Nawashukuruni Wana JmiiForum wote-KakaKiiza

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Asalam aleykum Jamii,
Nimatumaini yangu amjambo wote ningeomba kuchua wasaa huu kuelezea machache yaliyopo moyoni mwangu!
Ni majuzi tangu nilipoondokewa na mke wangu kipenzi , Subira Alfred Mwamasso mnamo wa saa 09:27hrs tarehe 31.Katika Hosptali ya Taifa Muhimbili
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote ambao walikuwa na mimi katika kipindi hiki kigumu na bado wanaoendelea kushirikiana na mimi kwa njia moja au nyingine ningewaomba ni wambie sina chakuwalipa kwa wema mkubwa waliouonyesha kwangu!!Ninawaomba wapokee hii shukurani yangu ya dhati kutoka kwangu kwani nimefarijika kwakiasi kikubwa kwa wale walio bahatika kufika msibani waliona nilikutana na mtu na kujitambulishas yeye ni mwana JF kwa jinsi nilivyo badrika na kuwa nafuraha naye kwakusema ukweli hii ilinifariji sana!!.
Kwakweli nikitu ambacho sikukitegemea mimi binafsi kuwa nitakuja kuwa na marafiki ambo siwakuwai kuwafahamu!Nilidhani rafiki niyule unayekutana naye barabarani,mgahawani,kwenye basi,Baa na sehemu za maofisini na hata kwenye misiba na harusi!!Kumbe la hasha!!
Hata nyuma ya keyboard kuna dunia nyingine inayoishi na inayoweza kuwa msaada mkubwa kwako bila wewe kujitambua!! hasa wewe mhusika utaitumia keyboard kwa uangalifu na kwa umakinai zaidi!!
Ninamengi sana ya kueleza lakini naona siwezi kuyamaliza!!
Hivyo ngoja nifupishe maneno nirudi kule nilikokusudia hapo awali!

********************************************************************************
Napenda niongozwe na utashi wa mwenyezi mungu kwakuwa ndiye amenipa huu uwezo nilionao kwa sasa.
Napenda kutoa shukurani njia moja au nyingine kwa wale wote ambao mliweza kunipa faraja kwenye hiki kipindi kigumu kwangu kwa walenitakao wa sahau nitawaombeni mniwie radhi sana kwani na mimi ni binadamu naweza kughafirika ila na wahaidi kuwa nitakuwa nana UPDATE pale nitakapo kuwa nimekumbuka!

Napenda kutoa shukurani kwa JF Management.

Napenda kutoa shukurani kwa mmoja mmoja kama ifuatavyo:-
(Special Thanks),


Maxence Melo Invisible @ X-PASTER Kiresua Mtambuzi mamamia YNNAH The Finest Preta Caroline Danzi RR Nicas Mtei TANMO BelindaJacob Dark City Gedeli Mr Rocky FirstLady1 Gaijin Liverpool Chauro Swts The secretary AshaDii afrodenzi tete'a'tete Fixed Point
Kwa wale ambao sijawataja naomba waniwie radhi nikikumbuka nitawaweka hapa!Nimesahau kwa bahati mbaya!


Kila siku ninawaombea wote mlioshirikiana na mimi katika kipindi hiki kizito kwangu napenda kusema

"SINA CHA KUWALIPA MUNGU AWAZIDISHIE BARAKA NA HEKIMA"


Asanteni wote muendelee na moyo huo!na mungu awabariki awahepushe nakila lilobaya awanyoshee njia.AMAN.

********************
NAOMBA KUMUALIFU MUHUSIKA ALIYENITUMIA RAMBI RAMBI KWAKUTUMIA TIGO NIMESHINDWA KUICHUKUA KWAKUWA SINA NAMBA YAKE YA TIGO!ANI-PM JINA LAKE NA NAMBA ALIYOITUMIA, KUNITUMIA HIYO RAMBI RAMBI!NAWASHUKURUNI SANA!KWA WEMA WENU NA MUNGU AWABARIKI!.
 
karibu tena kaka, na pole kwa matatizo. Mwenyezi Mungu aendelee kukufariji. . .
 
Asnteni wapendwa na washukuru sana kwa kuonyesha mnajali sana!
 
Kaka KakaKiiza karibu tena na pole sana mkuu. Uwe na moyo wa subira na uvumilivu. Mungu awe nawe kaka.
 
Last edited by a moderator:
Mkubwa! Pole sana kwa yote yaliyokukuta Kamanda wetu!
Uwe na Amani pamoja na familia Kamanda!
Hakika ni wakati mgumu kwetu binadamu lakini hakika kwake MUNGU ni mambo madogo sana!

Tukae kama wenye IMANI!
 
Pole sana Kaka Kiiza. Mwenyezi Mungu akupe nguvu, Imani na Amani katika hiki kipindi cha mapito kwako mwenyewe na familia yako yote. Ni mtihani mkubwa kuondokewa na Mwenza, Ila Inshaallah tumuombe Mungu aweze kukujaalia kupita hiki kipindi kigumu. Nakuombea kila la kheri na wepesi katika kipindi hiki.

Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Upendo amlaze pema peponi marehemu Subira... Pamoja sana.
 
Pole tena kaka. Waswahili wanasema ndio ukubwa. Mungu azidi kuwashindia, msipungukiwe kwa neno lolote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom