Vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika ni matokeo ya viongozi waliokosa utu na hekima

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Mmeshindaje wanaJF wenzangu?

Tukiangalia kona nyingi ama nchi nyingi za Afrika zipo ndani ya vita vya ndani ambapo wahanga wakuu ni wananchi ambao kila anayepigana anataka kuwwtawala. Riek Machari na Salva Kiir ni mfano wa kuangalia namna ambavyo kiongozi na aliyekuwa makamu wake wanavyoiona Sudani Kusini ni mali zao binafsi kiasi kwamba wanaamua kuua na kuumiza raia wao ambao waliwapambania kujitenga kutoka Sudan.

Tuiangalie Somalia ambapo tayari tumeona limejitokeza taifa la Somaliland na hata vivyo miamba ya kivita wakiisambaratisha Somalia kwa zaidi ya miaka 10 ikawa haina serikali na hatimaye kuzaa kiatamizi cha ugaidi na uharamia duniani.

Afrika ya Kati kulikuwepo na Aka Yesu ambao walitaka nchi hiyo iendeshwe kupitia Amri Kumi za Mungu, tulishuhudia wakichinja raia bila huruma (ingawa jumuiya za kimataifa zilifunga bakuli lao), tuangalie Libya ambapo kikosi kilichoasi kwa kusaidiwa na wahuni wasioipenda Afrika itulie walimpindua na kumuua Gadaffi lakini mpaka leo wanapigana wenyewe kwa wenyewe ili kuwatawala raia huku ikiwatumia kama kinga na target ya silaha zao.

Cabo Delgado ni mfano unaoibuka kuanza ama kuendeleza harakati za kutaka kutawala nchi ya Msumbiji huku wanaotaka kutawaliwa wakiuawa kinyama na silaha za wanaojiita wakombozi na watetezi wao.

DRC napo ni mwendo wa kutaka kupanua tawala za watu. Uganda hakujapoa bado. Africa Magharibi tukiitaja Mali, Senegal, Nigeria na kwingineko ni matukio ya kugombania hatamu za kutawala ama kujitawala huku wanaokufa kwa wingi ni wale ambao inasemwa hizo vita zinapiganwa kwa ajili yao.

TATIZO LILILOPO
  1. Kukosekana kwa mfumo mzuri wa maongozi ya nchi kwa viongozi na tawala nyingi kujimilikisha nchi bila kuzingatia uongozi bora na umajumui wa Kiafrika hasa hasa kuchechemiza ubunifu wa kifikra kuzikomboa kaya za Afrika kutoka kwenye udunishwaji wa elimu, Afya, Uchumi na rasilimali ni big factor
  2. Uroho na ulafi wa madaraka ambapo waliopo madarakani wameendeleza dhana ya kung'ang'ania madarakani huku walio nje ya madaraka wakitafuta fursa ya kutawala ili nao wafaidike na wizi mkubwa wa rasilimali za nchi huku wakilindwa na vyombo vya dola ambavyo havina nidhamu kwa nchi.
  3. Ombwe la kuwepo kwa Katiba nzuri ama maridhawa zinazotoa haki, wajibu na kuunda taasisi imara za kusimamia nchi
  4. Kukosekana kwa UTASHI wa kuheshimu katiba za nchi
  5. Uwepo wa viwanda vya silaha ambazo huletwa Afrika na kuoatiwa makundi hasimu waweze kupigana na kuuana.
  6. Kukosekana kwa taasisi inayowaunganisha Waafrika ili kuprovide usalama na ustawi wa Waafrika. Umoja wa Afrika uliopo siyo wa Waafrika bali ni wa Viongozi wa Afrika pekee.
  7. Kukosekana kwa Elimu. Hatuna elimu zaidi ya kurithi elimu isiyo na tija kwa Afrika
  8. ....

Je unadhani nini kifanyike kukomesha vita vya msituni vinavyoendelea Afrika?

Je kwa nini Jumuiya za Kimataifa hazijigusi kwenye kukomesha vita ambapo badala yake zimejazana huko na maasikari wao kwa kivuli cha kutoa misaada ya kibadamu?
 
Me nafikiri tuwaache waishi maisha yao,kama mtu amekimbia town ameacha vyote amekimbilia machaka kuwinda watu!!!! unafikiri Sisi tufanyaje,tuwafate machaka ili watuuwe na Sisi au
 
1 tribal violences
2 the quest for economic power

These things turning Africa into a killing field
 
Back
Top Bottom