DAWASA tupeni majibu kama mmeanzisha mgao wa maji huku Kimara Bonyokwa

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Asante kwa kuturudishia umeme, asante kwa kuchukua maji. Kazi iendelee mpaka tunyooke.

Kwa kifupi wananchi hatutakiwi kuwa na amani hata kidogo.

Siku kadhaa nyuma tulikuwa tunalia suala zima la mgao wa umeme, lakini naona sasa hivi angalau kuna nafuu.

Lakini sasa, limekuja suala la maji, kwa kifupi sisi wananchi hatutakiwi kuwa na amani hata kidogo.

Maji ni uhai, lakini cha ajabu tunakaa wiki nzima bila ya maji kutoka, hii sio sawa. Wiki iliyopita yalikaa wiki nzima, yakaja kutoka, baada ya hapo hayajatoka tena leo inakwenda siku ya sita.

Wakazi wa huku Kimara Bonyokwa, Dar es Salaam kilio chetu kikubwa ni ukosefu wa maji, kama kuna mgao tuambiwe mapema.

DAWASA MNATUKOSEA SANA.
 
Afadhali huko mna mgao mkuu. Nimesikia kwenye redio asubuhi huko Kingóngó na Matosa takribani miezi miwili sasa hawana maji ya DAWASA. DAWASA hebu tangazeni basi shida ya maji inatokana na nini wanachi wajue wajipange kwani mvua zimeisha juzi tu na maji watu hawayaoni na hawajui tatizo ni nini.
 
Back
Top Bottom