Hivi MWAUWASA wanatuuzia maji ya mvua?

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
7,693
17,257
Habari za mchana huu wana jukwaa?

Kuna kitu kimekua kinaendelea kwa muda sasa jijini Mwanza kinanishangaza.

Kwa muda mrefu sasa kuna baadhi ya maeneo jijini Mwanza yanapitia mgao mkali wa maji kwa sababu wanazozijua.

Kinachoshangaza sana ni kwamba pamoja na kwamba chanzo cha maji ya bomba yayanyosambazwa na Mwauwasa kuwa ziwa Victoria ambalo halikauki wakati wowote wa mwaka, mgao unakuwa mkali sana na wa kikatili wakati wa kiangazi.

Najiuliza nakosa majibu kama chanzo cha maji ni ziwa iweje kiangazi hali ya upatikanaji wa maji iwe ngumu sana ila mvua zikianza kunyesha na maji bombani yanakuwa ya kutosha?

Mtaa ninao kaa tunapata maji Jumatatu na Ijumaa ila wakati wa kiangazi maji yanaweza kutoka mara moja kwa wiki, yakitoka ni muda usioeleweka na mara nyingi usiku wa manane hali inayopelekea uchengane nayo ila pia kuna kipindi maji hayatoki hata wiki mbili na yakitoka unaweza kuambulia ndoo mbili yakakata.

Cha ajabu ni kwamba masika yanapoanza maji mgao unaenda vizuri kwa ratiba tena maji yana presha ya kutosha na wakati flani ni kama hakuna mgao mfano kuanzia jana mvua inanyesha sana jijini Mwanza na kwa mshangano ni kwamba maji pia bombani yanatoka toka asubuhi na muda huu bado yapo na yana presha kali sana.

Hali hii inanistaajabisha na kufanya niamini huenda mvua zinaponyesha huenda Mwauwasa wanakinga maji ya mvua na kujaza matenki yao na kutusambazia hivyo kuepuka gharama za ku operate pump zinazojaza maji kutoka ziwani. Mwenye ufahamu na hili anieleweshe
 
Mkuu ueleweshwe nini wakati umetusanua ...!!
Hapa kwenyewe thread imesha toa Majibu yote..
 
Back
Top Bottom