Nawatonya! Upinzani wataongea mambo ya ovyo kimkakati wa maridhiano na CCM kwa ahadi ya kurejeshewa majimbo yao 2025

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Hakika upinzani upo kimaslahi binafsi!
Hakuna chama cha upinzani chenye nia ya kushika dola!

Hata rais mbele ya bawacha alilisisitiza hilo, siyo kwamba alitania, ukweli ndiyo huo! Kelele za upinzani huwa ni za kutafta shibe hakuna chama hata kimoja chenye nia ya kushika dola kwa sasa!

Katika mazungumzo ya maridhiano na CCM mtashuhudia Viongozi wa upinzani wakiropoka hoja za kipuuzi ili kuipa nguvu CCM.

Screenshot_20230312-070043.png


1. Alianza Godbless LEMA Kufuta Bodaboda na hii hoja ya hovyo CCM wamenufaika nayo.

2. Msigwa naye kaleta hoja nyingine ya kipuuzi kwamba shule zote nchini ziwe day! Yaani tufute KIBAHA BWENI, TUFUTE ILBOLU BWENI, TUFUTE TABORA BWENI, TUFUTE BWIRU BWENI, TUFUTE MOSHI TECHNICAL BWENI, TUFUTE IFUNDA BWENI, LYAMUNGO,TOSA, OLDMOSHI. Shule Zoooote za bweni tufute!Ukiuliza ni kwanini majibu eti zinaleta Ushoga!

Yaani viongozi wa sampuli hii ni wa hovyo kabisa! Yaani kila changamoto suruhisho lake ni kufuta!? Wangapi tumepitia hizo shule mbona hatujawahi kuwa mashoga? Wangapi tumepita hizo shule hatukuvuta hata bangi!

Mimi nimesoma bweni najua umhimu wa bweni kuna faida nyingi:

1. Inapunguza mzigo kwa wazazi
2. Inapunguza usumbufu na hatari kwa mtoto
3. Inapunguza mimba za utotoni
4. Inaongeza Socialism kwa vijana
5. Inafudisha stadi za maisha ya kujitegemea
6. Unafundisha ukakamavu
7. Inaweza kuwa chachu ya kuibua vipaji kirahisi kwa vijana kushiriki michezo mingi
8. Ni rahisi walimu kuwasiliana na wanafunzi namna ya kuwasaidia
9. Zinakuza watoto kiimani (kujifunza kusali) n.k

Katika wanafunzi elfu 10 hata ikitokea mashoga wakipatikana 10 haiwezi kuwa chanzo cha kufuta bweni mkumbuke kuna wazima elfu 9990 walio bora.

Ukweli ni kwamba Upinzani wameahidiwa kupewa majimbo yao katika uchaguzi ifikapo 2025! Ili waendelee kutimiza Akidi ya Bunge, biashara zao zilindwe, ruzuku n.k

Tutarajie usalama wa taifa wengi ingizo jipya litajiunga na siasa kupitia upinzani. HAKUNA UPINZANI TANZANIA WENYE MPANGO WA KUSHIKA DOLA!

Chimbuko la upinzani mwalimu nyerere aliruhusu uwepo ili watu wenye mawazo mbadala wapate majukwaa ya kusemea lakini siyo kuongoza nchi!

Chama cha upinzani hakipo kwa sasa labda sheria ya vyama vya siasa iundwe upya, na katiba iundwe upya

Kwa sasa upinzani wameramba asali wataropoka ujinga mwingi kwa maslahi yao na mali zao!

Upuuzi wa LEMA KWENYE HOJA YA BODABODA huu hapa.
 
Kwamba boda zifutwe ni laana! Kwa akili hizo kura yangu upinzani hairambi tena! Mawazo ya hovyo kabisa
Kura ya Mtu mjinga ambaye Hana Elimu ya fikra chanya haina umuhimu , Watz kama wewe ni empty mind na kwa bahati mpo wengi mnafikiria kuhusu leo na kuwaza upolo wa Kesho


Nchi imejaa Alot of resources Kama Ardhi Then unawaambia watu bodaboda ni ajira what a fucking thoughts.
 
Kura ya Mtu mjinga ambaye Hana Elimu ya fikra chanya haina umuhimu , Watz kama wewe ni empty mind na kwa bahati mpo wengi mnafikiria kuhusu leo na kuwaza upolo wa Kesho...
Ujinga ni kuamini kila mtu ni mkulima
Ambacho hukijui na hutaki kuhangaisha kichwa kujua ni kwamba watu hufanya kilichorahisi kwao kuwaingizia kipato!

Kuwa boda boda haizuii kulima, kuwa bodaboda haizuii kutafta fursa zingine!

Bodaboda siyo ya kudumu kwamba unazeekea huko!

Ni wanasiasa wapuuzi wanaweza kushangilia kufuta boda boda!
 
Back
Top Bottom