Nchi za Afrika tunadharauliana wenyewe kwa wenyewe. Hii si sawa

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,514
Miaka ya nyuma tumesaidia nchi nyingi sana katika harakati za Ukombozi. Kupinga Ubaguzi,Ukandamizaji ba Uonevu.

Nchi nyingi. Tuna maeneo na mitaa mingi kwa Majina ya Wanaharakati na wakombozi wa Africa. Mitaa kama Nkrumah n.k na hata Shuleni nakumbuka kulikuwa na Mabweni kama Nkrumah, Samora, Mandela n.k

Leo hii nchi nyingi zinatudharau kwa kiburi tu. Rais wetu si wa wa kupokelewa na watu wa namna hii. Kuna shida gani? Kwani hakutoa taarifa? Hivi angekuwa ameenda Biden Ghana wangempokea hivi?

Jamaa amevaa vitu vya ajabu kabisa ameenda mpoke Rais wetu. Ba watu wa kuhesabu ambao unawatizama tu unaona huyu dada mmoja ni Afsa Ustawi wa Jamii, yule kule ni Nurse au Mkunga ambaye siku hiyo inaonekana alikuwa zamu.

Huyo jamaa mwenye suruali ya blue Injia alikuwa site na safety booty akaomba koti kwa mchina mmoja akaja mpokea Rais. Halafu yule dada anayeongea na Rais pale ni Bank Teller na amekuja na sandals zake sababu wakikaa pale kaunta huwa chini hatuwaoni ndo kaja hivyo hivyo.

Yaani unaona walio smart ni watu wetu walioongozana na Rais. Hili si jambo zuri kwa nchi zetu kufanyiana. Lazima wamheshimu Rais wetu. Swali je angekuwa anatoka USA au UK wangefanya hivi?

Screenshot_20220523-202945_Instagram~2.jpg
 
Huo ndio uhalisia, sio hapa unakuta viongozi wanapata imprest zisizoendana na uhalisia wa maisha ya wananchi. Hao jamaa wanapata mishahara yao ya halali, na hawalipwi ili wakanunue suit za kupokelea viongozi.

Hapa unakuta msafara wa magari kibao yakiwa na watu wamevaa masuti mazito mazito, wakati hawana ulazima wowote wa kwenda kumpokea kiongozi.
 
Huo ndio uhalisia, sio hapa unakuta viongozi wanapata imprest zisizoendana na uhalisia wa maisha ya wananchi. Hao jamaa wanapata mishahara yao ya halali, na hawalipwi ili wakanunue suit za kupokelea viongozi. Hapa unakuta msafara wa magari kibao yakiwa na watu wamevaa masuti mazito mazito, wakati hawana ulazima wowote wa kwenda kumpokea kiongozi.
Nchi yetu imekaa kitapeli sn
 
nadhani nchi nyingine wanaabudu mavazi kama nyie? hao ndio maafisa walioandaliwa kumpokea Rais wee unasema dharau ,kama hutaki dharau kaa kwenu acha kuzurura kwa watu, ni mara nyingi sana viongozi wanapokelewa na mawaziri then siku inayofuata ndio anakutana na Rais husika.
Well said
 
mwingine anasema tunadhalilishwa wakati ghana mm naijua ni miongoni mwa nchi za afrika ambayo demokrasia yake ni ya hali ya juu.mama atajifunza vitu kutoka kwao kama atapenda.hawana rasilimali za kuchezea wao rasilimali zao huenda moja kwa moja kwa wananchi.na huwezi kusikia vurugu za ajabu ajabu ktk nchi na usipokuwa mfuatiliaji wa mambo huwezi kuijua nchi hiyo ya ghana.
 
mwingine anasema tunadhalilishwa wakati ghana mm naijua ni mwongoni mwa nchi za afya ambayo demokrasia yake ni ya hali ya juu.mama atajifunza vitu kutoka kwao kama atapenda.hawana rasilimali za kuchezea wao rasilimali zao huenda moja kwa moja kwa wananchi.na huwezi kusikia vurugu za ajabu ajbu ktk nchi na usipokuwa mfuatiliaji wa mambo huwezi kuijua nchi hiyo ya ghana.
Ungejua Waghana wanavyomponda rais wao, Wala usingeandika hizi porojo
 
Back
Top Bottom