LHRC, THRDC, TLS Waungana kuwataka polisi kuwaachia Dkt. Slaa, Wakili Mwabukusi na Mdude

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Kufuatia taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi pamoja na wanaharakati Dk Wilbroad Slaa na Mpaluka Nyagali Mdude, baadhi ya watetezi wa haki za binadamu nchini wameungana kwa pamoja wakilaani kitendo hicho huku wakipinga kosa la uhaini wanalotuhumiwa nalo wanaharakati hao.

Wadau wa haki za binadamu
Akisoma taarifa hiyo ya pamoja leo Jumanne Agosti 15, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga amedai kuwa kati ya waliokamatwa wakihusishwa na ukosoaji wao ni pamoja na; Dk Willbroad Slaa, Peter Madeleke, Boniphace Mwabukusi na Mdude Nyagali.

ambapo wamelitaka Jeshi la Polisi kuwaachia watu wote wanaodaiwa kukamatwa na jeshi hilo kwa kuhusianishwa na ukosoaji wao katika mkataba baina Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA) kuhusu uwekezaji Bandarini.

Wadau hao walioungana kwa pamoja ni Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

"Kama ilivyofanyika kwa Wakili Boniface Mwabukusi na Nyagali, Dk Slaa alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi lakini baadae tuhuma zikabadilishwa na kuhojiwa tena kwa tuhuma za uhaini," amesema Henga.

Ikumbukwe wadau hao wanadaiwa kukabiliwa na tuhuma za uhaini, lakini kukamatwa kwa wanaharakati hao kulikuja siku moja ya baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kudai Camilius Wambura kuwa kuna watu ambao wanapanga kuiangusha Serikali huku akiwataka kusitisha mpango huo hususani maandamano yasiyo na kikomo.

FB_IMG_1692102609145_1.jpg
 
Tulieni utawala wa Sheria ufanye kazi. Mwenyewe katangaza kuipindua Serikali, acha apinduliwe kabla ya kupindua.
 
Kuwa kamata siyo hoja. Hapo ni kama kumpiga teke chura. Waleteni mahakamani afu tuone kama mtashinda. Shetani anajaribu kuwatumia ili watu wa Mungu waendelee kuteseka kama ilivyo kusudi lake toka alipofukuzwa mbinguni kwa ajili ya tamaa zake.”VOX POPULI,VOX DEI”. Ila one day yes,,,heko wanaharakati wetu, tunawaombea huko mlipo Mungu awatie nguvu,,,,Championship is on your side,,,,!!!.
 
Back
Top Bottom