Ndani ya muda mfupi Rais Samia amefanya kufuru, licha ya kuupiga mwingi sasa anakimbiza mwizi kimya kimya

Milioni 500 kila jimbo ndani ya miezi sita ngoja tufanye mahesabu.
Majimbo zaidi ya 264.
264x500=132,000,000,000Tsh
Inawezekana.
Shida ya hii ni impact haitaonekana...Pesa ndogo kama hii haiwezi weka barabara ya lami hata kilomita moja...Waliomshauri mama hawamtakii mema at the end hizo barabara baada ya mvua zitakuwa kama hazijafanyiwa kazi then ataonekana kama vile hizo pesa hazikufanya kazi...The back stops at her, she will be accountable for everything...Wanaomshauri wapo na interest ya kisiasa ambayo pia ni short lived

After sometime na hizi budget za kugusa hapa na pale you wont be able to see value for money zaidi ya pesa nyingi kuonekana kutumika
 
Kama tukiweka unafiki pembeni, Kwa muda mfupi ambao Rais Samia ameingia ikulu amefanya kazi kubwa sana ambayo kama ingefanywa na serikali iliyopita ingechukua miaka kadhaa kukamilika

Mama katika kipindi cha miezi sita ambacho ameingia ikulu kwenye sekta ya afya tayari ameidhinisha mabilioni ya pesa yanayoenda kujenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa ambazo hazikuwa na vituo hivyo kabla. Nje na ujenzi wa vituo vya afya pia ameimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu.

Kwenye elimu, ndani ya miezi sita mama amejenga vyumba vya madarasa 560 na shule moja ya sekondari ya wasichana kila wilaya ambapo ujenzi bado unaendelea.

Kwenye miundo mbinu kwa kipindi cha miezi sita mama ametoa milioni 500 kila jimbo kwaajili ya ujenzi wa barabara za vijijini na miradi mikubwa yote iliyoachwa na mtangulizi wake yote inaendelea kama kawaida na hakuna hata mradi mmoja uliokwama

Kwenye sekta ya anga na usafiri, tayari mama ameidhinisha zaidi ya bilioni 200 kama malipo ya awali ya ununuzi wa ndege tano kama mkakati wa kufufua shirika letu la ndege 'ATCL'

Kuhusu uhaba wa watumishi, ndani ya miezi sita mama ameajiri watumishi 9,675 wakiwemo walimu 6,749 na watumishi wa afya 2, 726. Kama hiyo haitoshi anatarajia kuongeza watumishi wengine zaidi ya 10,000 kwenye sekta ya elimu kwaajili ya kupunguza uhaba uliopo. Na itakumbukwa kuwa kwa miaka sita ambayo mtangulizi wake alikuwa madarakani hakuwahi kuajiri watumishi 10,000 kwa mkupuo mmoja lakini mama huyu anaenda kuifanya kazi hiyo ndani ya muda mfupi tangu aingie madarakani.

Ukiachana na watumishi wa afya na elimu, ndani ya miezi sita ameachia kibali cha kuajiri askari wa jeshi la polisi zaidi ya 3,000 kwaajili ya kuimarisha usalama wa Raia na mali zao.

Kwenye sekta ya kilimo Rais samia amepandisha bei ya mazao ukiwemo mtama, pamba, kunde na hivi karibuni serikali anayoiongoza inajipanga kununua mahindi ya wakulima ili kuwawezesha kiuchumi na kujikimu hadi msimu ujao.

Licha ya kazi kubwa anayofanya hakuna makelele ya kumsifu na kumpamba kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake na hii ndio dhana halisi ya usemi "mama anakimbiza mwizi kimya kimya"

Tuzidi kumpa support ili apate nguvu ya kutufanyia mambo makubwa
Wanajeshi kawapandisha vyeo, wanajeshi wanamkubari Sana Samia
 
unasubil teuzi?
 
Back
Top Bottom