News Alert:...... Uteuzi cabinet

kwi kwi kwi... Zitto Nyang'anya kadi hii mwanachama yako... haiheshimu yeye kwamba iko kaa na Mwanri kwa miaka miwili... sheee, napandishi mori shikilia mimi!!! hii ndio torono tukulu!!!

Torono -- maana yake "mtukukutu" kwa kimasa
Tukulu ---maana yake "saba" jwa kimasai

Yupo huru kabisa kutoa maoni yake. Sisi hatunyanganyani kadi kwa kupishana maoni. Kwa mwono wangu Mwanri ni mjamaa, kwa maneno na vitendo. Alipokuwa CCM kama Katibu Mwenezi alikuwa lazima atetee chama chake na sisi lazima tumlime kwani ndio siasa na ndio maana ya kuwa vyama tofauti. Mwanri ni mtu mzuri, ni mwadilifu sana na alifanya kazi vizuri sana na Mwenyekiti wetu walipokuwa wabunge wa Wilaya ya Hai na Halmashauri ikiwa chini ya CHADEMA. Tatizo lake ni mwoga sana. Woga wa kimaadili na sio woga wa kifisadi!
 
Nimeona wakati mjadala unaendelea niiweke hii taarifa rasmi ya Ikulu kwa ajili ya kutunza kumbukumbu:

TAARIFA YA SERIKALI KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: MABADILIKO MADOGO YA BARAZA
LA MAWAZIRI

Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Mheshimiwa Andrew Chenge hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:

MAWAZIRI:

1.1 Wizara ya Miundombinu:

Mheshimiwa Dk. Shukuru J. Kawambwa ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Miundombinu. Mheshimiwa Kawambwa anatokea Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

1.2 Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia:

Profesa Peter M. Msolla anakuwa Waziri

1.3 Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI

Mhe. Celina O. Kombani ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI. Mheshimiwa Celina Kombani alikuwa ni Naibu Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.

1.4 Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Mhe. Stephen M. Wassira - ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Mheshimiwa Wassira anatokea Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

NAIBU MAWAZIRI

1.5 Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI

Mhe. Aggrey Mwandri, Mbunge wa SIHA.

1.6 Miundombinu

Mheshimiwa Ezekia Chibulunje (anahama kutoka Wizara ya Kazi)

1.7 Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana

Mhe. Dr. Milton M. Mahanga (anahamia kutoka Miundombinu)
 
Hivi, akijiuzulu Msolla tena itakuwaje? Nadhani kuna haja ya Rais Kikwete kutumia the "Nuclear Option".. haiwezekani kufanya mambo hivi yanavyofanywa sasa.
 
Hivi, akijiuzulu Msolla tena itakuwaje? Nadhani kuna haja ya Rais Kikwete kutumia the "Nuclear Option".. haiwezekani kufanya mambo hivi yanavyofanywa sasa.

wewe na msolla ugomvi wenu ni nn? ni wa ukraine au kuna mengine?

vipi kuhusu ukaaji wako kihalali ushaushughulikia?/
 
Just to clarify - Prof Msolla's qualification are: Bachelor of Veterinary Science Nairobi 1972; MVM & PhD [Veterinary Medicine] Glasgow - Scotland [1980]. Toka hapo amekuwa akifundisha SUA kama Senior Lecturer [1981]; Associate Professor [1984] and full Professor [1987]. Katika mwaka 1988 akateuliwa kuwa Deputy Vice Chancelorr wa SUA nafasi aliyoishika mpaka alipostaafu mwaka 2005 na kwenda kupigania Ubunge huko kwao Iringa. Yeye ni profesa wa veterinary medicine kwa hiyo Kilimo labda asingeweza kiutaalamu - kama hiyo ndiyo criteria ya kuchagua waziri - yeye labda angefaa zaidi huko kwenye Wizara ya Kitoweo aliyopewa Ndugu Pombe Magufuli.

Nafikiri kumrudisha Wassira hapo Kilimo ni decision nzuri. Pia kumweka Dr. Kawambwa kwenye Miundo mbili ingawaje ni mechanical engineer ni decision nzuri - kuna mechanical infrastructure pia kama ATC; ferries etc under wizara hii. La muhimu lakini ni waziri kuwa na wisdom na leadership qualities na sio lazima awe amesomea fani ya wizara anayoongoza - technical inputs zina kuwa provided na civil servants katika ngazi ya Director etc. In fact the best Minister wa kilimo Tanzania alikuwa Marehemu Derek Bryceson [kwenye 1960s] ambaye hakusomea kilimo bali alikuwa airforce officer katika jeshi la uingereza. That is when kilimo cha Tanzania kilikuwa kina grow by 6-9% per annum.
 
Good point

Hapo ndipo tunapofungwa magoli, utakuta jitu linapewa uwaziri wakati halina hata chembe ya leadership quality. At the same time limevurunda kila mahali lilipokuwepo.
 
Jasusi

Karibu sana Mzee ulipotea siku nyingi.

Dua,
Ahsante rafiki yangu. NIlikuwa Bongo kwa shughuli za kibinafsi. Unajua tena internet za Bongo unalipa shilingi alfu moja mia saba kwa saa moja. Haikunipa muda mzuri wa kuchangia. Lakini nilipata fursa ya kukutana na wana JF kibao.
 
Yupo huru kabisa kutoa maoni yake. Sisi hatunyanganyani kadi kwa kupishana maoni. Kwa mwono wangu Mwanri ni mjamaa, kwa maneno na vitendo. Alipokuwa CCM kama Katibu Mwenezi alikuwa lazima atetee chama chake na sisi lazima tumlime kwani ndio siasa na ndio maana ya kuwa vyama tofauti. Mwanri ni mtu mzuri, ni mwadilifu sana na alifanya kazi vizuri sana na Mwenyekiti wetu walipokuwa wabunge wa Wilaya ya Hai na Halmashauri ikiwa chini ya CHADEMA. Tatizo lake ni mwoga sana. Woga wa kimaadili na sio woga wa kifisadi!

Mkuu Zitto,

Heshima mbele mkuu, ukiweza kuja mara kwa mara na kutoa maoni mazito kama haya yasiyojali chama cha siasa, basi utatusaidia sana hapa na wenzetu fulani ambao vyama vimewaingia hata hawawezi kuliona taifa,

wako ni mfano wa kuigwa hapa JF, wa kutojali chama badala yake kuwa mkweli tu kwa faida ya taifa letu, and let the chips fall where they may!
 
Kitu kimoja kizuri katika mabadiliko kadhaa anayofanya JK ni kupandisha manaibu kuwa Mawaziri. Hili ni zuri. Naunga mkono uteuzi wa Kombani TAMISEMI. Hivi hakuteua naibu Waziri TAMISEMI? Maana sijaona hapa au mmesahau?

Mwanri pia ni mzalendo sana, ni chaguo zuri ingawa angefaa kuwa Waziri Kamili. Jamaa ni marxist huyu, acha!

Mwanri ni genious lakini hapewi nafasi ya ku utilize ugenious wake badala yake wakamweka kwenye propaganda za Chama kwasababu jamaa naye ana convincing power ya ajabu!

Yani anaweza akakufanya uipende CCM penda usipende!

Ila kwasababu ya grassroot movement inayoendelea Tanzania hivi sasa ni wazi hatuna haja ya kujadili uwaziri atakaokuwa nao kwa less than two yrs kwani inabidi ajiandae huko jimboni mwake Siha kuwa atarun kwa tiketi ya CCM, AMA YA WAZALENDO!
 
Naona huyu Mwanri kifaa tosha kabisa, kiongozi yeyote asiyekuwa fisadi leo hii ni adimu hasa akiwa na elimu kama yake.
Najua sasa hivi atapanda daraja kwani wabaya wake wote wamesha pigwa chini. Na hilo alosema mh. Zitto kuwa ni mwoga wa maadili bila shaka ni kuonyesha tofauti yake na mafisadi ambao hujenga maadili pinzani, hivyo kama huna ubavu mkuu ni bora uwe mwoga..
Mwanri atapeta ni hard working guy na kama nilivyosema kuhusu Membe ingawa wengi wachangiaji hapa hawakumpenda..
Mfanyakazi kwa bidii siku zote malipo yapo njiani hata kama yatachelewa kwa miaka...
 
wewe na msolla ugomvi wenu ni nn? ni wa ukraine au kuna mengine?

vipi kuhusu ukaaji wako kihalali ushaushughulikia?/

Mkuu,
Labda na mimi nikuulize, Tatizo lako na mwanakijiji ni ni hasa? Kukukamata kwa hoja?

Na vipi kuhusu uhalali wako wa kuleta hizi personal issues kwenye mambo mazito ya Kitaifa?
 
Sijui nani awasaidie hawa wazee wetu wawili, Wassira na Msolla waweze kuzisoma dalili na nyakati waone kwamba sasa na sio baadaye waachie ngazi kwani hata Kikwete mwenyewe anawaonea haya tu kuwabakiza.Akufukuzaye sio lazima akwambie toka!
 
Anko Kikwete na mimi naomba wizara jamani, mbona Anko Shukuru Kawabwa kwa muda wa miaka miwili na nusu tu ameshazunguka wizara 4???? Je kwani unampango wa kumpa uwaziri mkuu??????? maana hizo mbio si bure lazima unampango nae mkubwa zaid.
 
Mazee hiyo ni kuhamisha kutoka kwenye pakacha na kuweka kwenye tenga vyote vinavuja tu.. Nadhani JK inabidi tuwe tunamsaidia ushauri wa bure angalau anyanyue macho mbele mita 100 ajue kuwa kuna vichwa kibao vinaweza kufanya kazi.....
 
Anko Kikwete na mimi naomba wizara jamani, mbona Anko Shukuru Kawabwa kwa muda wa miaka miwili na nusu tu ameshazunguka wizara 4???? Je kwani unampango wa kumpa uwaziri mkuu??????? maana hizo mbio si bure lazima unampango nae mkubwa zaid.

Kumbe I was right, Kawambwa ni anko! Ahsante Domo Kaya wewe ninakuamnia sana, vipi kulikoni siku hizi huopnekani mkuu?
 
Kaepusha Mwalimu Na Mwanafunzi Wake Kusigana Pale...kilimo Na Chakula.......kamtoa Mahanga Ili Kuepusha Kawambwa Kupelekeshwa Na Mahanga Maana Alishakuwa Gwiji Pale Miundombinu.....mnakumbuka Nec ?ile Ilikuwa Vita Kali Sana.....vijisenti Aganist Mahanga
 
Kumbe I was right, Kawambwa ni anko! Ahsante Domo Kaya wewe ninakuamnia sana, vipi kulikoni siku hizi huopnekani mkuu?

Mambo tu ndungu yangu yamekuwa mengi, si unajua mafisadi wamekomba pesa yote, na huko juu ndio kubebana mtindo mmoja, ndio maana na sisi tunakimbizana ili tuende nao sawa. ila nipo ndungu yangu.
 
Back
Top Bottom