Road map 2023-2025 na Maridhiano ya Kisiasa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Bado think tank ya CHADEMA inabaki kuwa bora kwa nyakati tulizoona. Bado CHADEMA inabaki kuwa akili kubwa kati ya vyama vyote vya siasa Tanzania kwasasa, kwanini nathubutu kusema haya?

Imeshatibitika wazi kwamba kuna kundi kubwa na lenye nguvu la wahafidhina kwenye mfumo ambao hawataki na hawako tayari kwa mabadiliko.

Imeshathibitika wazi ya kwamba kuna kundi kubwa la wafaidikaji, wakiwemo familia za wanasiasa wa CCM na marafiki zao, wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji katika sekta mbalimbali, imeshathibitika wazi ya kwamba kuna mataifa rafiki wa CCM, yanayofaidika kiuchumi na kijamii kwa CCM kuwepo madarakani, hivyo hayako tayari kuona CCM inaondoshwa.

Imeshathibitika wazi kwamba kupata Katiba Mpya kwasasa ni kipengele kigumu mno. Imeshathibitika wazi ya kwamba kupata Tume Huru ya Uchaguzi itakayokidhi mahitaji ya sasa kisiasa kwenye uchaguzi mkuu pia ni ngumu mno!

Sasa CHADEMA ifanyeje kuweza kutoboa?

~ CHADEMA inahitaji kufanya siasa kwa amani, usalama na utulivu.

~ CHADEMA inahitaji kuongeza wigo wa wanachama na kujiimarisha tangu chini kabisa bila mizengwe na kuleteana tafrani.

~ CHADEMA inahitaji kufanya siasa za kistaarabu na malumbano ya hoja, ili wananchi waweze kupambanua pumba na mchele.

~ CHADEMA inahitaji sana ulinzi na usalama wa viongozi wake wa ngazi zote, wanachama na wafuasi wake, mali, vitega uchumi na uwekezaji wake popote pale Tanzania

Sasa hili litawezekanaje?
Ilikuwa ni muhimu kupara mkakati wa maridhiano. Maridhiano ambayo kwa sehemu kubwa yanayomhitaji mkuu wa kaya kuliko timu zilizokuwa zimeundwa toka vyama mbalimbali kasoro CHADEMA.

Kwanini hili?
Katiba ya sasa inampa madaraka makubwa mkuu wa nchi, hata kama ana washauri nyuma ya pazia lakini anapojitokeza hadharani kauli yake ndio final!

~ Kwa kuliona hili maridhiano yalikuwa ni muhimu zaidi kati ya CHADEMA na CCM kupitia mkuu wa nchi, na ndio maana maridhiano husika yakabeba taswira ya mkuu wa nchi na CHADEMA na hakuna chawa wala kunguni aliyeleta fyoko zaidi ya kulalama mitandaoni.

Faida zake ni nini kwa pande hizi mbili?
Ndani ya CCM kuna makundi yaliyomsumbua sana mama, hasa yale makundi faidika na awamu iliyopita! Haya yamekuwa yakimpinga waziwazi hadharani mitandaoni na sirini pia, kuna haya makundi ya wataka Urais 2025 nayo yamekuwa yakiibuka mara kwa mara lakini yakakutana na nyundo ya mfumo na kusambaratishwa nayo haya ni masumbufu.

CHADEMA ni chama kikuu cha Upinzani Tanzania chenye wanachama milion kumi na wafuasi idadi sawa na hiyo ama kuzidi kidogo. Kwenye siasa watu ni mtaji mkubwa sana, kwa ubunifu wa maridhiano yaliyokuja mama ameweza kuwasambaratisha wakosoaji na wasumbufu wote hasa ndani ya chama chake! Kwahiyo sasa mama ana wasaa mzuri wa kupiga kazi huku wasiompenda wakimuogopa sasa kwa kudhani ana backup ya chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Faida kwa upande wa CHADEMA sasa;

Kufanya siasa za ukosoaji wa hoja kwa makada na wanasiasa wa CCM bila kumhusisha sana mama.

Lengo ni nini?
Kupata Katiba ni lazima uwe na Bunge lenye wabunge wenye utayari na uwezo wa kulisimamia hilo kidete. Kwa mfumo wetu wa sasa wa tume ya uchaguzi, system huwa inamakinika zaidi na kura za Urais.

CHADEMA kwa kudili zaidi na wanasiasa wa CCM ni kutafuta uungwaji mkubwa wakati wa uchaguzi ili CHADEMA ipate majority ya wabunge. Ukishakuwa na majority ya Wabunge hata Rais akitoka upande mwingine una faida ya kufanya mengi kupitia Bunge kama mhimili huru.

Chawa wa mama na Samia gang wameonekana ni uchuro zaidi ya kumsadia mama kuliko faida na political mileage anayoipata kupitia maridhiano na CHADEMA.

Hizi tuhuma za kulamba asali na ukosoaji mwingine wa kijinga ni hasira, wivu husuda na kijicho kwa wale wote ambao hawakuridhishwa na hayo maridhiano yanayowaweka CHADEMA na mama kwenye nafasi bora zaidi kisiasa Tanganyika!

Ni alfajiri nyingine tena ya faraja kuu!
 
Bwana asipoulinda mji, waulindao waukesha bure. CHADEMA kinalindwa na Mungu sisi wanachama kazi yetu nibkuongeza dua. Kama Nduli alishindwa kuifuta CHADEMA, akafutika yeye, basi CHADEMA ni taasisi imara sana.

Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi vinakuja, ni swala la muda tu. Na CCM Itafutika kabisa katika uso wa dunia
Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi vinakuja, ni swala la muda tu. Na CCM Itafutika kabisa katika uso wa dunia
 
Teh teh teh silly minds always thinks it is wise

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma hiki kitabu kitakusaidia sana
9d8405b8531b3a04fd9f677d62cd5697.jpg
 
Maridhiano ni Ukomavu wa kisiasa
Maridhiano ni ukomavu wa kifikra
Maridhiano ni Ishara ya kuridhika na kukinai Ulevi wa madaraka.

Maridhiano ni kutokuwa na tamaa ya madaraka,Maridhiano ni kutambua mchango wa mwenzio na kujua ww na yeye wote ni kitu kimoja.

Kwenye Maridhiano hakuna mshindi wala mshindwa bali wote kama Nchi tumeshinda.

Kongole Kwako Rais Mama Samia..
Kongole kwako Mwenyekiti Kamanda Mbowe..

Tanzania ni Zaidi ya CCM na CHADEMA
 
Maridhiano ni Ukomavu wa kisiasa
Maridhiano ni ukomavu wa kifikra
Maridhiano ni Ishara ya kuridhika na kukinai Ulevi wa madaraka.

Maridhiano ni kutokuwa na tamaa ya madaraka,Maridhiano ni kutambua mchango wa mwenzio na kujua ww na yeye wote ni kitu kimoja.

Kwenye Maridhiano hakuna mshindi wala mshindwa bali wote kama Nchi tumeshinda.

Kongole Kwako Rais Mama Samia..
Kongole kwako Mwenyekiti Kamanda Mbowe..

Tanzania ni Zaidi ya CCM na CHADEMA
Kwenye Maridhiano hakuna mshindi wala mshindwa bali wote kama Nchi tumeshinda.

Kongole Kwako Rais Mama Samia..
Kongole kwako Mwenyekiti Kamanda Mbowe..

Tanzania ni Zaidi ya CCM na CHADEMA
 
Majira ndio muhimu bro. Ushawahi kufika Bumbaa, DRC? Mwendo ni green all the times.

Utasubiri sana nyasi ziwe za kaki....
Ndio maana nikasema wakati si milele.. Je umenielewa vema hapo!? No matter what ccm haitakaa madarakani milele..
 
Back
Top Bottom