Ndani ya muda mfupi Rais Samia amefanya kufuru, licha ya kuupiga mwingi sasa anakimbiza mwizi kimya kimya

Na sisi tumsifie mwenyekiti wetu kwa kujenga makao makuu yetu kupitia ruzuku zetu. Japo ametumia mamilioni ya ruzuku zetu kwenda kula bata Dubai na Afrika kusini na familia yake ila si haba amefanya jambo.
CCM mmechoka akili ni wa kuwapumzisha Tu sasa

Miaka 60 mnamsifia Rais kujenga madarasa mnatia aibu

images (18).jpeg
 
UTAWALA WAKE UMEPIMWA NA HAKIKA UMEPUNGUA
Kuna kikundi kimejidhatiti kumpinga mama kwa kila kitu kwa interest za kisiasa huenda wewe ni kiongozi wa hicho kikundi ila uzuri ni kwamba licha ya kwamba mnapinga moyoni mnamkubali kiaina
 
Ni kweli kafanya vizuri kwenye mavitu vitu, ila suala la HAKI, UTAWALA BORA na UTAWALA WA SHERIA anahitaji kuwekeza nguvu ili afikie 99.9............% ya ubora
 
Tozo ndizo zinasaidia kuleta miradi ya maendeleo hata vituo vya afya 220 na madarasa 560 ni matunda yanayotokana na miambili miambili zetu tunazokatwa kama tozo kwahiyo hili sio la kulaumu kabisa kwa sababu matokeo tunayaona
 
Mama yenu amekwama sana maeneo yenye changamoto, bado anatembelea nyota ya mwendazake. Kashindwa kushughulika na bei ya mbolea na mazao kama tumbaku. Watumish wamemshinda. Ufanisi na nidhamu umeshuka uzembe rushwa na ufisadi unatamalaki . Tumuambie ukweli, tumpe mbinu na tumpe moyo
 
Nakubaliana na sentensi yako ya mwisho tumpe Mh Rais SSH support na kumtia nguvu kwa yale mema na mazuri anayo ya fanya. Jambo jema jingine nililoliona kwa serikali yake wanapo kosolewa kwa mambo nyenye mashiko wanayafanyia kazi. Yako mambo yaliyokosolewa na mengine kutolewa ushauri hapa jF na tumeona na kusikia serikali inayafanyia kazi. Tujiulize jF sisi ni nani kati ya Watanzani 60Millioni mpaka kustahili na kupewa heshima hii?!

Nisichokubaliana na wewe ni ulivyoanza kwa kumponda JPM na serikali yake. Wengine hatutanyamaza katika hilo.

Vinginevyo Mh Mama Rais ana miezi sita tu tangu ashike usukani tumpe muda na wanaomsaidia kazi wampe ushirikiano wa kutosha na kujitoa hasa, tutafika kwa pamoja. Wengine tunaendelea kumuombea na tumejitoa kwa hilo. Pale penye mapungufu tutasema na kwenye kustahili kupongezwa tutapongeza bila chembe yetote ya unafiki.
 
Kama tukiweka unafiki pembeni, Kwa muda mfupi ambao Rais Samia ameingia ikulu amefanya kazi kubwa sana ambayo kama ingefanywa na serikali iliyopita ingechukua miaka kadhaa kukamilika...
Akiweza kudhibiti kwenye dawa hapo ndio nitakubaliana na wewe, maana dawa kwa kweli lazima utaambiwa ukanunue pharmacy
 
Back
Top Bottom