News Alert:...... Uteuzi cabinet

Mojawapo ya kazi ya Rais ni kuteua wasaidizi wake watakaomsaidia

kuongoza wizara kadhaa alizoziunda. Kama ambavyo Kasheshe

ametangulia kusema kwamba mawaziri ni wasimamiaji wa utekelezaji

wa sera za chama kilicho madarakani, mimi napenda kuongezea kwa

kurudia kuwakumbusha wana-JF kuwa uendeshaji wa shughuli za

wizara hufanywa na technical people wakiongozwa au kusimamiwa na

katibu mkuu wa wizara husika. Kwahiyo uteuzi wa mawaziri wa

kumsaidia Rais sidhani kama nina haja ya kuhoji ilhali mwenye

kuwateua wamsaidie hana tatizo nao. Ni vema tukakumbuka kuwa

Rais wa Tanzania ni mmoja tu.

I have no objection kwa wote walioteuliwa.
 
Punda na Kasheshe nakubaliana na hoja zenu wote lakini kwa Tanzania kila uamuzi lazima uwe wa kisiasa.Laiti kama wangaliachiwa wajuao kazi hiyo nadhani mambo mengi yangalikuwa salama lakini utashi wa kisiasa unawekwa mbele na maslahi ya kundu ama kikundi na misho CCM, na ndiyo maana watu wanauliza naamini hakuna kiendacho kwa sasa watasema tungojee uteuzi mpya wa waziri .Mawazo yangu haya .
 
1

According to the dataz, huyu mkulu ni ndugu wa karibu wa muungwana, level ya ujomba, uwezo wake kikazi haufahamiki ila ni mstaarabu na ni mkimya huwa haongei kabisa! Sasa tutaaamua wenyewe kama anafaa, au?

2.

According to more dataz, huyu mkulu alikubali kutumiwa na Lowassa kutaka kuuvuruga mkutano wa NEC kule Butiama, akaomba kusema, na kuanza kudai kuwa kwa nini Lowassa hakupewa nafasi ya kujitetea, akaambiwa kwa lugha ya ukali sana na muungwana, kuwa akae chini na anyamaze, kwa hii ilikuwa ni kifuta jasho!

sielewi kabisa kwanini Mahanga amerudi, inamaana JK hajui jamaa hayuko upande wake kama ni kweli aliwatetea kina lowassa kikao cha NEC na akawatetea pale bungeni, hii inamaanisha nini?? inaonekana kabisa mahanga yoko ktk kundi la mafisadi anajaribu kila awezalo kurudisha mirija ya kula na ndiomaana anapigana kufa na kupona kutetea wizi pale ATC, kiongozi ganai utasema wafanyakazi wambea, kwa wafanyakazi kuwa wambea huoni kama ni wewe umeikuza hiyo tabia, kiongozi mzuri hasutani na wafanya kazi wake bwana, tena hadharani.....
JK ana zidi kubugi tuu
 
Ukimweka prof. wa mifugo hapo, kuna kazi kweli mpaka aje aelewe dunia ya mawasiliano inaenda wapi.

Prof. Mwandosya alikuwa na mwelekeo mzuri kwenye hiyo wizara, ila tu wizara yake ilikuwa kubwa mno na hivyo kumezwa na miundo mbinu ambako kuna matatizo kila siku.

Mtanzania;

Wote matatizo tu!!! tunataka yule jamaa pale utumishi ateuliwe kuwa mbunge wa taifa wa kuchaguliwa alafu apewe ile wizara... period...

Wote hao maprofessa... ndio wana shangaa vitu vinavyoendelea kwenye ICT.

Au Mgombelo arudishie ubunge na kupelekwa kwenye hiyo wizara. Una msifia Mwandosya wakati amesaini sheria mbovu za ICT!!!!
 
Kosa kubwa tunalofanya Watanzania na hata hapa JF ni kufikiri ubora wa kiongozi unatokana na kupiga kwake kelele bungeni au sehemu yoyote nyingine.

Ubora wa kiongozi unatokana na uwezo wake wa ku deliver na upimwe kwa mafanikio yake kwa kazi za nyuma.

Mtu anayeshindwa ku deliver kama mbunge sidhani kama ataweza kufanya hivyo kama waziri au kama rais.

Ni rahisi mno kuwa mpinzani au kuwa backbencher na kukosoa kila siku kama tunavyofanya hapa JF lakini ni kitu kingine kupewa usukani na kuambiwa sasa
lisukume hili gari letu kwenda kwenye nchi ya maziwa yanayotoka kwenye bomba.

Usomi ndio una faida lakini ni kigezo cha chini kabisa, ni indicator moja tu kati ya nyingi ambayo inakufanya uingie kwenye 100 bora kama lengo ni kumtafuta mtu mmoja.

Kwa dunia ya leo mtu yeyeote mwenye degree moja anaweza kabisa kuwa waziri mzuri sana ili mradi awe na sifa hizo zingine.

Tumeona maprofesa wetu wanavyochemsha kwenye wizara, tumeona madkatri ambao
hata hawafai kusimamia nyumba zao.

Hawa mawaziri wote ni wabunge, ingefaa tunapowajadili, basi tuanze na je kule wanakotoka wamefanya nini? Kama mtu anashinda kuzunguka Dar na Dodoma na kuacha jimbo lake linadumaa, mnafikiri akiwa waziri au rais kwanini asiwe naye Vasco Dagama? Wote tumeona ya JK, kila mtu alidhani ataleta maajabu, laiti tungejiuliza mapema, je kafanya nini kule kwenye jimbo lake? Huenda wala tusingeliweka matagemeo makubwa.

Yuo are absolutely right Mtanzania. Kimsingi nchi yetu inakabiliwa na leadership crisis. Tumechanganyikiwa kiasi kwamba tumeanza kupima uwezo wa kiongozi kwa kuweza kuongea yale ambayo wengine wanaogopa kuyasema. Watu wa namna hii mimi nawaita ni majasiri (na sina uhakika kama kuongea kwao inatosha kuwaita kuwaita heroes). Hata hivyo, kuwa jasiri au hero inaweza ikawa ni moja ya ingredient ya uongozi lakini peke yake haikufanyi uwe kiongozi mzuri!

Kuna Professor moja mkali sana pale Havard (sina uhakika kama bado yupo pale) wa mambo leadership anaitwa Joseph Nye Jr.; yeye anasema heroes are best watch dogs but they are not necessarily good leaders. Kuna sehemu pia anasema kuwa heroes are only good leaders at the time of a crisis na akatoa mfano wa Churchil wakati wa vita. Maneno ya huyu profesa sio msaafu lakini yanatoa kamwanga zaidi katika mjadala wetu huu muhimu.

Waliopo US na UK, mnaweza kutafuta hiki kitabu kipya cha March 2008 kinapatikana kwenye all major book stores. Title yake ni: The Powers to Lead.

Pengine huko mbele itabidi tusaidie pia kuelimisha maana ya hero. Nahisi tumekuwa tukilitumia hili neno so loosely.
 
Jamaa kweli kachoka, naona kabisa si muda tena atabadili baraza, na ndio utakuwa mwisho wake, maana hatutaendelea kunyamazia kubadili wezi wakati sisi huku tunakufa njaa
 
KITU MUHIMU NI integrity
Mojawapo ya kazi ya Rais ni kuteua wasaidizi wake watakaomsaidia

kuongoza wizara kadhaa alizoziunda. Kama ambavyo Kasheshe

ametangulia kusema kwamba mawaziri ni wasimamiaji wa utekelezaji

wa sera za chama kilicho madarakani, mimi napenda kuongezea kwa

kurudia kuwakumbusha wana-JF kuwa uendeshaji wa shughuli za

wizara hufanywa na technical people wakiongozwa au kusimamiwa na

katibu mkuu wa wizara husika. Kwahiyo uteuzi wa mawaziri wa

kumsaidia Rais sidhani kama nina haja ya kuhoji ilhali mwenye

kuwateua wamsaidie hana tatizo nao. Ni vema tukakumbuka kuwa

Rais wa Tanzania ni mmoja tu.

I have no objection kwa wote walioteuliwa.

Mimi naona suala la waziri kuwa amebobea katika mambo ya wizara anayosimamia sio kitu cha muhimu kwa sababu hata wale ambao wapo deep kwenye fani zao wamechemsha vibaya. Ma-mikataba aliyotusainisha chenge alipokuwa mwanasheria yote ya kipumbavu tu, suala ni kwamba alikuwa anakusanya vijisenti, hilo ndiyo lilikuwa la msingi kwake. Kwa hiyo sasa hivi tuangalie INTEGRITY tu na tuachane na usomi linapokuja suala la uwaziri. Mawaziri wote waliochemsha vibaya katika wizara zao wote wameenda shule vizuri tu tena kwa pesa zetu, wamefanya nini kwa taifa hili kama sio kulifilisi tu????
Lakini, hakuna kitu tunachoweza kuwafanya watu kama akina chenge jamani? Kwa mfano kuwapoteza katika sura ya dunia hii!! Anyway, mimi nipo tayari nyenzo zikipatikana.
Nina uchungu
 
Kama masuala ya wizara yanaendeshwa na technical personnel chini ya usimamizi wa Katibu mkuu basi tusiwe na mawaziri kabisa ili tupunguze gharama
 
Jamaa kweli kachoka, naona kabisa si muda tena atabadili baraza, na ndio utakuwa mwisho wake, maana hatutaendelea kunyamazia kubadili wezi wakati sisi huku tunakufa njaa

Kumbe JK ndio anakusabishia njaa!!! uvivu wako tu ndg!!!
 
Mwanri pia ni mzalendo sana, ni chaguo zuri ingawa angefaa kuwa Waziri Kamili. Jamaa ni marxist huyu, acha!

Mzalendo gani mwizi tu huyo? Waulize wakazi wa siha wakueleze ukweli. Mwanri ni mwanachama halisi wa Chama Cha Mafisadi, unajua kwani nini uliondolewa kwenye uenezi CCM?

Marxist gani? Huyu naye ni bepari uchwara. Ni wanafiki wenye kujifunika kwa kivuli cha marxism kama alivyokuwa Kingunge Ngombare Mwizi.
http://www.chadema.net/makala/kafulila/david_6.html
Umesahau haya makala?
http://www.chadema.net/makala/kafulila/david_6.html

Halafu unakumbuka kauli ya Mwanri alivyokuja kwetu Zanzibar?

Asha
 
Kuhani Mkuu,

Na huu ni ndio upumbavu na uhuni watanzania tunaoupigia makelele... ati tunafikiri billioni moja(1) ya mzee wa vijisenti itaondoa tatizo la uchumi.

Siku moja nikakutana na mkaanga Samaki pale Dar es Salaam akaniuliza hivi, "Hivi kaka hizo fedha za EPA zikirudishwa mambo yatabadilika eeeh" nikamwambia sio fedha za EPA tu, na Za Meremeta n.k. ni maji ya kifuu kwenye bahari... ni kitu kidogo sana kwa uchumi wa nchi... tufanye kazi ndio njia ya kukomboa taifa.

Lingine ni Ujinga pia kudhani kwamba Rais alitakiwa kufanya mabadiliko makubwa kipindi hiki ambacho baraza lina miezi michache sana.

Kibaya zaidi vyama vyetu makini wakombozi wa wananachi wanafanya kwamba hizo ndio hoja kuu za kufanya uchumi ukue!!! Taifa linazama hili chini ya CCM au hata chini ya Kile chama makini.

Kwanza:
Ilikuwa ni Jambo jemaa kutoleta waziri mwingine mpya... kwanza kama habari ziko kamili kweli, atakuwa ampenguza waziri mmoja, kwenye baraza lake.

Pili:
Wizara ya Miundo Mbinu ni wizara nyeti sana, fedha nyingi zinaenda huko kupeleka mwadilifu na huenda mtu anayemwamini ni njia moja ya kulinda masilahi yetu wananchi.

Tatu:
Tusichanganye mambo mawaziri ni wanasiasa, kazi ya msingi inafanywa na makatibu wakuu na wakurugenz;

Nne;
Waziri ni mtizama masilahi ya wananchi akipenda of course maana anaweza angalia masilahi yake... lakini zaidi Waziri ni mtu anayeangalia kwamba sera za chama chake kama zinatekelezwa vizuri.

Kumezuka utamaduni wa kuhalalisha mawaziri kuhamishwahamishwa na kufanya lolote kwa kisingizio tu eti ni nafasi ya kisiasa. Inaelekea watanzania hatujui kazi ya mawaziri. Kama tunadhani kama hawana maana kiasi hicho kwanini tuwe nao? Uwaziri ni nafasi ya kisiasa- lakini nafasi hiyo ni muhimu kutoa mwelekeo wa wizara na kusimamia utendaji. Waziri lazima atoe vision, na kusimamia utekelezaji. Sasa kama leo anakuja waziri yule na vision ile na style ile ya kusimamia watendaji kesho anabadilishwa anakuja huyu na lile basi tunapoteza maana nzima ya uongozi. Serikali sio kitalu cha majaribio. Hata hao makatibu nao wengi wao ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi, lazima wawe chini ya mawaziri proper. Kwa kweli nchi inakwenda harijojo

Asha
 
Jamani Magufuli Pombe kapelekwa wapi? Au ndio kazimwa? Au yuko katika kashfa zinazokuja za EPA au za nyumba?
 
Wakuu,
Sasa Jk kuhamisha vyombo kutoka kabati moja na kupeleke kabati lingine,kutamfanya aonekane amepiga shopping la nguvu au?

Yaani Msola anapelekwa mawasiliano? Elimu ya juu kumemshinda badala ya kumfukuzia mbali akampeleka Kilimo,leo hii opportunity ya kumweka benchi imekuja ameichezea tena (maanake ni muoga wa kufukuza hadi opportunity kama hizi zitokee)

Sasa pale kilimo atakua amefanya nini?maanake ni miezi miwili tu amekaa hapo halafu baadae aseme muda wa yeye kufanya kazi ulikua hautoshi.

Aggrey Mwamri kupelekwa TAMISEMI kuna interest za kichama zaidi ya kuchapa kazi kitaifa.
Pia ni turufu nyingine ya kujakumpatia kazi yenye nguvu zaidi ya hiyo.

Sasa Jk usanii unampeleka kubaya.Very comfused president! Anahitaji msasada zaidi! pia wafuasi na wapambe wake wamuambie kuna thread inaendelea huku JF ya kumtafuta atakaetufaa 2010.For the next 2 years watz tumeamua kuwa mbuzi wa shughuli but 2010 patakua hapatoshi!
 
Mzalendo gani mwizi tu huyo? Waulize wakazi wa siha wakueleze ukweli. Mwanri ni mwanachama halisi wa Chama Cha Mafisadi, unajua kwani nini uliondolewa kwenye uenezi CCM?

Marxist gani? Huyu naye ni bepari uchwara. Ni wanafiki wenye kujifunika kwa kivuli cha marxism kama alivyokuwa Kingunge Ngombare Mwizi.
http://www.chadema.net/makala/kafulila/david_6.html
Umesahau haya makala?
http://www.chadema.net/makala/kafulila/david_6.html

Halafu unakumbuka kauli ya Mwanri alivyokuja kwetu Zanzibar?

Asha

kwi kwi kwi... Zitto Nyang'anya kadi hii mwanachama yako... haiheshimu yeye kwamba iko kaa na Mwanri kwa miaka miwili... sheee, napandishi mori shikilia mimi!!! hii ndio torono tukulu!!!

Torono -- maana yake "mtukukutu" kwa kimasa
Tukulu ---maana yake "saba" jwa kimasai
 
Duh,yamekua haya tena? Tukishakulia kwenye mfumo wa kidikteta mambo ndio haya,kizuri hapo CHADEMA wamezoe debate nzito
 
kwi kwi kwi... Zitto Nyang'anya kadi hii mwanachama yako... haiheshimu yeye kwamba iko kaa na Mwanri kwa miaka miwili... sheee, napandishi mori shikilia mimi!!! hii ndio torono tukulu!!!

Torono -- maana yake "mtukukutu" kwa kimasa
Tukulu ---maana yake "saba" jwa kimasai

Kasheshe naungana na wewe kumpinga Da Asha kabisa. Huyu Naibu Waziri uwezo wake wa kikazi ni mkubwa sana na kumuita bepari ni kumuonea waziwazi.

Just because the last post he had was in CCM, does not necessarily means he will do things kichama.

Actually bado nashangaa kwamba kawekwa TAMISEMI mimi nilidhani miundombinu kwa sababu mkuu alihitaji ufanisi kwenye barabara, lakini unajua tena mambo ya Ikulu vitu vinabadilika minute by minute.
 
kwa baraza hili sijapata matumaini ya maendeleo.

tusubiri muibuko mwengine wa kashfa za ufisadi
 
Back
Top Bottom