Ndani ya muda mfupi Rais Samia amefanya kufuru, licha ya kuupiga mwingi sasa anakimbiza mwizi kimya kimya

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Kama tukiweka unafiki pembeni, Kwa muda mfupi ambao Rais Samia ameingia ikulu amefanya kazi kubwa sana ambayo kama ingefanywa na serikali iliyopita ingechukua miaka kadhaa kukamilika

Mama katika kipindi cha miezi sita ambacho ameingia ikulu kwenye sekta ya afya tayari ameidhinisha mabilioni ya pesa yanayoenda kujenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa ambazo hazikuwa na vituo hivyo kabla. Nje na ujenzi wa vituo vya afya pia ameimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu.

Kwenye elimu, ndani ya miezi sita mama amejenga vyumba vya madarasa 560 na shule moja ya sekondari ya wasichana kila wilaya ambapo ujenzi bado unaendelea.

Kwenye miundo mbinu kwa kipindi cha miezi sita mama ametoa milioni 500 kila jimbo kwaajili ya ujenzi wa barabara za vijijini na miradi mikubwa yote iliyoachwa na mtangulizi wake yote inaendelea kama kawaida na hakuna hata mradi mmoja uliokwama

Kwenye sekta ya anga na usafiri, tayari mama ameidhinisha zaidi ya bilioni 200 kama malipo ya awali ya ununuzi wa ndege tano kama mkakati wa kufufua shirika letu la ndege 'ATCL'

Kuhusu uhaba wa watumishi, ndani ya miezi sita mama ameajiri watumishi 9,675 wakiwemo walimu 6,749 na watumishi wa afya 2, 726. Kama hiyo haitoshi anatarajia kuongeza watumishi wengine zaidi ya 10,000 kwenye sekta ya elimu kwaajili ya kupunguza uhaba uliopo. Na itakumbukwa kuwa kwa miaka sita ambayo mtangulizi wake alikuwa madarakani hakuwahi kuajiri watumishi 10,000 kwa mkupuo mmoja lakini mama huyu anaenda kuifanya kazi hiyo ndani ya muda mfupi tangu aingie madarakani.

Ukiachana na watumishi wa afya na elimu, ndani ya miezi sita ameachia kibali cha kuajiri askari wa jeshi la polisi zaidi ya 3,000 kwaajili ya kuimarisha usalama wa Raia na mali zao.

Kwenye sekta ya kilimo Rais samia amepandisha bei ya mazao ukiwemo mtama, pamba, kunde na hivi karibuni serikali anayoiongoza inajipanga kununua mahindi ya wakulima ili kuwawezesha kiuchumi na kujikimu hadi msimu ujao.

Licha ya kazi kubwa anayofanya hakuna makelele ya kumsifu na kumpamba kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake na hii ndio dhana halisi ya usemi "mama anakimbiza mwizi kimya kimya"

Tuzidi kumpa support ili apate nguvu ya kutufanyia mambo makubwa
 
Unajua mambo yakiwa poa wala hauhitaji kukumbushwa wala kuambiwa kwamba mambo yanakwenda vizuri...

Ila simlaumu per se...., binafsi naona mambo yalianza kwenye mrama kitambo
Watu wengi hasa wa mitandaoni vichwa vyao wamekabidhi genge fulani la wanasiasa. Na kama umavyojua wanasiasa wana keleleee, usipowapa wanachotaka wanapiga kelele kuonesha kama vile hakuna unachofanya kwa vile wao hujawapa wanachotaka.

Samia is doing very good.

Ukiachana nange la wanasiasa uchwara, inahitajika marekebisho kidogo tu.
 
Mama anafanya maajabu kimya kimya tazama mandela road malori yanayoingia bandarini yalivyojazana,angalia jinsi mabarabara yanavyojengwa miradi ya mwenda zake inasonga mbele sijalalama hata kidogo kukatwa tozo naona ni halali kabisa atuondolee wabunge batili bungeni wana kila kodi za bure kabisa watanzania tunafurahi sana pale fedha tunazochangia zinapotumika kiuhalali.
 
Mama huwezi mlinganisha na wale mburukenge washamba ambao Kazi kubwa walioweza ni kujitutumua, kufoka na kukunja ndita, kudanganya, kujisifu na kuharibu uchumi kwa kujificha kwenye kichaka cha uzalendo..

Raha ya mama wala hana muda wa kuhangaika na wapumbavu, amewaacha mara walinganishe hivi, waseme hili lakini yeye Kazi zinaenda ..

Hii ndio inaitwa kuonyesha uongozi sio kupayuka hovyo na kujitutumua
 
Mama amefanya na bado anafanya mambo mengi makubwa, na ya maana ambayo milioni 60 ya watanzania tunayaona kwa macho yetu ukiacha idadi ndogo ya wale wanaoshikiwa akili, mawazo na fikra na hawa wachumia tumbo. Tena wengi wao wapo humu mitandaoni, ila ukiingia mtaani kuuliza wanaompinga mama huwaoni. Ni aibu kubwa kwa mtoto wa kiume kukubali kushikiwa akili na kuuza utu wake kwa sababu ya njaa yake.

images (26).jpeg
 
Back
Top Bottom