News Alert:...... Uteuzi cabinet

He, huyu jamaa alikuwa anasubiri Chenge ajiudhuru ndio abadilishe mawaziri wengine wizara! Si juzi tu ameunda baraza jipya! Kwa kweli huyu jamaa kachanganyikiwa! Na hata mabadiliko aliyoyafanya hayaonyeshi umakini wowote! Kweli hatuna kiongozi! Huyo Kawambwa kwa sababu ni jamaa wa nyumbani basi kila kukicha anamhamisha kwa sababu hajaona anapofit au sasa amemhamishia hiyo wizara yenye pesa ili wale wote! Kama kuna waziri asiyemzoeafu ambaye amekuwa akihama kila baraza linapobadilishwa basi ni huyo Kawambwa! JK amezidiwa jamani! Miundombinu ni wizara kubwa sana (kwa budget allocation) inatakiwa mtu mwenye uzoefu na commitment sana! Sio kupeleka tu recycled materials! Hizi barabara kweli zitaisha na michezo kama hii!!! Sitampe tena JK benefit of the doubt, hamna kitu hapo, nis msanii aliyeishiwa vichekesho!!! Wape wizara nyingine zecomedy wakusaidie
 
Hivi huko ikulu hakuna kazi ingine ya kufanya zaidi ya kuwapanga na kuwapangua mawiziri kila kukicha? Wataanza lini hasa kutekeleza ahadi zao walizotoa 2005?
 
Nimekusikia mkuu, tuendelee kukata ishus taifa liko njia panda hili!

Hapo ndio kwenye debate!

Nimeshangazwa sana na watu kuwa excited eti na baraza jipya!

Yani mambo ya uongozi yeshafanywa kama Ze Comedy!
Kwi kwi kwi kwi..Wastake N'cheke!
 
Mi naona tujirudie zetu tu kwenye makala ya nani atatufaa 2010!

Tumwache tu muungwana amalizie term yake moja then akajipumzikie kwasababu amefeli testi kubwa kuliko zote kwenye uongozi wa Taifa letu changa linalohitaji mtu madhubuti!

Hapa jipya hakuna ni the same ol mambo jamboz!
 
Hapa kwa Kikwete tumeumbuka kwa kweli. Watu wanahamishwa wizara mara kwa mara, hata mwishoni waliulizwa walifanya nini hawawezi kusema, mfano Kawambwa, Wasira, Msola tangu 2006 hadi leo (miaka 2 tu) wameshahama wizara 3, hivi kuna ufanisi hapo? Reshuffle ya sasa hivi ndio wehu kabisa, watu kawateua February tu juzi (miezi 3) keshawabadili! Hizi kazi watazifanya lini, au labda ni kweli hakuna kazi za mawaziri kwenye hizo wizara? Kenya baada ya uchaguzi waliendesha serikali kwa miezi 5 bila mawaziri katika baadhi ya wizara, na hatukusikia lolote lililoharibika, lakini alipokuja Kibaki kuteua mawaziri 80 ilibidi wakatafute hela za ziada za kuwalipa mishahara maana gharama yao ni kubwa mno! Hapo kwenye serikali ya JK kwa mfano kama waziri anaweza kutumia awamu yote ya serikali anatalii tu wizara moja hadi nyingine na bado kazi zinafanyika, pengine hatuhitaji mawaziri hao!
 
Duh wazee mtanisamehe nimechelewa na mimi listi niliyonayo so far ni hii

DR SHUKURU KAWAMBWA -MIUNDOMBIU

DR STEPHEN WASIRA- KILIMO

DR MSOLA-MAWASILIANO

KOMBANE TAMISEMI

CHIBULUNJE NAIBU WAZIRI MAWASILIANO

MAHANGA -NAIBU WAZIRI WIZARA YA KAZI


Mie nilishasema haya mabadiliko ya baraza la mawaziri kila miezi miwili hayataleta mabadiliko yoyote ya kweli bali uchaguzi tu ndio labda utaleta mabadiliko ya kweli. Huyu Msolla alivurunda sana pale elimu na hatimaye kutupwa nje ya cabinet, sijui amefanya lipi la kustahili kupewa uwaziri kwa mara nyingine tena!
 
Mie nilishasema haya mabadiliko ya baraza la mawaziri kila miezi miwili hayataleta mabadiliko yoyote ya kweli bali uchaguzi tu ndio labda utaleta mabadiliko ya kweli. Huyu Msolla alivurunda sana pale elimu na hatimaye kutupwa nje ya cabinet, sijui amefanya lipi la kustahili kupewa uwaziri kwa mara nyingine tena!

Msola hajawahi kutupwa nje ya kabineti.
 
Alikuwa waziri wa wizara gani katika mabadiliko yaliyofanywa february, 2008? Naona hili lilinipita kushoto mimi nilidhani aliachwa kama akina Meghji, Mramba na wengineo.
 
Jakaya Mrisho Kikwete wewe ni matatizo matupu, na ni bure kabisa wewe
Huna lolote wewe, nalazimika kusema hivi kwa sababu nadhani upeo wako wa kufikilia haulingani na madaraka uliyoyata(Upresident) sasa unatufanyia majaribio kila kukicha.

Wewe kweli ulikuwa hufai kuwa President sijui ni hizo chekacheka zako ndio zilikufanya upate Upresident?? Fanya urudi Jimboni kwako ukagombee Ubunge nchi imekushinda hii

==+++====++++xxxxx+++++++++
 
Kithuku:

Hii ni "Kasi na ari...........mpya," ikiwa na pamoja na kubadili mawaziri.

Tunaona kasi ya ufisadi kwenye chama na serikalini......, kuna kila sababu ya kuamini kuwa 'kauli mbiu' hii inatekelezwa ipasavyo katika miaka mitatu hii ya utawala.
 
Alikuwa waziri wa wizara gani katika mabadiliko yaliyofanywa february, 2008? Naona hili lilinipita kushoto mimi nilidhani aliachwa kama akina Meghji, Mramba na wengineo.

Msola alikuwa Waziri wa Elimu Ya Juu, kwenye reshufle ya Feb 2008 akapelekwa Kilimo ambako naibu wake alikuwa mwanafunzi wake wa SUA, David Matayo. Na hii reshuffle mpya ndio kapewa Mawasiliano! Masikhara tu!
 
Judge Joseph Sinde Warioba, Mbunge Aloyce Kimaro, Harrison Mwakyembe, Joseph Butiku, Dk Slaa na wengineo walio ukemea ufisadi hadharani...Coalition ya kuikomboa Tanzania 2010?
 
Hapa kwa Kikwete tumeumbuka kwa kweli. Watu wanahamishwa wizara mara kwa mara, hata mwishoni waliulizwa walifanya nini hawawezi kusema, mfano Kawambwa, Wasira, Msola tangu 2006 hadi leo (miaka 2 tu) wameshahama wizara 3, hivi kuna ufanisi hapo? Reshuffle ya sasa hivi ndio wehu kabisa, watu kawateua February tu juzi (miezi 3) keshawabadili!
Kitila said:
Hivi huko ikulu hakuna kazi ingine ya kufanya zaidi ya kuwapanga na kuwapangua mawiziri kila kukicha? Wataanza lini hasa kutekeleza ahadi zao walizotoa 2005?
Kithuku, Kitila; Ikulu kuna watu (aliowaweka JK) ambao hawana kazi, wanadhani kazi pekee ni kumshauri jinsi ya kupangua mawaziri!!

I cannot imagine you reshuffle someone on ministerial post within two months even if it's a political post. Haya ni ya FILAUNI nilizoea kuona ya Musa!!
 
Judge Joseph Sinde Warioba, Mbunge Aloyce Kimaro, Daniel Mwakyembe, Joseph Butiku, Dk Slaa na wengineo walio ukemea ufisadi hadharani...Coalition ya kuikomboa Tanzania 2010?

wengine opportunists tu, hawana jipya kukemea hata lowassa amekemea ufisadi
 
Mimi swali langu; Rais bado ana nafasi mbili za wabunge wa kuchagua, kuna ugumu gani wa kumchagua mtu ambaye hayumo katika wabunge waliopo sasa na kumpatia eneo kama Miundo Mbinu? Hata kwenye nafasi nyingine kwanini asilete mtu nje ya mfumo uliopo sasa.. say a certain engineer professor aliyeko hapa majuu akatikise kidogo wizara hiyo?
 
wengine opportunists tu, hawana jipya kukemea hata lowassa amekemea ufisadi
Ahsante!

Butiku na Warioba nao ni wasanii tu.

October 17, 2007 JOSEPH BUTIKU

``I personally don't believe that Mkapa conducted business during his reign at the State House. However I believe it would be noble of him to come out and clear the air…``

September 27, 2007 JOSEPH WARIOBA

"Hata Mkapa aliyemtangulia anaitwa fisadi, hivi hivi tu, habari hizi zinaleta picha gani? Kwamba alijitajirisha yeye na ndugu zake katika miaka yake 10. Mkapa kama binadamu alikuwa na weakness zake, lakini kwa nchi hii huwezi kufuta historia yake..."

"Tusiwadanganye wananchi, kuwa tukiwaondoa wala rushwa, matatizo ya Watanzania yataisha.

"Tunaanza kuwa na utamaduni wa kutafuta dosari hasa za viongozi na kusahau mambo ya msingi ya kulisaidia taifa. Ombi langu, hii tabia ya kupakana matope haiisaidii nchi, waandishi hizi habari ndizo zinapaswa kupewa kipaumbele?"
 
Back
Top Bottom