Naibu Waziri Mollel asema Rais Samia amefanya uwekezaji mkubwa Sekta ya Afya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini ili kuhakikisha afya za wananchi zinaimarika

Dkt. Mollel amebainisha hayo wakati alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uzinduzi wa Chuo cha Afya Litembo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Dkt. Mollel amesema kuwa rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza zaidi ya Trilioni 6.7 katika sekta ya afya ili kuboresha miundombinu, upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendaanishi, kuongeza watumishi wa afya pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wataalamu wa afya kupitia programu ya Samia Scholar ship ndani ya miaka miwili katika sekta ya afya.

“Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga nDkt. Sambia amewekeza zaidi ya Bilioni 4 ili kuhakikisha wananchi wa Mbinga wanapata Huduma bora za afya ili kuwa na afya bora na kuendelea na maisha yautafutaji ili kujenga nchini”, ameeleza Dkt. Mollel

Aidha katika kwendelea kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafs Rais Samia amekuwa ni kiunganishi ili kuhakikisha sekta binafsi wanafanya vizuri nchini.

Akizungumza amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi imara wa Rais Samia ndani ya mwaka huu imenunua magari ya kubeba wagonjwa 727 na magari 201 yameshafika ndani ya nchini na hivi karibuni yatazinduliwa na kusambazwa katika maeneo yenye uhitaji wa magari ya kubeba wagonjwa.
 
Huyu taahira angetuliaa wanaume huwa hatujikombi hivii.....asimame kama yeye....sio chawaa....kama chawa....upuuziii
 
Back
Top Bottom