Nawashukuruni Wana JmiiForum wote-KakaKiiza

Asalam aleykum Jamii,
Nimatumaini yangu amjambo wote ningeomba kuchua wasaa huu kuelezea machache yaliyopo moyoni mwangu!
Ni majuzi tangu nilipoondokewa na mke wangu kipenzi , Subira Alfred Mwamasso mnamo wa saa 09:27hrs tarehe 31.Katika Hosptali ya Taifa Muhimbili
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote ambao walikuwa na mimi katika kipindi hiki kigumu na bado wanaoendelea kushirikiana na mimi kwa njia moja au nyingine ningewaomba ni wambie sina chakuwalipa kwa wema mkubwa waliouonyesha kwangu!!Ninawaomba wapokee hii shukurani yangu ya dhati kutoka kwangu kwani nimefarijika kwakiasi kikubwa kwa wale walio bahatika kufika msibani waliona nilikutana na mtu na kujitambulishas yeye ni mwana JF kwa jinsi nilivyo badrika na kuwa nafuraha naye kwakusema ukweli hii ilinifariji sana!!.
Kwakweli nikitu ambacho sikukitegemea mimi binafsi kuwa nitakuja kuwa na marafiki ambo siwakuwai kuwafahamu!Nilidhani rafiki niyule unayekutana naye barabarani,mgahawani,kwenye basi,Baa na sehemu za maofisini na hata kwenye misiba na harusi!!Kumbe la hasha!!
Hata nyuma ya keyboard kuna dunia nyingine inayoishi na inayoweza kuwa msaada mkubwa kwako bila wewe kujitambua!! hasa wewe mhusika utaitumia keyboard kwa uangalifu na kwa umakinai zaidi!!
Ninamengi sana ya kueleza lakini naona siwezi kuyamaliza!!
Hivyo ngoja nifupishe maneno nirudi kule nilikokusudia hapo awali!

********************************************************************************
Napenda niongozwe na utashi wa mwenyezi mungu kwakuwa ndiye amenipa huu uwezo nilionao kwa sasa.
Napenda kutoa shukurani njia moja au nyingine kwa wale wote ambao mliweza kunipa faraja kwenye hiki kipindi kigumu kwangu kwa walenitakao wa sahau nitawaombeni mniwie radhi sana kwani na mimi ni binadamu naweza kughafirika ila na wahaidi kuwa nitakuwa nana UPDATE pale nitakapo kuwa nimekumbuka!

Napenda kutoa shukurani kwa JF Management.

Napenda kutoa shukurani kwa mmoja mmoja kama ifuatavyo:-
(Special Thanks),


Maxence Melo Invisible Kiresua Mtambuzi mamamia YNNAH The Finest Preta Caroline Danzi RR Nicas Mtei TANMO BelindaJacob Dark City Gedeli Mr Rocky FirstLady1 Gaijin Liverpool Chauro Swts The secretary AshaDii afrodenzi tete'a'tete Fixed Point
Kwa wale ambao sijawataja naomba waniwie radhi nikikumbuka nitawaweka hapa!Nimesahau kwa bahati mbaya!


Kila siku ninawaombea wote mlioshirikiana na mimi katika kipindi hiki kizito kwangu napenda kusema

“SINA CHA KUWALIPA MUNGU AWAZIDISHIE BARAKA NA HEKIMA”


Asanteni wote muendelee na moyo huo!na mungu awabariki awahepushe nakila lilobaya awanyoshee njia.AMAN.

Tuko pamoja kaka. Mungu akutie nguvu. AMEN
 
" Hata nyuma ya keyboard kuna dunia nyingine inayoishi na inayoweza kuwa msaada mkubwa kwako bila wewe kujitambua!! hasa wewe mhusika utaitumia keyboard kwa uangalifu na kwa umakinai zaidi!!" Nimefarijika na Nukuu hii. Pole Sasa (Wagila ibi)
 
pole sana na Mungu akuongoze ktk kipindi hiki kigumu na akupe ujasiri wa kuwalea wanao apumzike kwa amani Subra ameen
 
Mungu akutumie msaada toka patakatifu pake, jina la Munu wa Yakobo likuinue.
 
Tunashukuru sana kwa uwakilishi, inatia moyo kwa kweli kuona watu mnaowasiliana kwa keyboard tu wanajitokeza unapokuwa na tatizo. Nimewapenda sana wooooote mliotuwakilisha, Mungu atawabariki sana

Ameen!
Mimi nakiri kwamba JF ni zaidi ya Familia,
Japo tunawasiliana kwa Hisia,lakini Ni Kama tunaonana.
Nasi Tunakupenda wooote.
Asante mkuu Fixed Point
 
Last edited by a moderator:
Pole sana KakaKiiza,
Amani ya Bwana Yesu iwe nawe daima na akupe Nguvu ya kunyanyuka na kuendelea na maisha ili uweze kuendeleza aliyoacha mkeo. Kweli inauma.
 
pole sana,kuonana uso kwa uso humu jf sio sana lakini wengi tuna mioyo na hisia za utu,karibu sanA na pole!
 
Asalam aleykum Jamii,
Nimatumaini yangu amjambo wote ningeomba kuchua wasaa huu kuelezea machache yaliyopo moyoni

Napenda kutoa shukurani kwa JF Management.

“SINA CHA KUWALIPA MUNGU AWAZIDISHIE BARAKA NA HEKIMA”


Asanteni wote muendelee na moyo huo!na mungu awabariki awahepushe nakila lilobaya awanyoshee njia.AMAN.
Mkuu KakaKiiza, pole sana kwa mara nyingine tena, uwe na subra na Mwenyezi Mungu awe nawe katika kila jambo la kheri Insha'Allah.
 
" Hata nyuma ya keyboard kuna dunia nyingine inayoishi na inayoweza kuwa msaada mkubwa kwako bila wewe kujitambua!! hasa wewe mhusika utaitumia keyboard kwa uangalifu na kwa umakinai zaidi!!" Nimefarijika na Nukuu hii. Pole Sasa (Wagila ibi)
Elitagaraile mkuu ukweli ni huo kwani ndicho nimekigundua kuwa ya wezekana robo ya dunia inaishi nyuma ya keyboard na inategemea kilakitu nyuma ya keyboard!!
 
Pole sana KakaKiiza for the loss of your beloved wife.
Mungu amempenda zaidi, yakupasa kuwa na moyo mkuu na kushukuru kwa yote.

Mungu akujalie ujasiri na moyo wa subira ktk kipindi hiki kigumu, God wil heal your pain.
 
Pole KakaKiiza, hiyo ni challenge tu ya maisha believe in God and all will be well
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom