Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Torra Siabba

Senior Member
Jul 24, 2016
105
102
Nianze kwa kusema ukweli kwamba Waziri Juma Aweso, Anafanya kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba Tanzania tatizo la maji linakwisha lakini naamini watendaji wake ndio wanaomkwamisha.

Ni miezi mitatu sasa Jiji la Mwanza lililozungukwa na Ziwa Kubwa barani Afrika Wakazi wake tunakosa maji wakati ziwa hilo hilo linatumika kugawa maji kwenda mikoa ya Shinyanga, Tabora na sasa Mkakati ni kuona Maji yanafika Dodoma kutokea ziwa victoria.

Hoja yangu ni kwamba Kwa miezi mitatu Mkoa wa Mwanza karibia asilimia 90 ya maeneo yake kumekuwa na mgao wa maji jambo ambalo ni aibu kubwa na maeneo kama Kirumba, Kiseke, Pasiansi, Nyegezi na mengineyo ni maeneo ambayo maji huwa hayakatiki hovyo, ila kwasasa kuna mgao ambao hata hautangazwi.

Kiukweli wanatukosea sana Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) , naamini Waziri wa Maji kuna haja ya kuja kutumbua hata Mkurugenzi maana tatizo hili limekuwa sugu na ni aibu kubwa kuona Mwanza imezungukwa na Ziwa Victoria halafu maji yanakuwa tatizo kwa kiwango kikubwa hivi sasa.

Ni Aibu Jiji la mwanza kuwa na Mgao wa Maji.jpg
=============

UPDATES...

MWAUWASA: TUNAZALISHA MAJI LITA MILIONI 90 KWA SIKU, MAHITAJI NI LITA MILIONI 160

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mohamed Saif anafafanua:

"Kwanza sio kweli kwamba hatutoi taarifa kwa wateja wetu kuhusu mgao, mamlaka imekuwa ikitoa taarifa kupitia njia mbalimbali kupitia mitandao yetu, vyombo vya habari na kwa kuwatumia ujumbe wateja wetu kwa njia ya simu na kwa kutumia viongozi wa ngazi ya Serikali za Mtaa.

"Kuhusu suala la mgao wa maji, Kituo chetu cha Capri Point kinazalisha maji Lita Milioni 90 kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa Jiji la Mwanza ni zaidi ya Lita Milioni 160, hali hiyo inasababisha kuwepo na mgao.

"Kutokana na hali hiyo tunachagua baadhi ya maeneo ambayo yanalazimika kuwa na mgao hasa yaliyopo pembezoni mwa Jiji na ambayo yana miinuko.

"Mwanza maeneo mengi yana miinuko na maji hayapandi mlima, hali ambayo inalazimika kuhitajika kwa nguvu ya ziada kupandisha maji juu.

"Malengo yaliyopo ili kupunguza changamoto hiyo, kuna Mradi wa Butimba ambao ukikamilika utazalisha maji Lita Milioni 160 kwa siku.

"Mradi huo una Hatua Mbili, Hatua ya Kwanza ambayo itazalisha mali Lita Milioni 48 kwa siku, imekamilika kwa wastani wa 92%, Mungu akijaalia mwezi mmoja kutoka leo (Agosti 16, 2023) au ndani ya mwaka huu maji yanatarajiwa kuanza kuzalishwa kutoka katika mradi huo.

"Baada ya hapo Hatua ya Pili itafuata, wakati huohuo mpango mwingine wa baadaye ni maboresho ya chanzo chetu cha Capri Point ambapo mambo yakienda swa tunatarajia kuzalisha maji Lita Milioni 100 kwa siku, baadaye pia Serikali imepanga kujenga chanzo kingine maeneo ya Igombe ambacho kitazalisha maji Lita Milioni 200 kwa siku, hiyo ni miaka ya baadaye."

===
Pia soma Mwauwasa (Mwanza): Tunazalisha maji Lita Milioni 90 kwa siku, mahitaji ni Lita Milioni 160
 
Vumilieni, kuna miradi inaendelea. Mwaka huu inaweza kukamilika na kuondoa kero ya maji.
 
Tatizo la maji jiji la Mwanza!

Huweza sadiki na kusadifu kua Mwanza (Nyamagana) inatakribani wiki tatu bila maji!

Unaweza shangaa lakini ukweli ni kua jiji la Mwanza linakumbwa na tatizo la kutopatikana kwa maji na hususani hizi wiki tatu na watendaji wakitoa majibu mepesi kwa maswali magumu! Je, hata kama wadai kua kuna ongezeko la watu, je, maji yaliyokuwa yanapatikana hapo awali yameenda wapi? Watendaji wa idara ya maji jiji, jitafakarini, raia wanalalamika sana, au mnadeal na watu wanaosambaza maji?

Kama nyegezi inakosa maji, je, vijijini watapata kweli?
 
Kuna tatizo gani na MWAUWASA

Ziwa Victoria iko umbali wa kilomita mbili lakini wananchi wa Jiji la Mwanza tunateseka na ukosefu wa maji kila kukicha. Leo hii eneo la Mwananchi hapa Jijini tuna wiki nzima hakuna maji. Kulikoni?.
 
Maji yapo, Mungu kaumba ziwa kubwa na kulijaza maji, mnazalisha maji ya nini wakati maji yapo ni kusukuma tu?
 
Kama leo nimepita mahala yaani mtu anateka maji ya dimbwi yametuama zaidi ya miezi sita, ng'ombe wanapita ,uelewe akachota akawa anakunywa mpaka machozi yakanitoka. Kiukweli waafrika kujitawala kiukweli hatuwezi jamani. Tuwaambiwe wazungu waje kututawala.
 
Back
Top Bottom