Ngorongoro: Tamko baada ya Diwani, Watetezi wa haki za binadamu kukamatwa na Polisi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeelezewa kusikitishwa na matukio ya kukamatwa kwa watetezi wa haki za binadamu, jana Machi 23, 2022 Wilayani Ngorongoro.

f11630d0-5a67-4ef9-87e5-a246a5892bd2.jpg

-----------------------------------------------------------------------------------------


NGORONGORO: TAMKO BAADA YA DIWANI KUSHIKILIWA NA VYOMBO VYA USALAMA

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa tamko la kusikitishwa na matukio yanayoendelea Wilayani Ngorongoro yanayohusisha kukamatwa kwa Watetezi wa Haki za Binadamu na wengine wakidaiwa kusakwa na Jeshi la Polisi.

Kaimu Mratibu wa THRDC, Leopold Mosha amesema Machi 23, 2022, madiwani wa Malambo na Arash walishikiliwa kwa muda kuhojiwa na Jeshi la Polisi ikidaiwa ni kuhusu mgogoro wa wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro wanaotakiwa kuhamishwa.

Mosha anasema: “Jana (Machi 23) madiwani hao walishikiliwa kwa muda, wakahojiwa baadaye kuachiwa, upande wa Diwani wa Kata ya Arash, Mathew Siloma alichukuliwa na Polisi, hadi muda huu (Machi 24) mawakili wetu hawajaonana naye.

"Mawakili walipofika Kitu cha Kati Arusha wamefanikiwa kuonana na RCO ambaye amesema Siloma yuko katika vyombo vingine vya usalama, hayupo kwao, lakini ameahidi watakapomrejesha hapo kituoni watapata nafasi ya kuonana naye na kuzungumza naye, hivyo mawakili wetu wanaendelea kusubiri."
 
Hili tamko uchwara!!! Naona Wamewahi sana kulitoa au wamechelewa sana kwasababu inaonekana mpaka sasa hakuna mtu aliyemkononi Mwa polisi kwa mujibu wa Maelezo yao
 
Aiseee hawa huwa wanawahi kwenye fursa tu ili waitwe wapatie ka asilimia fulani. mbona kuna watu wananyanyaswa na wao hawaendi kuwatetea na kuwasaidia
 
Ni mwendelesho wa Ukoloni mamboleo.
Na haya chini ni Maoni yangu au uite Dukuduku zangu.

Chama cha Mapinduzi kilikuwa kinapigania haki za "Mwafrika" awe na uhuru wa Kisiasa, awe na uwezo wa kuhodhi ardhi yake n.k Leo hii Chama cha mapinduzi kimejikita katika nyanja inayo leta Tahararuki kwa makusudi au kwa kutojitambua kuwa linafanya hayo. Viongozi wao kwenda mbali(over reach) na hata kudiriki na kusema kuwa Wamasai ni wakuja tu kana kwamba hawana usemi wowote katika ardhi walioishi miaka nenda rudi huku wakitoa sababu lukuki ya kwanini wanataka Wamasai waondoke maeneo hayo. Rubbish!


Ukweli siko zote huwa unauma na kwa utafakari wa jambo hili naona kwamba ...

Chama Cha Mapinduzi sasa kinawakumbatia "Wawekezaji" badala ya Wananchi wake, kama vile Wamasai ambao sasa wako kwenye sintofahamu.

Leo hii Wananchi wakiendelea kukakaa kimya, leo hii wananchi wakitoa ridhaa kwa Chama Cha Mapinduzi na kukubali kuhamishwa Wamasai au kwa lugha fasaha kwangu "Ukoloni mamboleo" yaendelee na kukubali kuwa ni Serikali tu ndiyo inayojua Wananchi au eneo la ardhi wanamoishi ndio inayojua kinachohitajika kuleta maendeleo ni dhana potofu. Binafsi hili nalikataa lakini Ridhaa hiyo ikitoka basi hawatakoma hapo.

Hili binafsi nalikataa kwani linaingilia na kududumiza yale yote Babu zangu waliolipigania na hayo ni pamoja na haki na uhuru wa kisiasa pamoja na uwezo wa kuwa na uwezo wa kumiliki ardhi na nini naweza kufanya na Ardhi hiyo. Hilo pia halimaanishi kuwa ni kufanya nilitakalo bila kufuata sheria, na pale walakin utakapoonekana upo kwenye sheria hiyo basi niwe na uhuru wa kudai marekebisho bila kukurupushana.

Leo hii Wananchi wakakubali au niseme Wamasai wakakubali kuondoka basi with precedent au kukubali vigezo ambavyo havina miguu wala kichwa katika kuondoa na kuwahamisha Wamasai... hawatakoma hapo kwani hata yale maeneo ya Marangu au maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro yanaweza yakachukuliwa vivyo hivyo, Imagine shule ya marangu ndio iwe kuwa Hoteli! Au kule kwa Wakuriya ambapo wanadaiwa kuwa mavi na mikojo ya Ngo'mbe wao wanaua samaki wa ziwa , mkumbuke samaki nao wanalindwa na sheria kama hizo zinazowalinda wanyama wanaouzunguka maeneo na makazi ya Wamasai! hivyo basi wahamishiwe Kisarawe!

Wito wangu kwa Chama Cha Mapinduzi ambao ndio wanaohodhi madaraka ya kiserikali, waepuke na hizi taharuki, kwani hili jambo linadhihirisha kuwa Demokrasia halitendeki ndani ya Chama chao na hivyo basi Demokrasia hiyo inakuwa na ulakini katika Serikali wanayoongoza. Linadhirisha kuwa hawajali Wananchi wao bali "wawekezaji uchwara" kama hao watakaopewa maeneo hayo kufanya walitakalo...

#MWACHIENIMATHEWSILOMA
...kwani hatumiki na Wawekezaji bali Wananchi wanodai haki zao.

Aluta Continua
 
Nadhani darasa la Jiwe ile miaka sita halikueleweka. Wewe shindana na Serikali ambayo imeshajua maslahi yake ya utalii yanachezewa na nchi jirani!
 
"Mawakili walipofika Kitu cha Kati Arusha wamefanikiwa kuonana na RCO ambaye amesema Siloma yuko katika vyombo vingine vya usalama, hayupo kwao, lakini ameahidi watakapomrejesha hapo kituoni watapata nafasi ya kuonana naye na kuzungumza naye, hivyo mawakili wetu wanaendelea kusubiri."
Uhamiaji au Takukuru ?....
 
Back
Top Bottom