Mbunge Norah Mzeru ataka kujua hatma ya zahanati ya kata ya Mafisa, Morogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE NORAH MZERU ATAKA KUJUA HATMA YA ZAHANATI YA KATA YA MAFISA MKOANI MOROGORO

"Je, lini Serikali itamalizia ujenzi wa Zahanati ya Uwanja wa Ndege katika Kata ya Mafisa Mkoani Morogoro?" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Katika kusogeza huduma za afya kwa wananchi wa uwanja wa ndege mwaka wa fedha 2017-2018 Serikali ilipeleka Shilingi Milioni 70 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati ya Uwanja wa Ndege iliyopo Kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro. Ujenzi umekamilika na huduma zimeanza kutolewa mwezi Mei 2022. Kwa wastani huhudumia wagonjwa wapatao 750 kwa mwezi na wagonjwa 9000 kwa mwaka" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI

"Zahanati ya Kiwanja cha Ndege ina upungufu wa Wafanyakazi hasa Wauguzi (Nurses) na Madaktari. Je, ni lini mtawapeleka? Kituo cha Afya Mafiga kimekuwa na tatizo la Theatre (Upasuaji) na wanawake wengi wajawazito wanapenda kujifungulia na wanapata matatizo na kuwapeleka hospital kubwa. Je, ni lini Theatre itajengwa?" - Mhe. Christina Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Zahanati ya uwanja wa ndege ina watumishi watano na afisa tabibu mmoja, wauguzi wawili, mtaalamu wa maabara mmoja na muhudumu wa afya mmoja. Katika idadi ya wananchi wanaohudumiwa tunatakiwa kuongeza Wataalam" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI

"Serikali inaitambua Zahanati ya Mafiga, mara ajira zitakapojitokeza tutahakikisha tunawapa kipaumbele kwaajili ya kuongeza watumishi. Kituo cha Afya cha Mafiga kipo Mjini kinahudumia wananchi wengi, kina upungufu wa baadhi ya Miundombinu na majengo ya upasuaji. Tumeshamuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kuandaa mchoro wa Upanuzi wa kituo cha Afya cha Mafiga, tutafuatilia na kuona namna ya kuongeza majengo" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-02-13 at 06.15.50.mp4
    15.6 MB
  • IMG_9937.jpg
    IMG_9937.jpg
    39.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-29 at 16.27.05.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-29 at 16.27.05.jpeg
    165.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom