua wanyonge ni ngumu sana. Ni kazi inayohitaji kujitoa na kujitolea ,ni kazi ambayo haihitaji kumuangalia mtu usoni katika kufanya uamuzi,ni kazi inayohitaji moyo wa chuma,moyo wa ujasiri,moyo wa kujitoa ,moyo wakusema acha nikosane na na mapapa lakini niwaokoe na kuwafuta machozi wanyonge.
Huu Uzi umfikie mama yetu Samia suluhu Hassan,,,

Lakini pia watanzania tuendelee kumuombea kwa kujitoa kwake bila woga kufanya maamuzi magumu yanayolenga kutatua changamoto za wananchi na sio kulinda watawala.

Makonda piga kazi tunakukubali
Nchi yetu Bado inahitaji viongozi wa Kariba yako , maana wateule wengi wa Rais wanajisahau wakipata nafasi badala ya kushughulika na changamoto za wananchi hugeuka kushughulika na maisha Yao. ....
God be with you !!!
 
Style ya uongozi wa makonda ilishapitwa na wakati uwezi kuwatisha watendaji wa nchi kwa kelele na mikwara aliyafanya sana mwendazake ila haikusaidia sana sanasana iliumiza watu na familia zao.

Watendaji wanapaswa kuimizwa kufuata utaratibu na miongozo ya kazi zao katika kutumikia wananchi watendaji waelemishwe bila kuchoka majukumu yao na yeyeto atayeenda kinyume sheria zifuate mkondo wake bila kupapasa papasa..

Issue ya maadili na nidhamu kwa hii nchi sasa ni bidhaa hadimu sana kwa hawa viongozi wetu. Tujisahihishe.
 
Hatuhitaji uongozi wa mazoea katika Taifa letu.tunahitaji viongozi wabunifu ,wachapa kazi na majasiri aina ya Paul Makonda.
 
Huu Uzi umfikie mama yetu Samia suluhu Hassan,,,

Lakini pia watanzania tuendelee kumuombea kwa kujitoa kwake bila woga kufanya maamuzi magumu yanayolenga kutatua changamoto za wananchi na sio kulinda watawala.

Makonda piga kazi tunakukubali
Nchi yetu Bado inahitaji viongozi wa Kariba yako , maana wateule wengi wa Rais wanajisahau wakipata nafasi badala ya kushughulika na changamoto za wananchi hugeuka kushughulika na maisha Yao. ....
God be with you !!!
Kwa hakika Mheshimiwa Paul Makonda anahitaji kuungwa mkono na sisi watanzania wazalendo zidi ya wacheche wanaoweza taka kumkwamisha kiongozi wetu huyu aliyeamua kujitolea kwa ujasiri mkubwa kuwatetea na kuwasemea watanzania wanyonge.
 
Hatuhitaji uongozi wa mazoea katika Taifa letu.tunahitaji viongozi wabunifu ,wachapa kazi na majasiri aina ya Paul Makonda.
Makonda sio best kiongozi best kiongozi hafanyi vitu kwa kutaka kuoneka na au kuumiza wengine..

Yule ni mwanasiasa mjanjamjanja.
Kiongozi anakuelekeza hadi uelewe au ushindikane basi unaachwa.
 
Tutaona nani ataibuka mshindi ktk mnyukano huu wa Nchimbi na Makonda.

Nchimbi hataki watendaji wabwatukiwe na kudhalilishwa kama enzi za kayafa.

Makonda yeye anaona kuwabwatikia na kuwadhalilisha watendaji kama enzi za kayafa ndiyo uongozi.
 
Makonda sio best kiongozi best kiongozi hafanyi vitu kwa kutaka kuoneka na au kuumiza wengine..

Yule ni mwanasiasa mjanjamjanja.
Kiongozi anakuelekeza hadi uelewe au ushindikane basi unaachwa.
Mheshimiwa Makonda anaelekeza sana na kuwakumbusha sana viongozi juu ya kutimiza wajibu wao.anafanya kazi kubwa sana ya kuwasihi juu ya kuwasikiliza na kuwa wanyenyekevu kwa wananchi ambao ndio wenye nchi. Hafanyi mambo kwa kukurupuka au kutaka kuonekana au kumuumiza mtu. Ndio maana unaona namna wananchi wanavyoendelea kumiminika katika mikutano yake kila anakopita.
 
Tutaona nani ataibuka mshindi ktk mnyukano huu wa Nchimbi na Makonda.

Nchimbi hataki watendaji wabwatukiwe na kudhalilishwa kama enzi za kayafa.

Makonda yeye anaona kuwabwatikia na kuwadhalilisha watendaji kama enzi za kayafa ndiyo uongozi.
Hizo akili za fisi mlizonazo vichwani mwenu mtakonda tu na kupata presha tu maana chama kipo kimoja na hakuna mnyukano wala minyukano ya aina yoyote ile ndani ya chama.ndio maana mnaona kazi na shughuli za chama zikiendelea kama kawaida.
 
Back
Top Bottom