Mkutano wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) Kufanyika Tanzania, Wadau watakiwa kujisajili kushiriki

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 77 wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) ambao utafanyika Jijini Arusha kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano (AICC) kuanzia Oktoba 20, 2023 mpaka Novemba 9. 2023 ambapo vitafanyika vikao mbalimbali vikijadili masuala tofauti yanayogusa haki za Binadamu.

Akizunguzia maandalizi ya Mkutano huo Mratibu wa Mtandao wa watetezi wa waki za binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema wakiwa kama wadau muhimu ambao walihusika katika mchakato wa kushawishi Serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wakiwa sambamba na watendaji wan(ACHPR) ambao walifanya mazungumzo na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salaam na kuridhia ombi hilo, amewataka wadau wa haki za Binadamu ikiwemo mashirika wanachama wa mtandao kujisajili kushiriki.

Akiongea na waandishi wa habari Oktoba 11, 2023 kwenye ofisi kuu za mtandao huo Mikocheni Jijini Dar es salaam, Olengurumwa amesema kuwa mkutano huo ambao utaambatana na vikao utakutanisha wadau wa haki za binadamu kutoka kwenye Mataifa ya Afrika ambapo ameeleza kuwa mambo mbalimbali kwenye nyanja ya Haki za Binadamu yataweza kujadiliwa.

Amesema kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ndiyo waratibu wakuu wa mkutano huo ambao amesema utakuwa na tija kwa wadau wa haki za binadamu pamoja na jamii nzima kwa ujumla.

Amesema kuwa wadau wa haki za binadamu nchini ni fursa kwao kushiriki mkutano huo ambapo amedai kuwa katika Mataifa ya Afrika Mashariki Tanzania litakuwa Taifa la kwanza kuandaa mkutano huo.

Hivyo amesema kuwa itiakuwa fursa kwao kushiriki kwa kuwa kutakuwepo na unafuu wa gharama za kufika eneo ya mkutano sambamba na mahitaji mengi ambayo yamekuwa ni kikwazo pale mikutano hiyo inapofanyika nje ya Tanzania hususani nchini Gambia, Banjul yalipo makao makuu ya tume hiyo.

Aidha katika taarifa ya mtandao huo kupitia Mratibu wa Mtandao huo, imeelezwa kuwa mkutano huo ambao utabebwa kauli mbiu isemayo "Mwaka wa AfCFTA: Ukuzaji wa Utekelezaji wa Biashara Huria Barani Afrika" kati ya mada ambazo zitajadiliwa ni pamoja na Wajibu wa Vijana katika utekelezaji wa ajenda ya Umoja wa Afrika 2063 , Mafanikio na changamoto za Itifaki za Maputo (Muputo protocol) ikiwa na maana kuwa ni mkataba muhimu wa kimataifa ambao unashughulikia changamoto za haki za binadamu za kijinsia barani Afrika.

Mada nyingine ni pamoja na kujadili Jukumu la msingi la mashirika yasiyo ya kiserikali katika kazi ya mifumo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Kukuza mtandao wa haki za binadamu barani Afrika, ambapo mada hiyo imeelezwa kuwa italenga kukuza na kuwezeshwa kupitishwa kwa mikakati na mbinu bora za kuchangia katika kupatikana kwa amani, usalama na maendeleo barani Afrika.

Katika mkutano huo Mtandao huo wenye wanachama zaidi ya 150 nchini unatarajiwa kutoa tamko lake kuhusu hali ya haki za binadamu nchini.

Mkutano huo amabao unalenga kuwakusanya wadau wa haki za binadamu kwa pamoja imeelezwa kuwa mgeni rasimi katika uzinduzi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan, taarifa hiyo imeelezwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dr. Pindi chana Oktoba 10, 2023 wakati akihutubia washiriki wa katika mdahalo ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ukijadili kuhusu adhabu ya kifo.

Waziri huyo aliwataka wadau kujisajili kutupitia mfumo wa kimtandao au kutembelea tovuti ya Wizara kupata maelekezo ilikuthitisha ushiriki wao katika mkutano huo ambao tayari maandalizi yake yameanza.

Itakumbukwa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) ni moja ya vyombo vya Umoja wa Afrika (AU) kama ilivyoainishwa na Mkataba wa Afrika. Tanzania ikiwa kama mwanachama wa tume hiyo imekuwa ikiwasilisha ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu katika vipindi tofauti.
 
Back
Top Bottom