Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 787
"Tusiwadanganye wananchi, kuwa tukiwaondoa wala rushwa, matatizo ya Watanzania yataisha.
"Tunaanza kuwa na utamaduni wa kutafuta dosari hasa za viongozi na kusahau mambo ya msingi ya kulisaidia taifa. Ombi langu, hii tabia ya kupakana matope haiisaidii nchi, waandishi hizi habari ndizo zinapaswa kupewa kipaumbele?"[/SIZE]
Kuhani Mkuu,
Na huu ni ndio upumbavu na uhuni watanzania tunaoupigia makelele... ati tunafikiri billioni moja(1) ya mzee wa vijisenti itaondoa tatizo la uchumi.
Siku moja nikakutana na mkaanga Samaki pale Dar es Salaam akaniuliza hivi, "Hivi kaka hizo fedha za EPA zikirudishwa mambo yatabadilika eeeh" nikamwambia sio fedha za EPA tu, na Za Meremeta n.k. ni maji ya kifuu kwenye bahari... ni kitu kidogo sana kwa uchumi wa nchi... tufanye kazi ndio njia ya kukomboa taifa.
Lingine ni Ujinga pia kudhani kwamba Rais alitakiwa kufanya mabadiliko makubwa kipindi hiki ambacho baraza lina miezi michache sana.
Kibaya zaidi vyama vyetu makini wakombozi wa wananachi wanafanya kwamba hizo ndio hoja kuu za kufanya uchumi ukue!!! Taifa linazama hili chini ya CCM au hata chini ya Kile chama makini.
Kwanza:
Ilikuwa ni Jambo jemaa kutoleta waziri mwingine mpya... kwanza kama habari ziko kamili kweli, atakuwa ampenguza waziri mmoja, kwenye baraza lake.
Pili:
Wizara ya Miundo Mbinu ni wizara nyeti sana, fedha nyingi zinaenda huko kupeleka mwadilifu na huenda mtu anayemwamini ni njia moja ya kulinda masilahi yetu wananchi.
Tatu:
Tusichanganye mambo mawaziri ni wanasiasa, kazi ya msingi inafanywa na makatibu wakuu na wakurugenz;
Nne;
Waziri ni mtizama masilahi ya wananchi akipenda of course maana anaweza angalia masilahi yake... lakini zaidi Waziri ni mtu anayeangalia kwamba sera za chama chake kama zinatekelezwa vizuri.